Mahusiano seasonπŸ”ž
6.28K subscribers
200 photos
58 videos
14 files
138 links
Karibu katika ulimwengu wa mahusiano hapa tunajadiliana kila kitu kuhusu mahusiano, Utapata simulizi nzuri za kufundisha na kuelimisha,mashairi na mambo mbalimbali yanayohusu maisha yetu ya kila siku

Love Is Life
Live Happiest
Download Telegram
Shairi ::: Kigoma ni mashuhuri


1 Naikujuza khabari, zatoka huko kunani
Jiji hilo mashuhuri, kote huko duniani
Ni ukweli sio zuri, mji 'lojawa amani
Kigoma ni mashuhuri, lakini si kama Tanga

2 Halitaki na dalili, sifazo hazifanani
Daa kunayo madili, huko hayaonekani
Mji huo ni jalili, ukaone kwa yakini
Kigoma ni mashuhuri, lakini si kama Daa

3 Sendi hapa ninakifu, hii ni yangu mitaa
Huo ni mji nadhifu, watalii waja shang'a
Arusha nina isifu, na hapa ndio nakaa
Kigoma ni mashuhuri, lakini si ja Arusha


©Abuuabdillah ✍
0744883353
Arusha -- Tanzania
Kigoma ni mashuhuri katika gazeti la mwananchi
Shairi ::Kuvanga sasa tamati

1 Sina wakunituliza,akili kuchangamsha
Moyo akaubamiza, kilele kunipandisha
Ahadi kuzitimiza, sio kunipa hadaa
Yukupi ajitokeze , kuvanga sasa tamati

2 Mawazo tele kitwani , mambo yako vangu vangu
Nasfi ikomatatani , hima aje awe wangu
Nimpe yake thamani, la kwake likawa langu
Yukupi ajitokeze , kuvanga sasa tamati

3 Ninapata wasi wasi, matungu yaniandama
Nitaupata ukwasi, yasije kwenda mrama
Mimi bado ni mwepesi, naiogopa mitama
Yukupi ajitokeze,kuvanga sasa tamati

4 Hapa nifike tamati, nimeuchoka useja
Nipikiwe kalimati,ningali ninamngoja
Utafika tu wakati, 'tamke zile lahaja
Yukupi ajitokeze,kuvanga sasa tamati


OMARI JUMA KIMWERI
©Abuuabdillah ✍
0744883353
jumaomari5@gmail.com
ARUSHA = TANZANIA
1 Moyo naomba tulia
Sitaki kukulilia
Acha kuyakimbilia
Mapenzi yataka pesa

https://ujuzipesa.com/2020/02/03/mapenzi-yataka-pesa/
Mwanamke ni mtu muhimu katika maisha ya mwanaume hakika mambo hayaendi bila uwepo wa mwanamke na hii ni kwa sababu Mungu ametuumba hivyo na ametuwekea mwanamke kuwa sababu ya utulivu na msaidizi kwa mwanaume


Wasichana wengi wapo njia panda baada ya kuona mambo yanaenda tofauti na wanavyodhani wao kuhusu ndoa.

https://ujuzipesa.com/2020/02/06/kila-mwanaume-anahitaji-mwanamke-wa-aina-hiii/

*Sambaza kwa jamaa na marafiki iwafikie wengi zaidi*
Ninayo mazonge mie

1 Nimefukuzishwa kazi
Wala sinayo makazi
Ja dafu haliwi nazi
Ninayo mazonge mie

2 Namuhitaji tabibu
Amekimbia muhibu
Kaniachia ububu
Ninayo mazonge mie

3 Njaa menilaza chali
Imenidhoofu hali
Oh usiku silali
Ninayo mazonge mie

4 Mawazo tele kitwani
Sina kitu uko ndani
Ni mweupe mfukoni
Ninayo mazonge mie

5 Nipe njia ya Karima
Sina shamba nikalima
Kutwa nalishika tama
Ninayo mazonge mie

6 Nitachezaje kisasa
Sinayo tena hamasa
Nani wa kunitomasa
Ninayo mazonge mie

7 Nani anipe msa'da
Kwangu aje iwe ada
Nipate wangu kimada
Ninayo mazonge mie

8 Yamewaka kibatari
Yani mambo furi furi
Mola nitoe kiburi
Ninayo mazonge mie

9 Nikusanye masalali
Nipate wangu kimwali
Asitake zangu mali
Ninayo mazonge mie

10 Yaani nina mazonge
Ati dawa ni mronge
Au shingo niinyonge
Ninayo mazonge mie

11 Naona kizungu zungu
Yani kote vangu vangu
Umenijaa ukungu
Ninayo mazonge mie

12 Natoka kwangu baiti
Kumfuata banati
Nimekipigwa kibuti
Ninayo mazonge mie

13 Niko juu ya makuti
Niwasheni kibiriti
Nikaketi kwenye kiti
Ninayo mazonge mie

©️Abuuabdillah✍🏾
Omari Juma Kimweri
0744883353
Arusha -- Tanzania
www.ujuzipesa.com
Namtafuta mchumba


