JamiiForums
βœ”
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NORWAY YAONDOA VIZUIZI VYA #COVID19

Waziri Mkuu asema raia wake wanalindwa vyema kwa Chanjo ya #CoronaVirus

Watu hawatolazimika kuvalia Barakoa ktk maeneo ya Umma wala kukaa umbali wa Mtu na Mtu. Watakaoathirika watakaa Nyumbani siku 4 tu

Soma - https://jamii.app/NoCoronaNorway

#UVIKO3 #JFAfya
UJERUMANI: Raia wanamchagua Rais leo, Februari 13, 2022 kupitia Baraza la Wabunge na Wajumbe wa Majimbo yote 16

Rais wa Ujerumani huchaguliwa kila baada ya miaka 5 ambaye huwa Mkuu wa Nchi, tofauti na Kansela ambaye ni Mkuu wa Serikali

Soma - https://jamii.app/ElectionGermy

#Democracy
πŸ‘1
DAR: SOKO LA RANGITATU LAUNGUA MOTO

Soko hilo lililopo Mbagala limeungua usiku wa kuamkia leo (Februari 13, 2022) na Chanzo hakijafahamika

Matukio ya moto yameendelea kuripotiwa Nchini. Je, hatua stahiki zinachukuliwa kutatua changamoto hii?

Soma - https://jamii.app/MotoSokoMbagala

#JFMatukio #Accountability
Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio. Licha ya ukuaji wa Sayansi na Teknolojia, Redio imeendelea kuwa moja ya Vyombo vya Habari vinavyotumika na kuaminika zaidi

Hii ni kwasababu inaweza kusikilizwa kokote, hata maeneo yasiyo na Umeme wala Intaneti ya Uhakika. Kwa kiasi kikubwa, Redio imeziba pengo la kupata taarifa katika Jamii

#WorldRadioDay
TANZIA: EDWIN RUTAGERUKA AFARIKI DUNIA

Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi, Balozi Edwin Rutageruka amefariki dunia leo, Februari 13, 2022

> Rutageruka aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE)

#RIPRutageruka
TUNISIA: WANANCHI WAANDAMANA KUPINGA RAIS SAIED KUJIONGEZEA MADARAKA

Rais wa #Tunisia, Kais Saied, ameimarisha Madaraka yake dhidi ya Mahakama baada ya kutangaza Kanuni inayomruhusu kuwafukuza kazi Majaji au kuwazuia kupandishwa cheo

Soma - https://jamii.app/KaisTunisia

#Democracy
Jamii Forums kwa kushirikiana na Muhimbili University of Health and Applied Science (MUHAS), Muhimbili National Hospital (MNH), Tumaini la Maisha (TLM) na Wadau wengine wameandaa Mjadala utakaofanyika kupitia Clubhouse ya JamiiForums ili kuongeza uelewa juu ya Saratani kwa Watoto Nchini #Tanzania

Mjadala huu unatarajiwa kufanyika Jumanne, Februari 15, 2022

Link > https://jamii.app/MjadalaSarataniWatoto

#JamiiForums #CancerDay2022 #JFAfya
Marekani imetangaza dau la takriban Tsh. Bilioni 11.5 kwa atakayetoa taarifa zitakazofanikishwa kukamatwa kwa Kiongozi wa Waasi Nchini #Uganda, Joseph Kony

Joseph Kony ni kiongozi wa Kundi la Waasi la LRA na amesababisha mauaji zaidi ya 100,000

Soma - https://jamii.app/JosephKony

#JFMatukio
MAREKANI YAAHIRISHA UTOAJI WA CHANJO YA #COVID19 KWA WATOTO

Utoaji wa Chanjo kwa Watoto wenye miezi 6 hadi miaka 4 umeahirishwa baada ya idara ya Chakula na Dawa (FDA) kuhitaji Data zaidi

Chanjo hiyo ingeanza kutolewa Februari 21, 2022

Soma - https://jamii.app/COVID19Variants

#UVIKO3 #JFAfya
AFYA: Kwa mujibu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) mtu anaweza kupata madhara kiafya ikiwa kukosa usingizi wa kutosha ni sehemu ya maisha yake ya kila siku

