JamiiForums
βœ”
55.4K subscribers
33.4K photos
2.04K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SUMAYE: HATUTAKI WATU WANAOCHOCHEA FUJO KWASABABU WANATAFUTA MADARAKA

> Aitaka Serikali na Vyama vya Siasa kuchukua hatua dhidi ya wagombea wanaotoa kauli zinazohatarisha Amani

> Amesema, Amani ya Tanzania lazima idumishwe

Soma - https://jamii.app/SumayeAmaniTZ
#Uchaguzi2020
NIGERIA: JIMBO LA KADUNA LAPITISHA ADHABU YA KUWAHASI WABAKAJI

> Wabunge wamepitisha adhabu ya kuwahasi wataokutwa na hatia ya kubaka/kulawiti watoto chini ya miaka 14

> Gavana wa Jimbo anasubiriwa kutia saini Muswada huo ili kuwa sheria

Soma - https://jamii.app/LawRapistsNGR
PERU: BUNGE LAANZA MCHAKATO WA KUMSHTAKI RAIS

> Rais MartΓ­n Vizcarra (57) anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kujaribu kuzuia Uchunguzi wa Ufisadi

> Amekana mashtaka yote na kulishutumu Bunge kwa kuanzisha mapinduzi ya kisiasa

Soma - https://jamii.app/BungeRaisPeru
ZANZIBAR: CCM KUZINDUA KAMPENI ZA URAIS LEO

> Makamu Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuongoza uzinduzi

> Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi atatangaza ilani ya Chama hicho kwa Wananchi

Soma - https://jamii.app/ZNZKampeniCCM

#Uchaguzi2020
DR CONGO: WATU 50 WAHOFIWA KUFARIKI KATIKA MAPOROMOKO MGODINI

- Ajali hiyo imetokana na mvua kubwa zinazonyesha Mjini Kamituga

- Meya wa Mji huo ametangaza siku 2 za maombolezo na kutoa wito kwa Wananchi kusaidia kuopoa miili ya Marehemu

Soma - https://jamii.app/AjaliMgodiDRC
DAR: RAIA 7 WA KIGENI MBARONI KWA UTAPELI MTANDAONI

> Watuhumiwa hao wamekiri kupata Milioni 10 kwa udanganyifu

> Wametumia kiasi cha fedha hizo kuanzisha duka la pombe kali, kununua Toyota Mark X, runinga 2 na magodoro

Soma - https://jamii.app/PolisiUhalifuDar
#JFLeo
HOFU ILIYOPITILIZA HUSABABISHA KUSHUKA KWA KINGA YA MWILI

> Mtalaamu wa masuala ya saikolojia, Baraka Mushobozi amesema hofu hujidhihirisha kwenye mwili kwa kupata maumivu makali ya mgongo au kuumwa na kichwa sana na kupata magonjwa nyemelezi

Soma https://jamii.app/HofuKingaMwili
#JFLeo
UGANDA: MAAFISA WA KCAA WAKAMATWA BAADA YA JENGO KUANGUKA

> Walifika eneo la mradi na kuagiza ujenzi kusimamishwa lakini baadaye wakaruhusu uendelee

> Polisi wanaendelea kutafuta watu ambao inaaminika wamefukiwa na kifusi

Soma - https://jamii.app/BuildingCollapseUG
LISSU: MOROGORO IMEFANYWA KUWA SHAMBA LA BIBI NA WATAWALA

> Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema ni kwasababu Mkoa huo ni tajiri kwa kilimo kuliko Mkoa mwingine hapa nchini

> Akiwa Ifakara amesema, "Nikiwa Rais wa nchi hii, nikiunda Serikali ya CHADEMA, katika Mkoa wa Morogoro jambo la kwanza litakuwa kutaifisha haya mapande makubwa yaliyoibiwa na hawa wezi"

#Uchaguzi2020
ARSENAL YAANZA KWA KISHINDO. LEEDS INAITOA JASHO LIVERPOOL

> Magoli ya Arsenal yamefungwa na Lacazette, Gabriel na Aubameyang huku nyota Willian aliyetokea Chelsea akitengeneza magoli yote

> Crystal Palace imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Southampton

#Jamiiforums #JFSports
DAR: CHAMA CHA SAU KUZINDUA KAMPENI LEO

> Kampeni za Chama cha Sauti ya Umma zinatarajiwa kuzinduliwa maeneo ya Gongo la Mboto na Mombasa kuanzia saa 4 asubuhi

