CRYPTO CURRENCY
156 subscribers
907 photos
21 videos
3.12K files
637 links
Download Telegram
leo nimeona tuzungumzie kuhusu hizi memory card. mtu anapotaka kununua memory card huulizia brand name tu ipi nzuri wengine watajibu sandisk wengine watajibu kingstone ila kila mtu atajibu lake. lakini tujiulize kitu kimoja kama laptop au simu tunachagua kwa perfomance na matumizi yetu je hizi memory card hazina specs kama vifaa vyengine?

jibu ni kwamba ndio memory card zina specs kama vifaa vyengine na ni vizuri kuchagua inayokidhi mahitaji yako. kuna wakati unaweza ukaona simu ipo slow au haichukui vizuri video pamoja na kucheza game tatizo hili linaweza kuchangiwa na memory card.

kwenye kuchagua memory card mambo mawili ni muhimu kuangalia.

1. ukubwa wa memory.
hapa nafkiri kila mtu anajua na wala nisipaelezee kirefu kila mtu anajua gb ngapi zinamtosha kuhifadhi mambo yake.

2. speed ya memory card.
hapa ndio dhumuni la hii thread watu wengi hawafahamu kuwa memory card zinatofautiana speed unaweza nunua memory card ikawa kimeo na kufanya kifaa kiwe slow.

memory card zimeekwa class kutokana na speed zake kuna class hizi hapa.

-class 2
-class 4
-class 6
-class 8
-class 10

zipo class za juu zaidi ila hizi zinatosha kumuelewesha mtu. class 2 inamaana speed yake ni 2MB/ps ikiwa class 6 ina maana 6MB/ps na class 10 ni 10MB/ps

hivyo ina maana jinsi inavyopanda ndio jinsi memory card inavyokua na speed.

tuchukulie mfano huu una simu inayorekodi hd utakapokua unachukua video za hd na memory card class 2 hio video haitatoka vizuri sababu video ni kubwa na speed ya kuandika memory card ni ndogo. same kwenye activities nyengine itakua slow.

je utatambuaje class ya memory card?
hii utaiangalia kwa juu kabisa ya memory card wanaandika class yake. ukiona hawajaandika ujue hio memory card ina walakin.
hitimisho
ni vizuri ukanunua memory card class 10 yenye brandname nzuri ili kupata perfomance nzur
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DARASA:HURU UFUNDI LAPTOP(Beginners to Advanced)

INTRODUCTION


Habari wana Telegram

Nimepata Massage nyingi ukimya wa hii channel ya telegram Nikaona Sio Mbaya Kama Tutaanzisha Darasa La Laptop Repair Humu At Least Vipindi Viwili mpaka vitatu Kwa Kila Wiki.

Tutajifunza Katika Njia Ya Maelezo Kwa Kiswahili, Picha Na Discussion Na Supportive Link Kama Zitahitajika.

Darasa Litakuwa Na Part Mbili

Part 1
(Hapa Tutajifunza Softwares Tu, Mfano: OS Zote Za Windows, Recovery, Tech Tools, Forensic Tools, Recovery Tools, Partition Wizards, Drivers Installations And Troubleshooting, Wireless Network Troubeshooting Na Vinginevyo)

Part 2
(Hapa Tutajifunza Laptop Hardware Tu, Na Kwangu Hii Ndio Most Paid Job Kwenye Laptop Repair, Tutajifunza Kuhusu Laptop Assembly and Disassembly, Identification Of Laptop Hardware Components, General Power Rails Of Laptop, Power Signals, Chipset Level And Behaviours, Tools And Component For Laptop Motherboard Repair, Matatizo Mbali Mbali Ya Laptop Na Utatuz Wake Upande Wa Hardware Na Vinginevyo)

Tutakuwa Na Vipindi Vitatu Vitatu Kwa Kila Part Ya Somo

J4, Alhamisi Na Jumapili mda ukiwepo.

Vitu Vya Kuzingatia

1. Tujitahid Kutumia Lugha Za Kistaarabu Kueleweshana
2. Kama Kuna Mahali Haujaelewa Uliza Tu Utajibiwa Hata Mara 100
3. Mafunzo Ya Haya Ni Bure Na Hayana Malipo Yoyote, Malipo Ni kusubscribe Channel yangu ya youtube link hii hapa
https://www.youtube.com/channel/UC17NXUQTvQMi3jwRBzMI-Tw?sub_confirmation=1

Na Baraka Zako.

