JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
HOJA: Mshiriki wa #StoriesOfChange amesema ndoa ni muungano wa mume na mke hivyo jukumu la kutunza ndoa ni la wote

Mdau amekosoa sherehe za 'Kitchen Party' ambazo humuandaa mwanamke kwa ndoa huku mwanaume akiwa hana sherehe inayomuandaa na maisha hayo

Je, kuna mafunzo gani anayopatiwa Mwanaume kabla ya kuingia kwenye ndoa?

Soma https://jamii.app/MfumoDumeNdoa
Ripoti ya Uwajibikaji kutoka WAJIBU inasema Masoko ya Chakula Nchini yamekuwa ktk hali ya uchakavu na uchafu hivyo kuhatarisha #Afya za Watumiaji wa huduma za Masoko hayo

Halmashauri 8 zilishindwa kutenga 15% ya kiasi cha Fedha kinachokusanywa kama Mapato ktk Masoko ili kugharamia Usafi wa Masoko hayo

Soma - https://jamii.app/UchafuMasoko
#JFUwajibikaji
MFAHAMISHE DAKTARI KUHUSU 'ALLERGY' KABLA YA KUPATA CHANJO

WHO inashauri wenye historia ya mzio wa chanjo (Allergic reaction) kuwaeleza Wataalamu kabla ya kupata Chanjo ya #COVID19

Hii itasaidia kukupa mwongozo sahihi kabla ya kuchanjwa

Soma - https://jamii.app/ChanjoMzio

#UVIKO3
DAR: GUGAI NA WENZAKE WAACHIWA HURU

Aliyekuwa Mhasibu wa TAKUKURU, Godfrey Gugai na wenzake wawili wameachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kushindwa kuthibitisha Mashtaka yanayowakabili

Walikuwa wanakabiliwa na makosa 40

Soma https://jamii.app/GugaiWenzake
#JFLeo
KIGOMA: MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMPIGA HADI KIFO MTOTO ALIYEKATAA KUOLEWA

Mbaru Juakali (17) amepigwa na fimbo sehemu mbalimbali mwilini akilazimishwa kuolewa kwa mahari ya Ng'ombe 13

Baba mzazi na ndugu zake wawili wanashikiliwa na Polisi

Soma - https://jamii.app/KIgomaNdoa
#JFLeo
Utoaji wa Chanjo ya #COVID19 umekuwa ukihamasishwa kona zote za Dunia huku baadhi ya Nchi zikichukua hatua za kuweka Vikwazo kwa Watu ambao hawajapata Chanjo kurudi Maofisini, kusafiri au kushiriki shughuli za kijamii

Wasiochanja wana sababu mbalimbali ambazo zinawapelekea kusitasita katika kufanya Maamuzi.

Ungana na Jamii Forums katika Mjadala na wasiochanja utakaofanyika leo, Novemba 12, 2021 kupitia Clubhouse

#JamiiForums #UVIKO3
Yanayojiri katika Mjadala na ambao bado hawajapata Chanjo ya #COVID19 unaoendelea Clubhouse

#JamiiForums #UVIKO3 #CoronaVirus
MDAU: BODABODA ZITASABABISHA WATOTO WENGI KUWA NA MATATIZO YA KIFUA

Mshiriki wa #StoriesOfChange anasema baadhi ya Wazazi huruhusu Watoto kupelekwa Shule kwa pikipiki, na baadhi ya Madereva huwaweka watoto mbele

Anashauri kujali usalama wa Mtoto na si kuwahi Shule

Soma - https://jamii.app/BodabodaWatoto
#SUDAN: Jenerali aliyeongoza Mapinduzi ya Kijeshi hivi karibuni, Abdel Fattah al-Burhan amejiteua kuongoza Baraza Tawala la Mpito

Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo ambaye ni Mshirika wake wa karibu ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais

Soma - https://jamii.app/AjiteuaSudan

#Democracy #JFLeo
NI KWELI AJIRA INA UNAFUU NA UHAKIKA ZAIDI KULIKO KUJIAJIRI?

Mdau wa JamiiForums.com anasema Kuponda kuwa Ajira ni Utumwa ni sawa na "sizitaki mbichi hizi" kwasababu Ajira hazipo nyingi, na zikitangazwa hata waliojiajiri wanazishambulia pia

Anasema #Biashara ni nzuri ikiwa kuna Mfumo wa kupigana jeki na kubebana. Mfano Mzazi akifariki kuwe na Mtoto kaandaliwa kuendeleza

Una maoni gani kuhusu hoja hii?

Mjadala - https://jamii.app/UhakikaAjira
#JFLeo