Elimika🧠
9.19K subscribers
507 photos
3 videos
103 links
Learn something new every day
Contact @Elimikabongo for businesses
Download Telegram
3
The Pentagon.
Leo tuongelee kuhusu huu mjengo tata wenye sifa Kama zote duniani.
Pentagon ni mjengo wa offisi za idara kuu ya ulinzi wa marekani.
Lilijengwa tarehe 11/09/1941 na ilipofika tarehe 15/01/1943 mjengo huo ulikuwa umekamilika. Kwa ufupi lilijengwa kwa miezi kumi na sita 16. Yaani mwaka na miezi NNE.
Pentagon lilidizainiwa na bwana George Bergstrom na kujengwa na bwana John Mcshain.
👉 Pentagon Ina ukubwa wa mita za mraba 620.000 yaani futi ( 6.636 360 ). Na heka 27 za parking ya magari.
👉 Pentagon Ina orofa 7 tano za juu ya ardhi na mbili chino ya ardhi. Ina pembe tano na kila pembe Ina urefu wa mita 281 . pembe zake tano ndiomana ikaitwa The Pentagon.
👉 The pentagon iligharimu serekali ya marekani dollar za kimarekani million 83 miaka iyo sawa na dollar billion 1.19 mwaka 2021.
👉 The Pentagon Ina waajiriwa wa kijeshi 45.000 na 3000 RAIA wakawaida.
👉 The Pentagon imekuwa Mjengo mkubwa zaidi duniani kiofissi kwa miaka 80. Na hapo nibaada ya India kuzindua mjengo wao wa kioffissi za serekali hapo juni 20 mwaka huu.

BACKGROUND YAKE.
Vita kuu vya dunia vilipotokea pale ulaya Idara ya ulinzi ya marekani ilijikuta kupungukiwa na offisi kutokana na harakati zake nyingi za kijeshi. Hivyo aliekuwa the Secretary of state kipindi iko alitoa ombi kwenye bunge lawatu wazima lakutaka kuongezwa kwa offisi za kijeshi.
👉 Hivyo ombi lilikubalika bila kipingamizi na kusema Idara ya ulinzi kuu Ijengwe pale Arlington Virginia washington karibu na mtoni.
MATUKIO PENTAGON.
Tarehe 15/02/1967 Pentagon lilikabiliwa na waandamanaji zidi ya vita vya Vietnam. Kundi LA wanawake 2.500 walizingira eneo hilo uku wakishikilia mabango yaliohashiria amani Kati ya watu wazima USA na Vietnam.
👉 Tarehe 21 /10/1967 kundi LA anti war prontester wapatao 35.000 waliandamana kwenye offisi ya mkuu wa idara ya ulinzi uku wa kipigwa vimbola vya kutoa machozi.
👉 mwaka 19/05/1972 shirika LA hali ya hewa LA chini ya ardhi lilishambulia orofa ya NNE ya mapumzikio ya mjengo wa The Pentagon mwishoni mwa vita yao na Vietnam.
👉 mwaka 17/03/2007 watu wapatao 15.000 walihandamana zidi ya vita Kati ya USA na Iraq. Huku msafara wao ukianzia kutoka kwenye jengo LA ukumbusho LA lincolin hadi kwenye ukingo wa the Pentagon.
👉 11/09/2001 siku ya kusherekea miaka 60 ya The Pentagon Jengo hili lilishambuliwa na wanaume watano walioiteka ndege ya the american air line 77 na kuipigisha kwenye ukuta wa magharibi wa The Pentagon.
👉 Tukio hili lilitokea majira ya asubuhi 09;45 na kusababisha vifo vya watu 3000 na kuanguka kwa mijengo miwili ya the world trade center.
👉Hili limekuwa tukio lakwanza kuwai kutokea ndani ya marekani tangu taifa ilo kujinyakulia Uhuru wake 1776, ambalo limesababishwa na Sera za nje.
👉 Pamoja na kwamba ndilo jengo lenye ulinzi tata duniani baada ya The white house waajiriwa wengi siku iyo hawakukuwa kwenye offisi zao. Maana badala ya waajiriwa 45.000 siku hiyo walikuwepo waajiriwa 800 pekee hivyo wale ma alqaida wakapata mwanya na kupenya katika radari za ulinzi za The Pentagon.
👉 ikumbukwe mbali nakwamba baada tu ya uchaguzi wa urais huko Misri, Cairo watazindua offisi yao ya ulinzi mpya kubwa zaidi duniani itakayoitwa The Octagon yenye pembe nane , Ilisikika waziri wa ulinzi wa misri akitamka yakwamba The Pentagon itabaki kuwa Unbeaten katika nyanya zote maana imejengwa kwa ustadi usio wakaida.
👉Mwaka 2011 The pentagon liliboreshwa upya katika miundo mbinu ya hali ya juu yakisasa ya kuistamili makombora ya aina yoypte ikiwemo hata Yale yanayobeba vichwa vya nuclear.
Marekani imekuwa inachukuwa sifa nyingi katika maswala ya ulinzi nikutokana na uchokozi wake pamoja wivu anaowekewa na nchi jerani pamoja na nchi zenye utawala wa kimabavu.
USA ndio imekuwa nchi namba moja katika maswala ya ulinzi katika idara zote hadi The withe house pamoja na msafara wa rais wake unaojulikana Kama The Beast. Umeambiwa hapo ikulu yake bomo LA nuclear halipenye 60 km angani.
Imepenya hii au niongezee nyundo.??.
9
Big Bang Theory ni nadharia ya kisayansi inayoeleza jinsi ulimwengu ulivyoanza ni tofauti kabisa na ile ya kidini
🌌 Maelezo rahisi
Big Bang inasema kwamba:
Ulimwengu wote ulianza kama kitu kidogo sana, chenye joto kali sana na msongamano mkubwa sana
Kisha ulilipuka (sio mlipuko wa kawaida, bali upanuzi) na kuanza kupanuka
Tangu hapo hadi leo, ulimwengu unaendelea kupanuka

