HabariTech
197 subscribers
33 photos
4 videos
1 file
125 links
Bila shaka unataka kuwa na uhuru wa pesa (upate utajiri). Ni wazi kwamba unatamani kuifahamu tech vizuri kwa kuwa umeambiwa utajiri upo huku.

Ni kweli tech inapesa nyingi, ila kwanza ungana nasi ili usitumie pesa nyingi kujifunza na uweze kuokoa muda.
Download Telegram
🚨 BIASHARA 🚨

Kuna Samsung Galaxy A31 inauzwa hapa mkononi kwa mtu.

Bei yake ni nafuu anaanzia Tsh. 450,000. Imetumika kwa muda wa miezi 2 toka inunuliwe.

Muuzaji yupo Dodoma mjini.

RAM 4GB
Storage 128GB
Android version ni 11

Simu nimeikagua vizuri mimi mwenyewe haina shida. Kwa anayehitaji namba yangu ya Whatsapp ni hii 0753607400.

Karibuni.
HabariTech
Photo
Leo rasmi magazine ya kwanza ya Teknolojia kwa Kiswahili imeingia mtaani.

Hongereni kwa kuwa wa kwanza kuipata Makala hii. Unaweza pakua kupitia link hii https://habaritech.systeme.io/habaritech

Gharama yake ni ndogo sana Tsh. 0 😁.

Ndiyo, namaanisha ni bure kabisa.

Karibu.
Decentraland Metaverse

Tangu Facebook kubadili jina October 2021, kumekuwa na discussion nyingi mtandaoni kuhusiana na Metaverse.

Ila metaverse ni nini na tunaweza kuitumia vipi? Wengi bado hawajajua.

Metaverse ni ulimwengu wa kidijitali uliojengwa juu ya blockchain, sawa na ule wa kwenye movies za Ready Player One au Free Guy.

Tukiwa ndani ya metaverse ni sawa na kutoka katika ulimwengu halisi na kuanza kuishi kwenye ndoto kama vile tunavyopata ndoto tukilala.

Facebook wamekuwa wakitangaza nadharia ya metaverse ya kibiashara zaidi kuliko uhakisia wake.

Facebook wanasema kuingia metaverse lazima utumie VR Goggles.

Hii ni kauli isiyo na usahihi asilimia 100%, kwani kuingia metaverse unahitaji kuwa na Computer tu na bando la internet.

Ndani ya YouTube video hii nimekuelezea namna unaweza ingia metaverse na kuishi huko.

Iwapo utakuwa na swali lolote usisite kuniuliza.

YouTube Video 👇
https://t.co/nhVi3QsgGP https://t.co/BU3cf6IpKr
Nilikuwa naanda mpango mzuri niwenatoa exclusive content kwenye hii telegram channel.

Stay Tuned for exclusive content 😉
Binadamu tuko Hatarini

Feb 15, 2022, Niliandika tweet kusema sijapenda namna “You might Like” algorithmn ya twitter inaleta maudhui yasiyo nifaa.

Cha kushangaza sio mimi tu niliyekuwa na mawazo hayo na hii kitu ilinifanya nifikirie tunapoelekea sisi kama binadamu
https://bit.ly/3IjyiIq

Kuna vitu 5 ambavyo kila nikifikiria vinaleta picha ya kutisha kwa namna ambavyo mambo yanaenda sasa hivi. Kuanzia matumizi yetu ya mitandao ya kijamii mpaka namna serikali zinaendeshwa.

Ushawahi kukaa na kujiuliza mitandao ya kijamii inaleta athari gani kwenye mwenendo wa maisha yako?

Mitandao ya Kijamii

Natumia zaidi twitter kuliko mtandao wowote wa kijamii, ikifuatiwa na instagram kisha TikTok. Kila ninapotumia mitandao hii kuna kitu kimoja huwa kinakuja akilini dakika chache baada ya kuacha kutumia mitandao hii.

