Chakushangaza
4.69K subscribers
4.94K photos
168 videos
36 files
956 links
Njootukujuze tukushangaze tukuelimishe tuulishe ubongo wako madini

CHANNEL ILIANZISHWA RASMI MNAMO 11/06/2019
Download Telegram
#CHAKUSHANGAZA
👉Mnamo tarehe 1/4/1974, Alaska ,maeneo ya mlima Sitika, mtu mmoja aliejulikana kwajina la Porky, aliekuwa na Umri wa miaka 50,kwa wakati huo alizua gumzo baada ya kuwaweka wakazi wa eneo hilo katika taharuki.

Mtu huyo alikusanya matairi ya gari yaliyo haribika na kuyapandisha kileleni cha mlima huo wa Sitika ,ambao ni mlima wa volcano hai,iliyo kuwa ikizaniwa kulipuka kwa kipindi cha miaka iliyo fuata.

Jamaa huyo baada ya kupandisha matairi hayo, aliyawasha Moto na kusababisha moshi mkubwa, kiasi cha kuonekana Kama dalili ya volkano kulipuka.

Ilizua taharuki kwani watu wengi wali changanyikiwa na kukimbia wakizani volkano inalipuka , kitu kilichofanya hata serikali na vyombo vya habari kutangaza tukio hilo.

Lakini muda mchache baadae Moto ulizima na Jamaa akiwa anacheka baada ya kufanya tukio hilo, alikamatwa baada ya kuwaambia watu alichokifanya , alishambuliwa na kula kichapo na wakazi hao.

Lakini polisi wali mwokoa ,hata hivyo hakufungwa kwasababu alijitetea kuwa tarehe 1, mwezi wa 4, huazimishwa Kama siku kuu ya wajinga Duniani.

#chakushangaza
#CHAKUSHANGAZA
👉 Je , umewahi kuota ndototoni, Unafanya Jambo Fulani, umeona kitu Fulani au upo sehemu Fulani na katika maisha halisi ukafanya tukio lilelile ulilolifanya kwenye ndoto, kuona kitu kilekile Kamakwenye ndoto au kufika sehemu ileile Kama kwenye ndoto?. Kitaalamu Hali iyo inaitwa "Deja Reve" yani Ni Hali ya mtu kuishi maisha ya ndoto katika maisha halisi.


#CHAKUSHANGAZA
#CHAKUSHANGAZA

Part ..1: UFO & ALIEN.

Alien, Ni viumbe vya ajabu kutoka anga ya mbali ambao wanadaiwa kutembelea Duniani mara kwa mara kupitia vyombo vyao vya kusafiria vijulikanavyo kama UFO (undifined flying Object). Baadhi ya watafiti na wasomi wa maswala ya Ufology na Alien, wanaamini kuwa Viumbe hivi Alien ni kweli vipo.

Nakatika tafiti zao baadhi ya watafiti hao ambao ni wanasayansi wa Anga za mbali Kama Astronout Gordon Caper, na wengine Wana amini Viumbe hivi vinatoka katika Constellation ya Draconian au Orion.

Fununu za uwepo wa Viumbe hivi, ilishika hatamu kuanzia miaka ya 1940s, haswa Nchini marekani baada ya kuripotiwa kuonekana kwa vyombo vyao yani UFO.

Tokea kipindi hicho baadhi ya serikali zilianza kuamini na mpaka Sasa Asilimia kubwa ya serikali nyingi Duniani zinaamini katika hoja iyo ya UFO na ALIEN.

Hi kufanya baadhi ya watu kuamini kuwa baadhi ya serikali Duniani Zina shirikiana na Viumbe hao ALIEN katika maswala ya kiteknolojia.

Tokea mwaka 1940s zilipo Anza vuguvugu na minong'ono ya uwepo wa UF
#chakushangaza
WATU 10 AMBAO WALIPOTEA NA HAWAJAWI ONEKANA
#1
Kupotea kwa mwanasiasa Ben Saanane takribani miaka miwili iliyopita pamoja na kupotea kwa mwanahabari Azory Agwanda mwaka mmoja uliopita,kuliwashtua Watanzania walio wengi na kuibua minong'ono juu ya mahali walipo watu hao. Mpaka leo hatujui walipo Ben Saanane pamoja na Azory Agwanda. Miaka ya nyuma, aliwahi kupotea mwanasiasa mahiri wa miaka hiyo hapa nchini Abdallah Kassim Hanga, ambaye mpaka leo hajulikani alipelekwa wapi licha ya kuwa mpaka kupotea kwake alikuwa kwenye mikono ya dola. Hayo ni machache.

Leo tujionee watu maarufu ambao walipotea, hawajulikani walipo na hawakuwahi kuonekana tena hapa Duniani. Baadhi yao ni viongozi, wahalifu na watu wa kawaida tu.

10.Jim Sullivan

Huyu alikuwa ni mwanamuziki wa kimarekani. Mwaka 1969 alitoa albamu iliyoitwa U.F.O. Ndani ya albamu hiyo kulikuwa na vibao vyenye utata wa majina, kama vile Aliens, I"never die na vinginevyo vingi. Alitoweka mwaka 1975 na mpaka leo hajulikani ni wapi alipo.

9.Bison Dele

Alikuwa ni mchezaji wa mpira wakikapu katika ligi ya NBA na alichezea vilabu kadhaa vikiwemo Detroit Pistons, Chicago bulls nk. Alitoweka mwaka 2002 wakati akiwa na mchumba wake kwenye boti yao huko Tahiti katika bahari ya Pacific. Vyanzo mbalimbali vinadai kuwa Bison Dele alikuwa na kaka yake siku ya safari katika boti, pia aligombana na kaka yake hivyo walipigana wakiwa katika boti na kupelekea kuuliwa na bastola yeye pamoja na mchumba wake. Boti yao ilikuja kupatikana ikiwa haina mtu yoyote ndani yake.

