Millard Ayo
5.91K subscribers
29K photos
8.69K videos
36 files
1.04K links
BLUE BOY WA KISHUA
Journalist
Award winning TV/Radio Personality | Amplifaya @CloudsFMTZ |Journalist from Africa | I 💙 TIGO PESA APP | Bookings millard@millardayo.com
www.youtube.com/watch?v=g3NCUIuMVI0
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Find more inspiration to shine this festival season.
Shop new #babyshop festival collection now in our stores. @gsmmall

@millardayo
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Meza itapendeza na Watu wako watafurahi iwapo tu utatumia unga wa AZANIA kuandaa breakfast !! utofauti nimeuona @azaniagroup

@millardayo
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Tunaanza siku na habari njema kabisa kutoka @silent_ocean_ltd , sasa hivi mambo yamefikia hapa...

@millardayo
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Wakati Polisi Mkoani Arusha wakiendelea kumsaka Moses Pallangyo akidaiwa kumuua Mkewe Mary Richard Mushi Wilayani Arumeru kwa kumkata na shoka, mwili wa Mary umechelewa kuzikwa kutokana na Ndugu zake kusubiri kukamilika kwa pesa ya mahari.
_
Taarifa zinasema Moses hakuwahi kulipa Mahari ya kuishi na Mary na kwa mujibu wa Familia kwa taratibu zao licha ya tukio lililotokea lazima mahari ilipwe kwanza kwa Ndugu wa Mary ndipo azikwe.
_
Tayari vikao vya Familia za pande zote mbili vinaendelea na majadiliano ya mahari kisha baadae kupanga taratibu za mazishi.
#MillardAyoUPDATES

@millardayo
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha kwa mvua kubwa itakayoambatana na upepo mkali na radi kwa siku tano mfululizo katika Mikoa ya DSM, Morogoro, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Pwani pamoja na maeneo machache ya Visiwa vya Unguja na Pemba.
_
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Wilberforce Kikwasi amesema tahadhari hiyo imeanzia jana na ni kwa siku tano huku akiwataka wanaoishi maeneo yasiyokuwa salama wachukue tahadhari mapema kuepusha madhara.
_
Athari zinazoweza kujitokeza ni makazi kuzungukwa maji, ucheleweshwaji wa usafiri na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.
#MillardAyoUPDATES

@millardayo
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Watu wawili wa Familia moja (Baba na Mtoto) wanashikiliwa na Polisi Mkoani Rukwa kufuatia kuwauzia Wanakijiji nyama ya nguruwe ambae alikuwa mzoga na kusababisha Mtoto wa miaka miwili Mariam Peter kufariki Dunia huku Watu wengine 16 wakikimbizwa Zahanati katika Kijiji cha Utengule Wilayani Kalambo, Rukwa .
_
Familia ya Osward Simpungwe ilichinja nguruwe ambae alikufa mwenyewe bila kujua kilichomua na kuuza nyama ambayo iliwaletea madhara walaji.
_
Mtoto Mariam aliumwa tumbo baada ya kula nyama hiyo iliyonunuliwa na Baba yake na akafariki wakati akikimbizwa Zahanati.
_
"Matukio ya kulishwa mizoga yanajirudia mara kwa mara hapa, Serikali ituletee Wataalam wa kukagua nyama kabla ya kuliwa"- Mwanakijiji
#MillardAyoUPDATES

@millardayo
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Faru Fausta ambae amekufa akiwa na miaka 57 anatajwa kuwa ni Faru alieishi kwa miaka mingi kuliko wote Duniani, amekufa akiwa katika banda maalumu alilokuwa amehifadhiwa kwa zaidi ya miaka mitatu kwenye Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
_
Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt Fredy Manongi amesema bado Madaktari wapo kazini kuangalia chanzo cha kifo chake lakini anaamini umri umechangia.
_
"Ni rekodi ya Dunia hatujawahi kusikia Faru ameishi miaka 57 kama huyu, bado Madaktari wanamuangalia ili watuambie chanzo cha kifo chake,ila nadhani ni kifo cha asili na ni kifo cha kusherehekea maana ameishi miaka mingi"-Dkt. Manongi
Full Video ipo YouTube ya 'MillardAyo'
(📹 via @ayotv_)

@millardayo
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM