Mahusiano season๐Ÿ”ž
6.34K subscribers
204 photos
58 videos
14 files
138 links
Karibu katika ulimwengu wa mahusiano hapa tunajadiliana kila kitu kuhusu mahusiano, Utapata simulizi nzuri za kufundisha na kuelimisha,mashairi na mambo mbalimbali yanayohusu maisha yetu ya kila siku

Love Is Life
Live Happiest
Download Telegram
Wanipendeza machoni ninapokutazama,๐Ÿ˜ lanipendeza lako umbo utembeapo kwa madaha โค๏ธ sioni mwingine machoni ila wewe ๐Ÿ˜˜ Ni wewe pekee nikuwazae muda wote ๐Ÿ’ญ Ishi milele katika Moyo wangu
NINAKUOMBA MANANI

Ombi langu la awali,ninakuomba Manani.
Nipe wangu wa halali,niipate afuwani.
Naumwa miye silali,tele mawazo kitwani,na maumivu moyoni.

Ukitoapo kibali,niwe mkewe fulani.
Wito nitaukubali,nitaingia ndoani.
Usiniache Jalali,nikaanguka vitani,nipe wa ndani uoni.

Niepushe nae mbali,mvovu kiumbe shetani.
Nimpende Kila hali,uliyenipa mwendani.
Makosaye nisijali,sihesabu abadani,wala kinyongo rohoni.

Yanizidipo ukali,yakajaa kifuani.
Niondoke afadhali,asinipe kisirani.
Nikatulie pahali,penye upepo wa Pwani,unitibu msongoni.

Tama nisifanye hili,nikawa ja hayawani.
Haki nikamkatili,ya kuishi duniani.
Kwa kuchoma petiloli,mwenza nimwache chumbani,ateketee motoni.

ยฉ Jane David
mwanizuwagrace@gmail.com
Lafanana na asali, tamu yake ama tende
Penzi lako kwangu ghali, Sina budi nililinde
Nakupenda kweli kweli, nakupenda unipende
NIPO HOI JUU YAKO

Mie kwako Sina hali, haki yangu nikugande
Naomba kwa tafadhali, mke wangu chondechonde
Usikae nami mbali, kipenzi usinitende
NIPO HOI JUU YAKO

Maswaibu mbalimbali, yasitufanye tupinde
Tusitoke kwenye reli, wacha furaha tuunde
Wenye chuki na kejeli, kiaina tuwadunde
NIPO HOI JUU YAKO

Mie mpiga kabali, nawe ni kama afande
Nikamate usijali, usiniache niende
Watu wa hasira kali, wasinipige makonde
NIPO HOI JUU YAKO
โœNANI ANAFANYA HIVI KWA RAFIKI YAKE?

ยซู‚ูŽุงู„ูŽ ุงุจู’ู†ู ูˆูŽู‡ู’ุจู: ุณูŽู…ูุนู’ุชู ุจูุดู’ุฑูŽ ุจู’ู†ูŽ ุงู„ู’ุญูŽุงุฑูุซู ูŠูŽู‚ููˆู„ู: ูˆูŽู„ูŽู‚ูŽุฏู’ ุฌูŽุงุกูŽู†ููŠ ุตูŽุฏููŠู‚ูŒ ู„ููŠ ูˆูŽุนูู†ู’ุฏููŠ ุนูุดู’ุฑููˆู†ูŽ ุฏูุฑู’ู‡ูŽู…ู‹ุง ููŽุฃูŽุนู’ุทูŽูŠู’ุชูู‡ู ุชูุณู’ุนูŽุฉูŽ ุนูŽุดูŽุฑูŽ ุฏูุฑู’ู‡ูŽู…ู‹ุง ูˆูŽุจูŽู‚ู‘ูŽูŠู’ุช ู„ูู†ูŽูู’ุณููŠ ุฏูุฑู’ู‡ูŽู…ู‹ุงุŒ ููŽูููŠู‡ูู…ู’ ุงู„ู’ูŠูŽูˆู’ู…ูŽ ู…ูŽู†ู’ ูŠูŽูู’ุนูŽู„ู ู‡ูŽุฐูŽุง ุจูุตูŽุงุญูุจูู‡ูุŸยป

Amesema Ibnu wahbi Allaah amrehemu: Nilimsikia bishr ibnul haarith akisema:

Alinijia rafiki yangu nikiwa na dirhamu ishirini nikampa dirhamu kumi na tisha nikabakisha dirhamu moja kwa ajili yangu,yupo miongoni mwao anayefanya hivi kwa rafiki yake?.


