JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
COVID-19 HAISAMBAZWI NA TEKNOLOJIA YA 5G

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Virusi vya Corona haviwezi kusambaa kupitia mawimbi ya redio au simu

Tayari #CoronaVirus imeenea katika Nchi nyingi ambazo hazina mitandao ya simu ya 5G

Soma - https://jamii.app/Corona5G

#UVIKO3
SUDAN: Mamlaka zimerejesha Huduma ya Intaneti takriban Mwezi mmoja tangu isitishwe baada ya Jeshi kuondoa Madarakani Serikali ya Mpito

Mahakama iliamuru Kampuni za Mawasiliano kurejesha intaneti tangu Novemba 09, lakini tatizo liliendelea

Soma - https://jamii.app/InternetSudan
MDAU: MBINU ZA MALEZI YA MTOTO NI MUHIMU ZIENDANE NA HATUA ZA UKUAJI WAKE

Mbinu za Malezi zinazoleta matokeo mazuri kwa Mtoto wa miaka 7 zinaweza zisiwe na matokeo mazuri kwa Mtoto mwenye miaka 13

Kuna umri Mtoto akifikia huwa na kawaida ya kuuliza 'kwanini' kwa kila jambo unalomwambia. Hali hii ni ya kawaida lakini usipoelewa unaweza kuhisi Mtoto ameanza Dharau

Soma - https://jamii.app/MbinuMaleziUmri
#ParentingTips
Katika usimamizi wa mali za Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Ripoti ya CAG 2019/20 imeeleza kuwa Mali za kudumu zenye thamani ya Tsh. Bilioni 1.92 zilizonunuliwa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa 10 hazitumiki

Mapungufu haya yanaweza kupelekea upotevu wa mali za Halmashauri na kukosekana thamani ya Fedha

Soma - https://jamii.app/MapungufuMali

#JFUwajibikaji
Siku ya Kimataifa ya Wanaume huadhimishwa kila Novemba 19, ikiwa ni fursa ya kuwasherehekea Wanaume. Siku hii inalenga kuwathamini Wanaume wote pamoja na Mchango wao katika Familia na Jamii kwa ujumla

Mwaka huu, Kaulimbiu ya Siku ya Wanaume inasema "Uhusiano bora kati ya Wanawake na Wanaume kwa lengo la kuimarisha Usawa wa Kijinsia na kutengeneza Dunia iliyo salama"

#JamiiForums #InternationalMensDay #MensDay
Mwaka 2019/20, CAG alifanya Ukaguzi wa utekelezaji wa mapendekezo katika ripoti 5 zilizotolewa Aprili 2016. Ripoti zilikuwa na mapendekezo 63 kwa Taasisi 4 zinazosimamia utafutaji na uendelezaji wa Mafuta na Gesi Asilia

Kati ya mapendekezo 63, ni mapendekezo 9 (14%) ndiyo yaliyotekelezwa kikamilifu. Mapendekezo 38 (60%) yako kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji, mapendekezo 13 (24%) hayajatekelezwa kabisa

Soma - https://jamii.app/MapendekezoCAG

#JFUwajibikaji
MDAU: KWA RASILIMALI ZILIZOPO TANZANIA, TUNASTAHILI MAENDELEO TULIYONAYO?

Anasema Maendeleo tuliyonayo tangu Uhuru hayaendani na Rasilimali zilizopo, vilevile hayaendani na kasi ya mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia

Ametaja sababu mojawapo inayopelekea kusuasua kwa Maendeleo ni kukosa Mfumo madhubuti wa Uongozi, akisema Nchi ilitakiwa iwe na misimamo yake na matakwa ya Ilani za Vyama yawe kama Mapendekezo

Soma Makala yake - https://jamii.app/MaendeleoTZ

#StoriesOfChange
MAMILIONI WAKABILIWA NA UHABA WA CHAKULA NCHINI SOMALIA

Zaidi ya watu Milioni 2 wanakabiliwa na uhaba wa Chakula na Maji kutokana na hali mbaya ya ukame

Umoja wa Mataifa (UN) wasema takriban watu 100,000 wamekimbia makazi yao kutafuta Chakula

Soma - https://jamii.app/ChakulaMajiSomalia
MDAU: NI MUHIMU KUAJIRIWA/KUJITOLEA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA YAKO

Dawa ya kuondokana na tatizo la Ajira ni kujiajiri wenyewe, lakini kabla ya kujiajiri jambo muhimu tunapaswa kulifahamu vizuri ni Sekta Binafsi ilivyo na Idara gani ungependa kujiajiri

Mshiriki wa 'Stories Of Change' anasema Kampuni nyingi binafsi zina programu maalumu za kujitolea. Hii itakusaidia kujifunza jinsi Taasisi zinavyoundwa, kuajiri Watu na kuwasimamia na kutengeneza mahusiano ya kudumu kati ya Mteja na #Biashara.

