JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UTEUZI: RAIS SAMIA ATEUA WASAIDIZI WA OFISI YA RAIS, IKULU

> Said Ali Juma anakuwa Mnikulu

> Dkt. Blandina Kilama anakuwa Mshauri wa Rais, Uchumi

> Dkt. Salim Othman, Msaidizi wa Rais - Siasa

Zaidi, soma https://jamii.app/UteuziApril16
URUSI YAWAFUKUZA WANADIPLOMASIA 10 WA MAREKANI

- Ni katika hatua ya kulipiza kisasi baada ya kuwekewa vikwazo na Marekani

- Urusi imekana tuhuma dhidi yake na kusema huu ni wakati wa Marekani kugeuza mwenendo wa uhusiano wa Mataifa hayo

Soma > https://jamii.app/UrusiMarekani
FAHAMU KUHUSU KILIMO CHA UYOGA

- Mdau anasema aina za Uyoga zinazofaa kulimwa #Tanzania ni zile zinazostawi vizuri kwenye maeneo ya joto la wastani wa nyuzi 20c hadi 33c

- Malighafi zitumikazo kuzalisha Uyoga ni mabua, majani ya mpunga, ngano, pumba za mpunga au mahindi, masalia ya miwa baada ya kukamua ambayo hukatwa, huchemshwa na kutandazwa kwaajili ya mbengu kupandwa

Zaidi, soma - https://jamii.app/KilimoUyoga
#JFKilimo
MAREKANI: UCHAGUZI WA UGANDA ULICHAKACHULIWA. YAWEKA VIKWAZO KWA MAAFISA WA SERIKALI

Marekani imesema inaweka vikwazo kwa Maafisa waliodhoofisha mchakato wa #Demokrasia hasa wakati wa Uchaguzi uliofanyika Januari 2021 na kipindi cha Kampeni

Soma https://jamii.app/USSanctionsUG
TUNISIA: WATU 41 WAPOTEZA MAISHA BAADA YA BOTI KUZAMA

- Walikuwa wakijaribu kufika Kisiwa cha Italia cha Lampedusa

- Mwezi uliopita wahamiaji na wakimbizi 39 walipoteza maisha na Juni 2020 takriban watu 60 walifariki dunia baada ya boti kuzama

Soma > https://jamii.app/41BotiTunisia
CUBA KUTOKUWA NA KIONGOZI ANAYEITWA CASTRO BAADA YA MIAKA 62

- RaΓΊl Castro anatarajiwa kuachia Madaraka kama Katibu Mkuu wa Chama, cheo kinachotajwa kuwa na nguvu kuliko cha Rais

- Aliingia Madarakani 2008 baada ya Afya ya Fidel Castro kudhoofika

Soma https://jamii.app/CubaCastro
FAHAMU NAMNA YA KUWATOFAUTISHA CHIPMUNK NA KINDI (SQUIRREL)

- Chipmunk wana mistari 7 katika miili yao, mstari mmoja mweusi unaopita mgongoni na mistari 3 kila upande

- Kindi ana mistari 13, mistari 7 myeusi yenye vidoti vyeupe ikitenganishwa na mistari myeupe. Mistari yote inaenda hadi kichwani

- Chipmunks wana masikio yaliyosimama na yenye umbo la duara wakati Kindi wana masikio mafupi ambayo hayajatokeza juu ya kichwa

- Chipmunks wana mkia wenye manyoya mengi na mara zote unanyanyuka juu wakiwa wanatembea. Kindi wana mkia usio na manyoya mengi na haunyanyuki juu anapotembea

#JamiiForums
SERIKALI KUWASILISHA MUSWADA WA KUREKEBISHA KIKOKOTOO CHA MAFAO

- Serikali itawasilisha Bungeni Muswada wa marekebisho ya #Sheria ya mafao ya Wafanyakazi kuhusu kikokotoo kipya ili kuondoa vikwazo kwa Wafanyakazi kuchukua fedha wanapostaafu

Soma - https://jamii.app/MuswadaMafao
ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TPA AACHIWA KWA DHAMANA

- TAKUKURU imesema Deusdedit Kakoko ameachiwa kwa dhamana na Taasisi hiyo imekamilisha uchunguzi kwa 98%

- Alishikiliwa kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Bilioni 3 ndani ya Mamlaka ya Bandari

Soma https://jamii.app/KakokoDhamana
SHINYANGA: BABU ATUHUMIWA KUBAKA MJUKUU WA MIAKA 7

- Jeshi la Polisi linamshikilia Juma Emmanuel (53) kwa kumbaka Mjukuu wake wakati Bibi wa Mtoto akiwa amelazwa Hospitalini

- Wananchi watakiwa kutoa taarifa kuhusu Ukatili dhidi ya Watoto

Soma - https://jamii.app/KubakaMjukuuSHY
TAKWIMU: KUNA ONGEZEKO LA WATOTO KUACHA SHULE. WAVULANA WAONGOZA

- Wavulana 96,683 waliacha Shule mwaka 2020 na Wasichana 71,151. Mwaka 2017 ilikuwa Wavulana 36,434 na Wasichana 29,708

- Wanafunzi 167,834 waliacha Shule kutokana na utoro

Soma - https://jamii.app/WanaoachaShule
MAREKANI YAAMURU WANADIPLOMASIA WAKE KUONDOKA CHAD

- Ni kutokana na hofu ya kutokea mashambulio katika Mji Mkuu wa N’Djamena

- Marekani imetoa kauli hiyo wakati vikundi vyenye silaha vikionekana kujiimarisha kuingia katika Mji huo

Soma > https://jamii.app/USDiplomatsChad
PERU: KASHFA YA CHANJO YAPELEKEA RAIS WA ZAMANI KUPIGWA MARUFUKU KWA MIAKA 10

- MartΓ­n Vizcarra amepigwa marufuku kushika wadhifa kwenye Ofisi ya Umma kwa muda wa miaka 10 kufuatia madai kuwa aliruka foleni kupokea Chanjo ya #COVID19

Soma > https://jamii.app/VizcarraPeru
MIKATABA YA VIJANA 854 WA JKT WALIOGOMA NA KUANDAMANA YASITISHWA

- Vijana hao wa kujitolea walifanya hivyo kushinikiza kuandikishwa Jeshini

- Jenerali Venance Mabeyo amesema, "Kitendo hiki hakikubaliki, kugoma au kuandamana Jeshini ni kosa la uasi"

Soma > https://jamii.app/VijanaMikatabaJKT
RAIS SAMIA ASHIRIKI KONGAMANO LA KUMUENZI MAGUFULI

- Rais Samia Suluhu na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, leo wameshiriki Kongamano lililoandaliwa na Viongozi wa dini Chimwaga, kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa maisha ya Hayati Magufuli

Angalia - https://youtu.be/e4bSqKFNb3M
ASKOFU KONKI: KUMSIFIA RAIS SAMIA NA KUMKASHIFU DKT. MAGUFULI NI KUJIPENDEKEZA

- Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Tanzania, Peter Konki, amesema, "Watu hawa wanafanya hivyo kwa kutugawa Watanzania, tunaanza kushambuliana. Hayati Magufuli ni kipenzi cha Watanzania wengi kwahivyo wanasiasa msitugawanye"

Msikilize https://youtu.be/e4bSqKFNb3M
RAIS SAMIA: KUNA MIJADALA BUNGENI HAINA AFYA KWA TAIFA

- Amesema kipindi hiki wabunge wanapaswa kupitisha bajeti kwa maendeleo

- Asema "Jikiteni huko mengine tutayazungumza siku zinavyokwenda. Tufanye kazi kama Bunge linavyotakiwa kufanya kazi"

Tazama > https://youtu.be/FB7b1J8Dcuw
Rais Samia: Kamati ya kuchunguza #CoronaVirus imeshaundwa na hivi karibuni nitakaa nayo kujua namna tunavyokwenda

> Niwaombe viongozi wa dini, muwaombe waumini wenu wafuate hatua zote za kujikinga na #COVID19 kama kunawa mikono n.k
MAREKANI: WANAOJITOKEZA KUPATA CHANJO YA CORONA WAPUNGUA

> Mamlaka za #Marekani zimesema wanaojitokeza kupata Chanjo ya #COVID19 wamepungua sababu ikitajwa kuwa wengi wanasubiri kuona madhara ya chanjo hizo kwa ambao wameshapata

Soma https://jamii.app/ChanjoMarekani
TABORA: JELA MIAKA 21 KWA KUVUNJA NYUMBA NA KUIBA

> Hamisi Jilala Kwabi na Mohamedi Kassim wamehukumiwa kutumikia kifungo baada ya kukiri makosa 3 ya kuvunja na kuiba

> Ktk tukio mojawapo waliiba televisheni yenye thamani ya Tsh 1,100,000

Soma - https://jamii.app/JelaWizi
JE, NI SAHIHI KUFURAHIA MAHUSIANO YA VIJANA WADOGO?

> Mdau ameandika wazazi wengi hufurahia watoto wa kiume wakijihusisha na mapenzi wakiwa hata Shule ya Msingi na huonekana ni kawaida wakati huo huo wakichukizwa hali hiyo inapokuwa kwa watoto wao wa kike

> Je, ni kweli wazazi wako hivyo. Je unadhani ni sahihi?

Soma https://jamii.app/MaleziMahusiao