⬇️⬇️⬇️
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 3 - Novemba 6, 1899🖋📃📖📔
…‘Ewe Pendo Langu tamu kabisa, mimi ninakutolea sasa hivi vitendo vyote vya ujimudu wa mwili wangu, ambavyo wewe mwenyewe ulitaka niwe ninavitekeleza, na ninakutolea pia vitendo vingine vyote, ambavyo ninaweza nikavifanya mimi mwenyewe, kwa ajili tu ya kutaka kukupendeza Wewe peke Yako, na kwa ajili ya kukutukuza Wewe. Ah! ndiyo, mimi ningependa hata ujimudu wote wa kope zangu, hata ujimudu wa macho yangu yenyewe, ujimudu wa midomo yangu, na hata ujimudu wa nafsi yangu nzima, ujimudu wote huo uwe ukitendeka kwa ajili tu ya kukupendeza Wewe peke Yako. Lo, Ewe Yesu Mwema, chonde sana uruhusu kwamba, mifupa yangu yote, na neva zangu zote, viambizane kati yao vyenyewe, na kwa sauti zao nzuri na wazi, viweze kutoa ushuhuda Kwako Wewe kuhusu pendo langu Kwako’.
Yeye, ndipo hapo akaniambia:
“Chochote kile kinachotekelezwa kwa lengo pekee la kunifurahisha Mimi, hicho huwa kinang’aa na kuangaza mbele Yangu Mimi kwa jinsi kwamba huwa kinavuta macho Yangu ya kimungu hata yawe yamekaza kukiangalia sana, na Mimi huwa ninakipenda kweli kweli.
Huwa ninakipenda hivyo kitendo kama hicho, kiasi kwamba, hata kama kingekuwa ni peke yake kupepesa kwa kope za macho, Mimi huwa ninakipatia kitendo hicho ile ile thamani kubwa kabisa kama ile ya kitendo cha Kwangu Mimi Mwenyewe.
Kumbe lakini, vile vitendo vingine, ingawa kama ni vitendo vizuri kwa vyenyewe, na hata kama ni vitendo vikubwa, kama hivyo havikutendeka kwa ajili ya Mimi peke Yangu, hivyo huwa ni sawa na dhahabu yenye matopematope na iliyojaa kutu.
Dhahabu kama hiyo huwa haing’ai wala kuangaza, na Mimi huwa hata spendi kuviangalia kabisa vitendo kama hivyo”.…..

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 3 - Aprili 25, 1900🖋📃📖📔
Pindi nikiwa bado katika ile hali yangu ya siku zote, na pindi nikishindwa kumkuta Yesu Wangu Mtamu, ilinipasa niwe ninazungukazunguka nikimtafuta Yeye. Mwishowe, nilimkuta pale katika mikono ya Mama Malkia, akiwa ananyonya maziwa kutoka matiti yake. Kadiri nilivyozidi kuzungumza na kutenda, Yeye hakuonekana kupenda kunisikiliza. Au tuseme, na akawa hapendi kunitazama. Kwani ni nani atakayeweza kuyaelezea yale maumivu ya moyo wangu duni, katika kuona kwamba Yesu alikuwa hanisikilizi mimi? Basi, baada ya mimi kuyakatisha yale machozi yangu, na Yeye akiwa ananionea huruma, alinijongea na kuingia mikononi mwangu, na akaanza kumwaga sehemu ndogo ya yale maziwa ambayo alikuwa ameyanyonya kutoka kwa Mama Malkia.
Kishapo, mimi nikaangalia pale kifuani pake Yesu, na ndipo nikaona kuwa alikuwa na johari moja dogo, johari lililokuwa liking’aa na kuangaza hata kuweza kuufunika kwa mwanga ule Ubinadamu Mtukufu kabisa wa Bwana Wetu. Mimi, kwa kutaka nielewe maana halisi ya jambo hilo, nilimwuliza Yesu lile johari lilikuwa ni kitu gani, johari ambalo, ingawa kama lilionekana kuwa ni dogo tu, lakini likawa linasambaza mwanga mwingi kabisa. Ndipo Yesu akasema:
“Hilo johari ndiyo ule usafi wa hayo mateso yako. Hata kama mateso hayo ni kidogo tu, wewe unateseka tu kwa ajili ya kunipenda Mimi na hata upo tayari kuteseka zaidi kama mimi ningekuruhusu. Hiyo ndiyo sababu ya kutoka huo mwanga mkubwa na mzuri vile.
