CRYPTO CURRENCY
156 subscribers
907 photos
21 videos
3.12K files
637 links
Download Telegram
lakin haichaji, pin ya kati ambayo ni ya signal inakuwaga na 4V ndiyo inakuwaga imemis hivyo ukifanya Test kwa Multimeter utaona una Njia Mbili Zenye 19V Lakin Charger Haichaji.

UTAJUAJE
Pima kwa kutumia Multimeter All Three Pins Kwenye Chager Cord lazima Ziwe Na Umeme, Au Ukichomeka Charger Halafu Ile LED Kweny Adapter Ikizima, au Ukiona Cheche Kwenye Charging Port Wakati Ukichomeka Charger.

SULUHISHO
Kama Kuna Uwezekano Wa Kuzi Arrange Tena Hizo Charger Basi Fanya Hizo Then Rudishia Na Hot Glue, Ikishindikana Basi Badili Adapter Nzima.

TATIZO LA 3
Adapter Kuungua: Hii sasa ni tatizo kubwa ila sio sana kwa maana ni mara chache sana kutokea kama charger adapter imeungua, suluhisho ya hili ni kufanya manunuzi ya adapter mpya kama huna skills advanced za electonics kwa maana utakuwa una deal na live AC Current, hivyo upo katika hali kubwa ya kupata madhara yatokanayo na umeme.
Kwa advanced learner unaweza kuipasua na kuangalia shida na mara nyingi inakuwaga ni Shorted Cap.

TUTAIANDALIA SESSION YAKE ADVANCED LAPTOP CHARGER REPAIR KWA SASA TUISHIE HAPA

TUIFUNGUE LAPTOP

Moja kati ya vitu muhimu na vya kuvifahamu sana na ni mtihani wa kwanza kwa mafundi wengi ni kujua kufungua laptop (DISASSEMBLE) Pamoja na kuirudishia, Hapa ndipo unapomaliza kuifunga laptop yote na kukuta Screw Zinabaki Hazijafungwa na hujui za wapi.
Kabla Hujafungua Laptop Hakikisha Una Vitu vifuatavyo:

1. Screwdrives (Kariakoo Set Elu 5-10)
2. Pry Tools (Hii kwa ajili ya kutolea lock za case ya laptop naa simu)
3. Tweezers (Kazi nyingi lakin hapa kubwa ni kutolea Ribbon cable)
4. Screw Container and Organizers (Hii ni simu haswaa kwa wale wanaobaki na screw baada ya kufungua)
5. Meza Safi Ya Kufanyia Kazi ( Hakikisha mahali unapofanya kazi ni safi na salama, hakuna vimiminika, hakuna uchafu uchafu, pako na mpangilio mzuri, hii itakurahisishia kutopoteza muda na vifaa)

HATUA ZA KUFUNGUA LAPTOP

1. Hakikisha laptop haina chanzo chochote cha umeme, Toa battery na hakikisha umeichomoa kwenye charger. (Hii inasaidia kuepuka short wakati wa kutoa cable cable slot zake, na pia kuepuka madhara ya umeme kwako pia inagawaje umeme unaokuja kwenye motherboard sio mwingi)
2. Anza Kufungua Screws Zinazohusika Na Vitu Muhimu Nyuma Ya Laptop, Kuna Screw Za KEYBOARD, CD DRIVE na Za Hard Drive Kwenye Bahadhi ya laptop za zamani haswaa dell mfano: 620, So anza kufungua kwanza hizi kama zipo.
3. Fungua Screw zote za nyuma ambazo zipo katikati au zimeshikilia part ya nyuma inayoweza kutoka kirahisi mfano: Cover la nyuma lenye Hard drive, RAM na Network card.
4. Jaribu Kutoa Hilo cover la nyuma, kama lipo na kama ukifanikiwa basi fungua nut nyingine zote unazoziona nyuma ya laptop yako.
5. Jaribu kuitoa keyboard na kama utafanikiwa basi fungua pia screw zilizopo chini ya keyboard ambazo huwa zinashikiria motherboard moja kwa moja. HAPA KUWA MAKINI NA CONNECTOR YA KEYBOARD NI RAHISI KUKATIKA
6. Hakikisha screw zote zimeisha, Then Anza Kujaribu Kutoa Cover Lolote Laptop Kwa Kutumia Pry Tools Fanya Taratibu Kubandua Ili Usije Vunja Lock Za Case, kwa laptop nying cover la juu ndio linatoka then la chini ndio linashikilia keyboard ila usikariri, laptop mpya kama Lenovo Case ya chini huwa inatoka kwanza, HAPA KUWA MAKINI SANA NA CONNECTOR ZA TOUCHPAD, SPEAKER, POWER BUTTON, Hakikisha zote umezichomoa.

7. Ukifanikiwa Vyote Hivyo Basi Utakutana Kitu Kama Hiki Hapa Chini, Wewe ni Shujaa Kwa Part Hii

Sio vitu vigumu ukijifunza unaweza.
Naomba Kwa Leo Tuishie Hapa,

Softcopy(PDF) Ya Notice Hizi nitaituma soon.

Tukutane Alhamis Kwa Ajil Ya PART 2 EP02.

@softwaretz