JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: RC Amos Makalla ametangaza Jumamosi ya kila mwisho wa Mwezi kutumika kufanya usafi kwa mkakati aliouita ‘Safisha Pendezesha Dar es Salaam’

Katika mkakati huo baadhi ya nyumba za Watu binafsi, Mashirika na Kampuni zimetakiwa kupakwa rangi

Soma - https://jamii.app/UsafiDar
#JFLeo
HOJA: LIPIA TANGAZO MTANDAONI ILI KUPATA WATEJA WANAOHITAJI BIDHAA YAKO

Mdau wa Jamiiforums.com ameandika kuhusu umuhimu wa kulipia matangazo mtandaoni ambapo hufanya bidhaa yako imfikie Mtu mwenye uhitaji nayo badala ya kumfikia Mtu yeyote

Teknolojia ya Mtandao kama #Facebook kwa matangazo yanayolipiwa huyafanya yawafikie Watu ambao walishawahi kutafuta bidhaa unayoitangaza hivyo utapata Watu wenye uhitaji na kuuza

Soma - https://jamii.app/SponsoredAds
#SponsoredAds
SERIKALI: UKIJENGA KWENYE MAENEO HATARISHI TUTABOMOA

Waziri wa Ardhi, William Lukuvi ametangaza kuvunja Nyumba zilizo maeneo hatarishi na mabondeni hata kama wamiliki wana Hati

Asema walio maeneo hatarishi mara nyingi hupewa Hati kijanja janja

Soma - https://jamii.app/NyumbaKubomolewa
MAREKANI YATAJWA KUPOROMOKA KIDEMOKRASIA

Ripoti ya Taasisi ya Kimataifa ya Demokrasia na Usaidizi wa Uchaguzi(#IDEA) imeitaja Marekani kurudi nyuma Kidemokrasia tangu 2019

Mtu 1 kati ya Watu 4 Duniani anaishi ktk Taifa linalorudi nyuma Kidemokrasia

Soma https://jamii.app/DemocracyUS
#ETHIOPIA: Wakati vita ya mwaka mzima kati ya Serikali ya Ethiopia na Vikosi vya TPLF ikikaribia Addis Ababa, Waziri Mkuu Abiy Ahmed asema ataongoza Vikosi vya Usalama

Wajumbe wamejaribu kusuluhisha mvutano lakini kumekuwa na maendeleo kidogo

Soma https://jamii.app/AbiyEthiopia
#JFLeo
SONGWE: Watu 24 wa Kijiji cha Chang’ombe wanashikiliwa kwa tuhuma za kuzingira Kituo cha Polisi Galula wakidai mikoba ya Waganga wa Jadi iliyokamatwa na Askari

Waganga maarufu lambalamba wanadaiwa kuwadhalilisha Watu wakiwatuhumu ni wachawi

Soma - https://jamii.app/24Songwe

#JFLeo
Jamii Forums inatoa nafasi 2 za ajira kwa Wasanifu Grafiki (Graphic Designers)

MAJUKUMU: Kuandaa na kusanifu picha kulingana na mahitaji, Kuandaa na kuhariri picha mjongeo zitakazotumika kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii

Kwa Maelezo zaidi tembelea - https://jamii.app/GraphicDesignersJF
Ripoti ya CAG 2019/20 ilibaini zaidi ya Miradi ya Maendeleo 68 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 18.3 ilikuwa imekamilika lakini haitumiki. Miradi hii ilitekelezwa kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa 40

Ilihusisha Miradi ya Ujenzi wa Masoko, Ujenzi wa Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati, Ujenzi wa Miundombinu ya Shule (nyumba za Walimu, Vyoo na Madarasa) na ujenzi wa maeneo ya machinjio

Soma - https://jamii.app/MapungufuMiradi

#JFUwajibikaji
FAHAMU TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU KWENYE FIZI (1)

Mara nyingi kuvimba au kutokwa Damu kwenye Fizi huweza kusababishwa na magonjwa mbalimbali ya Kinywa na Meno ambayo husababishwa na kutofanya usafi wa Kinywa kwa usahihi au maambukizi ya Bakteria ambao husababisha utando mgumu kwenye Meno

Ugonjwa wa Fizi ni hatari kwa kuwa hautambuliki mapema

Soma - https://jamii.app/FiziDamu

#Afya
Rais Samia asema bado Askari wanalalamikiwa kwa masuala kadhaa ikiwemo kushikilia Leseni za Madereva kwa muda mrefu au kuwalazimisha kulipa faini papo hapo

Pia, amesema kuna ukamataji mwingi wa Vyombo, na Pikipiki nyingi zimepangwa Vituo vya Polisi