Ewe Binti Yangu, usafi wa moyo wakati wa kutenda shughuli ni jambo kubwa mno jinsi kwamba mtu anayetenda akiwa na lengo pekee la kunifurahisha Mimi peke Yangu, huyo huwa hatendi chochote kingine isipokuwa anasambaza mwanga kutokana na zile shughuli zake zote. Lakini, yule asiyetenda shughuli zake katika uadilifu, hata katika shughuli zilizo nzuri, huyo hatendi lolote isipokuwa anasambaza giza tu basi”.
Halafu nikaangalia ndani ya kifua chake Bwana Wetu, na pale Yeye alikuwa na kioo cha kujitazamia, kioo kinachong’aa na kuangaza, na ikaonekana kama vile wale wote wanaotembea katika uadilifu, walibaki wamezama pale ndani ya kile kioo, na kumbe wale wote ambao hawakutembea kiadilifu, wakawa wamebaki nje kabisa ya kile kioo, na hawakuweza kuupokea mhuri wowote ule wa sura ya Yesu Mhimidiwa. Ah, Ee Bwana, tafadhali unishikilie mimi nibaki nimezamishwa ndani ya hicho kioo cha kimungu, ili, nisiweze kuwa na kivuli kingine chochote kile cha nia fulani katika shughuli zangu na utendaji wangu.

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 12 - Agosti 14, 1917🖋📄📖📔
......Ndani ya Utashi wa Mungu fadhila huwa zinapewa nafasi yao katika ngazi na daraja ya kimungu. Lakini kumbe, nje ya Utashi wa Mungu, katika utaratibu wa kibinadamu, fadhila hizo huwa zinaingiliwa na mambo ya kujikweza, majigambo, na matamaa mbalimbali. Oh! Ni kazi nyingi ngapi njema, ni Sakramenti nyingi ngapi zilizotolewa kwa watu ambazo budi kuzitolea machozi mbele ya Mungu, na ambazo budi kuzilipia fidia, tu kwa vile zimekosa kabisa kuwa na Utashi wa Mungu na kwa hiyo zinakosa kuleta matunda yao. Laiti Mbingu zingependa na kuruhusu watu wote wafikie kuelewa maana ya utakatifu wa kweli. Oh! Ni mambo mengi mengine mangapi yangefikia kufifia kabisa.
Ni kwa sababu hiyo watu wengi sana wanajikuta wapo katika njia potovu ya utakatifu. Wengi wanauweka utakatifu katika vitendo mbalimbali vya ibada ibada - na ole yao watu wale wanaojaribu kuwahamisha kutoka misimamo yao. Oh! Ni jinsi gani wanavyodanganyana. Kama tashi zao hazijaunganika kuwa kitu kimoja na Yesu, na kama hawajageuzwa kuwa Yeye – ambayo ndiyo sala endelevu – licha ya vitendo vyao vyote vya ibadaibada, utakatifu wao ni kitu cha wongo kabisa. Tena, inaonyesha jinsi watu hawa, kutoka vitendo vyao hivyo vya ibadaibada, huwa wanaishia kuingia kwenye makosa, kwenye vichekesho, kupandikiza chuki na magomvi na mambo mengine. Oh! Ni jinsi gani utakatifu wa aina hiyo unavyoweza kudharaulika…..