1 Hodi naleta maombi, ya uchumba
Hapa niiweke kambi, na kulimba
Nile za maziwa tambi, nina sumba
Namtafuta mchumba, ajilani


2 Barua hii iwazi ,isomeni
Na awe yangu saizi, mleteni
Wajulisheni wazazi, dalihini
Namtafuta mchumba, ajilani

3 Rangi sitazichagua, auswadi
Na wala sitamgua, niafidi
Nami nitamchungua, nifaidi
Namtafuta mchumba, ajilani

4 Kiuno kiwe dondora, ajimali
Abadi sitamsora ,mi hamali
Anivalie na gora , ni ulili
Namtafuta mchumba, ajilani

5 Niufunge ukurasa, wa kitabu
Awe banati kisasa, sitasubu
Kwake yeye 'tajinasa, niwe dubu
Namtafuta mchumba,ajilani


©️Abuuabdillah✍🏾
Omari Juma Kimweri
0744883353
Arusha -- Tanzania
*SIMULIZI ::: NILIMUOA MWANANGU*

*MTUNZI ::: ABUUABDILLAH*

*Sehemu ya kwanza*

Naitwa Joseph Bahati Kiluwa ni mkazi wa Arusha, nina miaka 72.
Baada ya kumaliza elimu yangu ya chuo nilienda kuishi kwa mjomba wangu aliyekuwa anaishi mkoani Mwanza, sikuwa na kazi kwa wakati huo hivyo mjomba wangu alinitafutia kibarua nisikae nyumbani, nilifanya kazi katika duka moja la jumla, sikuchagua kazi, nilijua fika ajira zitakapo toka nitaajiriwa sikuwa na shaka na hata pesa zangu nilizitumia zaidi katika starehe sababu hazikuwa za malengo kwa wakati huo.

Baada ya miezi 6 nilihama kwa mjomba na kupanga chumba changu mwenyewe ili niwe na uhuru wa kufanya starehe zangu kwa uhuru zaidi, nilipata marafiki wa kunionyesha maeneo mengi ya Mwanza ambayo sikuwa nikiyafahamu, nikawa mwenyeji katika jiji hilo lenye kona tamu za starehe ukiwa na pesa, nilitembea na wanawake wengi walionipendeza katika macho yangu sikujali lolote niliwatumia na kuwaacha.

Kuna msemo maarufu wa waswahili husema "kila jini lina mbuyu wake" nami nikapata mbuyu wangu ni binti aliyeukonga moyo wangu hakika kwakwe nilishikika ana sifa zisizo elezeka , Neema ndio ! kweli alikuwa na neema kwangu kama jina lake. Neema alifanya kazi katika hotel kubwa kakatika jiji hili, sikupenda kazi ya Neema na nikamshauri aache kazi aje tuishi wote jambo lililokuwa gumu sana kwa Neema kulikubali, " Jose unataka niwe mtumwa wa mapenzi kwako niache kazi nitaishi vipi na hali ya maisha si unaiona "
Inamaana huniamini ? au unadhani sina uwezo wa kukutunza "sio hivyo mume wangu nitaacha ila kwa sharti kama utakubali nitaacha " .....

Itaendelea sehemu ya pili

Omari Juma Kimweri
Arusha -- Tanzania
0744883353
*SIMULIZI :: NILIMUOA MWANANGU*

*SEHEMU YA PILI*

Ilipoishia ..
Jose unataka niwe mtumwa wa mapenzi kwako niache kazi nitaishi vipi na hali ya maisha si unaiona "
Inamaana huniamini ? au unadhani sina uwezo wa kukutunza "sio hivyo mume wangu nitaacha ila kwa sharti kama utakubali nitaacha " .....

Endelea nayo ...



Sharti gani !! nilisema kwa kuhamaki , ghafra akanikumbatia na kunibusu mdomoni na kunihemea sikioni mwangu huku akisema kwa sauti ya kuchombeza " mume unajua nakupenda sana hata mimi sitaki kuwa mbali na wewe ila naogopa je ukiniacha na kwetu hujajitambulisha nitaishi vipi nikiwa sina kazi ? nimekubali kuacha kazi ila sharti langu nifungulie biashara " nilimjibu kwa sauti nzito ya huba, aah kumbe ni sharti hilo tu, ni wazo zuri sasa we tafuta eneo angalia na biashara gani utafanya.