8.Frank Morris

Huyu alikuwa ni mfungwa aliyekuwa anatumikia kifungo cha miaka 10 katika gereza la Alcatraz huko nchini Marekani. Alipelekwa katika gereza Alcatraz baada ya kutoroka gereza la Louisiana. Hivyo baada ya kukamatwa alipelekwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali na lililopo kisiwani Alcatraz, gereza hilo limezungukwa ma maji yenye kina kirefu na eneo lenye samaki wengi aina ya papa.

Mwanaume huyu na mapacha wawili walifanikiwa kutoroka mwaka 1962 na mpaka leo hajulikani alipo licha ya msako mkali wa FBI. Kuna wanaoamini huenda Frank aliuwawa na papa ndani ya bahari lakini hakuna aliyethibitisha. Mpaka leo jalada la kesi yake bado lipo wazi.

7. Mapacha John and Clarence Anglin

Hawa ni mapacha ambao kwa pamoja waliungana na Jambazi Frank Morris kutoroka katika jela yenye ulinzi mkali na iliyozungukwa na maji ya Alcatraz. Walitoroka mwaka 1962 na mpaka leo hawajwahi kuonekana tena. Inasemekana baada ya kutoroka walikimbilia nchini Brazil ambapo wamekuwa wakiishi na kwasiliana na familia zao kwa siri lakini hakuna aliyewahi kuthibitisha madai hayo. Sasa ni zaidi ya miaka 56 toka watoroke jela hawajawahi kuonekana tena na jalada lao lipo wazi bado halijafungwa.

6.Oscar Zeta Acosta

Alikuwa ni mwanasiasa, mwanafasihi na mwanasheria nguli kutoka nchini Marekani ambapo alikuwa ni mkosoaji mkubwa sana wa biashara ya madawa ya kulevya. Alipotea mwaka 1974 alipokuwa anaelekea Mexico. Inaaminika Acosta aliuwawa na wafanya biashara wa madawa ya kulevya na kuna wanaoamini Acosta aliuwawa kwasababu za kisiasa lakini mpaka leo hakuwahi kupatikana tena.

5.Amelia Earhart

Alikuwa ni rubani mahiri wa ndege huko Marekani. Pia alikuwa ni mwalimu, mwanamitindo na Mhariri wa majarida mbalimbali. Alikuwa mwanamke wa kwanza kurusha ndege peke yake na kuzunguka bahari ya Pacific.

Alitoweka na ndege yake mwaka 1937 akiwa angani na mpaka leo hajulikani alipo. Japo kuna wanaoamini kuwa alipewa kazi ya ujasusi na utawala wa Rais wa kipindi hiko Marekani ndugu Franklin D. Roosevelt ya kwenda kuichunguza Japan. Pia wapo wanaoamini kuwa aliamua kujibadilisha kimwili na jina na kuishi maisha yake nje ya awali. Mpaka leo hajawahi kupatikana tena.

4.Camilo Cienfuegos

Ni mwanamapinduzi wa Cuba aliyeshiriki kikamilifu Mapinduzi ya Nchi hiyo akiwa sambamba na akina Fidel castro, Che Guevara na wengineo. Ndege aliyopanda akitokea Camaguey alikotoka kumkamata mwanamapinduzi mwenzake aliyeasi Huber Matos, ilipotea angani na haijaonekana tena mpaka leo hii. Wengi wanadai Camilo alifanyiwa faulo na wenzake hasa Fidel Castro ili kuizima nyota yake
yokuwa inang'aa kwa kasi.

3.Jimmy Hoffa

Alikuwa ni kiongozi wa chama cha wafanyakazi nchini Marekani. Pia alikuwa anajihusisha na makundi ya kihalifu. Anajulikana kama kiongozi mtata, mpendwa rushwa na mwizi ambapo kuna wakati alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela kwa kosa la utakatishaji pesa. Aliachiwa kwa msamaha wa Rais wa kipindi hiko wa Marekani Richard Nixon.

Mchana wa july 30 mwaka 1975 katika parking ya Mgahawa wa Red Fox, Jimmy hoffa alitoweka na hakuonekana tena mpaka leo. Haijulikani ni akina nani haswa walihusika katika kumteka, kuna wanaosema Serikali, kuna wanaosema Mafia. Licha ya msako mkali wa FBI kiongozi huyo hakuwahi kupatikana tena.

2. Harlod Holt

Alikuwa ni Waziri Mkuu wa 17 wa Australia mpaka kupotea kwake. Jioni ya 17 december mwaka 1967 wananchi wa Australia hawatoisahau katika kumbukumbu zao baada ya kupotea kwa Waziri Mkuu wao.

Waziri Mkuu Holt alipotea alipokuwa anaogelea baharini huko Portsea, Victoria nchini Australia alipokuwa katika likizo ya mwisho wa mwaka.Licha ya msako mkali wa kwenye maji, mwili wa Waziri Mkuu Holt hakuwahi kuoekana tena. Minong'ono ilizuka kuwa Waziri mkuu huyo alitekwa na Submarine (nyambizi) ya China kwakuwa alikuwa ni jasusi wao lakini hakuna aliyethibitisha. Kuna wanaosema Harold Holt alifeki kifo chake ili aishi kwa uhuru mara baada ya kuchoshwa na maisha ya siasa ikiwa ni miaka miwili tu toka achaguliwe kuwa Waziri Mkuu. Mpaka leo mwili wake haukuwahi kupatikana tena.

1.D.B Cooper

D.B.Cooper ni jina linalotumika kumrejelea mwanaume mmoja wa makamo ambaye jioni ya November 24, mwaka 1971 alichukua kiasi cha Dola za Kimarekani 200,000 kama malipo mara baada ya kuiteka ndege huko portland nchini Marekani.

Licha ya msako mkali wa zaidi ya miaka 45 uliofanywa na FBI kwa kushirikiana na idara nyingine za kiusalama nchini Marekani, bado D.B Cooper hafahamiki ni wapi alipo wala pesa alizopewa hazikuwahi kuingia kwenye mzunguko wala kupatikana. kuna wanaoamini kuwa D.B Cooper alitengenezwa na kusaidiwa na FBI wenyewe ili wajipatie pesa. Kuna wanaoamini Cooper alifariki mara baada ya kuruka toka kwenye ndege angani lakini mbona pesa hazijapatikana? D.B Cooper ameacha maswali mengi kuliko majibu na mpaka leo hajawahi kuonekana tena baada ya jioni ile ya mwaka 1971.