Soma https://jamii.app/KeroAskari
RAIS SAMIA: VIJANA WAHANGA WAKUBWA WA AJALI ZA BARABARANI

Amesema takwimu zinaonesha zaidi ya 90% ya Ajali za Barabarani husababishwa na makosa ya kibinadamu ikiwemo mwendokasi, kutovaa mikanda na kupita gari lingine bila tahadhari

Soma - https://jamii.app/VijanaAjali

#JFLeo
TANESCO: TAASISI ZA SERIKALI NI CHANGAMOTO KWA KUTOLIPA BILI ZA UMEME

Changamoto nyingine ni Watu kutumia vyanzo vingine vya Nishati kwa kuwa TANESCO haina uthabiti wa huduma

Pia, Uharibifu wa miundombinu, gharama na ushindani wa matumizi ya Maji

Soma - https://jamii.app/ChangamotoTANESCO
TANZANIA YAPOKEA DOZI 499,590 ZA #PFIZER

Waziri kwa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima amesema Tanzania imepokea Dozi 499,590 za Chanjo hiyo dhidi ya #COVID19

Asema kufikia Novemba 19 takwimu zinaonesha Wananchi 1,359,624 wamefikiwa na Chanjo

Soma - https://jamii.app/PfizerTanzania

#UVIKO3
UGANDA: WATU 7 WAUAWA NA 106 WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA UGAIDI

Zaidi ya mara moja #Uganda imepata mashambulizi ya mabomu ikiwa Miezi kadhaa baada ya Uingereza kutoa tahadhari kwa Nchi hiyo

Shambulio la Novemba 6 lilisababisha Vifo vya Watu 7

Soma - https://jamii.app/UgandaUgaidi

#JFLeo
MDAU ASHAURI NAMNA YA KUPAMBANA NA TATIZO LA USAFIRI KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SERIKALI

Shule za Serikali hazina Magari hivyo huwapa shida Wanafunzi kwa kuwa Daladala hazipendi kubeba Wanafunzi kutokana na udogo wa nauli zao

Mshiriki wa 'Stories Of Change' ameshauri Serikali kuweka bajeti ya kuwa na Mabasi ya kubeba Wanafunzi, au kuwalipia kwa kuweka mfumo wa Wanafunzi kuweka Kidole wakipanda Daladala

Soma - https://jamii.app/WanafunziUsafiri

#StoriesOfChange
Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu ukiituhumu Demokrasia kukwamisha Maendeleo huku wengine wakidai kuwa ili maendeleo yatokee kunahitajika utawala wa kiimla

Je, wewe una mtazamo gani kuhusu hili?

Ungana nasi katika Mjadala utakaofanyika Alhamisi Novemba 25, 2021 kuanzia saa 12 jioni kupitia Clubhouse

#JamiiForums #Democracy
SUDAN: MAWAZIRI 12 WAJIUZULU KUPINGA MAKUBALIANO NA JESHI

Wamewasilisha barua za kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Abdalla Hamdok aliyerejeshewa Madaraka siku kadhaa zilizopita

Wanapinga Makubaliano ya Kisiasa kati ya Waziri Mkuu na Baraza la Kijeshi

Soma - https://jamii.app/12MinSudan
RIPOTI: COVID-19 IMEATHIRI ZAIDI WANAWAKE KIUCHUMI NA KIJAMII

Ripoti ya Shirika la Msalaba Mwekundu inasema Wanawake wameathiriwa zaidi na upotevu wa Mapato, kuongezeka ukatili, Ndoa za utotoni na biashara haramu ya usafirishaji binadamu

Soma - https://jamii.app/CoronaWanawake

#UVIKO3
NCHI KADHAA ZATAKA RAIA WAKE KUONDOKA ETHIOPIA

Ufaransa na Ujerumani zimewataka Wananchi wake kuondoka mara moja Nchini #Ethiopia

Marekani na Uingereza nazo zimetoa angalizo hilo kutokana na hali ya usalama kuendelea kudorora

Soma - https://jamii.app/VitaEthiopia

#JFLeo
UNDP: MTOTO HUFARIKI KILA BAADA YA DAKIKA 9 KUTOKANA NA VITA YEMEN

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo(UNDP) lasema 80% ya Wakazi wanahitaji Msaada wa Kibinadamu

Vita ikiendelea watu wapatao Milioni 1.3 watapoteza maisha hadi 2030

Soma - https://jamii.app/UNDPYemen
UHOLANZI: Serikali ya Uholanzi imeanza kupeleka Wagonjwa wa #CoronaVirus Nchini Ujerumani kutibiwa ili kupunguza msongamano unaozizonga Hospitali zake

Idadi ya Wagonjwa imeongezeka sana kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana tangu Mei

Soma - https://jamii.app/CovidRiseNether

#UVIKO3