JamiiForums
55.4K subscribers
33.4K photos
2.03K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
BORIS JOHNSON: WAANDAMANAJI WA UBAGUZI WA RANGI WAMEKUWA WAFANYA FUJO

> Waziri Mkuu wa Uingereza amesema watu wana haki ya kuandamana kwa amani lakini hawana haki ya kuwashambulia Polisi

> Ni baada ya Waandamanaji kuwajeruhi Polisi 8

Soma https://jamii.app/WaandamanajiFujo
KAHAMA: ADHA YA MAJI YASABABISHA WANAWAKE 2 KUUAWA NA FISI

> Inaelezwa wanawake wa Kata ya Ngogwa wamekuwa hatarini kwa miaka mingi kutokana na adha ya maji ambayo huwalazimu kufuata maji umbali mrefu na hulazimika kuamka nyakati za usiku

Soma https://jamii.app/WauawaNaFisi
#JFLeo
MEXICO: AFISA WA SERIKALI ATHIBITIKA KUWA NA #COVID19 SIKU CHACHE BAADA YA KUWA NA RAIS

- Mkurugenzi wa Taasisi ya Hifadhi ya Jamii, Zoé Robledo ametangaza jana kuwa na #CoronaVirus

- Ni siku 2 tangu awe pamoja na Rais Andrés Manuel Obrador

Soma https://jamii.app/COVID19Updates
#JFLCOVID19_Updates
TUNDU LISSU ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS

- Asema akipata dhamana ya kuongoza, Serikali haitatumia Vyombo vya Dola dhidi ya Wapinzani na Wanahabari. Atakuwa mfariji Mkuu, hatakimbilia Kijijini kwao wakati wa majanga kama tetemeko au #COVID19

- Amesema “Nina uwezo wa kuwafuta machozi. Ninaweza kuwatibu machungu mengi mliyosababishiwa. Nikiwa Rais nitafuta Sheria kandamizi zinazoumiza Wananchi”

Soma https://jamii.app/LissuNiaUrais
#JFLeo
#CORONAVIRUS-UGANDA: WAGONJWA WAPYA 30 WATHIBITISHWA

- Wagonjwa 5 ni madereva, 4 wafanyakazi wa Afya, 3 ni Walinzi na 18 ni waliokutana na Wagonjwa

- Aidha, Madereva wa Kenya-43, Tanzania-4, Burundi-3 na Eritrea-1 wamerudishwa baada ya kukutwa na #COVID19

Soma https://jamii.app/COVID19UG-646
#JFCOVID19_Updates
MADEREVA WA MAGARI YA MIZIGO WAOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI YANAYOENDELEA MPAKANI

> Madereva 6 wa Kenya wanadai magari yao yanashikiliwa Tanzania, mpakani Sirare

> Imedaiwa maafisa wa Tanzania hawaridhishwi na wanachotendewa madereva wa Tanzania nchini Kenya

Soma https://jamii.app/KEMaderevaTZ
#JFLeo
FAHAMU KUHUSU TATIZO LA MAUMIVU YA MAGOTI

> Maumivu ya magoti ‘Osteoarthritis’ huwapata hasa wazee, wanawake na watu wanene. Husababisha uharibifu wa minofu migumu myeupe katika magoti

> Dalili zake ni pamoja na maumivu kwenye magoti wakati wa kusimama au kutembea

> Kwa sasa hakuna tiba kwa ajili ya ‘Osteoarthritis’ lakini matumizi ya Bamia na mazoezi hupunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa huu

Soma https://jamii.app/MaumivuMagoti
#JFAfya
#CORONAVIRUS: WAGONJWA 95 WAONGEZEKA KENYA

- Ni baada ya sampuli 1,096 kupimwa ndani ya saa 24. Jumla ya visa yafikia 2,862

- Wagonjwa 97 wamepona na jumla ya waliopona ni 849. Mgonjwa mmoja amefariki na waliofariki jumla ni 85

Soma https://jamii.app/COVID19KE-2862
#JFCOVID19_Updates
AZIMIO: KUTAKA BUNGE KUTOPITISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA NAMBA 3 WA 2020

Muswada huo unakiuka Misingi mikuu 3 ya Demokrasia
> Usawa mbele ya Sheria
> Uhuru wa Mihimili ya Dola
> Haki ya Kulinda Katiba

Saini azimio (petition) hapa >> https://jamii.app/SainiAzimio
KAMPUNI YA MAFUTA YA BP KUPUNGUZA WAFANYAKAZI 10,000 ULIMWENGUNI

- BP itapunguza 15% ya Wafanyakazi ili kupunguza gharama za uendeshaji zilizotokana na #COVID19

- Imesema bei ya mafuta imeshuka na matumizi ya Kampuni yamekuwa makubwa kuliko mapato