MWISHO
#chakushangaza
#CHAKUSHANGAZA
Orodha ya Marais waliofariki wakiwa bado wapo madarakani Barani Afrika.

Ifuatayo ndiyo orodha ya maraisi kutoka nchi mbalimbali barani afrika waliofariki wakiwa bado wapo madarakani:

Lansana Conte, Rais wa Guinea
Baada ya miaka 24 Lansana Conte alifariki na ugonjwa usiojulikana akiwa na umri wa miaka 74. Alipambana na matatizo ya kisukari na maradhi ya moyo. Kuanzia Aprili 1984 mpaka kifo chake Desemba 2008 alikuwa ni rais wa pili kushika madaraka nchini Guinea. Mbali na matatizo ya afya aliyokuwa nayo aliweza kushinda uchaguzi.

Omar Bongo, Rais wa Gabon
Saratani ya tumbo iliosambaa ndio iliyosababisha kifo cha Rais Omar Bongo June 2009 mjini Barcelona, Uhispania, baada ya kuwa rais kwa miaka 42 mfululizo. Alifariki akiwa na umri wa miaka 72 na pia alikuwa ni kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu katika historia na alikuwa akiongoza katika mambo ya rushwa. Bongo alijikusanyia utajiri mkubwa huku akiiacha nchi yake katika hali ya umasikini.

Joao Bernardo Vieira, Rais wa Guinea-Bissau
Joao Bernardo Vieira rais wa Guinea-Bissau aliuwawa nchi mwake Machi 2009, akiwa na umri wa miaka 69. Alikuwa kiongozi wa nchi kwa muda wa miaka 31. 1978 alikuwa waziri mkuu na kuchukua madaraka 1980 na alitawala kwa miaka 19. Alibadilika na kuwa kiongozi wa umma na aliongoza miaka minne mingine zaidi. 2005 alishinda tena uchaguzi wa uraisi.

Umaru Musa Yar’Adua, Rais wa Nigeria
Umaru Musa Yar’Adua, alifariki akiwa na umri wa miaka 58 mwaka 2011 akisumbuliwa na matatizo ya moyo nchini Nigeria. Alikuwa madarakani kwa miaka mitatu pekee. Alikosekana katika kampeni za uchaguzi kwa sababu za kiafya. Baada ya kuchaguliwa kwake 2007, afya yake ilidhoofika kwa haraka.

Muammar Gadhafi, kiongozi na mwana mapinduzi wa Libya
Mwathirika wa mauaji, Muammar Gadhafi aliuawa akiwa na umri wa miaka 69 na vikosi vya waasi katika mazingira yasiyoeleweka nchini Libya, baada ya kuwa kiongozi wa taifa hilo kwa muda wa miaka 42. Aliuondoa uongozi wa kifalme bila ya kumwaga damu wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1969 lakini utawala wake ulifikia kikomo baada ya matokeo ya vuguvugu la mapinduzi ya uarabuni.

Malam Bacai Sanha, Rais wa Guinea-Bissau
Kiongozi huyu alifariki mwaka 2012 alikuwa ni Malam Bacai Sanha rais wa Guinea-Bissau. Aliugua ugonjwa wa kisukari na alifariki mjini Paris baada ya miaka minne kama rais akiwa na umri wa miaka 64. Katika kipindi chote cha utawala wake alisumbuliwa na matatizo kadhaa ya kiafya yalosababisha kwenda hospitali mara nyingi.

Bingu wa Mutharika, Rais wa Malawi
Rais mwingine aliyefariki mwaka 2012 ni Bingu wa Mutharika, rais wa Malawi. Alipata mshutuko wa moyo mwezi Aprili na kufariki siku mbili baadae akiwa na umri wa miaka 78. Uongozi wake ulikuwa ni wa miaka nane na alipata mafanikio makubwa katika sera zake za kilimo na chakula. Sifa yake iliharibika kufuatia maandamano makubwa yalopinga ununuzi wa ndege ya rais iliyogharimu Dola milioni 14

John Atta Mills, Rais wa Ghana
Pia mwaka 2012, John Atta Mills, rais wa Ghana alifariki akiwa nyumbani kwake kwa mshutuko wa moyo na saratani ya koo akiwa na umri wa miaka 68. Alishinda uchaguzi wa rais wa 2008 alishika madaraka kwa miaka mitatu pekee. Alianzisha mikakati mingi ya kiuchumi na mageuzi ya kiuchumi yalomletea sifa kutoka ndani na nje ya nchi.

Meles Zenawi, Waziri Mkuu wa Ethiopia
Meles Zenawi alifariki Agosti 2012 nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 57 kwa maambukizi yasiyojulikana. Ameiongoza Ethiopia kwa miaka 5 kama rais kuanzia mwaka 1991 hadi 1995 na kama Waziri Mkuu kwa miaka 17 kuanzia 1995 hadi 2012. Anajulikana kwa kuanzisha mfumo wa siasa wa vyama vingi, lakini pia kwa ukandamizaji wa maandamano halali ya watu wa Oromia wa kaskazini mwa Ethiopia.