🕰️ Ilitokea lini?
Takribani miaka bilioni 13.8 iliyopita

🔬 Nini kilitokea baada ya Big Bang?
Sekunde za mwanzo: nishati na chembe ndogo zilianza kuundwa
Dakika chache baadaye: atomi rahisi kama hidrojeni na heliamu
Miaka milioni kadhaa: nyota na galaksi zilianza kutengenezwa
Baadaye: mifumo kama jua na sayari (ikiwemo Dunia)

🧠 Ushahidi wa Big Bang
Wanasayansi wanaamini nadharia hii kwa sababu ya:
Upanuzi wa ulimwengu (galaksi zinaenda mbali na sisi)
Mionzi ya zamani (cosmic microwave background) – mabaki ya mlipuko wa mwanzo
Uwiano wa gesi kama hidrojeni na heliamu
7🤝2🔥1👏1🏆1
📚 UNAJITAMBULISHA KUNDI GANI?
Katika mijadala kuhusu dini na uwepo wa Mungu, mara nyingi utakutana na makundi haya manne. Haya ndiyo maana zake kwa ufupi:
🔹 THEIST (Muumini) Ni mtu anayeamini kwamba kuna Mungu au miungu inayotawala ulimwengu.
💬 "Ninaamini Mungu yupo."

━━━━━━━━━━━━━━
🔹 ATHEIST (Asiyeamini Mungu) Ni mtu ambaye haamini kuwepo kwa Mungu au miungu yoyote.
💬 "Sioni sababu ya kuamini kwamba Mungu yupo."
Kutokuwa atheist hakumaanishi lazima mtu hana maadili au hana msimamo wa maisha; ni mtazamo kuhusu uwepo wa Mungu.
━━━━━━━━━━━━━━
🔹 AGNOSTIC (Asiye na Uhakika) Ni mtu anayesema hajui kama Mungu yupo au hayupo, au anaamini kuwa suala hilo haliwezi kuthibitishwa kwa uhakika.
Agnosticism ni msimamo wa kutokuwa na uhakika, si lazima kukataa au kuamini.
━━━━━━━━━━━━━━
🔹 PAGAN (Mpagani) Ni mtu anayefuata dini za jadi au imani za kale zinazohusisha miungu, mizimu, roho au nguvu za asili.
Katika historia, neno "mpagani" lilitumika kuelezea watu walio nje ya dini kuu kama Ukristo na Uislamu.
4🔥1👏1
🧠 AINA 3 ZA AKILI ZINAZOKUONGOZA KILA SIKU
Watu wengi huamini kwamba maamuzi yao yote hutokana na mawazo wanayoyafahamu. Lakini saikolojia inaonyesha kuwa akili ya binadamu ina viwango tofauti vinavyoathiri namna tunavyofikiri, kuhisi na kutenda.

