JamiiForums
55.4K subscribers
33.4K photos
2.04K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: SOKO LA KARUME LATEKETEA KWA MOTO

Soko la Karume lililopo Wilayani Ilala Dar es Salaam limeteketea kwa moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika

> Taarifa zaidi kukujia

Soma - https://jamii.app/KarumeMoto

#JFMatukio
Polisi Nchini #Haiti imesema Seneta wa zamani, John Joel Joseph ambaye ni mshukiwa mkuu ktk mauaji ya aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo ametiwa mbaroni Nchini #Jamaica

Rais Moise alivamiwa Nyumbani kwake Julai 7, 2020 na kuuawa kwa kupigwa risasi

Soma - https://jamii.app/JosephHaitiArr

#Accountability
TANGA: TRENI YA ABIRIA YAPATA AJALI, MTOTO AFARIKI

Treni iliyokuwa inatoka Arusha kuelekea Dar ikiwa na abiria 700 imepata ajali alfajiri ya leo, Januari 16 Wilayani Pangani

Mabehewa 5 yamepinduka, 4 yameacha njia na kusababisha majeruhi 5

Soma - https://jamii.app/AjaliTRC

#JFMatukio
AUSTRALIA: Mahakama ya Shirikisho la #Australia imeikataa rufaa iliyoletwa na Bingwa wa Tennis Duniani, Novak Djokovic akipinga kufutwa kwa 'visa' yake na kufukuzwa kwa kutochoma Chanjo

Michuano ya #Tennis ya Australian Open inaanza leo, Januri 17 ambapo alikuwa amenuia kutafuta taji la 21 la Grand Slam

Soma - https://jamii.app/DjokovicNoRufaa

#JFSports
RIPOTI: MATAJIRI WATAJIRIKA ZAIDI WAKATI WA COVID-19

Shirika la Oxfam lasema utajiri wa Mabilionea 10 wakubwa zaidi umeongezeka maradufu wakati wa #CoronaVirus

Mapato ya chini ya Mataifa masikini zaidi yalichangia vifo vya watu 21,000 kila siku

Soma - https://jamii.app/OxfamReport

#JFMatukio
MDAU: WANASIASA WANAWACHUKULIAJE WANANCHI WA KAWAIDA?

Anasema kwa Mfano katika Kampeni za Uchaguzi, Mwanasiasa huweza kuwaambia Wananchi jambo fulani litakamilika muda mfupi tu baada ya kumchagua, lakini inaweza kupita hata miaka 10 hakuna kinachofanyika

Anashauri wananchi kujitahidi kadri ya uwezo wao kung'amua Mwanasiasa anayefaa na asiyefaa kupitia vitendo vyao na si maneno. Pia, Wanasiasa wanapaswa kujua zama zimebadilika, sasa sio kama zamani

Soma - https://jamii.app/SOCSiasa

#StoriesOfChange #JFSiasa #Uwajibikaji
MDAU: MAMBO YA KUZINGATIA KABLA HUJAANZA KUFUGA KUKU KIBIASHARA

1. Uwepo wako (Availability): Anasema kabla ya kuanza ufugaji wa Kuku Kibiashara hakikisha unapata nafasi ya kushiriki kwa karibu katika mradi wako

2. Kujitoa (Commitment): Unatakiwa kujitoa kweli kwa kuweka imani kuwa hawa Kuku ndio ajira yangu, watanisaidia kuendesha familia yangu

Zaidi, soma - https://jamii.app/KukuBiashara

#JFMdau
DAR: Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amesema hakuna mtu yeyote anatakiwa kumwingilia au kumpigia simu Hakimu ambaye suala au kesi fulani ipo mbele yake

Ameeleza hayo katika Hafla ya kuapishwa Mahakimu Wakazi na kuwataka waepuke kuzungumzia masuala ya Mahakama kwenye makundi ya WhatsApp

Soma - https://jamii.app/UapishoMahakimu

#JFSheria
DAR: Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya Wafanyabiashara wa soko la Karume (Mchikichini) wakishinikiza kuruhusiwa kuendelea na biashara ktk soko hilo lililoungua

Walitumia mawe na magogo kufunga Barabara ktk makutano ya Uhuru na Kawawa, Ilala Boma

