JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
CHANJO ZA COVID-19 HAZIATHIRI 'DNA'

UNICEF imesema chanjo haziathiri au kuingiliana na 'DNA'

Chanjo hufunza Seli jinsi ya kutengeneza Protini ambayo huchochea mwitikio wa Kinga ndani ya mwili ili kuulinda dhidi ya Virusi

Soma - https://jamii.app/ChanjoDNA

#COVID19 #UVIKO3
BUNGENI: Rais Samia Suluhu Hassan awasilisha Muswada wa Hati ya Dharura kuhusu Mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ya Tozo ya Kodi ya Mazao akitaka iondolewe

Sheria inaruhusu Mamlaka ya Mapato (TRA) kutoza ushuru wa bidhaa wa 2% kwa Mazao

Soma - https://jamii.app/HatiSamiaBunge
SUDAN: MAHAKAMA YAAMURU HUDUMA ZA INTANETI KUREJESHWA

Huduma hizo zilikatwa wakati wa Mapinduzi ya Kijeshi zaidi ya wiki mbili zilizopita

> Kesi ilifunguliwa na Kundi la Wanasheria na Jumuiya ya Ulinzi wa Wateja wa Sudan

Soma - https://jamii.app/IntanetiSudan
#HumanRights
Tanzania imekuwa ikipokea misaada kutoka nje ya nchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kumekuwa na hoja kuwa misaada tajwa haileti tija stahiki kwa umma ikilinganishwa na malengo. Je, ni kweli? Nini kifanyike kuleta tija?

Ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika kupitia Clubhouse ya JamiiForums

#JamiiForums #JFUwajibikaji
AFYA: Utafiti uliofanywa na Watanzania na kuchapishwa ktk Jarida la BMC Neurology la Uingereza umebaini wanaougua Shinikizo la Damu muda mrefu wapo hatarini kupoteza kumbukumbu na uwezo wa kufikiri

Utafiti ulitumia dodoso lililowahoji wagonjwa 1,201

Soma https://jamii.app/ShinikizoLaDamu
IFAHAMU CHANJO AINA YA #MODERNA

imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa ni salama kukinga #CoronaVirus kwa Watu wenye miaka 18 na zaidi

Inatolewa kwa Dozi mbili ambapo Dozi ya pili hutolewa siku 28 baada ya Dozi ya kwanza

Soma - https://jamii.app/FahamuChanjo

#UVIKO3
Tanzania imekuwa ikipokea misaada kutoka nje ya nchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kumekuwa na hoja kuwa misaada tajwa haileti tija stahiki kwa umma ikilinganishwa na malengo. Je, ni kweli? Nini kifanyike kuleta tija?

Ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika kupitia Clubhouse ya JamiiForums

#JamiiForums #JFUwajibikaji
Fuatilia Mjadala wa "Nini kifanyike ili Nchi ipate tija stahiki kutokana na Misaada inayotoka nje ya nchi?" unaoendelea hivi sasa kupitia Clubhouse

Link - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/LYWyFrn2/PQDz7y5w

#JFUwajibikaji
Yanayojiri katika Mjadala unaoendelea hivi sasa kupitia Clubhouse

Ungana nasi - https://www.clubhouse.com/room/PG4vRR0p

#JFUwajibikaji
Baadhi ya yaliyozungumzwa katika Mjadala wa "Nini kifanyike ili Nchi ipate tija stahiki kutokana na Misaada inayotoka nje ya nchi?" uliofanyika kupitia Clubhouse

#JFUwajibikaji #WAJIBU #JamiiForums
Mapungufu yaliyobainishwa katika utekelezaji wa Miradi kwa utaratibu wa 'Force Account' yamepelekea kuwepo kwa viashiria vya rushwa na udanganyifu katika mchakato wa ununuzi wa Umma

Pia, Kuwepo kwa upotevu wa Fedha za Umma na kukosekana kwa thamani ya fedha katika miradi iliyotekelezwa. Mfano; Majengo kupata nyufa muda mfupi baada ya kukamilika

Soma - https://jamii.app/AthariForceAcc
#JFUwajibikaji
ZANZIBAR: Waziri wa Nchi, Uchumi na Uwekezaji, Mudrick Soraga amesema watakutana na Wadau ili kujua kama kuna haja ya kutumia Fedha za Mtandao (Cryptocurrency) kwenye miamala

> Wadau hao ni Wizara ya Fedha, Benki Kuu pamoja na Benki nyinginezo

Soma https://jamii.app/CryptocurrencyZnz
👍1
CHANJO ZENYE 'VIRUSI HAI' HAZISABABISHI CORONA

Kituo cha CDC kimesema chanjo zenye 'Virusi Hai' hazisababishi mtu kupata #COVID19

Chanjo hizi hutumia virusi visivyo na madhara kuchochea mfumo wa kinga kupambana na unachodhani ni maambukizi

Soma https://jamii.app/LiveVaccine
#UVIKO3
MICHEZO: Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo itavaana na DR Congo katika Mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia hatua ya Makundi. Katika Mchezo wa awali, timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao moja kwa moja Nchini Congo

Mechi hiyo itapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Saa 10 jioni. Taifa Stars inaongoza Kundi J ikiwa na point saba katika michuano hiyo ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2022

#JamiiForums #Sports #Michezo