๐Ÿ“šยซุงู„ุขุฏุงุจ ุงู„ุดุฑุนูŠุฉ ูˆุงู„ู…ู†ุญ ุงู„ู…ุฑุนูŠุฉยป (2/ 4):
*โœ ุจู…ุงุฐุง ุชุทูŠุจ ุงู„ุญูŠุงุฉ ู„ู„ุฑุฌู„ ูˆุงู„ู…ุฑุฃุฉ ููŠ ู‡ุฐู‡ ุงู„ุฏู†ูŠุง ุŸ*

_Kwa kitu gani maisha ya mwanaume na mwanamke yanakua mazuri katika hii dunia?_

โ•โ•โ•โ•โ•โ• โโœฟโ โ•โ•โ•โ•โ•โ•

โ–ชู‚ุงู„ ุงู„ุนู„ุงู…ุฉ ุฃุญู…ุฏ ุงู„ู†ุฌู…ูŠ - ุฑุญู…ู‡ ุงู„ู„ู‡ - :

Amesema al-Allaamah AHMAD IBNU YAHYA An-najmy (Allaah Amrehemu)

*- ูุงู„ุฑุฌู„ ู„ุง ูŠุชู… ุญุงู„ู‡ ูˆู„ุง ุชุทูŠุจ ู„ู‡ ุงู„ุญูŠุงุฉ ุฅู„ุง ุจุงู„ุฒูˆุฌุฉ ุงู„ุตุงู„ุญุฉ .*

_Mwanaume hali yake haitimii wala maisha yake hayawi mazuri ispokua kwa kupata mwanamke mwema_

*- ูˆุงู„ู…ุฑุฃุฉ ู„ุง ุชุทู…ุฆู† ูˆู„ุง ุชุทูŠุจ ู„ู‡ุง ุงู„ุญูŠุงุฉ ุฅู„ุง ุจุงู„ุฒูˆุฌ ุงู„ุตุงู„ุญ .*

_Na mwanamke hatulii wala hawi na maisha mazuri ila kwa kupata mwanaume mwema._

ุฃู†ุธุฑ ูƒุชุงุจ ุชุฃุณูŠุณ ุงู„ุฃุญูƒุงู… [ ุฌ- 172/ 4].
Mahusiano ya wapenzi wawili yanatakiwa yawe kma mahusiano ya mkono na jicho,kama mkono ukiumia jicho linalia na kama jicho linalia mkono unafuta machozi..๐ŸŽฏ
"Mwanaume ukitaka kuishi kwa furaha oa unayempenda,Na ukitaka kuishi kwa furaha zaidiiii mpende uliyemuoa".
Naitangazia hadhira

1 Mrefu umbile lake, mwili wanitosha mimi
Meusi midomo yake, ndio hunikosha mimi
Naupenda mwendo wake, mzuri wake ulimi
Natangaza hadharani, nimempenda Aisha

2 Chepesi chake kiuno, mjuvi wa siri zangu
Si mtu wa majivuno, nimempa moyo wangu
Tuwe ja fizi na jino, tuzitoe vangu vangu
Natangaza hadharani, nimempenda Aisha

3 Nimempa kila kitu, vya akhera na dunia
Kisu mekitoa butu, na sijapotea njia
Sita sikiza ya watu, pendo nimetia nia
Natangaza hadharani, nimempenda Aisha

4 Mikono yake laini, ya duara macho yake
Nishayampa maini, hadi figo iwe yake
Anikubalie hani, niwe peke mume wake
Natangaza hadharani, nimempenda Aisha

5 Mtakufa na laiti, nitampenda dawamu
Pendo ninalizatiti, kama Hawa na Adamu
Nimwite hani na switi, anendeshe ja sanamu
Natangaza hadharani, nimempenda Aisha

ยฉ๏ธ Abuuabdillahโœ๏ธ
OMARI JUMA KIMWERI
0744883353
Kilimanjaro Tanzania
Kufanya Mapenzi Ni Moja ya Njia Bora ya Kupunguza Mawazo..
Bad News; Rafiki Zetu Hawatushirikishi Kwenye Michongo, Ila Wanatukumbuka Kwenye Michango.
Nauza mchele safi kabisa kwa bei rafiki kwa kila Mtanzania Tsh 1200 1 kg, Tsh 1300 1kg na Tsh 1500 1kg Napatikana MOSHI KILIMANJARO Mbuyuni barabara ya masai kona mawasiliano 0744883353

