JamiiForums
56K subscribers
33K photos
1.91K videos
30.1K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
KATAVI: WATOTO 3 WA FAMILIA 1 WAFARIKI KWA KULA KUNDE PORI

> Imeelezwa kuwa jana mchana watoto 6 walikula kunde pori na baadae kukimbizwa Zahanati kutokana na kupata maumivu ya tumbo

> Mwaka 1988, watu 4 nao walifariki kwa kula kunde hizo na mtu mmoja alinusurika kifo mwaka jana

Soma https://jamii.app/KataviKundePori
20 PERCENT: NARUDI KWENYE MUZIKI KUONDOA MUZIKI WA MATUSI

- Baada ya kimya cha muda mrefu Mwanamuziki 20 Percent amesema anafarijika kuona bado mashabiki wake wana upendo naye

- Amesema, “Mimi silengi soko, nalenga fikra za mlalahoi na mtu yeyote ambaye huzuni yake ipo na hamna mtu wa kuiongelea.”

Angalia; https://youtu.be/JkbbH3wZXfY
#JFBurudani
#COVID19 – KENYA: JUMLA YA WATU 487 WAMEFARIKI KWA #CORONAVIRUS

> Ni baada ya Watu 4 zaidi kufariki dunia. Maambukizi yamefikia 30,636 baada ya watu 217 kugundulika kuwa na #COVID19

> Watu 208 wamepona na kufanya idadi ya waliopona kufikia 17,368

Soma https://jamii.app/KE4DeathsCOVID19

#JFCOVID19_Updates
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MAPINDUZI YA KIJESHI: RAIS WA MALI NA WAZIRI MKUU MBARONI

- Kwa mujibu wa Reuters, Jeshi limewatia nguvuni Rais Ibrahim Boubacar Keita na Waziri Mkuu

- Wananchi wanataka Rais ajiuzulu kwa Uchumi kuporomoka na kushindwa kukabiliana na masuala ya kiusalama

Soma https://jamii.app/MaliMutiny
#MaliCoup
BAADA YA MAPINDUZI YA KIJESHI, RAIS WA MALI AJIUZULU

- Rais Ibrahim Boubacar Keita amejiuzulu akisema hataki kuona umwagaji damu ukitokea

- Kabla ya uamuzi huo, Wanajeshi waliofanya mapinduzi walimuweka kizuizini pamoja na Waziri Mkuu Boubou Cisse

Soma https://jamii.app/RaisMaliAjiuzulu
#MaliCoup
FAHAMU HAYA BAADA YA PSG KUTINGA FAINALI YA MICHUANO YA KLABU BINGWA ULAYA

- Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) jana imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kuifunga Klabu ya RB Leipzig goli 3-0

- Huu ulikuwa mchezo wa 110 wa PSG kwa michuano ya Ulaya - michezo mingi kuchezwa na timu kabla ya kufika fainali ya kwanza, wamevunja rekodi ya Arsenal ya michezo 90

Zaidi, soma https://jamii.app/PSGRekodiUlaya
#JFSports
FAHAMU JINA LA SEHEMU REFU ZAIDI DUNIANI

>Taumatawhakatangihangakoauauotamateaturipukakapikimaungahoronukupokaiwhenuakitanatahu ni jina la mwinuko ulioko Porangahau, New Zealand

> Jina linabeba historia ya Taumata ambaye alitumia sehemu hiyo kuomboleza

Soma https://jamii.app/JinaRefuDuniani
MAREKANI: JOE BIDEN ATEULIWA KUGOMBEA URAIS KUPITIA DEMOCRATIC

> Bill Clinton na Jimmy Carter, wamemsifu Biden kuwa ni mtu wa kuinusuru Marekani iliyoathiriwa na #CoronaVirus

> Michelle Obama amesema Rais Trump ameshindwa kuliongoza Taifa hilo

Soma https://jamii.app/USJoeBidden
#JFSiasa
UMOJA WA MATAIFA WALITAKA JESHI KUWAACHIA HURU RAIS WA MALI NA VIONGOZI WAKE

> Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres ametaka kurudishwa kwa utawala wa Katiba na sheria nchini Mali

> Baraza la usalama la UN litakutana leo kujadili hali ya #Mali

Soma https://jamii.app/MaliJeshiUN
#JFLeo
IGUNGA: MKURUGENZI WA MAJI ASIMAMISHWA KAZI AKIDAIWA KUNYANYASA WAFANYAKAZI

- Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemsimamisha kazi Raphael Merumba na Bodi yote kupisha uchunguzi

- Watendaji wanadai kunyanyaswa na wengine kudaiwa rushwa ya ngono

Soma https://jamii.app/MrkngzMajiIgunga
BAADA YA KIPIGO KIZITO, BARCELONA YAMTAMBULISHA KOCHA MPYA

