JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KESI YA MBOWE: PINGAMIZI LA HATI YA UKAMATAJI MALI ZA WASHTAKIWA LATUPILIWA MBALI

Jaji Joachim Tiganga ametupilia mbali pingamizi lililowekwa na Upande wa Utetezi wakipinga Mahakama kupokea Hati ya Ukamataji Mali za washtakiwa 2 ktk kesi hiyo

Soma https://jamii.app/PingamiziMali
'PLATFORM' YA SIASA AFRIKA SIO CHAGUO SAHIHI LA MAENDELEO KWA VIJANA

Mshiriki wa Shindano la 'Stories of Change' anasema kuna mifano mingi ya Wanasiasa Vijana ambao baada ya kuondoka kwenye Mfumo walipoteza Mali na kuanza kuhangaika

Anasema Vijana wa Kiafrika wakiwekeza nguvu kubwa katika Sekta ya #Biashara na Ujasiriamali wana nafasi kubwa sana ya kufanikiwa kwasababu ni rahisi kukutana na 'connection' kwa Watu mbalimbali.

Msome - https://jamii.app/SiasaVijana
#JamiiForums
JE, WAJUA: Kutafuna 'Big G' (Bubble Gum) huongeza Umakini kwenye kazi, huongeza Mtiririko wa Damu kwenye Ubongo na kusaidia kuboresha kumbukumbu

Tafiti zinaonesha Kutafuna 'Big G' mara mbili kwa siku kwa muda wa Wiki mbili huweza kusaidia kupunguza Wasiwasi, Msongo wa Mawazo, Uchovu, na Magonjwa mengine ya Akili

Soma - https://jamii.app/FaidaBigG
#Afya
RAIS CHAKWERA: WANANCHI WAWAJIBIKE KWENYE MAENDELEO YA TAIFA, WAACHE KULALAMIKIA WANASIASA

Rais wa #Malawi amesema anapokea SMS nyingi kwenye Simu yake kutoka kwa Watu wanaomtaka awasaidie kulea Familia kwasababu tu yeye ni Rais

Ameongeza "Lazima tujitibu na tabia hii ya kuomba kutoka kwa Wanasiasa. Nchi yetu kamwe haiwezi kuendelea kwa tabia hiyo"

Soma - https://jamii.app/ChakweraMalalamiko
CHANJO ZA COVID-19 HAZIATHIRI UCHANGIAJI WA DAMU

Wataalamu wa Afya wanasema kuchanja dhidi ya #CoronaVirus hakukuzuii kuchangia au kuchangiwa damu

Chanjo inajenga kinga mwili lakini mchanganyo wa dawa haubaki kwenye damu

Soma - https://jamii.app/ChanjoDamu

#UVIKO3
TANGA: Polisi wasema wamebaini kiwanda bubu kimoja cha bunduki kilichokuwa msituni na wamemkamata mtu mmoja anayetuhumiwa kuhusika nacho

Vitu vinavyodaiwa kukutwa kiwandani hapo ni pamoja na vifaa vya kutengenezea silaha na magobore 11

Soma https://jamii.app/KiwandaBubu

#JFLeo
TMA: KUSOGEA JUA LA UTOSI CHANZO CHA JOTO KUONGEZEKA

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) yasema joto kali litaendelea Novemba na kupungua kidogo ifikapo Disemba

Joto Mkoani Kilimanjaro limeripotiwa kuongezeka kwa nyuzi joto 4.6 na kufikia 36.4

Soma - https://jamii.app/JotoOngezeko
UDHAIFU WA MFUMO WA MANUNUZI WA KIELETRONIKI (TANePS)

Ukaguzi wa CAG ulibaini mfumo wa TANePS hauna uwezo wa kutoa taarifa kuhusu jumla ya Taasisi zinazofanya manunuzi Nchini

Aidha, Mfumo haujaunganishwa na Mifumo mingine ya Serikali. Pia, Muuzaji wa Mfumo hakuiwezesha Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuifikia Seva na Kanzi-data ya TANePS

Soma - https://jamii.app/UdhaifuTANeps
#JFUwajibikaji
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuondoka kesho, Novemba 10 kuelekea #Cairo - Misri kwa Ziara ya Kiserikali ya Siku tatu

Akiwa huko, atashuhudia utiaji saini wa mkataba mmoja na hati saba (7) za makubaliano kati ya Tanzania na Misri.

