JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UTUMIKISHAJI WATOTO AFRIKA MAGHARIBI NA KATI WAONGEZEKA

Wanatumiwa kama wapiganaji, wapelelezi, wapishi, walinzi na wabeba mizigo

Watoto 21,000 waliandikishwa na Vikosi vya Kijeshi na makundi yenye silaha kati ya 2016 na 2020

Soma - https://jamii.app/ChildLabourWA

#ChildViolence
SERIKALI: NGUVU YA PAMOJA INAHITAJIKA KUKOMESHA UKATILI WA KIJINSIA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema licha ya Sheria kali bado Ukatili unajitokeza

Asema, "Rushwa ya ngono imekua changamoto Vyuo Vikuu na maeneo ya kazi"

Soma - https://jamii.app/VitendoUkatiliTZ

#16DaysofActivism2021
AFRIKA KUSINI: Serikali imeomba Kampuni za Johnson & Johnson na #Pfizer kuchelewesha utoaji wa Chanjo kutokana na kuwa na Chanjo nyingi kwenye maghala

35% ya Wananchi wameshapata Chanjo kamili huku Nchi ikiwa na dozi Milioni 16.8 ghalani

Soma - https://jamii.app/StockVaccineSA

#UVIKO3
Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu ukiituhumu Demokrasia kukwamisha Maendeleo huku wengine wakidai kuwa ili maendeleo yatokee kunahitajika utawala wa kiimla

Je, wewe una mtazamo gani kuhusu hili?

Ungana nasi katika Mjadala kuanzia saa 12 jioni kupitia Clubhouse

Link - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/3RJTuGde/P08pBBww
Aidan Eyakuze: Demokrasia inaturuhusu sisi kama binadamu wa nchi fulani kujiuliza maswali 2 ya msingi

1. Nani atazalisha yale yote tunayohitaji kama binadamu?

2. Nani atalipia uzalishaji huo?

Fuatilia - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/3RJTuGde/P08pBBww

#JamiiForums #Democracy
Fuatilia Mjadala huu kupitia Clubhouse ya JamiiForums

#Democracy #JamiiForums
Yanayojiri katika Mjadala wa "Je, Demokrasia inakwamisha Maendeleo?" unaoendelea kupitia Clubhouse

#Democracy #JamiiForums
TETESI: MANCHESTER UNITED KUMPA RANGNICK UKOCHA WA MUDA

- Inadaiwa Klabu ya Man. Utd imefikia makubaliano na Kocha Ralf Rangnick (63) ili awe kocha wao wa muda hadi mwisho wa msimu 2021 - 22

- Rangnick amewahi kuwa Kocha wa Hannover, Schalke, Hoffenheim na RB Leipzig

#JFSports
SUDAN: Maelfu ya watu wameandamana Jijini #Khartoum pamoja na Miji mingine. Vikosi vya Usalama vimetumia mabomu ya machozi dhidi ya Waandamanaji huko Omdurman

Wananchi wamepinga Makubaliano yaliyomrejesha Madarakani Waziri Mkuu, Abdalla Hamdok

Soma - https://jamii.app/ProtestsKhartoum
Ili kutatua kasoro zilizoainishwa katika Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, Serikali inashauriwa kuwezesha Halmashauri kukamilisha miradi iliyoanza kabla ya kuanza miradi mipya

Pia, Taasisi ya WAJIBU inashauri Wizara ya Fedha na Mipango (Hazina) pamoja na watekeleza miradi kufuata makubaliano waliojiwekea na Washirika wa Maendeleo

Soma - https://jamii.app/MapungufuMiradi

#JFUwajibikaji
AINA MPYA YA KIRUSI CHA CORONA YAGUNDULIKA AFRIKA KUSINI

Wanasayansi Nchini humo wameelezea wasiwasi wao kuhusu aina mpya ya Kirusi cha Corona kiitwacho B.1.1.529

Wataalamu wa Shirika la Afya Duniani(WHO) wanatarajiwa kukutana kukitathmini

Soma https://jamii.app/NewVariantSA

#UVIKO3
Jamii Forums inatoa nafasi 2 za ajira kwa Wasanifu Grafiki (Graphic Designers)

MAJUKUMU: Kuandaa na kusanifu picha kulingana na mahitaji, Kuandaa na kuhariri picha mjongeo zitakazotumika kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii

Kwa Maelezo zaidi tembelea - https://jamii.app/GraphicDesignersJF
MADHARA YA UKATILI WA KIJINSIA MITANDAONI

Ukatili una madhara Kisaikolojia, na unaweza kupelekea watendewa kupata Msongo wa Mawazo/kupoteza mwelekeo

Pia, inajenga hofu na kuvunja moyo Wanawake kushiriki kwenye ngazi za Uongozi

Soma - https://jamii.app/UkatiliMitandao

#16DaysofActivism
MDAU: MAPENDEKEZO YA HATUA ZA KUCHUKUA KUPUNGUZA WIZI WA FEDHA ZA UMMA

Amesisitizia suala la Uwazi akisema ukiwepo, ni rahisi hata kwa Wananchi kufuatilia na kutoa taarifa mapema pale inapoonekana mradi unafanyika ndivyo sivyo

Anasema TAKUKURU haitakiwi ifanye kazi kwa kupewa maelekezo bali inatakiwa inuse viashiria vya rushwa kila sehemu na ijikite zaidi kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi

Soma Makala yake - https://jamii.app/WiziFedhaUmma

#StoriesOfChange