1️⃣ CONSCIOUS MIND
(Akili ya Ufahamu)

Hii ni sehemu ya akili unayotumia kwa sasa kusoma ujumbe huu.

💡 Kila unapochagua utakula nini, utaenda wapi au kujibu swali, unatumia Conscious Mind.
━━━━━━━━━━━━━━
2️⃣ SUBCONSCIOUS MIND
(Akili ya Chini ya Ufahamu)

Hii ni hifadhi kubwa ya kumbukumbu, uzoefu, mazoea, imani na hisia ulizokusanya tangu utotoni.

💡 Mara nyingi kile unachojiambia kila siku hujengeka ndani ya subconscious mind na baadaye huathiri namna unavyoishi.
━━━━━━━━━━━━━━
3️⃣ UNCONSCIOUS MIND
(Akili ya Kina)

Hii ndiyo sehemu ya ndani zaidi ya akili ambayo huwezi kuifikia moja kwa moja.
💡 Wakati mwingine mtu anaweza kuchukia au kuogopa jambo fulani bila kujua sababu yake halisi; wataalamu wa saikolojia huona hili kama ushawishi wa michakato ya unconscious mind
4🔥1👏1🤝1
Mwaka 2018 Mtoto Valeria wa Umri wa Miaka 12 na Mvulana Arkady wa Umri wa Miaka 22 Kutoka Urusi Walimuuwa Mfanyakazi wa Ndani, Wakavikaanga Viungo Vyake na Wakala. Polisi Walisema Kuwa Walivuta Bangi Kwanza. "Moyo Wake Ulikuwa Mtamu Sana."
4🤔21
Hizi code ni muhimu sana kuzijua wewe Mwanamtandao 😎👇


🌐💠 CALL FORWARD (Simu kuelekezwa kwa namba nyingine) 💠🌐

📞 All Calls: **21*NUMBER# ➤ Simu zote ziende kwa hiyo namba

📞 When Busy: **67*NUMBER# ➤ Ukiwa kwenye simu nyingine calls zitaenda Kwenye hyo namba

📞 No Answer: **61*NUMBER# ➤ Usipopokea, calls zitapelekwa Kwenye hiyo namba

📞 Not Reachable: **62*NUMBER# ➤ Simu ikiwa imezimwa au mtandao jau
Futa zote: ##002#

🔐💫 CALL BARRING (Kuzuia Simu/SMS) 💫🔐
🚫 Zuia simu kutoka (Outgoing): *33*0000#
🚫 Zuia simu kuingia (Incoming): *35*0000#
📩 Zuia SMS kutoka: *16*0000#
📩 Zuia SMS kuingia: *17*0000#
Ondoa barring zote: #33*0000#
🔑 PIN default ni 0000 (unaweza ibadilisha kwa usalama zaidi)

🛰️ CALL WAITING (Kusubiri Simu nyingine ukiwa kwenye Call) 🛰️
Washa: *43#
Ukiwa Kwenye call haitosema kama unatumika
Zima: #43#
📞 Ukipokea simu mpya, wa kwanza atakuwa umemsubirisha

🚫🔎 CALLER ID (Kuficha namba yako) 🔎🚫
📞 Piga bila kuonekana: #31#NUMBER
👉 Mfano: #31#0754000000
Inafaa sana kama mtu unamdai afu unampigia haokoti 😁

📡💥 NETWORK RESET (Kurudisha settings zote) 💥📡
🔄 Code: ##004# ➤ Inafuta forwarding, waiting & barring zote kwa pamoja

💡 BONUS TIP 💡
Unataka simu yako ionekane haipatikani bila kuzima? Za
➡️ Fanya forward kwenye namba ambayo haipo (mfano *62*000#)
😂 Mtu akipiga atasikia “Namba unayopiga haipatikani kwa sasa...”