Ninapata hisia ya KUJILAUMU kwa kutumia zaidi ya dakika 20 bila kufanya chochote kila mara ninapokuwa katika mitandao hii. Mbaya zaidi sio kukaa katika mitandao hii bila kufanya chochote, ila ni vitu ninavyoangalia ninapo kuwa mtandaoni.

Mimi ni mtu napenda sana tech gadgets toka nikiwa na umri mdogo, hivyo huwa nina kuwa na hamu kali ya kumiliki kila gadget nzuri inayopita machoni mwangu.

Bahati mbaya picha za gadgets nakutana nazo sana instagram na Tiktok kama content inayokuwa recommended kwangu na algorithm za mitandao. Kwa mtu mwingine anapenda kuwa na maisha mazuri.

Unapita zako Instagram unakuta picha za couple goals wakiwa baecation serengeti au Dubai. Wakati una scroll hizo reels, unakutana na picha ya kijana mdogo amepiga mbele ya BMW X6 alafu kwa background kuna mjengo wa bei mbaya.

Hapo nafsi yako inaridhika na unashawishika kuscroll zaidi kuona mengine kama hayo. Ukija kutoka hapo ndipo unagundua ulijifungia ndani ya dunia yako ndogo ndani ya mtandao.

Unaamka kujua kwamba umepoteza 75% ya bando lako kuangalia vitu usivyoweza kumiliki kwa muda huo.

Ukiangalia mazingira uliyopo hayakuridhishi na unayachukia kwa kuwa umeshaona mazingira ya hali ya juu yanakuaje.
Badala ya kufanya kitu productive, unapata msongo wa mawazo na unaenda ongeza bando kwa kigezo cha kwamba utapitwa na vitu usipokuwepo online.

Ubaya wa mitandao ya kijamii ni kwamba hujui kama unachokiona ni kweli au sio kweli. Na hiyo ni kwa sababu mitandao inatushawishi kuonyesha upande mzuri tu wa maisha yetu. Ndiyo sababu ukipata kazi kampuni kubwa utatangaza, ila ukiachwa na mpenzi wako hauta tangaza kwa sababu unaogopa maoni hasi ya watu. Na hii inanipeleka kwenye kitu cha pili.

Negativity ya watu
Binadamu tuna asili ya kuvutiwa zaidi na taarifa hasi kuliko taarifa chanya. Mfano nikipost vichwa hivi vya habari Apple Wamefeli sana kwenye iPhone 13 na iPhone 13 ni simu bora.

Nakuhakikishia post itakayopata engagement KUBWA ni ile ya kufeli kwa iPhone 13. Hiyo ni kwasababu tunamekuwa na asili ya kupenda kuona taarifa mbaya au kutoa maoni hasi kwa kila kitu mtandaoni.

Unaweza chukulia kwamba hivi vitu vinaishia tu mtandaoni, lakini kwa chini chini vinaenda mpaka kwenye uhalisia kuanzia ngazi ya familia mpaka kitaifa.

Ukipita kwenye trending tweets, kila siku unaweza kuta mada moja ambayo inabeba pande mbili. Ndani yake kuna watu wenye mabishano endelevu ambayo hayajawahi kuwa na mwisho. Upande mmoja wakiwa upande chanya na wengine hasi.

Hawa watu huwa wanafikia makubaliano?

Hapana, haijawahi kutokea waafikia makuabaliano kwa sababu kila mmoja hayuko tayari kuungua akili yake kusikia maoni ya mwingine na kuangalia jambo hilo kwa jicho la pili.

Kizazi chetu kinaweza ishi na hili na tukalipuuzia, lakini kuna watoto wadogo sasa hivi ambao wanaona haya mambo na wanayachukulia kwamba ndiyo mwenendo wa maisha unavyotakiwa kuwa. Haya ni mambo yanatakiwa kudhibitiwa kabla hayajatuzidi nguvu.