Soma https://jamii.app/PunguzoWafanyakaziBP

#JFCOVID19_Updates
FAHAMU KUHUSU KILIMO CHA PILIPILI MTAMA/MANGA

> Zao hili humea katika mazingira ya wastani wa nyuzi joto 24-26, mvua za Milimita 1,500 mpaka 2,000 kwa mwaka na udongo wenye rutuba

> Maua ya kwanza hutokea baada ya miezi 24 tangu kupandwa na matunda yake hukomaa kwa miezi 9 hadi 10

Soma https://jamii.app/PilipiliMtama
#JFKilimo
UTARATIBU WA MAONESHO YA SABASABA KUZINGATIA KANUNI ZA AFYA ILI KUJIKINGA NA #COVID19

> Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara Jijini Dar (DITF) yanatarajiwa kuanza Julai Mosi

> Mikutano ya ana kwa ana ya Wafanyabiashara (B2B) mwaka huu itafanyika mtandaoni

Soma https://jamii.app/2020Maonyesho77
#JFLeo
UINGEREZA: WATU 36 WAKAMATWA KWA KUWASHAMBULIA POLISI KATIKA MAANDAMANO

> Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi na ukatili wa Polisi yanaendelea Jijini London

> Polisi 35 wamejeruhiwa na waandamanaji, na wawili kati yao wako hospitali

Soma https://jamii.app/LondonWaandamanaji
#BlackLivesMatter
URUSI KUONDOA MASHARTI YALIYOWEKWA KUPAMBANA NA #COVID19

> Urusi imetangaza kuondoa masharti hayo kuanzia Juni 09, licha ya kurekodi maambukizi mapya kila siku

> Urusi ni nchi ya tatu kwa wingi wa maambukizi ya #COVID19 ikiwa na maambukizi 476,658 na vifo 5,971

Soma https://jamii.app/UrusiVizuiziCOVID19
#JFCOVID19_Updates
WHO: WAGONJWA WENGI WA #COVID19 KWA SIKU MOJA WAMERIPOTIWA JUNI 7

- Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Wagonjwa zaidi ya 136,000 wameripotiwa jana na takriban 75% wanatokea katika nchi 10 za Mabara ya Amerika na maeneo ya Asia Kusini

Soma https://jamii.app/COVID19Updates
#JFCOVID19_Updates
ATHARI ZA #COVID19: BENKI YA DUNIA YATABIRI UKUAJI WA UCHUMI TANZANIA KUFIKIA 2.5%

- Imetabiri ukuaji utafikia asilimia hizo mwaka huu kutoka 6.9% iliyoripotiwa na Serikali 2019

- Aidha, imetabiri Watu 500,000 zaidi wataingia katika kundi la umasikini hususan walio katika mazingira ya mijini wakitegemea biashara za kujiajiri na biashara zisizo rasmi/ndogo

Soma https://jamii.app/KuporomokaUchumiTZ-WB
#JFLeo
DODOMA: FREEMAN MBOWE ASHAMBULIWA NA KUJERUHIWA NA WATU WASIOJULIKANA

> Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman A. Mbowe ameshambuliwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake jijijini Dodoma

Fuatilia zaidi https://jamii.app/MboweAttack
UTABIRI WA HALI YA HEWA TANZANIA KWA KIPINDI CHA JUNI HADI AGOSTI

> TMA imesema Ukanda wa Pwani utapata vipindi vichache vya baridi tofauti na miaka iliyopita

> Imeshauriwa kuchukua tahadhari kama kuzingatia matumizi mazuri ya maji

Soma https://jamii.app/HaliYaHewa
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman A. Mbowe ameshambuliwa na kujeruhiwa majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake jijijini Dodoma

Zaidi, soma https://jamii.app/MboweAttack
MAREKANI: GEORGE FLOYD KUZIKWA LEO, JUNI 9 HUKO HOUSTON

> George Floyd (46) aliyefariki Mei 25, 2020 anazikwa leo huko Houston, sehemu aliyokulia

> Floyd aliuawa kwa kukandamizwa na Polisi shingoni, tukio lililozusha maandamano makubwa

Soma https://jamii.app/GeorgeFloydAzikwa
UMOJA WA ULAYA WAIPATIA KENYA NYONGEZA YA DOLA MILIONI 78 KUPAMBANA NA #COVID19

- EU imeongeza fedha hizo ambazo ni sawa na takriban Tsh. Bilioni 180 ili zisaidie kushughulikia madhara ya #COVID19 katika Uchumi na Kijamii

- Awali, EU iliipatia Kenya Dola Milioni 84 (takriban Tsh. Bilioni 194) ili kushughulika na #Corona

Soma https://jamii.app/EUGrants-Kenya
#JFLeo