Michael Sata, Rais wa Zambia
Michael Sata ni kiongozi wa hivi karibuni aliyefariki madarakani akiwa na umri wa miaka 77 kwa maradhi ambayo hayakuwekwa wazi Oktoba 28 2014, nchini Uingereza. Baada ya uchaguzi wa 2011, uvumi juu ya afya yake ulisambaa nchini Zambia. Kukosekana kwake katika shughuli kubwa za kitaifa kuliibua wasiwasi wa afya yake ingawa msemaji wake
isema alikuwa katika afya nzuri.
#chakushangaza
#CHAKUSHANGAZA
TUJIKUMBUSHE MATUMIZI YA KALAMU KWA KUFUATA RANGI

Nakuja tu na maswali chokonozi

1. Hivi ni Kwa Nini Waalimu wanatumia kalamu ya rangi nyekundu na si bluu kama wanafunzi?

2. Ni Kwa Nini pia Maraisi ndio Huandikia peni nyekundu?
Kwa nini Wakaguzi aghalabu wa Hesabu hutumia peni ya kijani?
3. Vipi Kuhusu Kalamu Nyeusi?

nauliza hivi kwa sababu hizi rangi ukigeukia muktadha mwingine zinamaana tofauti sana mfano wengine husema unapotumia kalamu nyeusi inaa maana unatengeneza pesa na bluu maana yake unapoteza pesa ilihali nyekundu ikielekezwa zaidi kwenye mikosi

MAJADILIANO COMPILED

RANGI ZA KALAMU NA MATUMIZI YAKE .......@@!!!

Mara Nyingi sana tumekuwa tukitumia pen bila kujipa angalizo fulani hivi ama kujua mantiki yake ..................

1. Kalamu ya rangi ya Samawi/samawati (Bluu) ndiyo maarufu kutumika na wengi na hasa kwenye official document za kawaida (not mandated or authentic)
We basically have two choices when it comes to pens: black or blue. Unless you are a teacher in which case you get to use red as well........."Of course blue pens. Because they contrast better with the documents you're writing on..................The modern tradition is THAT only blue ink for all in Government.

2. Kalamu Nyeusi aghalabu hutumika kwenye miamala ya Kibiashara zaidi............."Black edges it on the grounds that it looks more professional and is a legal requirement for signing legal documents and form-filling............."Some entities are now requiring signatures in blue ink in order to differentiate the original from a copy.......Black ink is used ( where bold remarks are needed ) for business deals, display credit in a bank statement, headings etc.

3. Kalamu Nyekundu Aghalabu Hutumiwa na wenye Mamlaka Katika Kusaini Official Documents na hasa Sheria na Hati fulani fulani na mara nyingi anayeruhusiwa kutumia kalamu nyekundu ni Mh Rais na Waalimu katika kujitofautisha na wanafunzi na kuweka msisitizo zaidi kwenye masahihisho ingawa utafiti uliofanywa Marekani umewezesha kupelekea kupigwa marufuku kwa kalamu nyekundu kwa wanafunzi kutokana na wengi kutaarifu kwamba zinawatisha (psychological trauma)
http://www.dailymail.co.uk/news/article-2263874/Teachers-shouldnt-use-red-coloured-pens-mark-homework-like-shouting-upsets-pupils.html

4. Kalamu ya Chanikiwiti (KIJANI) inatakiwa kutumiwa na Wakaguzi na hasa wa HESABU, aghalabu Peni ya kijani hutumiwa pia na Mawaziri...Majaji....ma RCs na Kamishna wa kiapo...aghalabu wataalamu wa dawa/wafamasia pia hutumia kalamu ya kijani .....Green ink is used by very senior bureaucrats as well as Ministers to sign files indicating their approval....also green color pen are used by Managers, gazetted officers, Judges and big people. Green testifies the high position and no one can question the authenticity when signed by the green color.

5. Kimsingi na KISHERIA, UNATAKIWA KILA MTU KUWA NA PENI MAALUM YA SIGNATURE. tumewahi kupata kesi ya mtu ambaye saini yake ilidukuliwa na yeye kukiri dhahiri shari kwamba ni saini yake kabisaaaa ila kwenye utetezi akasema kwamba peni iliyotumika siyo peni yake kwani ana peni maalum ya kuweka saini nyaraka zake zote za kisheria
https://keetonsonline.wordpress.com/2013/02/18/how-to-choose-the-right-pen/

6. Si salama sana kutumia kalamu nyeusi kwenye maandishi meusi, kisheria hiyo ni kopi na si halisi, jitahidi sana kutumia kalamu ya bluu kwenye maandishi meusi na hasa typed (Many copiers are so good now that black ink can look like part of a photocopy."-

7. Ball Pen ndiyo offical pen kwa nchi nyingi duniani. kumbuka Kama unatumia 'jel pen' basi ukitumia 'ball pen' mwandiko 'kitaalamu' unatofautiana (hasa kama kalamu hizo zikiwa na ukubwa wa maandishi unaotofautiana.)
"bic, speedo, cello, etc" ndio ballpoint pens.Na jell pens ni kama zile kalamu za zamani za kuchovya wino "tulikuwa tunaziita fountain - ambazo siku hizi zimeboreshwa zinawekewa wino.

8. Kuna Baadhi ya nchi;
i. mwanafunz unaruhusiwa kuandika kwa penseli na kalamu ya rangi yeyote ile (bluu, kijani, nyekundu, nk).

ii. Hawaruhusu kuweka sahihi (signature) kwa
lamu ya rangi nyingine yeyote ile isipokuwa 'bluu'. Kuna sehemu zingine hata kujaza fomu iliyochapwa ni lazima utumie kalamu ya rangi ya bluu......kalamu ya bluu ndiyo inayotambulika duniani kote (official pen)

iii. Wanatumia kalamu nyekundu kuandika jina la mtu aliyefariki (marehemu). Yaani hairuhusiwi na huwezi kuandika jina la mtu aliyehai kwa kalamu nyekundu.Mathalani ukiwa Ureno na unatumia kalamu nyekundu unahesabika ni mkaidi ama mleta mikosi ( It's considered rude to write in red ink in Portugal.)

iv: Jeshi la Marekani utatumia rangi kulingana na wadhifa (rank) wako Jeshini
In US Navy there is a long tradition of prescribed ink colors for officers - blue color for officers, black color for departmental heads, green color for Executive officers and red color for commanding officers.

v. Huko Ujerumani, rangi ya Hudhurungi (Brown) hutumika kuweka saini HUKUMU YA KIFO ILIHALI huko Pakistan wao hutumia kalamu nyekundu kwa lengo hilohilo-Brown color ink is used to sign death warrants in Germany and red color ink was used for same purpose in Pakistan.

mfano nchi ya Australia officials pen ni NYEUSI TU! hata baadh ya benki hapa kwetu mfano NBC official pen ni nyeusi ingawa pia si salama sana kisheria .....NMB official ink ni blue,kwa documents zao....tofauti na hapo....hupokelewi.
Exim.....nyeusi na blue, CRDB.....Blue ama nyeusi; nyekundu, kwa wenye uoni hafifu na maafisa wa benki hasa kuthibitisha nyaraka
#chakushangaza
#CHAKUSHANGAZA
GEREZA LA GITARAMA: Jehenamu duniani!

