Chakushangaza
4.69K subscribers
4.94K photos
168 videos
36 files
956 links
Njootukujuze tukushangaze tukuelimishe tuulishe ubongo wako madini

CHANNEL ILIANZISHWA RASMI MNAMO 11/06/2019
Download Telegram
#CHAKUSHANGAZA
Njia ya mafanikio haijawahi kua rahisi,wakati unatafuta mafanikio kudharauliwa na kuonwa kama usiyejituma ni kati ya vitu vinavyochochea wewe kupambana ili waone juhudi zako. Wanatudharau tukiwa hatuna kitu na tukipata waanza kutuonea wivu na choyo tukiongeza juhudi wanaanza kutupiga vita wakidhani tunashindana nao ilihali sie tunapambana kuitengeneza kesho yetu.Inaumiza sana kuona wale waliokua wakiona hatuna umuhimu na tumebweteka tulipo kua hatuna kitu na saivi tumepata cha kufanya wamegeuka kutuombea tukose kile tulichonacho ili tubaki katika hali ile ya mwanzo,tunashindwa kuelewa kipi kinawafurahisha wao kwetu je ni sisi kua juu au tuzidi kua chini tubaki kuwalamba miguu wao?.Ni ngumu sana kumridhisha binadamu muhimu ni kumheshimu kila aliyekaribu nawewe lakini sio kujitahidi kumfurahisha au kumridhisha kwani katu hutaweza kumridhisha maana binadamu hatayeye mwenyewe ameshindwa kujiridhisha. Pia kumbuka mtaji mkubwa wa kua masikini ni kujitahidi kumridhisha kila mtu, fanya kilicho sahihi,jihedhimu,waheshimu,omba Mungu na zidisha juhudi waseme ...wasiseme.. we endelea ...

Ukibahatika kufanikiwa katika jambo fulani jitahidi sana kumwomba Mungu akupe hekima ya kulipokea hilo jambo maana wapo watu wengi waliobahatika kupata walichotarajia kwa wakati sahihi kwao na baadae wakageuka nyuma nakuanza kuwasimanga wale waliochekewa kufanikiwa au kupata jambo wanalopigania.Unajisifu wewe hujawahi kufeli katika mipango au masomo yako na unafikia hatua ya kubeza wenzio walioshindwa kufaulu, swali je umewshi kumuuliza aliyefeli ni nini kilimfanya afeli?...Kuna watu licha ya kufeli kwao lakini juhudi zao zikikua kubwa kuliko hata wewe uliyefaulu maana waliyokumbana nayo ungekua wewe pengine hata nguvu ya kuingia kwenye chumba cha mtihani usingepata. Mshuukuru mungu kwa ulichopata na waombee wanaoendelea kukitafuta Mungu awakumbuke hakuna ajuaye nini mwenzie anakipitia,wapo wengine wao ndio nguzo ya familia na hata ukoo kila anachokipata anagawana na ukoo unadhani huyo atakua sawa na wewe unayepata chako na unatumia mwenyewe na kuna wakati hata unaongezewa na nduguzo....!!!!!..? By admin @benlaysh
Nilileta wazo la kusaidia wenye shida mbalimbali ila nkatumia jina la Çhakushangaza foundation kwani nilitamani kusaidia huko kusiwe na mipaka tuguse kila engoo katika maisha ya watu,,,,,,siwez jilaumu kwa hilo kwa kufikiria hilo ila najilaumu huenda nilitumia njia mbaya kuelezea hilo,,,,!! Tuliombwa tukajiunge kwa lile grupu ila tupo 5 ad saiiv,,,
Sjui why ila s vyema kumsemea mtu,,,nimeona niandike tu ili tukumbushiane tu,,,huenda kuna wazo jinginee zaid ya hili la kutoa msada unaweza lileta pia ili tusiwe watu wa kuachiwa vitu vya kumbukumbu kwamba Pele kacheza mpira hatare wakati hata sisi twawez acha alama iishiyo milele kwamba kundi letu liliweza saidia mamia kwa mamia na baraka zikatawala kwetuu hvyo niwaombe,,,,tushiriki sotee,,,mawazo ushauri njia gani tutumie vinahitajika anii,,,,,,huenda nakosea ila daaah nisameheni tuu!