Kujitenga na mazingira yanayotuzunguka

Tunaelekea wapi kama vijana wa dot com? Fanya hili zoezi popote ulipo sasa hivi kama ni eneo la watu wengi. Hebu acha kutumia simu yako, angalia watu wangapi wamekaa wakiangalia tu simu zao. Vizuri zaidi pita eneo kama restaurant angali meza ya watu waliokaa kama marafiki.
Je, wanaongea au kila mmoja yuko busy na simu yake?

Tumekuwa watu ambao tunatafuta kukubalika mtandaoni kuliko na watu wanaotuzunguka. Hii ni kwa sababu simu zetu zimekuwa vizuri sana kufanya kazi ambazo watengenezaji wake wamelenga kuliko sisi kujua inatakiwa kufanya nini. Kwa sababu hiyo tukikaa pamoja tunaona ni bora kuangalia videos TikTok kuliko kuzungumza na wanaotuzunguka.
Hii ni kwa sababu hatuko tayari kupokea maoni ya wanaotuzunguka pale ambapo kuna jamii za mtandaoni ambazo zinatupa majibu tunayotaka kusikia.

Mimi kama naamini dunia ni tambarare nitajiunga na jamii zinazokubaliana nami na sio na rafiki zangu wanao amini kwamba dunia ni duara.

Echo Chambers

Niliposema mitandao na simu zetu zinafanya kazi ambazo zimeundwa kufanya namaanisha hiki kitu kinaitwa echo chambers. Echo ni Mwangwi, yaani sauti yako kurudi kwako ukiongea.

Echo chambers kazi yake ni kukuonyesha wewe maudhui ambazo zinaendana na wewe ili kuendelea kukuweka kwenye mtandao husika.

Sio uongo kuwa instagram wanataka uendelee KUPERUZI mtandao wao na Ali Express wanataka uendelee KUNUNUA kutoka kwao.

Wanafanyaje ili kuhakikisha hilo?

Leo hii ukiingia google kutafuta neno “Good gaming PC available 2022” unaweza pewa link za maduka yanayouza PC. Ukifungua tu link moja wapo, nakuhakikishia ukipita AliExpress au instagram utaanza kuona matangazo kuhusu Gaming PCs.

Hii ni kwa sababu algorithm yao imeamini kwamba kwa muda huo umevutiwa na mada zinazohusu gaming PC. Hii ndiyo tunaita echo chamber. Na kwa sababu hii utajikuta unaendelea kuperuzi huo mtandao kwa kuwa wanakuonyesha unachotaka kuona.

Kinachoendelea hapa ni mitandao kukuamlia ufikirie nini kwa muda mrefu. Ukiongelea Samsung utaanza kuona matangazo kuhusu Samsung. Mpaka tweets na posts za watu utakazoona ni zile zinaongelea Samsung tena kwa kuwasifu.

Ghafla utajikuta unaanza kuwa shabiki wa Samsung. Unaweza jikuta unaenda mbali zaidi na kuanza tumia bidhaa zao (Simu, TV, fridge, nk). Kinachoogopesha hapa ni kwamba akija mtu wa iPhone kukwambia tofauti hautataka kumuelewa kabisa. Na hii inaweza kukupelekea kurudi kwenye point yangu ya Negaitvity.

Ufuatiliaji
Tumefikia hatua ambayo teknolojia inaendelea kukua kwa kasi ya ajabu sana na hakuna mtu anataka iache kukua. Teknolojia bora maana yake ni kwamba maisha yetu yanakuwa bora zaidi na rahisi zaidi, hata silaha za kijeshi zinakuwa za kisasa kuzidi miaka ya nyuma.

Bahati mbaya wakati kila kitu kutuhusu kinakuwa cha kidijitali, kuanzia mahusiano mpaka uhalifu. Serikali na kampuni za mitandao na mawasiliano inabidi zitafute namna mpya ya kudhibiti haya yote ili kuwa na control juu ya watu wake.
Namna ya udhibiti ambayo itatumika hapa haitakuwa rafiki kwetu sisi wananchi.

Mfano mzuri ni sera mpya ya Apple kufatilia picha zote ndani ya simu yako, kuona kama kuna child abuse (Unyanyasaji wa watoto) unafanyika na kukuripoti kwa mamlaka husika.