Soma - https://jamii.app/SamiaCairo
#JFLeo
MBEYA: Mkuu wa Mkoa, Juma Homera amesema Watendaji wa Vijiji na Kata walioshindwa kufikia kiwango cha ukusanyaji Mapato ya Ndani kilichowekwa wametakiwa kupangiwa kazi nyingine

> Asema hatua hiyo itaongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato

Soma https://jamii.app/MapatoWatendaji

#JFLeo
Tanzania imekuwa ikipokea misaada kutoka nje ya nchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kumekuwa na hoja kuwa misaada tajwa haileti tija stahiki kwa umma ikilinganishwa na malengo. Je, ni kweli? Nini kifanyike kuleta tija?

Ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika kupitia Clubhouse ya JamiiForums

#JamiiForums #JFUwajibikaji
Mapendekezo ya CAG yameendelea kuongezeka kuanzia Mwaka wa Fedha 2018/19 huku utekelezaji wa mapendekezo ukiendelea kushuka

Taasisi ya WAJIBU imesema kutofanyia kazi mapendekezo kunaondoa ufanisi na kupelekea upotevu wa Fedha za Umma

Soma https://jamii.app/MapendekezoYaCAG

#JFUwajibikaji
Watu wenye Ulemavu mara nyingi ni miongoni mwa Watu Masikini zaidi na waliotengwa katika jamii. Ulemavu huleta athari kubwa kwenye Afya, Ajira na Elimu

Kiwango cha kutokujua Kusoma na Kuandika miongoni mwa Watanzania wenye Ulemavu ni kikubwa na hii inazuia sana Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi.

#JamiiForums #FUWAVITA #Disabilities #JFPartnership
HOJA: Mshiriki wa #StoriesOfChange anasema Taasisi za Umma zinatoa Huduma duni ikilinganishwa na Taasisi Binafsi

Ashauri Serikali kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza maslahi ya Watumishi

Watumishi wazembe wawajibishwe badala kuhamishwa Vituo

Soma - https://jamii.app/TaasisiUmma
CHANJO ZA COVID-19 HAZIATHIRI 'DNA'

UNICEF imesema chanjo haziathiri au kuingiliana na 'DNA'

Chanjo hufunza Seli jinsi ya kutengeneza Protini ambayo huchochea mwitikio wa Kinga ndani ya mwili ili kuulinda dhidi ya Virusi

Soma - https://jamii.app/ChanjoDNA

#COVID19 #UVIKO3
BUNGENI: Rais Samia Suluhu Hassan awasilisha Muswada wa Hati ya Dharura kuhusu Mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ya Tozo ya Kodi ya Mazao akitaka iondolewe

Sheria inaruhusu Mamlaka ya Mapato (TRA) kutoza ushuru wa bidhaa wa 2% kwa Mazao

Soma - https://jamii.app/HatiSamiaBunge
SUDAN: MAHAKAMA YAAMURU HUDUMA ZA INTANETI KUREJESHWA

Huduma hizo zilikatwa wakati wa Mapinduzi ya Kijeshi zaidi ya wiki mbili zilizopita

> Kesi ilifunguliwa na Kundi la Wanasheria na Jumuiya ya Ulinzi wa Wateja wa Sudan

Soma - https://jamii.app/IntanetiSudan
#HumanRights
Tanzania imekuwa ikipokea misaada kutoka nje ya nchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kumekuwa na hoja kuwa misaada tajwa haileti tija stahiki kwa umma ikilinganishwa na malengo. Je, ni kweli? Nini kifanyike kuleta tija?

Ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika kupitia Clubhouse ya JamiiForums

#JamiiForums #JFUwajibikaji
AFYA: Utafiti uliofanywa na Watanzania na kuchapishwa ktk Jarida la BMC Neurology la Uingereza umebaini wanaougua Shinikizo la Damu muda mrefu wapo hatarini kupoteza kumbukumbu na uwezo wa kufikiri

Utafiti ulitumia dodoso lililowahoji wagonjwa 1,201

Soma https://jamii.app/ShinikizoLaDamu
IFAHAMU CHANJO AINA YA #MODERNA

imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa ni salama kukinga #CoronaVirus kwa Watu wenye miaka 18 na zaidi

Inatolewa kwa Dozi mbili ambapo Dozi ya pili hutolewa siku 28 baada ya Dozi ya kwanza

Soma - https://jamii.app/FahamuChanjo

#UVIKO3