Jiji la Gitarama hupatikana katikati ya nchi ya Rwanda, kwa makadirio kilomita arobaini na tano toka kwenye jiji kubwa nchini humo; jiji la Kigali, jiji pekee lililoitangulia Gitarama kwa ukubwa.

Kama haitoshi ni hapahapa katika jiji hili ndipo kuna historia kubwa ya makutano yaliyofanyika mwezi wa kwanza; mwaka 1961, Rwanda ikatangazwa rasmi kama jamhuri. Vilevile jiji hili (kipindi hicho mji) likatoa raisi wa kwanza wa Rwanda, bwana Gregoire Kayibanda, ambaye kumbukumbuye mpaka sasa imesimamishwa katikati ya eneo hili.

Mazuri hayo hayakomei hapo, hapana! Bali pia hili jiji likabarikiwa na kutunukiwa vivutio kadha wa kadha vya utalii na taasisi lukuki za elimu ambazo aidha zaweza jaza ukumbi nikizianisha hapa. Na kwa namna moja ama nyingine nachelea kusema taasisi hizo zilijengwa (zimejengwa) kwa lengo chanya la kuwafanya watu wapate elimu na hatimaye kujikomboa kifikra na kimwili.

Lakini mbali na taasisi hizo, na aidha vivutio na uzuri wa jiji hili, upande wa pili wa sarafu ukisikia jina hili ‘Gitarama’, yakupasa uhofie na hata kushikwa na huruma kwa namna binadamu kama wewe wanavyotendwa, tena bado wakiwa hai kabisa. Binadamu hao wakiwa wanaishi ndani ya eneo ambalo hakuna binadamu yeyote juu ya uso wa dunia angelipenda kuwamo kwa gharama yoyote ile!

GITARAMA; ‘JEHANAMU DUNIANI’:

Sehemu nyingi duniani zimewahi kuitwa jehanamu. Na jina hili lilishamiri zaidi baada ya vita vya pili vya dunia ambapo maeneo kadhaa yalipewa jina hili kuwakilisha maeneo yasiyokalika, hatari na yasiyo na afya stahiki kwa wanadamu. Maeneo hayo mathalani ni Blood Falls (Maanguko ya damu) huko Antarktika, Danakil Depression (bonde la Danakil) huko Ethiopia, Door to Hell (mlango wa kuzimu) huko Turkmenistan, Kamchatka Peninsula huko Russia na kadhalika, na kadhalika.

Japokuwa sehemu hizo zipo nyingi zikipatikana maeneo mbalimbali, ni dhahiri kuna sifa ambazo hushirikiana na hivyo basi ndio maana huwekwa chini ya mwamvuli mmoja wa ‘jehanamu’.

Upande wa kusini magharibi mwa jiji la Kigali, ndipo ilipo jela hii Gitarama. Kwa sasa inaitwa jela ya Muhanga ikichukua jina la wilaya ambayo ndiyo makazi yake mpaka sasa. Majengo ya jela hiyo yalikuwa yanamilikiwa na waingereza British housing complex mnamo mwaka 1960 yakiwa yamejengwa kama makazi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Pale kampuni ilipofungwa, eneo hilo likakodiwa na serikali ya kwanza ya Rwanda iliyokuwa imedhamiria kufanya majengo hayo kuwa jela ya kisiasa (political prison). Tangu hapo hakuna chochote kilichobadilika ndani ya jela hiyo isipokuwa tu serikali ya Rwanda ambapo kila serikali iliyoingia madarakani ilionekana kuipatia ama kuitafutia matumizi eneo hilo.

Kwa mujibu wa gazeti la London Independent mwaka 1995, hii ndiyo jela mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani. Pia wanda za tovuti nyingi za mitandao, zinakiri na kuiweka jela hii kwenye kumi, ama tano, ama tatu bora zaidi ya jela hatari mno kuwahi kutokea duniani.

Gitarama ilijengwa kwa ajili ya kumudu wafungwa mia nne tu, lakini mpaka sasa inabebelea wafungwa elfu saba! Mara kumi na nane kwa makadirio. Hali hii inapelekea mahesabu ya wafungwa wanne kurundikana katika eneo la hatua tatu (three feet). Hili laweza likawa la kawaida sana ukilisoma hapa, lakini ukijaribu kutoka nje ya bandiko hili na kujikuta ukiwa umekaa na watu wengine watatu ndani ya eneo la hatua tatu tu, kidogo waweza kuelewa.

Hakuna mahali pa kulala, kujilaza, wala pa kuketi. Wafungwa husimama wakikung’utwa na jua na wakipoozwa na mvua kwakuwa jela hii kwa kiasi kikubwa haina paa la kuwakinga wafungwa na jua, mvua wala baridi.

Kutokana na kutapakaa kwa wafungwa hao kwenye eneo hilo dogo, inakuwa ngumu sana kwa mfungwa kutaka kwenda chooni akafanikiwa kwa muda, hali hii inapelekea wafungwa kujisaidia popote pale na hivyo basi kujaza vinyesi, mikojo na harufu kila eneo. Wafungwa huozeshwa na kumomonywa miili na bakteria mpaka kufa kwasababu ya kujiweka karibu, aidha kwa kulala ama kusimama kwenye vinyesi na uchafu wa kila aina (gangrene).

Wafungwa wengi hawana vidole, nyayo na miguu kwasababu ya kuoza
kiwa hai. Miguu hubadilika rangi na hata kutoa madonda. Ni kawaida kuona mtu ana wadudu miguuni huku wakitembea.

