JamiiForums
51.2K subscribers
34.6K photos
2.54K videos
31.6K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
HUSSEIN BASHE ATEULIWA KUWA WAZIRI WA KILIMO

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Hussein Bashe kuwa Waziri wa Kilimo. Awali Bashe alikuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo

Anthony Mavunde ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo

#Governance
PROF. ADOLF MKENDA AHAMISHIWA WIZARA YA ELIMU

Aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amehamishiwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambayo awali Prof. Joyce Ndalichako alikuwa Waziri

Rais Samia amemhamisha Prof. Ndalichako kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu; Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu

#Governance
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu amembadilisha Wizara George Simbachawene aliyekuwa Wizara ya Mambo ya Ndani kwenda Wizara ya Katiba na Sheria

Pia, amembadilisha Innocent Bashungwa aliyekuwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda Wizara ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI

#JFUteuzi #Governance
👍1
MOHAMED MCHENGERWA KUWA WAZIRI WA UTAMADUNI

Rais Samia amemhamishia Mohamed Omary Mchengerwa aliyekuwa Ofisi ya Rais, Menejimenti, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo awali ilikuwa chini ya Innocent Bashungwa

#Governance
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amembadilisha Wizara, Ashatu Kijaji aliyekuwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

#JFUteuzi #Governance
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amembadilisha Wizara Jenista Mhagama aliyekuwa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kwenda Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora

#JFUteuzi #Governance
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Angelina Mabula kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Pia, amemteua Ridhiwani Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo

#JFUteuzi #Governance
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Pindi Chana kuwa Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu atakayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu

#JFUteuzi #Governance
RAIS SAMIA ABADILI WIZARA 3

Ameunganisha Wizara ya Uwekezaji na Wizara ya Viwanda na Biashara kuwa na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Ameunda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Wizara ya Afya kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

#Governance
#AFCON2021: NANI KUWA BINGWA?

Michuano hiyo inaanza kesho Januari 9, kwa wenyeji #TeamCameroon kuivaa #TeamBurkinaFaso majira ya saa 1:00 jioni (EAT)

#TeamAlgeria ambaye ni Bingwa Mtetezi, #TeamCameroon, #TeamSenegal na #TeamEgypt zinapewa nafasi kubwa kuwa Bingwa

#JFSports
JWTZ wamekanusha taarifa zilizochapishwa katika YouTube channel ya News24 ikiwa na kichwa 'MKUU WA MAJESHI AINGILIA KATI SAKATA LA RAIS NA SPIKA'

> Wamesema wanafanya kazi kwa weledi na hawaingilii masuala ya kisiasa

Soma https://jamii.app/KanushoJWTZ

#Accountability
#AFCON2021: CAMEROON YAANZA KWA USHINDI

- Mtayarishaji wa Mashindano hayo #TeamCameroon imeanza kwa ushindi wa goli 2-1 dhidi ya #TeamBurkinaFaso katika mchezo wa ufunguzi

- Mchezo unaofuata saa 4:00 usiku (EAT) ni kati ya #TeamEthiopia na #TeamCapeVerde

#JFSports
KILIMANJARO: BINTI ADAIWA KUMUUA MAMA YAKE KWA TAMAA YA MALI

Wendy anadaiwa kumuua Mama yake mzazi (Mama Ipepu) ambaye ni Nesi mstaafu wa KCMC

Ni takriban mwaka sasa watu wamekuwa wakimuulizia Mama huyo na kuambiwa amekwenda kutibiwa nje ya Nchi

Soma - https://jamii.app/BintiKifoMama

#JFMatukio
USWISI: WANAJESHI WATAKIWA KUACHA KUTUMIA WHATSAPP, SIGNAL NA TELEGRAM

Kwasababu ya ulinzi wa taarifa, Wanajeshi wametakiwa kutumia Mtandao wa Uswisi uitwao Threema Messenger

Jeshi litagharamia kuwa na Threema ambayo ni Dola 4.35 (Tsh. 8,900)

Soma - https://jamii.app/SwissArmy

#Governance
#KAZAKHSTAN: Jumla ya Watu 164 wameuawa tangu yalipoanza machafuko yaliyotokana na maandamano wiki moja iliyopita

Ktk machafuko hayo, zaidi ya Watu 5,000 wamekamatwa na Mamlaka za Nchi hiyo. Raia wanapinga kupanda kwa bei ya Mafuta

Soma - https://jamii.app/DeathTollKaza
#HumanRights
IKULU, CHAMWINO: Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan awaapisha Mawaziri, Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu aliowateua Januari 8, 2022

Uapisho huo unafanyika Ikulu, Chamwino, Dodoma

Fuatilia - https://jamii.app/UapishoIkuluDodoma

#Governance
NAIBU SPIKA: KAZI YA BUNGE SIO KUKOSOA SERIKALI TU

Dkt. Tulia Ackson asema itakapohitajika watakosoa Serikali kwa heshima na kuzingatia muktadha

Amesema Rais ni Mkuu wa Serikali na ni Mkuu wa Nchi, hayuko sawa na wakuu wa Mihimili mingine

Soma - https://jamii.app/RaisVsBunge

#Governance
RAIS SAMIA: LUKUVI HATOKUWA SPIKA WA BUNGE

Akanusha uvumi William Lukuvi ameandaliwa kuwa Spika wa Bunge baada ya kutoteuliwa katika Baraza la Mawaziri

Pia, amekanusha kuwa Lukuvi ni kati ya watu waliokuwa wanataka kugombea Urais 2025

Soma - https://jamii.app/UapishoIkuluDodoma

#Governance
RAIS SAMIA: NILIWAACHA LUKUVI NA PROF. KABUDI ILI WAJE KWANGU KUWASIMAMIA MAWAZIRI

Amesema amewaacha Wiliam Lukuvi na Prof. Palamagamba Kabudi kwasababu ya umri, hivyo atafanya nao kazi kwa ukaribu ili kuweza kuwasisimamia mawaziri

Soma - https://jamii.app/UapishoIkuluDodoma

#Governance
UTAFITI: GONGO HUSABABISHA SARATANI YA TUMBO

Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani, IARC limebaini gongo, Chang'aa na Kachasu zinasababisha Saratani ya Tumbo hasa kwa wanaume

Saratani hii imeshamiri zaidi Kusini na Mashariki mwa Afrika

Soma https://jamii.app/GongoSaratani

#JFAfya
SOMALIA: Viongozi wa kisiasa wamefikia makubaliano ya kukamilisha Uchaguzi wa Bunge la chini kati ya Januari 15 na Februari 25, 2022

Waziri Mkuu na Rais wamekuwa wakijibizana kuhusu zoezi hilo, hali iliyozua wasiwasi wa ghasia Nchini humo

Soma https://jamii.app/UchaguziSomalia
#Democracy