JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu ukiituhumu Demokrasia kukwamisha Maendeleo huku wengine wakidai kuwa ili maendeleo yatokee kunahitajika utawala wa kiimla

Je, wewe una mtazamo gani kuhusu hili?

Ungana nasi katika Mjadala utakaofanyika Alhamisi Novemba 25, 2021 kuanzia saa 12 jioni kupitia Clubhouse

#JamiiForums #Democracy
SUDAN: MAWAZIRI 12 WAJIUZULU KUPINGA MAKUBALIANO NA JESHI

Wamewasilisha barua za kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Abdalla Hamdok aliyerejeshewa Madaraka siku kadhaa zilizopita

Wanapinga Makubaliano ya Kisiasa kati ya Waziri Mkuu na Baraza la Kijeshi

Soma - https://jamii.app/12MinSudan
RIPOTI: COVID-19 IMEATHIRI ZAIDI WANAWAKE KIUCHUMI NA KIJAMII

Ripoti ya Shirika la Msalaba Mwekundu inasema Wanawake wameathiriwa zaidi na upotevu wa Mapato, kuongezeka ukatili, Ndoa za utotoni na biashara haramu ya usafirishaji binadamu

Soma - https://jamii.app/CoronaWanawake

#UVIKO3
NCHI KADHAA ZATAKA RAIA WAKE KUONDOKA ETHIOPIA

Ufaransa na Ujerumani zimewataka Wananchi wake kuondoka mara moja Nchini #Ethiopia

Marekani na Uingereza nazo zimetoa angalizo hilo kutokana na hali ya usalama kuendelea kudorora

Soma - https://jamii.app/VitaEthiopia

#JFLeo
UNDP: MTOTO HUFARIKI KILA BAADA YA DAKIKA 9 KUTOKANA NA VITA YEMEN

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo(UNDP) lasema 80% ya Wakazi wanahitaji Msaada wa Kibinadamu

Vita ikiendelea watu wapatao Milioni 1.3 watapoteza maisha hadi 2030

Soma - https://jamii.app/UNDPYemen
UHOLANZI: Serikali ya Uholanzi imeanza kupeleka Wagonjwa wa #CoronaVirus Nchini Ujerumani kutibiwa ili kupunguza msongamano unaozizonga Hospitali zake

Idadi ya Wagonjwa imeongezeka sana kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana tangu Mei

Soma - https://jamii.app/CovidRiseNether

#UVIKO3
CHANJO YA COVID-19 NI SALAMA KWA WENYE SARATANI

Wataalamu wa Afya wa Chuo Kikuu cha Texas wanasema Chanjo za #COVID19 ni salama kwa wenye Magonjwa ya Saratani

Daktari anaweza kusaidia kuamua wakati unaofaa kuchanjwa ili kunufaika na Chanjo

Soma - https://jamii.app/ChanjoCancer

#UVIKO3
FAIDA ZA KULA TOFAA KIAFYA

Tofaa/Apple lina Kemikali ambazo husaidia kufyonza sumu hivyo kusaidia katika usafishaji wa Damu, Ini na Ngozi. Matumizi mazuri ya Tofaa huleta unafuu kwa Watu wanaokosa choo

Pia, Ganda la Tofaa linasaidia kushusha kiwango cha Sukari katika Damu kwa wale wenye Kisukari, pamoja na kuondoa Magonjwa yanayosababishwa na kujaa kwa Mafuta Mwilini

Soma - https://jamii.app/FaidaTofaa

#Afya
APPLE YAIFUNGULIA MASHTAKA KAMPUNI INAYOMILIKI PEGASUS

Mashtaka ya Apple dhidi ya NSO yanakuja wakati Kampuni hiyo ikikabiliwa na madai kuwa maelfu ya wanaharakati, Waandishi wa Habari na Wanasiasa walikuwa walengwa wa Programu ya upelelezi

Soma - https://jamii.app/ApplePegasus

#JFLeo
Jamii Forums inatoa nafasi 2 za ajira kwa Wasanifu Grafiki (Graphic Designers)

MAJUKUMU: Kuandaa na kusanifu picha kulingana na mahitaji, Kuandaa na kuhariri picha mjongeo zitakazotumika kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii

Kwa Maelezo zaidi tembelea - https://jamii.app/GraphicDesignersJF
SOMALIA: Waziri Mkuu wa Nchi hiyo, Mohamed Hussein Roble ametangaza Hali ya Dharura kutokana na Ukame mbaya, akiwataka Wananchi na Jumuiya ya Kimataifa kusaidia wahanga