Soma - https://jamii.app/MachingaMabomu

#JFMatukio
SUDAN: Madaktari Nchini humo wameandama kupinga mashambulizi dhidi ya Hospitali na Vikosi vya Usalama

Aidha, Mamlaka imekifuta kibali cha kituo cha Habari cha Al Jazeera Mubasher cha #Qatar pamoja na vibali vya Waandishi wake wawili

Soma - https://jamii.app/BanAlJazeeraSudan

#PressFreedom
MDAU: USIKIMBILIE UJASIRIAMALI KISA UMECHOKA BARUA ZA ONYO ZA MWAJIRI WAKO

Anasema Ujasiriamali ni kazi ngumu ambayo kila kitu kinategemea jitihada na Akili zako mwenyewe. Kwa Mwajiri una uhakika wa Mshahara lakini kujiajiri inategemea kiasi gani ulijitoa

Anasema kama kazi ya Mwajiri unaona ni mzigo, basi kinachokusumbua ni uvivu. Ujasiriamali unahitaji Nguvu na Nidhamu ya kiwango cha juu kuliko ulivyokuwa kwa Mwajiri wako.

Mjadala, soma - https://jamii.app/AjiraVsUjasiriamali

#Ujasiriamali #JFMdau
MICHEZO: Tiketi za Michezo ya Olimpiki ya Msimu wa Baridi 'Winter Olympics' iliyopangwa kuanza Februari 4, 2022 huko Beijing zitatolewa kwa makundi kadhaa ya watu na hazitauzwa kwa Umma

China inapambana kudhibiti maambukizi ya #Omicron

Soma - https://jamii.app/BeijingWO

#JFSports
#AFCON2021: CAMEROON, BURKINA FASO ZAFUZU HATUA YA MTOANO

Mwenyeji wa michuano, #TeamCameroon ameingia hatua ya mtoano baada ya kutoka sare ya goli 1-1 na #TeamCapeVerde

Aidha, #TeamBurkinaFaso imetinga hatua hiyo baada ya kutoka sare ya goli 1-1 na #TeamEthiopia

#JFSports
LIBYA: Umoja wa Mataifa (UN) umependekeza Uchaguzi wa Rais ulioshindwa kufanyika Desemba 2021 kufanyika Juni 2022

Mshauri Maalum wa UN kuhusu Masuala ya Libya, Stephanie Williams asema Raia wanataka kuchagua Serikali ya Kidemokrasia

Soma - https://jamii.app/UNUchaguziLibya

#Democracy
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Ashatu Kijaji ametoa siku 3 kwa Tume ya Ushindani (FCC) kutoa sababu ya kupanda kwa bei za vinywaji Baridi Nchini

Pia, ametoa siku saba kwa FCC kueleza sababu za kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi

Soma - https://jamii.app/FCCBeiSoda

#JFBiashara
#Uganda inakabiliwa na uhaba wa Mafuta ya Petroli kutokana na foleni kubwa ya Magari ya kusafirisha bidhaa hiyo kwenye mipaka ya Busia na Malaba

Foleni inakadiriwa kufika hadi Kilometa 70 kutokana na Madereva kulazimika kufanyiwa vipimo vya Corona

Soma - https://jamii.app/LackPetrolUG
UTEUZI: Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Mcha Hassan Mcha kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA)

Vilevile, Balozi Celestine Joseph Mushy ameteuliwa na Rais Samia kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Austria

Soma - https://jamii.app/UteuziViongozi2

#Governance
AFGHANISTAN: Kundi la Wataalamu 36 wa Haki za Binadamu kutoka Umoja wa Mataifa limesema Viongozi wa Taliban wanafanya Ubaguzi na Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake

Jumuiya ya Kimataifa yasisitizwa kuongeza kasi ya misaada ya kibinadamu

Soma - https://jamii.app/WomenTaliban

#WomensRights #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: MABASI YA MIKOANI KUONGOZWA NA ASKARI WA BARABARANI

Akizungumza na JamiiForums, Kamanda Onesmo Lyanga amesema Watakuwa wanaweka Askari kwenye Basi la Kwanza, na Mabasi mengine hayatakiwi kulipita hilo basi la kwanza

Lengo ni kudhibiti ajali zinazotokana na Uzembe. Utaratibu huo pia umeonekana kufanyika kwa Mabasi yatokayo Mbeya kama kwenye Video

Soma - https://jamii.app/MabasiEscort