Kati ya wafungwa kumi ndani ya jela hii, nane hufa kwa kukosa hewa ama magonjwa mbalimbali. Lakini wanapotoka kwenda kuzikwa, basi huingizwa wafungwa wengine ndani ya mlango mkubwa wenye kutu wenye kutoa malalamiko ya ukuukuu.

Lakini ajabu na kweli ni kwamba, wafungwa waliomo humo ndani hakuna hata mmoja ambaye amepitia mahakamani akathibitishwa ya kwamba ana makosa na anastahili kufungwa.
Wengi wao, kama si wote, ni wa Hutu. Na walianza kujazwa humo miaka ya 1990's wakituhumiwa kwa mauaji ya Kimbari yaliyokwapua maisha ya wana Rwanda zaidi ya milioni moja. Na hii huonekana ni sababu kubwa inayofanya serikali kutokujali kabisa jela hiyo achilia mbali aliye madarakani ni mtutsi.

"Watu wanafanyana vitoweo."

Si tu kwamba hakuna mahali pa kupumzikia, bali ndani ya jela hii kuna rekodi kadha wa kadha mfungwa kumuua mwenzake kisha kumla kama chakula.

Mgawo wa chakula ni finyu sana. chakula na maji hutolewa mara moja tu kwa juma, tena kikiwa kibovu na hakitoshelezi; mara nyingine chakula kinakosekana kabisa na hivyo basi kuwalazimu wafungwa kumaliza siku kadha wa kadha pasipo kutia kitu tumboni.

Kwakuwa kila mtu anataka kuishi, wafungwa wengine huamua kuchukua hatua ya kulinda uhai wao kwa kuwanyonga wenzao, kuwabamiza ukutani mpaka mauti kisha kuwatafuna wakiwa wabichi na wakivuja damu moto.

Wengine hucheza kamari kabisa, ambapo wahusika huchaguliwa kwa kukurupushwa. Mwisho wa siku wahanga wa Kamari hiyo hupotea isijulikane wameenda wapi ndani ya jela, bali matumboni.

Kumbuka kwamba yote haya yanawezekana tena kwa urahisi kwa sababu ndani ya jela hii hakuna hata mlinzi anayediriki kuingia, ni wafungwa wenyewe tu ndio ambao hujihudumia wenyewe. Chakula na maji vikiletwa, huachwa mlangoni kabla ya wafungwa wenyewe kunyakuwa na kuanza kujigawia. Ndio maana mtu anaweza akafa mpaka akaoza ndani ya jela hii kabla hajaja tolewa na kwenda kuzikwa kwenye makaburi ya pamoja.

Kulana wenyewe kwa wenyewe si jambo geni wala la kushhtukiza kwa walinzi wa jela hiyo wala tawala husika.

Juhudi za kubadilisha hali ya Gitarama:

Kwa namna moja ama nyingine kuna watu na mashirika yaliyoguswa na hali ya kusikitisha kuhusu Gitarama. Japokuwa kweli waliomo humo wanaweza wakawa ni watu waliofanya makosa mbalimbali, ikiwemo hata kuua, lakini halibadilishi dhana ya kwamba na wao wanahitaji haki za binadamu kama wengineo.

Shirika la Global Giving, likisukumwa na kiongozi wa projekti hii Karen Tse, ni moja ya shirika lisilonuwia faida lililoguswa na hata kuanzisha kampeni ya kutafuta pesa kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa hao. Mpaka sasa shirika hili li wazi na unaweza ukawachangia.

Pesa waliyoichangisha mpaka sasa ni dola za kimarekani 325 huku wakifadhiliwa na mashirika mawili fadhili na huu ukiwa ni mwaka wa sita sasa wapo moto (active).

Mbali na hapo wanajitutumua kuwasaidia wafungwa hao kisheria ili kesi zao zipatwe kusikilizwa mahakamani. Japokuwa swala hili linaonekana ndoto zaidi ya uhalisia tangu mkono wa serikali unakuwa mzito sana kutingisha kidole.

“Hiyo ndiyo Gitarama; jehanamu juu ya uso wa dunia. Ama tuseme tawi dogo la jehanamu duniani.”
#chakushangaza
#CHAKUSHANGAZA
JE UNAFAHAMU JINA HALISI LA JOSEPH KABILA ANAITWA "HYPOLITE KANAMBE KAZEMBEREMBE"? NA NI MTOTO WA KUFIKIA WA LAURENT DESIRE KABILA?.

Kumekuwepo maswali mengi sana ndani ya Kongo DRC na nchi nyingi Afrika juu ya uhalisia wa Joseph Kabila Kabange (JKK) kuhusishwa na Unyarwanda (Rwandese), kumetolewa taarifa nyingi za siri zinazo mtaja JKK kuwa sio mtoto wa kuzaa wa Mzee Laurent Desiree Kabila raisi wa tatu wa Kongo DRC na kiongozi wa zamani wa kundi la uasi la AFDL, aliye uondosha madarakani utawala wa vipindi virefu wa Mobutu Seseseko Kuku Ngwendu wa Zabanga kupitia ile iliyoitwa Operation Banyamrenge/Bahima.

Joseph Kabila mwenyewe na wafuasi wake wamekuwa wakikanusha hilo na kuhusisha taarifa hizo na njama chafu za kumchafua. Mwaka 2010 kwenye maadhimisho ya miaka kumi ya kifo cha Laurent Desire Kabila, Joseph Kabila mwenyewe alitoa maelezo kuhusiana na taarifa hizo zinazo muhusisha na unyarwanda. Pamoja na maelezo yaliyokanusha ya yeye kuhusishwa na taarifa hizo bado kumekuwepo taarifa na ushahidi mwingi unaoendelea kutolewa kuthibitisha kuwa Joseph Kabila ni Mnyarwanda na sio mtoto wa kuzaa wa Mzee Kabila.