Mama lishe pia wakaribie sana tuna utaratibu maalum kwa ajili yao
Tunafanya na delivery
Official dating site page welcome All

Ni free kwa sasa

Huduma safi kwa vigezo hitajika na faragha yetu ni ya kiwango cha juu baina yetu na mteja wetu
Mahusiano season๐Ÿ”ž
Karibu katika ulimwengu wa mahusiano Hapa tunatatua changamoto za mahusiano kwa pamoja
https://t.me/mahusianoseason


Official dating site page welcome All

Ni free kwa sasa

Huduma safi kwa vigezo hitajika na faragha yetu ni ya kiwango cha juu baina yetu na mteja wetu
....SIWAWEZI....
1
Leo nasema ukweli,unitokao moyoni...
Ningasemwa si rijali,katu siipingi dini..
Niliyawaza awali,ila hali yangu duni...
Siwezi wake wawili,kwa wangu umaskini!

2
Nna hamu kweli kweli,niingie mathinani...
Wanipe raha a'ali,wakiwepo mitalani...
Ila hali sio hali,nalikiri siwezani...
Siwezi wake wawili,kwa wangu umaskini!

3
Wallahy nimekubali,mmoja abaki ndani..
Wa moja hapati mbili,hili nimeliamini...
Lilinizuga akili,ila sasa sitamani...
Siwezi wake wawili,kwa wangu umaskini!

4
Zingelinitosha mali,mihela mamilioni...
Ningelijitosa Ali,mbili nikaziauni...
Nna uwezo wa mwili,tiba wangepata sini...
Siwezi wake wawili,kwa wangu umaskini!

5
Sitaki nije wadhili,niambwe ni limbukeni...
Mmoja kuwa sahali,naridhika suduruni...
Mana sina afadhali,ntakuja wapa nini!?. .
Siwezi wake wawili,kwa wangu umaskini!

6
Kama swala ntaswali,na funga za Ramadhani...
Zaka mithili mithili,kutoa sioni kani...
Ila hizi nyumba mbili,itakuwa mtihani....
Siwezi wake wawili,kwa wangu umaskini!

7
Tama ya yangu kauli,nalisema kwa yakini...
Uchochole ndo usuli,nisingie kufuruni...
Siwezi hili na hili,kila nikitathmini...
Siwezi wake wawili,kwa wangu umaskini!
##
Ali Salim Masito

MUDIRI

#Mraibu_wa_tungo
*TUJIFUNZE KIDOGO KUHUSU HIZI LINKS NA EMAILS*

*โœ๏ธKwanza naomba nianze na maana ya hizi htpp:// na htpps://*

*โœ๏ธhtpp://๐Ÿ‘‰๐Ÿผ hii ambayo haina (s) mwishoni yaani http: hiyo hufahamika kama (hypertext tansfer protocol, hiyo kitaalamu Ni search engine inayotumika kutafuta au kukupeleka kwenye website fulani Sasa Ukiona umetumiwa link na imeanza na http: bila (s) mwishoni basi ujue hiyo sio salama*

*โœ๏ธHiyo (s) inakazi yake kubwa sana ambayo ni ulinzi wa taarifa kwa anaye bofya link*

*โœ๏ธhttps: maana yake ni (hypertext transfer protocol secure).....hapo utaona hiyo (s) kazi yake ni (secure) yaani ulinzi*

*โœ๏ธSasa links zote ambazo zina (http:) na siyo (https:) hizo zina viruses kwa lengo baya kwako*

*โœ๏ธHizi Links huwa zinatengenezwa kwa sababu mbalimbali na sababu kuu ikiwa ni kudukua (ku-hack) taarifa za watu*

*โœ๏ธNa kwakuwa watu wanapenda vitu vya bure na rahisi basi huwa wanaandika utapewa zawadi pale utakapowatumia watu hiyo link*

*โœ๏ธSasa ukibonyeza hiyo link unaweza ukaambiwa weka namba zako za simu au email yako*

*โœ๏ธUkiweka hizo taarifa zako basi wao wanaweza kuchukua taarifa zako na kuweza kufuatilia mawasiliano yako au kukuibia pesa zako kwenye account zako zakifedha*

