JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: KUMBUKUMBU YA MIAKA 19 YA SHAMBULIO LA 'SEPTEMBA 11'

> Shambulio hilo la Septemba 11, 2001 linatajwa kuwa kubwa kuwahi kufanyika nchini Marekani na kusababisha vifo vya watu takriban 3,000 na kujeruhi wengine 6,000 baada ya kundi la kigaidi la Al-Qaeda kuteka ndege 4 na kuzilipua kwenye majengo ya New York

> Osama Bin Laden (aliyekuwa Kiongozi wa Al-Qaeda) alitangaza vita dhidi ya Marekani kutoka katika pango moja eneo la Tora Bora mnamo Februari 1996

Fahamu zaidi - https://jamii.app/Sept11Anniversary
#JFHistoria
UTAFITI: MGODI WA PETRA WASHUTUMIWA KWA UTESAJI NA KUPIGA WATU RISASI

> Shirika la RAID ambalo hufichua ukiukwaji wa Haki za Binadamu limepokea ripoti za mauaji takriban 7, mashambulio 35 yakiwemo ya kupigwa risasi, kupiga na kutesa tangu 2009

Soma https://jamii.app/UtafitiRAIDPetra
UGANDA YATANGAZA KUFUNGUA ANGA LAKE OKTOBA 1

- Ni baada ya kuzuia safari za ndege kwa takriban miezi 5 ili kudhibiti maambukizi ya #CoronaVirus

Baadhi ya Mashirika yanayotarajiwa kufanya safari ni Air Tanzania, Kenya Airways na Emirates

Soma - https://jamii.app/SafariNdegeUG
KISUTU: WAHUKUMIWA KULIPA MILIONI 16 KWA KUTUMIA JINA LA MKE WA RAIS KUTAPELI

> Masse Uledi (43) na Nkinda Shekalage (34) wamehukumiwa kulipa fidia na kifungo cha nje cha miezi 7 baada ya kukiri kutumia jina la Mama Janeth Magufuli kutapeli

Soma - https://jamii.app/UtapeliMkeRais
UCHAGUZI 2020: IJUE ILANI YA CCM INASEMA NINI KUHUSU KILIMO?

> Kuongeza eneo lenye miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji kutoka hekta 561,383 mpaka kufikia hekta 1,200,000 ifikapo mwaka 2025

> Kujenga mabwawa ya kuhifadhi maji kwa ajili ya umwagiliaji katika maeneo yanayopata mvua chache kama Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini ya umwagiliaji na kuwashirikisha wakulima kwa kila mwaka

Soma zaidi - https://jamii.app/IlaniCCM
#Uchaguzi2020
TCRA YAKIFUNGIA KITUO CHA WASAFI FM KWA SIKU 7

> TCRA imeifungia Wasafi FM kuanzia Septemba 12 hadi Septemba 18 kwa kukiuka kanuni za Mawasiliano ktk vipindi vya The Switch na Mashamsham

> Wasafi FM imetakiwa kuomba radhi kwa Watanzania

Soma - https://jamii.app/BanWasafiFM
#CORONAVIRUS: INDIA YAREKODI VISA ZAIDI YA 96,000 NDANI YA SAA 24

> Maambukizi mapya 96,551 yameripotiwa, idadi hiyo ni kubwa zaidi kurekodiwa duniani

> #India ina jumla ya visa 4,566,726 na vifo 76,336 huku waliopona wakiwa 3,542,663

Soma - https://jamii.app/COVID19Updates
ZEC YAMPITISHA MAALIM SEIF KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR

> Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imempitisha Mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, Maalim Seif kuwa mgombea wa Urais

> Mwenyekiti wa Tume hiyo amesema mapingamizi yaliyowekwa dhidi ya Maalim hayana mashiko

#Uchaguzi2020
DAR: AFISA TAKUKURU MBARONI KWA RUSHWA YA MILIONI 4.9

- Nina Sipilon Saibul amekamatwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa Mfanyabiashara

- Aliwekewa mtego uliopelekea yeye na Mumewe, Ramadhan Makoye kukamatwa wakipokea fedha hizo

Soma https://jamii.app/RushwaAfisaTAKUKURU
AKAUNTI YA TWITTER YA BALOZI WA CHINA-UINGEREZA KUCHUNGUZWA BAADA YA KU-LIKE MAUDHUI YA NGONO

> Ubalozi wa China - Uingereza umeomba mtandao wa Twitter kuchunguza akaunti ya Liu Xiaoming kama imedukuliwa au la! kutokana na ku-like maudhui ya ngono