Takriban Raia Milioni 3.5 tayari wanakabiliwa na uhaba wa Chakula

Soma - https://jamii.app/UkameSomali
Kwa mwaka 2019/20, jumla ya Miradi ya Maendeleo 266 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 184 katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa 101 haikukamilika

Ripoti ya CAG ilibaini Miradi ya Maendeleo 76 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 4.4 iliyopangwa kutekelezwa kwenye Halmashauri 6 haikutekelezwa kutokana na kutopokea Fedha

Soma - https://jamii.app/MapungufuMiradi

#JFUwajibikaji
Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali itaendelea kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa fursa za #Elimu

Amefafanua, "Fursa hizo zitajumuisha Wasichana ambao wanapata Ujauzito wakiwa Shule za Msingi na Sekondari. Wanafunzi hao wataruhusiwa kuendelea na Masomo yao katika Mfumo rasmi baada ya kujifungua"

Soma - https://jamii.app/ElimuUjauzito

#JFLeo
Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu ukiituhumu Demokrasia kukwamisha Maendeleo huku wengine wakidai kuwa ili maendeleo yatokee kunahitajika utawala wa kiimla

Je, wewe una mtazamo gani kuhusu hili?

Ungana nasi katika Mjadala utakaofanyika Alhamisi Novemba 25, 2021 kuanzia saa 12 jioni kupitia Clubhouse

#JamiiForums #Democracy
MDAU: MAADILI AMBAYO MTOTO ANATAKIWA KUFUNDISHWA

1. Heshima: Usimfundishe kuheshimu Wazee/Wakubwa tu bali mfundishe kila Mtu anastahili heshima, bila kujali umri au hadhi ya kijamii

2. Uwajibikaji: Mfundishe kuchukua hatua juu ya kila ambacho anatakiwa kukifanya pasipo ulazima wa Mzazi kumwelekeza kila mara

Soma - https://jamii.app/MaadiliWatoto

#Malezi
CHANZO CHA UGONJWA WA FIZI

Kuna mambo kadhaa yanayochangia kupata Ugonjwa wa Fizi. Utando wa Bakteria ambao kwa kawaida hutokea kwenye meno ndicho chanzo kikuu

Usipotolewa, Bakteria husababisha kuvimba kwa Fizi. Hatua hiyo inapoendelea fizi huachana na meno, hivyo utando huo wa Bakteria husambaa na kuingia chini ya Fizi

Soma - https://jamii.app/FiziDamu

#Afya
MDAU: CHANGAMOTO KUBWA KWA VIJANA KUJIAJIRI NI UVUMILIVU NA UZOEFU

Anasema pamoja na kuwepo changamoto lukuki zinazokwamisha Vijana kujiajiri, uvumilivu na uzoefu ndizo za msingi na Vijana wengi wanashindwa kuvumilia machungu ya kujiajiri ambayo yanapatikana mwanzoni tu

Msome - https://jamii.app/VijanaUjasiriamali

#StoriesOfChange
👍1
DALILI TATU HATARISHI ZA COVID-19

WHO wanaeleza dalili hizo ni kupata tabu ya kupumua, kushindwa kuzungumza na maumivu kifuani

Huanza kuonekana Siku 5 - 6 tangu kupata Maambukizi

Ukipata dalili hizi fika haraka Hospitali kupata Matibabu

Soma - https://jamii.app/DaliliHatariUviko

#UVIKO3
LIBYA: TUME YAKATAA MAOMBI YA URAIS YA MTOTO WA GADDAFI

Tume imesema Saif al-Islam Gaddafi aliyezua utata baada ya kutangaza atawania Urais wa Libya anakosa vigezo kwasababu alihukumiwa

ICC ilitoa Hati ya kumkamata kwa tuhuma za uhalifu wa kivita

Soma - https://jamii.app/UraisGaddafi
Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu ukiituhumu Demokrasia kukwamisha Maendeleo huku wengine wakidai kuwa ili maendeleo yatokee kunahitajika utawala wa kiimla

Je, wewe una mtazamo gani kuhusu hili?

Ungana nasi katika Mjadala utakaofanyika kuanzia saa 12 jioni kupitia Clubhouse

Link - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/3RJTuGde/P08pBBww
SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Hii ni Kampeni ya Kimataifa ya kila mwaka inayoanza Novemba 25 na kuhitimishwa Desemba 10

Siku hii inalenga kuhamasisha Raia na Mashirika duniani kote kupaza sauti kuhusu kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana

Soma - https://jamii.app/16DaysActivism

#OrangeTheWorld #16DaysofActivism