- Aliyekuwa Kocha wa timu ya Taifa ya Uholanzi, Ronald Koeman (57) amepewa mkataba wa miaka miwili

- Koeman anachukua nafasi ya Quique Setien, aliyefukuzwa baada ya Barcelona kufungwa goli 8-2 na Bayern Muchin

Soma https://jamii.app/KoemanBarca

#JFSports
RC MGHWIRA: HAKUNA UHALALI MISAFARA YA WAGOMBEA KUPIGWA MAWE

> RC wa Kilimanjaro amesema hayo wakati akimjibu Askofu Shoo aliyeitaka Serikali kukomesha wanaoharibu misafara ya wagombea

> Asema atalifanyia kazi suala hilo na kulitolea ufafanuzi

Soma https://jamii.app/AnnaMghwira
#JFSiasa
UTAFITI: TANZANIA YAONGOZA KWA KUWA NA AMANI AFRIKA MASHARIKI

> Tanzania imekuwa ya 52 duniani huku Rwanda ikiwa ya 81, Kenya 125, Uganda 109, Burundi 132 na Sudan Kusini 160

> Nchi ya 1 kwa amani duniani ni Iceland ikifuatiwa na New Zealand huku Iraq, Syria na Afghanistan zikishika mkia

Soma https://jamii.app/GrobalPeaceIndex
PWANI: MWALIMU MBARONI AKITUHUMIWA KUMSHAMBULIA MWANAFUNZI KWA FIMBO

- Evata Mboya wa shule ya Msingi Mwendapole, Kibaha anadaiwa kumshambulia kwa fimbo Mwanafunzi (12) kwa kosa la kupiga kelele na kumsababishia maumivu makali ya kichwa

Soma https://jamii.app/MwalimuMbaroniPWN
JE, UNAZIJUA AINA ZA NYAYO ZA KIDIGITALI?

> Nyayo za Kidigital za hiyari: Hizi hujumuisha taarifa unazoziacha kwa kujua unapotembelea tovuti mbalimbali

> Nyayo za Kidigitali zisizo za hiyari: Hizi zinachukuliwa kwako bila ya kujua

Soma > https://jamii.app/DigitalFootPrints

#UlinziWaTaarifa
SAME: WANACCM KATA YA BWAMBO WAMPINGA MGOMBEA UDIWANI ALIYEPITISHWA NA HALMASHAURI KUU

- WanaCCM Kata ya Bwambo wameandamana kumpinga mgombea aliyeshika namba 2 kwenye kura za maoni na kupitishwa na Halmashauri Kuu kugombea Udiwani

Soma https://jamii.app/CCMUdiwaniBwambo
#Uchaguzi2020
DAR: WATU 3 KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA UGAIDI

> Wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa 7 waliyodaiwa kuyatenda kati ya Mei 1 na Agosti 1, 2020

> Wamekutwa na silaha, vifaa vya milipuko, sare za JWTZ na #DawaZaKulevya aina ya Heroin

Soma https://jamii.app/KisutuUgaidi
LIFAHAMU KUNDI LINALOTOA HUDUMA YA KUVUNJA MAHUSIANO - WAKARESASEYA

> Kundi hili liko Japan likitoa huduma ya kumuacha mpenzi wao bila kumuumiza au kuwaachanisha watoto ikiwa mpenzi aliyenaye kama mzazi unaona hamfai

> Tafiti zinaonesha watu wengi hupenda huduma hii

Soma https://jamii.app/UjasusiWaMapenzi
UTEUZI WA MKURUGENZI MPYA WA JIJI LA DODOMA

- Rais Magufuli amemteua Joseph Constantine Mafuru kuwa Mkurugenzi akichukua nafasi ya Godwin Kunambi

- Awali, Mafuru alikuwa Mkuu wa Idara ya Ardhi, Mipango Miji na Maliasili wa Jiji hilo

Soma https://jamii.app/KunambiAondolewaDDM
WASAFIRI KUTOKA NCHI 130 WATAINGIA KENYA BILA KUWEKWA KARANTINI, TANZANIA HAIMO

> Orodha imejumuisha Wasafiri kutoka India ambayo ni nchi ya 3 kwa maambukizi ya #COVID19 Duniani

> Kwa Afrika Mashariki nchi zilizopo kwenye orodha hiyo ni Rwanda na Uganda

Soma https://jamii.app/CountriesExempted

#JFCOVID19_Updates
SUDAN KUSINI: BENKI KUU YAISHIWA PESA ZA KIGENI

> Wataalamu wanasema ni kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa mafuta kulikosababishwa na rushwa na migogoro ya ndani

> Paundi ya nchi hiyo imeshuka thamani. Kwa muda mrefu mfumuko wa bei umebaki 35%

Soma https://jamii.app/ForeignReserve