Baada ya week 3 nilimfungulia Neema duka kubwa la kuuza nguo za mitumba halikuwa kubwa saana lakini kwa mtaa huo hakukuwa na duka la kushindana na duka la Neema. Nilitumia akiba yangu yoote kuwekeza dukani kwake mpaka sikubakiwa na kitu chochote sikuwa naweka akiba pesa nyingi, pesa ilishia kwenye kula na starehe ndogo hazikuwa kubwa sana kipato kilikuwa kidogo
Ilikuwa asubuhi ya jumatatu nilienda kwenye Internet cafe kuangalia jina langu katika ajira mpya zilizotolewa na serikali nilipata mshangao sikuliona jina langu katika orodha ya waajiriwa wapya, hili liliniumiza sana. Malengo yangu yalikuwa makubwa sikuona yakikamilika kwa kazi ninayoifanya sasa hainipi kipato kikubwa niliwaza sana sikupata majibu

"Honey mbona leo haupo kama kawaida yako umepoa sana umefukuzwa kazi ??" Neema aliniuliza kutokana na jinsi nilivyozama katika dimbwi zito la mawazo nisijue la kufanya nikamjibu kwa sauti ya kinyonge sana vipi na biashara inaendeleaje "Biashara imekuwa ngumu kidogo mzigo hautoki sana kama mwanzo ila nataka nitafute vijana wanisambazie mzigo unaobaki ili niweze kusambaza mzigo mpya kwa haraka " ni wazo zuri mke wangu niwekee maji ya kuoga bafuni, siku hii ilikuwa siku mbaya kwangu nimeanza kuwaza maisha mapya ya baadae kwa kazi ya kipato cha chini kama hiki.
Fedha ya Neema haikuingia katika matumizi ya nyumbani na hivyo vitu nilitumia pesa yangu kununua hata chumvi hakutoa pesa ila aliomba kwangu mpaka sikuona haja ya yeye kuwa na biashara ambayo mtaji pia unatoka kwangu hata ukipunguwa

Nikiwa kazini nilipigiwa simu na rafaki yangu niliesoma nae chuo alinipa habari ya kunibadilisha kidogo

"Haloo Josee unaongea na Rasuul hapa" ,ooh Rasuul za masiku ndugu yangu umepotea hutaki ata kunisalimia "nipo ndugu mambo yamekuwa mengi saana na huku kijijini kwetu mtandao unasumbua leo ndio nimekuja mjini ... ajira zimetoka sijaona jina langu wala la kwako je wewe umefuatilia ?? " Ndio nilifuatilia kupitia mtandao ila sikufanikiwa kuona majina yetu "tumekosa ajira tuangalie jinsi gani ya kuendesha maisha yetu na kama utakuwa huna ramani nzuri ya kueleweka nitafute, mimi naishi Mombo mkoa wa Tanga nitakupa ramani " baada ya kuongea hivyo Rasuul alikata simu hakusubiri jibu langu daah mambo yameenda kinyume kabisa na matarajio yangu. Nilishindwa kuendelea na kazi nilibaki njia panda niende njia gani, "Kipenzi changu nina taarifa njema nimetoka hospital kupima si unajua sijaona siku zangu yapata miezi miwili sasa mimi ni mjamzito jiandae kuitwa baba na pia naomba uwahi kurudi tuongee kuhusu mipango ya mtoto " Taarifa hii ya mimba ya Neema iliniduwaza sana sikumjibu zaidi ya kukata simu nikijuliza maswali mengi kichwani. "huyu mwanamke hana akili eeh tutapanga nini na hela zote anachukua yeye, au kaniroga ? lakini ngoja nitamuonyesha hanijui huyu naona ananitawala " ni mawazo niliyokuwa nikiwaza sikuwa na pesa sikuwa na kazi ya kueleweka mtoto ataishi vipi ? nilipata wazo. "Mbona Rasuul kama alijua tutakosa ajira hakuwa na wasi wasi katika maongezi yake kama anajiamini hivi, mhmh yule mshamba vile na upole wake atakuwa na ramani gani ya hela nyingi ? nitampigia jioni"

We kijana subiri "mbona hamlipi pesa yangu kwa wakati ninao taka ile sio nyumba yenu kama hamna pesa ondokeni niweke wapangaji wengine
" ni baba mwenye nyumba wangu aliongea kwa ukali sana "hata umeme wapangaji wenzenu wanasema mnalipa kwa usumbufu hivyo basi nipeni kodi yangu ya miezi 3 msipoweza hameni kwaheri " lakini lakini mzee "aah ondokeni sitaki shida zenu kwangu mkitaka amani lipa pesa yangu tena nawapeni ofa mkiondoka sitawadai chochote " nilisimama nikiwaza mambo yanavyoingiliana kichwa kilipata moto ama kweli uanaume ni mateso.