👑 Mtoto wa kwanza wa kambo wa Clemence Mwandambo nimemalizaa🥹
4👍1
2🤝1
Mwanaume Huyu Pichani Anaitwa Bratislav Stojanovic Raia wa Serbia, Hadi Mwaka 2013 Akiwa na Umri wa Miaka 43 Alikuwa Anaendelea Kuishi Makaburini Peke Yake Tangu Miaka 15 Nyuma. Alichimba Shimo Kubwa na Kuishi Humo. Anafurahia Kuishi Makaburini Hapo.
👏2💯1
🚀 QUANTUM COMPUTER NI NINI? ⚛️💻

Fikiria kompyuta ya kawaida kama mtu anayefungua milango mmoja baada ya mwingine kutafuta njia sahihi. Quantum computer ni kama mtu anayejaribu milango mingi kwa wakati mmoja! 🔓🚪 Kompyuta za kawaida hutumia bits zenye thamani ya 0 au 1. Lakini quantum computers hutumia qubits, ambazo zinaweza kuwa 0 na 1 kwa wakati mmoja kutokana na kanuni za fizikia ya quantum. 🌌🧠

🤔 Hii ina maana gani?
Kwa baadhi ya matatizo magumu sana, quantum computer inaweza kufanya mahesabu ambayo yangewachukua kompyuta za kawaida miaka maelfu au hata mamilioni ya miaka. 💥

🌍 Matumizi yake yanayotarajiwa:
Kutengeneza dawa mpya kwa haraka zaidi 💊
Kuboresha akili bandia (AI) 🤖🧠
Kutatua matatizo magumu ya kisayansi 🔬📊
Kuboresha usafirishaji na logistics 🚚📦
Kutafiti siri za ulimwengu na fizikia 🌌🔭

⚠️ Quantum computers zenye nguvu za kutosha zinaweza kuvunja baadhi ya mifumo ya usalama wa kidijitali inayotumika leo, ndiyo maana wataalamu wanatengeneza teknolojia mpya za ulinzi. 🔐🛡️
4🔥1😁1
🧠 ELIMIKA | Je, Unajua Kwa Nini Tunasahau Ndoto Mara Tu Tunapoamka? 🌙
Umewahi kuamka ukiwa na uhakika ulikuwa unaota ndoto nzuri, lakini baada ya dakika chache hukumbuki chochote? Hii ni hali ya kawaida kabisa na ina maelezo ya kisayansi.
Wakati wa usingizi wa REM (Rapid Eye Movement), ambapo ndoto nyingi hutokea, ubongo huwa na shughuli nyingi za kutengeneza picha na hisia. Hata hivyo, sehemu ya ubongo inayohusika na kuhifadhi kumbukumbu za muda mrefu (hippocampus) haifanyi kazi kwa kiwango cha kawaida. Matokeo yake, ndoto nyingi hazihifadhiwi vizuri kwenye kumbukumbu.
Pia, unapoamka ghafla na kuanza kufikiria shughuli za siku, ubongo huanza kuzingatia taarifa mpya, na kumbukumbu ya ndoto hupotea haraka.
💡 Je, unataka kukumbuka ndoto zako zaidi?
Amka taratibu bila kuruka kitandani.
Jaribu kukumbuka ndoto kabla ya kushika simu.
Andika ndoto zako mara tu unapoamka kwenye daftari au simu.
📌 Fun Fact: Watafiti wanaamini mtu wa kawaida huota ndoto 4–6 kila usiku, lakini nyingi huzisahau ndani ya dakika chache baada ya kuamka.
#Elimika #Sayansi #Ubongo #Usingizi #Ndoto
🤝21