Tukutane Weekend hii Kwa Part 1 Ya Software Na Hardware.

Mda wowote somo litaruka hewani
Forwarded from Daudi
TUIFAHAMU BIOS MENU NA UMUHIMU WAKE KWA SOFTWARE REPAIR

(PART 1 EP 01)
Forwarded from Daudi
Habari Wanandugu.

Ni jumamosi ya kwanza leo ya somo letu la laptop repair, na katika part 2 hii tutaangalia SOFTWARE Issues Tu.
Tujue Kidogo Nini Maana Ya Software Kwenye Laptop Au Computer Yoyote

Software Kwa Lugha Rahisi Ni Part Ya Computer Ambayo Huwezi Kuishika Na Mkono, Virtual Unakiona Lakini Huwezi Kukishika, Kama Vile Application, Themes, Cursor Etc
Software Ndio Inakupa Wewe Hali ya kuzungumza na computer, Kwa lugha nyingine ni USER INTERFACE.
Kwenye laptop repair practically, Software Inajumlisha, ALL Computer Apps, Operating System, BIOS, Etc.

Kwa Leo Tuangalie BIOS MENU Ambao Ni Msingi Mkubwa Wa Software Repair Na Kwa IT Professional Yoyote Hapa ndipo pa kuanzia kwenye software repair.

BIOS ni nini?
BIOS ni program iliyo na mahusiano mojamoja na laptop au computer yoyote kwa sababu ina chip iliyopo ndani ya motherboard, chip hiyo ndiyo inafanya kazi ya kuunganisha vifaa vyote vilivyopo ndani ya computer kufanya kazi kwa usahihi, kwa lugha sahihi huu ndiyo moyo wa software kwenye computer, hii ndio mwalimu mkuu wa software zote ikiwemo Operating System, Ukibonyeza Button ya kuwasha laptop anayeguswa na kutoa ruhusa ni bios na yeye ndio anaielekeza computer, Utachukua Software Wapi Either Kwenye HDD, USB Drive Au CD ROM,Etc.

BIOS Menu Ni Nini?
Ni Mpangilio Wa BIOS Katika Laptop Unaompa Ruhusa Mtumiaji Kufanya Chaguzi Mbali Mbali Kabla Ya Kufikia Katika Operating System.

Kipi Naweza Kukifanya Kwenye BIOS Menu?

* Unaweza Kuiwekea Password Laptop Yako (Hii ni safe Zaidi kuliko ya windows)
* Unaweza Kuangalia Taarifa Za Laptop Yako (System Info)
* Unaweza kuiamrisha laptop yako ifuate windows kutoka kwenye Nini Mfano: HDD, USB Drive Au CD ROM
* Unaweza Kufunga Matumizi ya Kifaa Kimoja Au Vingi Kwenye Laptop Yako, mfano: Port za USB, Speaker, Touchpad, WLAN Etc
* Unaweza Kupunguza Nguvu za matumizi ya Laptop yako kwa kutumia menu ya Multiprocessing na Virtual Technology
* Unaweza Kuangalia Life time na Status ya battery lako
* Kubadili saa na kujua OS Ya Kwanza Kuwekwa Kwenye Laptop Yako.
* Etc

NITAIPATAJE BIOS MENU?
Laptop zote zina bios menu tofauti, zinafanana baadhi kwa brand name mfano: DELL Nyingi Bios Ni F2 Na HP nyingi Bios Ni F9.
List Ya Bios Ipo Hapa Chini:
Forwarded from Daudi
Forwarded from Daudi
* Zima laptop yako
* Bonyeza Key Kama Zinavyoonekana Hapo Juu (Hutegemea na BRAND YAKO)
* Bonyeza kwa kuachia achia kama unaipiga ipiga mara nyingi maana mara nyingin hapa tunaotea
* Unabonyeza pale laptop inapowaka na kuonyesha brand name (kuwa makini sio zote zinaonyesha brand name nyingine zinakuwa kwenye FAST BOOT)
* Kama itagoma jaribu kwa kubonyeza huku ukiwa umeishikilia Function Key (Fn).