Ili kupata usingizi mzuri, inashauriwa kuweka pembeni vifaa vya kielektroniki wakati wa kulala. Pia, kufanya mazoezi ya mwili kunaweza kukusaidia kulala kirahisi

Soma - https://jamii.app/AfyaUsingizi

#JFAfya
UJERUMANI: RAIS FRANK-WALTER STEIMEIER ACHAGULIWA KUONGOZA MUHULA WA PILI

Ameungwa Mkono na Vyama vyote 3 vinavyounda Serikali ya Mseto, pamoja na Chama cha Upinzani cha Wahafidhina cha CDU

Wadhifa wa Rais Nchini Ujerumani ni wa Heshima

Soma - https://jamii.app/RaisUjerumani

#Governance
SPIKA TULIA: HALIMA MDEE NA WENZAKE WAPO BUNGENI KIHALALI

Amesema, "Nchi yetu inaendeshwa Kisheria. Jambo moja tu linalosubiriwa ni watu kumaliza michakato yao inayohusika"

Ameeleza, Mtu anakosa Uhalali wa kuwepo Bungeni akifukuzwa Uanachama

Soma - https://jamii.app/UhalaliWabunge19

#Democracy #JFSiasa
MDAU: VIJANA TUSIISHI KWA NADHARIA, MAZOEA NA KUKARIRI

Anasema kati ya vitu vinavyofelisha sana Vijana ni kuogopa kuthubutu, akieleza wamekuwa waoga na wenye aibu kupindukia

Asema masuala ya "watanionaje au watanichukuliaje" yamefanya wazidi kuwa masikini

Msome - https://jamii.app/MafanikioSOC

#StoriesOfChange #JFMdau
WAZIRI MKUU: HUWEZI KUZUNGUMZIA UTALII BILA KUWATAJA WAMAASAI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hauwezi kuzungumzia Utalii wa #Tanzania bila kutaja Wamaasai na suala la wao kuishi na Wanyamapori Hifadhi ya Ngorongoro linavutia

Soma - https://jamii.app/WamaasaiNgorongoro

#Utalii #JFLeo #Governance
SARATANI KWA WATOTO: Kila mwaka, inakadiriwa takriban Watoto/Vijana 400,000 wa umri kuanzia 0 - 19 hupata Saratani

Katika Nchi zilizoendelea zaidi ya 80% ya Watoto hupona. Kwa Nchi zenye kipato cha Chini na Kati, Watoto chini ya 30% ndiyo hutibiwa

Soma - https://jamii.app/ChildCancers

#JFAfya
Shirika la UN linaloshughulika na Idadi ya Watu (UNFPA) linasema Wasichana milioni 12 Duniani huolewa kabla ya kufikisha miaka 18

Kwa siku ya wapendanao, UNFPA wanasema β€˜Mtaje Valentine wako, lakini tafadhali asiwe Mtoto’

Soma - https://jamii.app/ChildMarriage

#EndChildMarriage #HakiMtoto
PARIS, UFARANSA: Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron katika Ikulu ya ElysΓ©e leo Februari 14, 2022

Rais Samia yupo Nchini Ufaransa kwa ziara ya kikazi

Soma - https://jamii.app/RaisSamiaParis

#JamiiForums #Governance
MBOWE: TUMEKOSA HAKI YA CHAKULA MCHANA KWA MIEZI MITANO

Amesema, "Mwanzo tuliambiwa kuwa kama Chakula tuchukue kutoka Jela, tutoke nacho Jela tuje nacho Mahakamani. Tukitoka hapa tunakuta Magereza wameshakula tunakwenda kulala na njaa siku zote"

Soma - https://jamii.app/MboweHakiChakula

#JFSiasa
MARA: KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MJUKUU WAKE

Nkwandu Kayenze (76) Mkazi wa Natta, Wilayani Serengeti amefikishwa Mahakamani kwa kosa la kumpiga na kumsababishia kifo Matoja Deus (11) aliyetumia Tsh. 2,000 bila ruhusa

Soma https://jamii.app/MaraBibi

#JFMatukio