Soma - https://jamii.app/FaidaKujitolea
CHINA: Umoja wa Mataifa umetoa rai kwa China kumwachia huru Zhang Zhan ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 4 baada ya kuhoji namna Mamlaka zinavyoshughulikia #COVID19

Familia na Ripoti kadhaa zimedai anakaribia kifo kutokana na mgomo wa kula

Soma - https://jamii.app/UNZhangChina
#AUSTRIA: Kansela Alexander Schallenberg amesema hatua ya kufungwa kwa shughuli za Umma itaanza kutekelezwa Jumatatu ili kudhibiti Maambukizi

Ulazima wa kumtaka kila Mtu kupata Chanjo dhidi ya Virusi vya Corona utaanza Februari mosi

Soma - https://jamii.app/LockdownAustria
#UVIKO3
ZANZIBAR: Rais Samia Suluhu Hassan asema Maendeleo ya Nchi huletwa na Wananchi wake. Amesema Sheria za Tanzania Bara na Zanzibar zimetoa Uhuru (usiovunja Sheria) kwa watu kufanya kazi

Ameeleza, "Ninaamini Tanzania bila Rushwa inawezekana"

Soma - https://jamii.app/RaisSamiaZnz

#JFLeo
MDAU: VICOBA VINAWATESA WANAWAKE NA KULETA MIGOGORO YA KIFAMILIA

VICOBA ni utaratibu wa kuweka na kukopa kwa Watu waliojiunga kwa pamoja na kuunda kikundi kwa malengo ya kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo

Mshiriki wa 'Stories Of Change' anasema Wanawake wengi wamekuwa wakijifunga kwenye mikopo ya VICOBA kwa kuchukua Fedha nje na malengo. Huishia kupoteza vitu, Ndoa na wengine kufikishwa Polisi kutokana na MAREJESHO.

Soma zaidi - https://jamii.app/MatesoVicobaMke
#StoriesOfChange
SERIKALI YAPIGA MARUFUKU DAWA ZA KUULIA WADUDU KUPULIZWA BUCHANI

Bodi wa Nyama Nchini imesema Dawa hizo ni sumu zinazofanya kazi taratibu ndani ya mwili wa Binadamu na husababisha maradhi ikiwemo Saratani

Wenye Bucha wametakiwa kuzingatia Usafi kuzuia Nzi

Soma - https://jamii.app/BanDawaBuchani
Siku ya Watoto Duniani huadhimishwa tarehe 20 Novemba kila mwaka. Pamoja na kuboresha hali zao za Maisha, Siku hii pia inalenga kuimarisha Haki zao

Watoto na Vijana wamekuwa wakipaza sauti kwenye masuala yanayowagusa, na ni muhimu kwa Viongozi kusikiliza mawazo na matakwa yao

#JamiiForums #WorldChildrensDay
TETESI: MANCHESTER IMEAMUA KUMFUTA KAZI SOLSKJAER

- Inadaiwa kuwa Bodi ya timu ya Man. Utd, imeamua kumfukuza kazi Kocha Ole Gunnar Solskjaer

- Fletcher/Carrick ataiongoza timu hiyo kama Kocha wa muda iwapo Kocha wa kumrithi Solskjaer hatapatikana hivi karibuni

#JFSports
SUDAN: Wanaharakati wanaopinga Mapinduzi Nchini #Sudan wameitisha Maandamano leo Jumapili, wakati idadi ya Watu waliouawa ikifikia 40

Marekani na AU zimelaani ukandamizaji na kuwataka Viongozi wa Sudan kuacha matumizi ya nguvu

Soma - https://jamii.app/ActivistRiotsSudan

#Democracy
RASMI: MAN. UTD YAMFUKUZA SOLSKJAER

Baada ya Mkutano wa dharura wa Bodi ya timu hiyo kukaa jana kutokana na mlolongo wa matokeo mabovu, klabu imeachana na Ole Gunnar Solskjaer

Solskjaer alichaguliwa kuinoa timu hiyo Desemba 2018 baada ya Jose Mourinho kufutwa kazi

#JFSports
UGANDA: Rais Yoweri Museveni amewataka Waasi wa Kundi la ADF wanaoshutumiwa kuhusika na milipuko ya hivi karibuni kujisalimisha

Amesema Jeshi limewahi kupambana na kuwashinda Waasi hao kabla, hivyo wajitokeze au wote watauawa

Soma - https://jamii.app/MuseveniADF

#JFLeo
SUDAN: Baada ya wiki kadhaa za maandamano, Jeshi limemrejeshea Madaraka Waziri Mkuu wa Nchi hiyo, Abdalla Hamdok na kutangaza kuwaachia huru Wafungwa wote wa kisiasa

Hamdok amesema amekubali ili kuzuia umwagaji damu zaidi Nchini humo

Soma - https://jamii.app/JeshiWaziriMkuu

#JFLeo
KENYA: Serikali imesema kuanzia Desemba 21, anayehitaji huduma za Serikali za ana kwa ana lazima awe amepata chanjo kikamilifu

Baa, migahawa na biashara zinazohudumia watu zaidi ya 50 kwa siku zimeelekezwa kuomba uthibitisho wa Chanjo

Soma - https://jamii.app/ProofVaccineKE

#UVIKO3