Kwa sasa hili ni jambo zuri, ila itakuaje huko mbeleni kama serikali zitaanza kuweka sheria kwamba hizi kampuni za simu zifatilie kila kitu unachofanya na simu yako. Na hapa sina maana ya vitu vya kihalifu, naongelea vitu kama kwenda google na kutafuta “Bunduki inafanya vipi kazi?”. Kwamba ukitafuta kitu kama hicho wewe ni mhalifu unatakiwa kuwekwa mbaroni?

Unaweza dhani ni kitu haiwezekani ila China tayari wanafanya kitu kama hicho. Wananchi wa China wanakuwa rated kulingana na vitu wanavyofanya kwenye jamii. Vitu vinavyo zingatiwa hapa ni kama kuweka muziki kwa sauti kubwa eneo la watu wengi sio sahihi au kuvuka barabara sehemu isiyo na kivuko cha watembea kwa miguu.

Hivi ni vitu vidogo ambavyo vikiendelea sana vinaweza pelekea mwananchi wa China kuzuiliwa kusafiri kwa ndege kutoka nje ya nchi au hata kuondolewa haki ya baadhi ya vitu kama kwenda kumbi za starehe.

Mwisho

Binafsi napenda sana teknolojia na sitaki kusema kwamba tuachane nayo kwa kuwa inatupeleka pabaya. Ukweli ni kwamba mpaka sasa imetuletea maendeleo mazuri.
Kama umetumia dakika 40 instagram kuangalia instagram models usioweza kuwa nao sio kwamba umepoteza muda. Hapana, hiyo ni instagram inafanya kitu ilitakiwa kufanya. Kitu ambacho ni kukuonyesha wewe maudhui unayopenda ili usiache kutumia Instagram.

Ninachojaribu kusema ni kwamba sio mbaya kama mara moja moja tutaacha kutumia mitandao ili kuona tunaelekea wapi sisi kama jamii.
Point ni Zile zile

Huwa tunasema "Serikali haitoi sapoti ya kutosha kwa vijana wa Kitanzania."

Wengine wanasema "Sina mtaji wa kutosha kuanza sasa hivi."

Wakati tunatoa hizi excuses kuna vijana tayari wamefanya makubwa na kuleta solutions zinazosaidia Watanzania wengi.

Kujua ni kina nani na wamefanya nini, ni kupitia magazine ya 5 ya HabariTech.

Link https://habaritech.gumroad.com/l/habaritech5
AVAX Staker Review: Katika video hii nitakuonyesha project yenye high risk ambayo unaweza pata faida ya mpaka 20% ROI kwa siku kulingana na muda unawekeza katika project hii.

Avax Staker ni nini?

Huu ni muda mzuri wa kuweka AVAX zako katika yield returns na kupata ROI nzuri. Hii ni project inayoendeshwa na jamii. Jamii hii inashawishi wana jamii wake kuwekeza asilimia ndogo ya faida zao ili kuifanya project iishi kwa muda mrefu.

Unaweza kutumia Avax Staker reward calculator kuona utapata faida kiasi gani kabla hujaamua kuwekeza AVAX zako katika project hii. Pia ni vizuri ukatumia Avax Staker referral program kupata faida zaidi na AVAX ulizonazo.

Tazama Full video kupitia link hii ya YouTube https://youtu.be/-xx0gNggWm4
Iwapo mtu unaswali zaidi usisite kuuliza hapa hapa kwa ajili ya manufaa ya wengine pia.

Maswali yanayokuja inbox sitayajibu.
Kama kuna mwingine hizi terms zina mchanganya. Majibu ni hayo.
This is a test message
Kutofautisha Simu Feki na Original

Ukikaa muda mrefu sana mtandaoni kuna uhakika utakutana na watu ambao wako tayari kutumia mamilioni kununua simu feki na ni mara chache sana huwa wanajua kwamba walichonunua ni feki.

https://habaritechtz.com/kutofautisha-simu-feki-na-original/