VILIVYOPO KWENYE BIOS MENU NA MATUMIZI YAKE

Hapa hutegemea na Bios Yenyewe Hapo Chini Nimetumia mfano wa Phoenix But Inaweza kuwa WARD Etc So Usikariri ila vingi vinafanana.

Tutumie mfano hapo chini.
Forwarded from Daudi
Forwarded from Daudi
MAIN = Hapo utaakuta sifa za laptop yako au STEM INFORMATION
Utajua Size ya RAM, HDD, Processor Na Serial Number Ya Laptop
Sio muhimu sana kwa repair technician

ADVANCED = Hapa ni muhimu kwa technician kwa maana hapa utapata Option ya Kuzima Ports, Au WLAN au Fn Key Au Speaker, Na Touchpad Hapa Utapata Menu ya Kupunguza Nguvu Ya Pc Na Processor, Na Kwa Gamers Amba Ndio Kuna Virtual Technology, Pia Hpa ndio kuna SATA MODE Ya HDD Ukibadili Hii Windows Hauwez Run Kwa Mode Tofauti na uliyoweka wakat unafanya installation.

SECURITY = Hapa utapata menu ya kufunga Password Za Laptop Yako (BIOS PASSWORD, HDD PASSWORD, ADMIN PASSWORD).

BOOT: Hapa utapata menu ya kuiamrisha laptop wapi ikachukue windows wakat inawaka, hapa ni muhimu sana wakati unataka kufanya installation ya windows kwa kutumia external device kama USB FLASH, UEFI MODE NA LEGACY MODE Zinapatikana hapa.

MATATIZO YA BIOS NA UTATUZI WAKE



Kuna matatizo mengi ya laptop lakini yafuatayo ni common na nimekumbana nayo sana.

1. BIOS PASSWORD
Hili ni tatizo sana na huwa nacharge pesa nzuri kulitatua, hii ni ile password tuliyoiona pale juu ambayo inatokea kabla booting haijafanyika.
Ukiwasha PC Utaona Hivi
Forwarded from Daudi
Forwarded from Daudi
JINSI YA KUTATUA TATIZO HILI
Kuna njia nyingi za kutatua BIOS Hutegemea Brand na Model Ya Laptop na Skills Alizo nazo Technician

* Kutumia Backdoor Password: hii ni common password ambazo zipo tayari kwenye bios kutoka kwa manufacture lengo la hizi ni kutumika wakat wa Emergency Ku Reset, Ili Kupata Hizi Password, Washa PC Nenda Kwenye BIOS Password Ingiza Randomly Psssword Zozote Mara 3, Then laptop itakuandikia SYSTEM DISABLE, Na itakupa namba Tano Copy Hizo Namba,Then Tafuta laptop nyingine nzima Nenda Kwenye Hii Site BIOS Master Password Generator for Laptops. Andika Disable code zako then Utapewa List ya Password Za Kujaribu Kufanya Reset.

* Toa CMOS Battery.
* Kama unaweza kufungua na kutoa CMOS Battery basi unaweza kufanya hivyo, Then ukawasha pc Unaweza Ukaitoa.
Forwarded from Daudi
1
Forwarded from Daudi
* CMOS Discharge.
* Hii ni advanced kwa tech yoyote anatakiwa kuifanya lakini ni lazima kuwa makini kwa maana ukishindwa kujua PIN Out za CMOS unaweza kuiharibu motherboard, Hii Inafanywa kwa kutoa CMOS Battery na kutafuta CMOS Pin Out Kweny Board na kupigisha Short. Means Unawasha laptop then unagusanisha hizo pin kwa kutumia Tweezer, The PC Itajizima, Ukiwasha Itakuwa haina Tena Password, Mchezo Huu Tunaufanya Sana Kwa Toshiba Na ACER, Kumbuka Kila motherboard ina PIN OUT Zake, So Kuangalia Schematica Au Ku Google Hakuepukiki.
* Mfano wa PIN OUT Huo hapo Chini:
Forwarded from Daudi