Moja ya tafiti hizo zinazo zungumzia sintofahamu hii ya Joseph Kabila ni "Waraka" ulio chapishwa na jarida la "Africa Federation" jarada hilo lilipewa jina la (titled) : CONCERNING THE TRUE IDENTITY OF MR. HYPPOLITE KANAMBE ALIAS “JOSEPH KABILA” ndani ya jarida lina mtaja Joseph Kabila kuwa sio mtoto wa kuzaliwa na Kabila mzee, waraka huu unaonesha kuwa mke wa Kabila mzee aliyeitwa Sifa Mahanga alikuwa na watoto sita (6) tu ambao alizaa na mzee Laurent-Desire Kabila. Kati ya watoto hao ambao Sifa Mahanga mke wa mzee Kabila alio zaa nao ni Josephine, Cecile, Masengo, Gloria, Kiki and Maguy. Katika list hiyo Joseph kabila hayumo.

Je huyu Joseph Kabila Kabangee (JKK) anaye tajwa kuwa sio mtoto wa kuzaa (biological child) wa Mzee Kabila ni nani? Kimsingi huyu Joseph Kabila aliyekuwa rais wa nne wa taifa la Kongo DRC jina lake halisi anaitwa Hypolitte Christopher Kanambe na alizaliwa tarehe 04 June 1971 katika kijiji kidogo cha Hewabora, kilichopo katika mji wa Fizi jimboni Kivu ya kusini (South Kivu Province in the Eastern Congo) huku baba yake akiitwa Christopher Kanambe Kazemberembe na mama yake akiitwa Marcellina Mukambukuje.

Baba yake alikuwa ni muasi kutoka kabila la Watuttsi aliyepinga utawala wa Juvenal Habyarimana raisi wa Rwanda kipindi hicho. Huyo Christopher Kanambe alikimbia Rwanda yeye na familia yake na kukimbilia nchini Kongo DRC mwaka 1960 baada ya machafuko ya kwanza ya kikabila nchini Rwanda yaliyo anza mwaka 1959, na katika harakati hizo za kutaka kuuondoa utawala wa Juvenal Habyarimana madarakani akafanikiwa kutana na Mzee Laurent Kabila mwaka 1964 aliyekuwa kwenye mapigano ya kumpinga Mobutu Seseseko huko mashariki ya Kongo DRC ,wakawa marafiki chanda na pete kwenye issue zao za kivita.

Baada ya kukutana na kuendelea na ushirikiano wao kwa makubaliano kwamba Mzee Kabila amsaidie Christopher Kanambe kumuondoa Juvenal Habyalimana madarakani kisha yeye atamsaidia Kabila kumuondosha Mobutu ikulu ya Kinshasa. Walikubaliana hayo kwakua utawala wa Mobutu ulikuwa umewekeza base yake kubwa Rwanda chini ya utawala wa Juvenal Habyalimana (Mtoto wake wa ubatizo) hivyo kufatia sababu hizo Rwanda ilikuwa kikwazo kikubwa kufanikisha mapambano dhidi ya utawala wa Mobutu.

Mwaka 1977 bwana Christopher Kanambe ambae ndie baba yake wa kumzaa Joseph Kabila alifariki dunia (duru za ndani zinataja Mzee kabila kuhusika, tutalitazama hili baadae) na kwa mujibu wa mila zao na taratibu za kijeshi ilibidi kabila amrithi mke wa Kanambe yani huyo mwanamama Marcellina pamoja na watoto wake wawili mapacha ambao ni Hypolitte na Jenny (wale wa karibu na escape 1 mnakumbuka utajiiri na matanuzi ya huyu dada).

Baada ya kuchukuliwa na Mzee Kabila wote rasmi wakaanza kuitwa kabila, yani huyo Hypolite na Jenny walibadili majina yao kwa Hypolite kuitwa Joseph kabila na huyo Jenny kuitwa Jennifer Kabila. Ila katika harakati za Mzee Kabila za mapambano yalipo mzidi alikimbilia Tanzania na familia yake ingawaje
uwa na wanawake 13 na watoto 25 katika sehemu mbalimbali huko Kongo DRC.

Huyu Joseph Kabila (JKK) a.k.a Hypolite ni mpwa wa mkuu wa majeshi wa zamani wa Rwanda anae aitwaye James kabarebe na hadi mwaka 1996 huyu Hypolite alikuwa ni dereva wake kwenye vita ya Banyamulenge ya kumsaidia Mzee Kabila kumtoa Mobutu madarakani, hilo linathibitishwa na waziri wa mambo ya nje kipindi cha utawala wa Mzee Kabila aliyeitwa Bizima Karaha ambae alikuwa ni mnyarwanda, ambae mara kadhaa Karaha anasema anakumbuka kumuona Kabila akiwa dereva wa Kabarebe mwaka 94 na 95 alikuwa porini na jeshi la kagame la RPF ambalo lilikuwa likimsaidia Mzee Kabila katika vita vya msituni dhidi ya Mobutu.

Je ni Kwanini Joseph Kabila alipewa uraisi wa Kongo DRC kama hakuwa raia wa Kongo DRC? Katika kujibu swali hilo na kulielewa vizuri ni vyema turejee historia ya kifo cha baba yake Kabila aliyeitwa Christopher Kanambe ambae alikuwa ni mtusi wa Rwanda. plan hii ya kupewa uraisi Joseph Kabila ni plan iliyo injiniwa na Paul Kagame rais wa Rwanda ambae baada ya kuvulugana na Mzee Kabila kufatia kukwama kwa makubaliano ya kile kilichoitwa "Mkataba wa Lemela" ilikuwa ni mpango wa kumuondoa Laurent Kabila duniani na kumuweka mnyarwanda huyu Joseph (Hypolite) mkakati huu ulifanyika kwa umakini wa hali ya juu sana ambapo kijasusi mbinu hizi huitwa "TROJAN HORSE TECHNIC".