Kwa aliye tayari njoo gusa link hii ujiunge nasi
T.ME/Chakushangazafoundation
Tunao umoja wetu wenye lengo la kutoa misaada kwa wenye uhitaji hivyo kama unatamani kuungana nasi karibu gusa hapo
t.me/chakushangazafoundation
#chakushangaza
Chakushangaza
#CHAKUSHANGAZA KAMA ULIKUWA HUJUI...... Zaidi ya watoto elfu ishirini (20000) wanafariki kila siku kutokana na umasikini Hivyo jifunze kusaidia wenye uhitaji Kama una watoto wawili unaweza ukachukua mtoto mmoja mwenye uhitaji na kumlea MUNGU ATAKULIPA…
#CHAKUSHANGAZA
KAMA ULIKUWA HUJUI......

Zaidi ya watoto elfu ishirini (20000) wanafariki kila siku kutokana na umasikini

Hivyo jifunze kusaidia wenye uhitaji

Kama una watoto wawili unaweza ukachukua mtoto mmoja mwenye uhitaji na kumlea MUNGU ATAKULIPA APENDAVYO YEYE


Tunao umoja wetu wenye lengo la kutoa misaada kwa wenye uhitaji hivyo kama unatamani kuungana nasi karibu gusa hapo
t.me/chakushangazafoundation
#chakushangaza
Tunao umoja wetu wenye lengo la kutoa misaada kwa wenye uhitaji hivyo kama unatamani kuungana nasi karibu gusa hapo
t.me/chakushangazafoundation
#chakushangaza
Tunao umoja wetu wenye lengo la kutoa misaada kwa wenye uhitaji hivyo kama unatamani kuungana nasi karibu gusa hapo
t.me/chakushangazafoundation
#chakushangaza
Tunao umoja wetu wenye lengo la kutoa misaada kwa wenye uhitaji hivyo kama unatamani kuungana nasi karibu gusa hapo
t.me/chakushangazafoundation
#chakushangaza
Tunao umoja wetu wenye lengo la kutoa misaada kwa wenye uhitaji hivyo kama unatamani kuungana nasi karibu gusa hapo
t.me/chakushangazafoundation
#chakushangaza
RONALDO EFFECT

Nguvu ya Cristiano Ronaldo kwenye mitandao ya kijamii haimithilika.

Kuna muhuni mmoja kutoka Saudi Arabia 🇸🇦 amepost YouTube bao la kwanza la Cristiano Ronaldo akiwa katika klabu yake mpya ya Al Nassr.. Video hiyo ya mchongo ambayo ukiifungua hukuti hilo goli tayari imefikisha VIEWS 12 Milioni ndani ya saa 20 pekee !😮

IKUMBUKWE ;
Cristiano Ronaldo hajacheza mchezo wowote mpaka sasa katika klabu yake mpya ya Al Nassr analazimika kukaa nje ya pitch akitumikia adhabu ya kutocheza mechi mbili aliyoipata ikiwa England 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿

📌 Kabla ya kuhusishwa kujiunga na klabu ya Al Nassr, klabu hiyo ilikuwa na followers wasiozidi 400k (laki 4) Instagram,, Yaani wafuasi wachache wakizidiwa hadi na klabu ya Azam football club ya Tanzania 🇹🇿

Baada ya CR7 kuhusishwa na klabu hiyo followers wakapanda hadi 860k, yaani laki (8).. Alipotangazwa rasmi kasajiliwa, hivi sasa baada ya siku (5) kupita followers wamefika MILIONI (10) 😮

Al Nassr imeweka rekodi Duniani kuwa klabu iliyopata followers wengi ndani ya muda mfupi...Kutoka kuzidiwa followers na Azam fc hadi kuzizidi followers kwa muda mfupi tu klabu hizi kubwa Duniani zilizosota kwa muda mrefu kupata followers hao !!

Ronaldo Effect 🙌

10.0 Milioni - 🇸🇦 Al Nassr

9.1 Milioni - 🇪🇬 Al Ahly
8.8 Milioni - 🇮🇹 Inter Milan
8.3 Milioni - 🇹🇷 Fenerbahce
7.9 Milioni - 🇳🇱 FC Ajax
7.1 Milioni - 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Leicester city.
7.4 Milioni - 🇦🇷 Boca Juniors
6.9 Milioni - 🇦🇷 River plates
5.2 Milioni - 🇮🇹 AS Roma
3.3 Milioni - 🇮🇹 Napoli
2.8 Milioni - 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Everton
2.4 Milioni - 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Astonvilla
1.9 Milioni - 🇪🇸 Sevilla

Nk .......

NB ; Cristiano Ronaldo ndiye binadamu mwenye wafuasi wengi zaidi kwenye mitandao ya Instagram na Facebook Duniani.

529 Milioni - Instagram
159 Milioni - Facebook


Tunao umoja wetu wenye lengo la kutoa misaada kwa wenye uhitaji hivyo kama unatamani kuungana nasi karibu gusa hapo
t.me/chakushangazafoundation
#chakushangaza
Chakushangaza
#CHAKUSHANGAZA JAMBAZI MTUKUTU. Nchini Tanzania, kuna manju 'Dj' fulani wa muziki anayejulikana kwa jina maarufu la 'DJ JD' au kwa kirefu *'DJ John Dilinga'.* Huyu ni moja kati ya maDj wakongwe na mahiri sana tuliobahatika kuwa nao hapa nchini Tanzania.…
#CHAKUSHANGAZA
JAMBAZI MTUKUTU.

Nchini Tanzania, kuna manju 'Dj' fulani wa muziki anayejulikana kwa jina maarufu la 'DJ JD' au kwa kirefu *'DJ John Dilinga'.* Huyu ni moja kati ya maDj wakongwe na mahiri sana tuliobahatika kuwa nao hapa nchini Tanzania. Kwa wale wapenzi na wadau wa muziki wa 'bongofleva' hususani wa miaka ya nyumanyuma kidogo, bila shaka mtakua mnamfahamu Dj huyu.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikitamani kufahamu ni kwanini anaitwa John Dilinga..nikiwa nataka kujua kama hilo ni jina lake halisi au ni 'a.k.a'. Maana ni kawaida kuona watu mbalimbali hususani walio kwenye tasnia ya burudani wakitumia majina ya ziada (a.k.a) kuliko majina yao halisi.

Kitu kilichonifanya nianze na DJ JD ni baada ya kugundua kuwa tarehe 22 Julai. Tarehe ambayo ulimwengu mzima unamtaja bwana mmoja mtukutu sana, aliyewahi kusumbua vichwa vya maofisa usalama wa nchi ya Marekani, akifahamika kama *John Dillinger.* Huyu alikuwa ni moja kati ya wahuni wakubwa nchini Marekani aliyetamba sana katika miaka ya 1930 kwa kujihusisha na matukio ya kihalifu hususani uporaji wa fedha kwenye mabenki.

Tofauti ni kwamba John Dilinga wa Tanzania ni DJ, wakati John Dillinger wa Marekani alikuwa ni jambazi mtukutu.

Utukutu wake ulianza angali ana umri mdogo na hata aliweza kuacha shule ili kwenda kutafuta pesa!! Alianza kama mdokozi wa vitu vidogovidogo lakini tukio lake la kwanza lilikuwa ni *kuiba gari*, kisha 'kwenda misele' kwa mpenzi wake mpya. Siku chache baadae alikuja kukamatwa na mapolisi akiwa anazurula mtaani japokuwa alifanikiwa kuchoropoka na 'kutokomea kusikojulikana'.

Baadae alipata kazi katika jeshi la majini 'navy', akifanya katika meli ya jeshi ya 'USS Uttah'. Baada ya miezi kadhaa John Dillinger alitoroka kazini.

April 1924 akiwa hana shughuli ya kumuingizia kipato, John Dillinger alifunga ndoa na mwanadada Beryl Hovious ambapo walienda kuishi kwenye nyumba ya baba yake ambapo John Dillinger aliahidi kwamba sasa atatulia na kuacha utukutu wote. Lakini wiki chache baada ya ndoa, Dillinger alikamatwa na hata kufikishwa mahakamani kwa kosa la wizi wa kuku, "nadhani alikuwa anatafuta mboga ya kwenda kula na mkewe".

Lakini kwa msaada wa Baba yake, kesi ya Dillinger iliweza kufutwa. Baadae Dillinger aliamua kutoka kwenye nyumba ya baba yake na kwenda kuishi kwenye nyumba ya wazazi wa mwanamke ambapo huko alibahatika kupata kazi kwenye duka la kuuza vifaa vya ujenzi. Akiwa huko, Dillinger alikutana na rafiki yake wa muda mrefu aitwaye *Edgar Singleton,* ambapo walipanga mikakati ya kuiba pesa. Ndipo tarehe 6 septemba 1924 waliiba pesa katika moja ya Grocery japokuwa walikamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo John Dillinger alihukumiwa kifungo cha miaka 20 katika Gereza la "Indiana State Reformatory in Pendleton".

Alipokuwa jela, alikutana na wafungwa wengine ambao walimfundisha mbinu nyingine za uhalifu mkubwa hususani uporaji wa fedha kwenye mabenki. Alitumikia kifungo chake hadi mwaka 1933 kwa paroli. Siku chache tu baada ya kutoka jela, John Dillinger alifanya uhalifu mkubwa, safari hii akivamia benki na kuiba pesa benki ingawa alikamatwa na kuhukumiwa kifungo katika gereza la Lima.

Siku chache baada ya Dillinger kuingia jela, wafungwa 12 ambao baadhi yao ni rafiki zake Dillinger, waliweza kutoroka katika gereza la "Indiana State Prison". Hili ni gereza alilowahi kufungwa John Dillinger baada ya kuhamishwa toka kwenye gereza lile la awali.

Miongoni mwa hao waliotoroka, ambao baadhi yao ni marafiki wa Dillinger, walifika katika gereza alilofungwa Dillinger lengo ni kumtorosha rafiki yao. Walimuua askari mmoja na kuchukua funguo kisha kufungua mlango wa selo alilomo Dillinger kisha kutoroka naye. Baada ya kutoroka, John Dillinger na wenzake walielekea mjini Chicago ambapo waliunda genge kubwa la kihalifu *Dillinger Gang*. Maombeni maoni tuishie hapa???

Tunao umoja wetu kwaajiki ya kuchangia na kuwasaidia watu wenye uhitaji naomba tuungane kwa pamoja kwaajili ya kupaza sauti na kuwasaidia wenzetu wenye uhitaji gusa link hapo t
t.me/chakushangazafoundation
Tunao umoja wetu wenye lengo la kutoa misaada kwa wenye uhitaji hivyo kama unatamani kuungana nasi karibu gusa hapo
t.me/chakushangazafoundation
#chakushangaza
JAMBAZI MTUKUTU
PART 2
Genge hili lilipora pesa kwenye mabenki mbalimbali, na ili kuongeza nguvu, walivamia ghala la silaha na kuiba silaha nzitonzito walizozotumia katika shughuli zao za kihalifu.

Wahuni hao walitokea kupata umaarufu mkubwa pale Marekani, hususani huyu Dillinger ambaye alikuwa maarufu sana zaidi ya 'nyota wa hollywood' kwani kila siku jina lake lilikuwa likitajwa kwenye vyombo vya habari na kuandikwa magazetini. Sifa nyingine ya genge hili ni kwamba walikuwa watanashati mno wakipendelea kuvaa suti na kofia nyeusi.

Januari 15 1934, Dillinger alivamia benki kuiba pesa. Katika tukio la majibizano ya risasi, Dillinger alimuua askari mmoja aliyejulikana kwa jina la William O'Malley. Yeye alipigwa risasi kadhaa japokuwa hakufa kwasababu alivaa 'bullet proof'.

Baadae, 'Dillinger Gang' walikuja kukamatwa, ambapo Dillinger alipelekwa katika gereza la *crown point* kwa kosa la kumuua Askari. Gereza hilo lilipewa jina la 'escape proof' kwakuwa lilikuwa nj ngumu kutoroka hapo. Umaarufu wake ulipelekea wananchi kufurika mahakamani na gerezani kwa ajili ya kutaka kumuona John Dillinger.

Tarehe 3 Machi 1934, John Dillinger alifanikiwa kutoroka tena katika gereza la *Crown point,* safari hii akitoroka kwa kutumia 'bunduki feki' aliyoichonga kwa kutumia mbao na kuipaka rangi nyeusi. Aliitumia bunduki hiyo kumtisha askari kisha akapora gari la askari na kutoroka nalo. Kitendo hiko kiliwafanya polisi waombe msaada kutoka *FBI* ambao walifanya msako kabambe wa kumkamata John Dillinger.

Alipotoroka, alikimbilia mjini Chicago ambako huko aliunda Genge jipya safari hii akimchukua mtu hatari aliyejulikana kama 'Baby Face Nelson'. Genge hilo liliendelea kufanya matukio mengi ya uporaji wa pesa benki na hata wizi wa silaha. Katika kipindi hiki, John Dillinger alianzisha mahusiano na binti aliyeitwa 'Polly Hamilton' mhudumu wa mgahawa pale Chicago ambaye hapo kabla alikuwa akijihusisha na ukahaba. Ifahamike kuwa kipindi yupo jela, Dillinger alitalikiana na yule mkewe.

MSAKO wa kumpata John Dillinger ulikuwa ukiendelea ambapo FBI walisambaza picha za Dillinger pamoja na kutangaza dau nono kwa yeyote atakayefanikisha upatikanaji wake. FBI walitangaza dau la dola $10,000 kwa yeyote atakayefakiwa kumkamata Dillinger na $5,000 kwa yule atakayetoa taarifa za kupatikana kwake. John Dillinger alisumbua sana vichwa vya maafisa usalama kiasi cha FBI kumtangaza kuwa *"Public Enemy Nō 1".* Ukiona hadi mtu anaitwa Public Enemy Nō 1 ujue huyo alikuwa ni 'kiboko pasua kichwa'.

John Dillinger naye hakuwa nyuma katika kuhakikisha hakamatwi. Unajua alifanyaje??.

Aliamua kufanya operesheni ya uso *"plastic surgery"* ili kubadilisha muonekano wa sura yake. Pia alifanya uperesheni ya kubadilisha alama za vidole yaani 'finger prints'.

Mkuu wa FBI bwana J. Edgar Hoover alimteua bwana Samuel Cowley kuongoza misheni ya kumkamata John Dillinger. Cowley naye aliungana na Afisa *Mervin Purvis* kutoka mjini Chicago. Kwa pamoja walishirikiana na polisi kuhakikisha huyu 'Adui namba moja' anapatikana.

Ilikuwa ni siku ya tarehe 21 Julai 1934 ambapo maafisa usalama walipokea simu kutoka kwa mwanadada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Anna. Binti huyu alitoa taarifa za siri kwamba 'kesho jioni, yeye, John Dillinger pamoja na mpenzi wake, Polly Hamilton, wataenda kuangalia filamu kwenye moja ya majumba ya sinema, akaeleza kwamba watachagua kwenda aidha Biograph Theater au Marbo Theater. Na wakapanga kwamba atavaa vazi la rangi nyekundu ili iwe rahisi kwa maofisa hao kumtambua.

Ilipofika kesho yake, maofisa wakampigia simu Anna Sage ili 'ku-comfirm' ni wapi wataenda kati ya Biograph au Marbo??. Lakini kwakua Anna alikuwa bado hajui ni wapi haswa wataenda, tuliona maofisa usalama wakiongozwa na Marvin Purvis wakijigawa kwenda 'kukava' sehemu zote mbili.
Hatimaye ilipofika majira ya saa 2:30 usiku, Anna, John Dillinger pamoja na Polly Hamilton, walionekana wakiingia kwenye jumba la sinema la *Biograph Theater*. Baada ya kina Dillinger kuingia, tukaona wale maofisa wengine waliokuwepo kule 'Marbo Theater' wakiwasili haraka pale 'Biograph Theater' kwa ajili ya kuongeza nguvu.

Saa 4:30 usiku, baada ya filamu kumalizika, alionekana John Dillinger akiwa na wale warembo wake wawili, ....

Tunao umoja wetu wenye lengo la kutoa misaada kwa wenye uhitaji hivyo kama unatamani kuungana nasi karibu tunahitaji sana support yako ili tufanikishe nikioata watu 10 tuu watakao ungana nasi nitaimizia hii story gusa hapo
t.me/chakushangazafoundation
#chakushangaza
PAID PATNERSHIP WITH FANTASTIC AGENCY
http://www.fantasticagency.co.tz/register?ref=benlaysh

INVEST AND GAIN 5+K everyday to activate your account you are to make transaction of 11K 🙏🙏🙏🙏
JAMBAZI MTUKUTU
PART 3
Saa 4:30 usiku, baada ya filamu kumalizika, alionekana John Dillinger akiwa na wale warembo wake wawili, mmoja kulia mwingine kushoto, wakiwa wanatoka nje. Wakati wanakuja usawa wa aliposimama ofisa Purvis. Purvis aliwasha sigara yake kama ishara ya wale wenzake kusogea jirani.

Wakati anafanya hivyo, kumbe Dillinger alikuwa 'ameshahisi hali ya hatari', akatoa bastola yake huku akijihami kwa kujaribu kukimbia.

Lakini kabla hajafika mbali, risasi tatu zilifika kwenye mwili wa John Dillinger. Risasi moja ikipenya upande wa nyuma wa shingo na kutokezea kwenye sikio. Dakika chache zilizofuata, hospitali ya Alexian Brothers ilitangaza kifo cha John Dillinger. Na hiyo ndio ikawa mwisho wa mtukutu huyu ambaye alifariki tarehe kama ya leo *22 Julai 1934.* Baada ya kuenea taarifa za kifo chake watu wengi walifurika eneo la tukio angalau waweze kuuona mwili wa John Dillinger.

****

Lakini nafahamu utakuwa unajiuliza yule mwanadada aliyetoa taarifa za siri za kurahisisha kukamatwa kwa John Dillinger ni nani na kwanini alifanya hivyo?!! Baadae nitaeleza kisa hiko. Lakini kwa sasa tuishie hapa.



Tunao umoja wetu wenye lengo la kutoa misaada kwa wenye uhitaji hivyo kama unatamani kuungana nasi karibu tunahitaji sana support yako ili tufanikishe nikioata watu 10 tuu watakao ungana nasi nitaimizia hii story gusa hapo
t.me/chakushangazafoundation
#chakushangaza


Ahsante.
#chakushangaza
Forwarded from SOMA VITABU (READ BOOKS) (Mimi Chakushangaza)
Measure-What-Matters-John-Doerr.pdf
10.9 MB
Forwarded from SOMA VITABU (READ BOOKS) (Mimi Chakushangaza)
Chakushangaza
Measure-What-Matters-John-Doerr.pdf
Title of the book
MEASURE WHAT MATTERS
Written by
JOHN DOERR
#CHAKUSHANGAZA
#FAHAMU

"ALCATRAZ" GEREZA HATARI ZAIDI KUWAHI KUTOKEA ULIMWENGUNI.

Alcatraz lilikuwa gereza hatari na maarufu zaidi Nchini Marekani. Hapa ndipo nyumbani kwa watukutu walioshindikana wa Marekani miaka hiyo.

Alcatraz inapatikana katika jimbo la California kwenye kisiwa cha Alcatraz. Lilifunguliwa rasmi mwaka 1934 hadi mwaka 1935 tayari lilikuwa na wafungwa 242. Gereza hili lilifungwa rasmi tarehe 21 March 1963 hivyo lilidumu kwa miaka 29 tu.

Mambo yaliolifanya gereza hili kuwa maarufu zaidi ulimwenguni ni yafuatayo:

(A). Aina ya watuhumiwa waliopatikana humu

(B). Lilikuwa likizungukwa na bahari, pia ulinzi usiokifani.

(C). Mazingira na maisha ndani ya gereza lenyewe yalikuwa tatanishi yenye kuhitaji roho ngumu kuyavumilia.

HAWA NI BAADHI YA WATEMI WALIOWAHI KUFUNGWA GEREZA HILI.

I). George Kelly.

Huyu mtemi alifahamika kwa jina "The Machine Gun" alipewa jina hili kutokana na utundu wake kwenye zana hii wakati wa utekelezaji uhalifu wake. Huyu alikuwa kiongozi wa kundi la mamafia wa wizi wa mabenki na utekaji. Alifungwa gerezani humu baada ya kumteka mfanyabiashara tajiri wa kutupwa bwana Charles F. Urschek na kujipatia kiasi cha dollars 200,0000.

(II). Alivin Fransis Karps.

Mbabe huyu alikuwa kiongizi wa kundi lililoitwa "barber-Karpis" mbishi huyu pekee ndiye mfungwa aliyekaa miaka mingi katika gereza hili kwa miaka 26.

Alcatraz ilikuwa limegawanywa katika blocks nne, block A, B, C na D, chumba cha Mkuu was Gereza, chumba ya wageni, Maktaba na Saluni ya kunyolea wafungwa, huku block "D" likiwa ndio block hatari zaidi kwa msoto kiasi kwamba pamoja na uhalifu wao katika uhalifu, watukutu hawa waliligwaya sana block hili!.

Gereza lilizungushiwa uzio wa umeme. Hatari zaidi ni kwamba gereza lilijengwa kwenye kisiwa kilichozungukwa na maji ya baridi mno pande zote huku yakiwa na mkondo mkali sana.

Mazingira haya ndio yaliyolifanya gereza hili kuwa la kipekee na kuaminika kuwa gumu kuliko yote kwa mfungwa kutoroka.

Watemi waliopata kupitia ndani ya Alcatraz mara kadhaa walinukuniliwa wakisema
"haikuwa sehemu salama kwa kiumbe chochote kilichoumbwa na Mungu kuishi", kulikuwa na ukatili na maisha magumu sana, watemi walipata shuruba Kali kutoka kwa walinzi lakini wao kwa wao walifanyiana ukatili mkubwa mno. Mfungwa "Edward Wulke" ni mmoja wa watukutu aliyekutana na ukatili humo ndani, huyu alikatwa mikono yake kwa shoka na baadae alikuja kujinyonga.

Mazingira yalikuwa machafu mno kama inavyofahamika magerezani, kazi ngumu kwa muda mrefu huku likiwa ni kawaida sana kupitisha Siku tatu hadi nne bila kula.

Block "D" ndio lilikuwa kiboko yao hii ilikuwa na selo zilizochimbwa shimo, yaani ukiingizwa humu lazima uzame kwenye maji kama usiposimama. Pia humu kulikuwa hakuna umeme na kulikuwa na baridi Kali sana, huku wafungwa wanakuwa nusu uchi. Vitanda kamwe havikuwa vikipatikana ndani ya block D, wafungwa walitembea peku peku, harufu mbaya ilikuwa nyumbani kwake!

Mmoja wa watu waliopata kuishi anakili kwamba Alcatraz ilikuwa ni kama jehanum na kama wangepewa nafasi ya kuchagua kuishi humo na kifo basi wangechagua kifo.

Kiufupi watukutu hawa walikuwa ni kama wafu walio hai, hadi hapo walikuwa na wazo moja tu, kutoroka Au uendelee kuwa maiti inayoishi Alcatraz.

Ndani ya miaka 29 ya uhai wa gereza hili, yalifanyika majaribio zaidi ya 14 yakihusisha watu 46, kati ya hapo wawili walikufa maji, sita walipigwa risasi, 23 walikamatwa na watatu hawajulikani walipo hadi sasa!.

Mtu wa kwanza kujaribu aliitwa Joseph Bowers juhudi zake ziliishia mikononi kwa walinzi, walipigwa risasi baada ya kugoma kutii amri ya kujisalimisha.

Baaadae Theodore Cole na Raph Rae walikuja kufanikiwa kutoroka baada ya kukata nondo ya dirisha lakini wakafia majini kutokana na baridi kali.

June 11 mwaka 1962 wabishi watatu, Frank Morris, John Anglin na Clearance Anglin walifanikiwa kuvunja mwiko ......coming soon