Itaendelea sehemu ya tatu


Mwandishi/Mtunzi :: Abuuabdillah
Omari Juma Kimweri
0744883353
jumaomari5@gmail.com
Wanawake wengi hawajui kulea

nitakuelezea hili baadae
SIMULIZI :: NILIMUOA MWANANGU

SEHEMU YA KWANZA, PILI NA YA TATU
https://ujuzipesa.com/2020/02/23/simulizi-nilimuoa-mwanangu/
NAUKODISHA UPENDO
1 Njoooni njoooni
Nawaita uwanjani
Jamaa nisikizeni
Naukodisha upendo

2 Fununu nazifunua
Ua limeshachanua
Au wataka nunua
Naukodisha upendo
https://ujuzipesa.com/2020/02/23/naukodisha-upendo/
#MWANAMKE_ANAIJUA_THAMANI_YAKE_KATIKA_JAMII !??

Ikiwa Leo ni Siku ya wanawake duniani kwako wewe unaesoma makala hii
Nitakuuliza haya maswali ambayo sitakupa majibu ila utajijibu wewe katika nafsi yako
Kaka unaesoma ujumbe huu muulize mke wako au mpz wako maswali haya na ayatafakari kupata majibu
1⃣ πŸ‘‰πŸ½ Nini kusudi la mwanamke kuwepo duniani ??
2βƒ£πŸ‘‰πŸ½ Thamani ya mwanamke ni nini ??
3βƒ£πŸ‘‰πŸ½ Jamii inamuhitaji mwanamke kwa kias gani ??
4βƒ£πŸ‘‰πŸ½ Ni ipi nafasi ya mwanamke katika Mapenzi ??
5βƒ£πŸ‘‰πŸ½ Kwa nini thamani ya mwanamke inapotea katika jamii na kuonekana wa kawaida ??
Leo ni wazi kwamba mwanamke Amepoteza thamani katika jamii na hili ni kutokana na yeye mwenyewe kutofahamu thamani yake na kuishi nje ya kusudio lake
Jamii zetu Leo zimeharibika kwa sababu mwanamke kaondoka katika nafasi yake
Mwanamke akirudi katika usawa wake dunia itapata utukufu
Nimalizie kwa kukuambia maneneo haya
Daima huwezi kuwa bora kwa kukaa nafasi ya mtu mwingine
Huwezi kuwa bora kwa kudharau wengine

Imeandaliwa na
Abuuabdillah
0744883353
Channel name was changed to Β«Mahusiano seasonπŸ”žΒ»
SHAIRI :: MAKINIKA UTAPATA
JIBU KWA DR SAUL KALIVUBHA ( nitapataje mkamilifu)



1 Yakaribie maziwa, nasaha nitazikupa
Na mikono yako nawa, wala usiwe na pupa
Uwaweza kuchaguwa, ila uwapata dupa
Wakamilifu wapapo, makinika utapata

2 Ukiingia ndoani, ufanye kujihafadhi
Si ujuzi tu chumbani, bali uchunge lafudhi
Usiweke hadharani, shaini lenda kwa kadhi
Wakamilifu wapapo, makinika utapata

3 Itoe yako aibu, utampata kisura
Uende kwa taratibu, muweze kuifanya gura
Mdomo usiwe bubu, msemeze yule Sara
Wakamilifu wapapo, makinika utapata

4 Wamekithiri wabora, waliofundishwa kazi
Punguza wako ukora, utajionea wazi
Kisha na uwe imara, ufuatishe wazazi
Wakamilifu wapapo, makinika utapata

5 Wazuri waona wengi,na kesha walo sifika
Kama Fatuma haringi, ijapo umemruka
Weye ingali ni Kingi, chunga usijipe buka
Wakamilifu wapapo,makinika utapata


©️Abuuabdillah✍🏾
+255744883353
Arusha -- Tanzania
https://ujuzipesa.com/2020/03/26/mwanamke-ni-nani-mjue-hapa/

Mwanamke ameumbwa katika ubavu wa mwanaume kama yasemavyo maandiko matakatifu na baada ya kuumbwa akafanywa kuwa mlezi na msaidizi. Mwanamke ni kiumbe wa pekee katika ulimwengu wa dunia hii ni mtu muhimu kuliko wengi wanavyofikiri.....
Kuanzia sasa tutakuwa na group rasmi kwa hapa Telegram hivyo bhas kama unaswali karibu sana