Sasa turejee kwenye habari ya kifo cha BABA YAKE HYPPOLITE........
Christopher Kanambe Kazemberembe na Mzee Laurent Kabila walikutana na kuanza ushirikiano wao mwaka 1964 kila mmoja akiwa anapambania nchi yake, Kanambe Vs Wahutu (Juvenal Habyarimana) na Kabila Vs Mobutu Seseseko, kufatia mapambano hayo mambo yakawa magumu mwaka 1966 kufatia jeshi la Mobutu kujibu mapigo kwa kusambalatisha uasi wote huko mashariki ya Kongo, kufatia hali hiyo Kanambe na Kabila wakakimbilia Tanzania chini ya mwamvuli wa P.R.P. (Parti de la Revolution du Peuple).

Baada ya vita ya Moba, Mobutu seseseko alituma watu kumuhonga hela nyingi Christopher Kanambe ambaye ni baba halisi wa Joseph Kabila ili amuue Laurent Kabila lakini mission ilibuma, baada ya mzee Laurent kabila kupenyezewa taarifa hizo, hivyo Kabila akaitisha kikao sehemu iitwayo Nyunzu huko mashariki ya Kongo DRC wanajeshi wake kadhaa wakapatikana na hatia akiwemo Christopher kanambe na wakahukumiwa kifo, lakini kabla ya hukumu ya Christopher Kanambe kutekelezwa aliuwawa na askali wake mwaka 1977 kisha huyo askali nae kuuwawa na walinzi wa Kanambe.

Baada ya kifo cha Kanambe Laurent Desiree Kabila akamuoa Marcelina mke wa Kanambe na kuwa adopt watoto wake mapacha Jenny na Hypolitte......... Ukweli ni kwamba huyu Hypolite (JKK) alizaliwa Kongo, na baba yake Christopher Kanambe alikuwa ukimbizini akifanya uasi dhidi ya serikali ya wahutu ya Habyarimana, na baada ya kifo chake zilitumika mila za kivu, kurithiwa na mzee Kabila.

Joseph Kabila, jina lake harisi anaitwa Hyppolite Kanambe Kazemberembe, baba yake wa kufikia Mzee Laurent Kabila alikua na wake zaidi ya 13 na watoto zaidi ya 25 na wengine hawajulikani kwani mzee Kabila hakua na muda wa kuwalea watoto hao kwani kipindi wanaishi Msasani Dar es salaam ambako Hyppolite Kanambe alilazimika kufanya kazi za ufundi, taxi dreva na barman katika Jiji la Dar es salaam na Kigoma kipindi hicho baba yake wa kufikia Laurent Desiree Kabila alikua ana ishi Tanzania huku anapigana vita na Mobutu Sese Seko huko Kongo DRC wakati huo ikiitwa Zaire.

Mwaka 1995, Hyppolite Kanambe aliamua kurudi kwao Rwanda ambako alipokelewa na mjomba wake James Kabarebe, ambae alikuwa ni mkuu wa intelijensia ya Rwandan Patriotic Army (APR), alimkaribisha Kanambe nyumabni kwake na kumtafutia kazi ya udereva wa ma lori na baadae akawa dereva wake katika jeshi.

Mwaka 1996, Marekani ilipoandaa shambulio dhidi ya Zaire, kupitia ile iliyoitwa "Operation Banyamrenge" chini ya Paul Kagame, Kagame alimchagua Kanal James Kabarebe kuwa kiongozi mkuu wa Operation hiyo na kuhakikisha Mobutu anapinduliwa.

Katika kuajilia wanajeshi watakao husika na operation hiyo Banyamrenge Kabarebe aliamua kumweka mpwa wake Hyppolite Kanambe (Joseph
la) katika mazoezi ya kijeshi ili baadae ampatie nafasi jeshini, baada ya Hippolyte Kanambe kuhitimu mafunzo aliajiliwa kwenye jeshi la Rwanda kupitia mgongo wa James Kabarebe na alitumika katika jeshi la Rwanda kuanzia mwaka 1995 mpaka 1997, na alitumika pia kama mlinzi wa kagame kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 1998 alipo rudi Kongo DRC na kuteuliwa kuwa Major General kwenye special Force iliyokuwa ikiendesha operation maalumu huko mashariki ya Kongo DRC.

Je Kuna uhusiano wowote wa Joseph Kabila kuhusika katika mauaji ya Laurent Desiree Kabila?... Je kuna lolote lile linalohusishwa na ulipaji kisasi cha baba yake marehemu Kanambe Kazemberembe? Au upi uhusiano baina ya "Operation Banyamrenge" na mkakati wa Bahima Platform dhidi ya Joseph kabila na kifo cha Mzee Kabila?... Itaendelea sehemu ya pili.

Endelea kuwa na mimi katika sehemu ya Pili kupata majibu ya maswali hayo....upate kujua kuwa nchi ya Kongo DRC bado ipo contolled by remote from kigali maana Tshisekedi ni pambo tu.
#chakushangaza
#CHAKUSHANGAZA
JE WAJUA GEREZA ZURI ZAIDI HAPA DUNIANI?
Kwa kawaida kama tunavyojua sisi gereza ni sehemu mbaya zaidi mtu kuweza kuishi anapokuwa amethibitika kuwa katenda kosa fulani, lakini katika pitapita za hapa na pale leo nimfanikiwa kupata habari za gereza zuri zaidi kuliko yoteapa chini ya jua. Amini usiamini kuna gereza ambalo hata wewe ukiliona hua amini macho yako. Mpendwa gereza la Justizzentrum Leoben ndiyo jina la gereza zuri zaidi hapaDuniani, gereza hili linapatikana katika taifa la Austria, na hili ndilo gereza linalowajali zaidi wafungwa kuliko magereza yote yale Duniani. Mfungwa akifungwa humu anapata mahitaji yote ya muhimu ya binadamu na ikiwemo mahitaji ya ziada. Mfungwa anakuwa na chumba chake chenye TV, radio na compyuta vile vile kuna sehemu maalum iliyotengenezwa kwaajili ya kufanyia mazoezi. Nimekuletea tu baadhi ya picha za gereza hili la kifahari ili angalau tu uweze kusuuza mboni zako.
#chakushangaza
#chakushangazaFunMoment
Bado unampenda Ex wako!?
Anonymous Poll
52%
Ndio
26%
Hapana
22%
Sijui