*โœ๏ธNa Kama ulitumiwa link yenye (htpp:) kwenye Facebook au Instagram au mtandao mwingine wakijamii na ukabofya hiyo link maana yake HIYO ACCOUNT YAKO TAYARI WAMEISHIKILIA NA WAKATI WOWOTE WAKIAMUA WANAWEZA KUICHUKUA AU KUTUMA KITU CHOCHOTE KWENYE ACCOUNT YAKO*

*MUHIMU*

*โœ๏ธEmail za kweli inapoandikwa, huwa likitoka jina la kampuni ndio linafuata neno kama vile (@gmail.co)*

*โœ๏ธMfano Ukiona imeaandikwa (Coca-Cola@gmail.com) basi hiyo link ni ya Coca-Cola, lakini ukiona imeandikwa (Coca-Cola.money@gmail.com) hiyo email ni ya uongo, hivyo email ya kweli ni lazima ianze jina la kampuni au jina la mtu ndipo ifuate ile (@gmail.com) Ukiona umeandikiwa jina la kampuni halafu yakafuata maneno mengine, halafu ndio (@gmail.com), basi tambua huo ni wizi, mfano hata link ikiwa hivi๐Ÿ‘‰๐Ÿผ (www.amazon.com), hiyo ni sahihi kwasababu Amazon ndio kampuni na ndio wamiliki wa link website hiyo hivyo kivyovyote vile taarifa zako ziko salama lakini ukiona (www.amazon.wd.com) hiyo sio yakweli maana tayari kuna vitu vimeongezewa hapo mbele*

*โš ๏ธKampuni zote zinafahamu wateja wake zikitaka kutoa offer basi zitawafuata kupitia taratibu zao na sio kutuma links zenye viruses*

*ASANTENI NAAMINI TUMEJIFUNZA KITU*
Kuna mtu aliye katika kikundi moshi naomba kuzungumza nae
KUPENDA USIPO PENDWA

1 Nikimpigia simu, hataki kuipokea
Natamani kunywa sumu, kwa anavyo nifokea
Kumbe kupenda kugumu, ndivyo inanitokea
Ni kubwa sana adhabu, kupenda usipo pendwa

2 Kosa alifanya yeye, na radhi niombe mimi
Dunia yangu na yeye, sasa tumekuwa kumi
Yamini mekula naye, afe yeye au mimi
Ni kubwa sana adhabu, kupenda usipo pendwa

3 Kwa wengine yuwacheka, tena kwa furaha tele
Kwangu yuwakasirika, na kuwa mwingi wa kele
Pendo langu la viraka, na maudhiko belele
Ni kubwa sana adhabu, kupenda usipo pendwa

4 Jumbe zangu hazijibu, ingali yuwazisoma
Nimegeuka bawabu, imenishika na homa
Kupenda kwani adhibu, na nimekuwa kilema
Ni kubwa sana adhabu, kupenda usipo pendwa

ABUUABDILLAHโœ๐Ÿฝ
jumaomari5@gmail.com
0744883353
MOSHI, TANZANIA
18/09/2021
Audio
Audio from Abuuabdillah
WEWE NDIE UPENDAE.

Kwanza ninakupa pole, kwayako mahuzuniko,
Mungu kakupa upele, halafu kucha sizako,
Naomba tizama mbele, acha nyuma utokako,
Wewe ndie upendae, hana habari mwenzako.

Kitambaa ulikata, hukuujua mshono,
Fundi ulie mpata, ukamlipa vinono,
Sasa kwako nisakata, paguu kashona kono,
Wewe ndie upendae, hana habari mwenzako.

Tia kiraka uzibe, usitiri utuwako,
Kula mwenzangu ushibe, haya siyapeyako,
Wengi washanyea debe, tuliza hasira zako,
Wewe ndie upendae, hana habari mwenzako.

Japo huwa nivigumu, ndege kuhama kiota,
Ila ikimlazimu, hasubirii kutota,
Ukisha kwisha msimu, wachumao huokota,
Wewe ndie upendae, hana habari mwenzako.

Hakuna gumu milele, tia pamba masikio,
Usisikie kelele, wala kwikwi za vilio,
Daima tizama mbele, yanyuma sema weleo.
Utashinda majaribu, yanayo kufika leo.

MWINYI HAMAD
@Rais Mwinyi
Zanzibar.