> Vilevile, SAU itafanya uzinduzi wa Ilani katika eneo la Kwazoo

Soma - https://jamii.app/SAUIlaniKampeni

#Uchaguzi2020
MANYARA: DAKTARI NA MTAALAMU WA USINGIZI MBARONI KWA KUOMBA RUSHWA

> TAKUKURU inawashikilia Dkt. Martin Kongora na Fabiona Aweda kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Tsh. 180,000 kutoka kwa mzee(60) aliyekuwa anasumbuliwa na tezi dume

Soma - https://jamii.app/DktRushwaKiteto
SERIKALI: NCHI INA CHAKULA CHA KUTOSHA, HATUTEGEMEI KUWA NA UHABA

> Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema Tanzania imejitosheleza kwa Chakula kwa 124% na ina ziada ya tani za Milioni 3

> Amehimiza Chakula kutumika na kuhifadhiwa vizuri

Soma - https://jamii.app/UhabaChakulaTZ
LIBERIA: UBAKAJI WATANGAZWA KUWA DHARURA YA KITAIFA

> Rais George Weah ameagiza taratibu mpya kuchukuliwa ili kukabiliana na tatizo hilo

> Serikali imesema itaunda Kikosi Kazi cha Usalama wa Taifa kwa ajili ya unyanyasaji wa kijinsia

Soma - https://jamii.app/RapeLiberia
CHATO: TANZANIA NA UGANDA ZASAINI MAKUBALIANO YA KUANZA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA

> Rais John Magufuli (Tanzania) na Rais Yoweri Museveni (Uganda) wamesaini makubaliano ya kuanza ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga

> Hapa nchini bomba hilo litapita kwenye Mikoa 8, Wilaya 24 na Kata 132. Aidha, watu zaidi ya 90,000 watalipwa fidia inayokadiriwa kufikia Bilioni 21

Soma - https://jamii.app/JPM-MuseveniChato
Tundu Lissu (Iringa): Tukipata Serikali Oktoba 28 tutahakikisha kila Mtanzania atakuwa kwenye Bima ya Afya

> Tofauti yetu na hii bima ambayo haiwasaidii ni kwamba bima tunayoisema sisi itamuhusu kila mtu anayekaa nchi hii, uwe Raia au sio Raia

#Uchaguzi2020
NEC YAENDELEA KUCHAMBUA RUFAA, MADIWANI 25 WARUDISHWA

> Rufaa 4 za Ubunge kutoka Jimbo la Babati Mjini zimekataliwa

> Pia, Tume ya Uchaguzi imekataa Rufaa 12 za Wagombea ambao hawakuteuliwa na 9 za kupinga Wagombea walioteuliwa

Soma - https://jamii.app/NECWagombeaRufaa

#Uchaguzi2020
GWAJIMA: MIMI SI KILAZA, NILIENDA MAREKANI 2019, NIMEANDIKA VITABU 5 KWA KIJAPANI

> Mgombea wa Ubunge wa Kawe(CCM) amesema, akichaguliwa ataweka Ambulance kila Kata, watu watakimbizwa hospitalini kwa haraka na jambo hilo ni jepesi halihitaji Manispaa wala Serikali

Soma zaidi https://jamii.app/KilazaGwajima
SALUM MWALIMU: TUTASEMA KWA AJILI YA ASKARI WETU HATA KAMA MNATUPIGA

> Mgombea mwenza wa Urais kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu amesema wanataka Jeshi la Polisi linalofanya kazi zake kwa haki, kwani sheria bila haki ni unyanyasaji

> Ameongeza kuwa, CHADEMA haitaleta askari wake bali itatumia waliopo isipokuwa watalifanya kuwa Jeshi la kutoa huduma badala ya dhuluma na kutumia nguvu

#Uchaguzi2020 #JamiiForums #Siasa
COSMAS CHEKA AJINYAKULIA MKANDA WA 'UBO'

> Bondia wa Tanzania, Cosmas Cheka amejinyakulia Mkanda baada ya kushinda pambano dhidi ya Hannock Phiri

> Pambano lilikuwa la round 12 na alishinda kwa alama

Soma https://jamii.app/ChekaVsPhiri
#JFMichezo
WASTANI WA UMRI WA WANAWAKE WANAOPATA SARATANI YA MATITI WAPUNGUA

> Mwaka 2008/2009 waliougua Saratani ya Matiti walianzia miaka 64 huku 2019 walianzia miaka 56

> Hii inaonesha Saratani hiyo imeanza kushambulia wanawake wenye umri mdogo pia

Soma https://jamii.app/SarataniWanawake
#JFLeo