Soma - https://jamii.app/XiaomingTwitter
SUMAYE: HATUTAKI WATU WANAOCHOCHEA FUJO KWASABABU WANATAFUTA MADARAKA

> Aitaka Serikali na Vyama vya Siasa kuchukua hatua dhidi ya wagombea wanaotoa kauli zinazohatarisha Amani

> Amesema, Amani ya Tanzania lazima idumishwe

Soma - https://jamii.app/SumayeAmaniTZ
#Uchaguzi2020
NIGERIA: JIMBO LA KADUNA LAPITISHA ADHABU YA KUWAHASI WABAKAJI

> Wabunge wamepitisha adhabu ya kuwahasi wataokutwa na hatia ya kubaka/kulawiti watoto chini ya miaka 14

> Gavana wa Jimbo anasubiriwa kutia saini Muswada huo ili kuwa sheria

Soma - https://jamii.app/LawRapistsNGR
PERU: BUNGE LAANZA MCHAKATO WA KUMSHTAKI RAIS

> Rais MartΓ­n Vizcarra (57) anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kujaribu kuzuia Uchunguzi wa Ufisadi

> Amekana mashtaka yote na kulishutumu Bunge kwa kuanzisha mapinduzi ya kisiasa

Soma - https://jamii.app/BungeRaisPeru
ZANZIBAR: CCM KUZINDUA KAMPENI ZA URAIS LEO

> Makamu Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuongoza uzinduzi

> Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi atatangaza ilani ya Chama hicho kwa Wananchi

Soma - https://jamii.app/ZNZKampeniCCM

#Uchaguzi2020
DR CONGO: WATU 50 WAHOFIWA KUFARIKI KATIKA MAPOROMOKO MGODINI

- Ajali hiyo imetokana na mvua kubwa zinazonyesha Mjini Kamituga

- Meya wa Mji huo ametangaza siku 2 za maombolezo na kutoa wito kwa Wananchi kusaidia kuopoa miili ya Marehemu

Soma - https://jamii.app/AjaliMgodiDRC
DAR: RAIA 7 WA KIGENI MBARONI KWA UTAPELI MTANDAONI

> Watuhumiwa hao wamekiri kupata Milioni 10 kwa udanganyifu

> Wametumia kiasi cha fedha hizo kuanzisha duka la pombe kali, kununua Toyota Mark X, runinga 2 na magodoro

Soma - https://jamii.app/PolisiUhalifuDar
#JFLeo
HOFU ILIYOPITILIZA HUSABABISHA KUSHUKA KWA KINGA YA MWILI

> Mtalaamu wa masuala ya saikolojia, Baraka Mushobozi amesema hofu hujidhihirisha kwenye mwili kwa kupata maumivu makali ya mgongo au kuumwa na kichwa sana na kupata magonjwa nyemelezi

Soma https://jamii.app/HofuKingaMwili
#JFLeo
UGANDA: MAAFISA WA KCAA WAKAMATWA BAADA YA JENGO KUANGUKA

> Walifika eneo la mradi na kuagiza ujenzi kusimamishwa lakini baadaye wakaruhusu uendelee

> Polisi wanaendelea kutafuta watu ambao inaaminika wamefukiwa na kifusi

Soma - https://jamii.app/BuildingCollapseUG
LISSU: MOROGORO IMEFANYWA KUWA SHAMBA LA BIBI NA WATAWALA

> Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema ni kwasababu Mkoa huo ni tajiri kwa kilimo kuliko Mkoa mwingine hapa nchini

> Akiwa Ifakara amesema, "Nikiwa Rais wa nchi hii, nikiunda Serikali ya CHADEMA, katika Mkoa wa Morogoro jambo la kwanza litakuwa kutaifisha haya mapande makubwa yaliyoibiwa na hawa wezi"

#Uchaguzi2020
ARSENAL YAANZA KWA KISHINDO. LEEDS INAITOA JASHO LIVERPOOL

> Magoli ya Arsenal yamefungwa na Lacazette, Gabriel na Aubameyang huku nyota Willian aliyetokea Chelsea akitengeneza magoli yote

> Crystal Palace imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Southampton

#Jamiiforums #JFSports
DAR: CHAMA CHA SAU KUZINDUA KAMPENI LEO

> Kampeni za Chama cha Sauti ya Umma zinatarajiwa kuzinduliwa maeneo ya Gongo la Mboto na Mombasa kuanzia saa 4 asubuhi

> Vilevile, SAU itafanya uzinduzi wa Ilani katika eneo la Kwazoo

Soma - https://jamii.app/SAUIlaniKampeni

#Uchaguzi2020