TO READ THE PASSAGE:
⬇️⬇️⬇️
https://telegra.ph/Yesu-kwa-Mtumishi-wa-Mungu-LUISA-PICCARRETA-Binti-Mdogo-wa-Utashi-wa-Mungu---KITABU-cha-MBINGU---JUZUU-na-12--Agosti-14-1917-06-15

Telegraph
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 12 – Agosti 14, 1917🖋📄📖📔
Yesu hakufanya jambo lolote lingine isipokuwa kujitoa Mwenyewe kama chombo cha Utashi wa Mungu Baba. Tofauti iliyopo kati ya kuishi katika utii kwa Utashi wa Mungu na utakatifu uliopo katika kuishi ndani ya Utashi wa Mungu. Mifano mbalimbali. Kama nilivyokuwa…
na Baba yako aonaye sirini atakujazi (Mt 6: 4)
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 22 - July 30, 1927🖋📃📖📔
…. Kutokana na hilo, mimi, nikaendelea kuufuatilia Utashi Mtukufu na mwabudiwa wa Kimungu, na Yesu Wangu Mtamu akaendelea kuniambia:
“Binti Yangu, matendo ya ndani mwa mtu anayetekeleza Utashi wa Mungu, huwa hayana ubaya au uovu wowote ule na hayana kivuli cha kasoro yoyote ile. Ni Mola peke Yake ndiye huwa ni shuhuda wa tendo fulani la ndani. Na ingawa kama hakuna mtu anayeweza kulionyesha, hakuna anayeweza kulitazama na anayeweza kulizungumzia, Mola, kama shuhuda pekee wa utendaji wa mwanadamu, utendaji wa pale ambapo hajaruhusiwa yeyote yule kupenyeza pale ndani ya mwanadamu, analionyesha hilo tendo, analiangalia na analizungumzia mbele ya Mbingu yote, na mara nyingi sana analionyesha na kulizungumzia hata kwa dunia. Mola anazungumzia yale maajabu makuu ya huo utendaji wa ndani wa huyo mwanadamu. Huko kuonyeshwa, huko kuangaliwa na kumfanya Mola awe anamzungumzia mwanadamu huwa ni tendo kuu kabisa, na huwa ni heshima kuu kabisa ambayo mwanadamu anaweza akaipata. Na huyo mwanadamu hawezi akaachwa kando kutoka zile kazi kuu ambazo Mungu atakuwa akizitimiza kwa kupitia huyo mwanadamu. Yale matendo ya ndani huwa ni majeraha, huwa ni vile vimikuki, ile mishale inayolengwa kwenye ubavu wa kimungu, na huwa ni kama matarishi wa kimbingu ambao huachiliwa toka kule kwa mwanadamu na huwa wanaruka kwenda kwa Muumba Wake kwenda kufikisha ule mhuri wa utukufu, ule mhuri wa pendo na ule mhuri wa kumpendeza na kumfurahisha Yule pekee aliyekuwa amemwumba.
Na kwa kweli, ni nani huyo anayeona, anayesikiliza, na anayethamini kila kitu unachokitenda hapo ndani mwako? Hakuna yeyote yule. Ni Mimi tu hapa ndiye Shuhuda. Mimi ndiye ninayeyasikiliza mambo yako, na ni Mimi ndiye ninayeyathamini. Ni kwa hoja hiyo, katika zile kazi Zetu kuu kabisa, Sisi huwa tunawachagua watu ambao, kwa kuonekana kwa nje, huwa hawachangii chochote kile kikubwa au cha ajabu au cha pekee, lakini, huwa ni watu wasiotenda mengi kwa nje bali ni watu wa matendo ya ndani, watu wasiolaumiwa kwa maoni ya kibinadamu, wasiolaumiwa kwa makelele mbalimbali, wasiolaumiwa kwa utukufu na kujikweza wenyewe kupitia matendo yao ya nje. Na kwa kweli, katika kazi ya Ukombozi tulimchagua Bikira wa kawaida kabisa, asiye na makuu yoyote yale ya nje, lakini alikuwa na hali yake ya ndani iliyokuwa ikizungumza, hali ambayo ilimwezesha mwenyewe kusema kitu moja kwa moja, ana kwa ana kwa Muumba Wake kwa jinsi kwamba aliweza kumshinda na kufanikisha ule Ukombozi.
Na sasa tumefanya hivyo hivyo kwa ajili ya Ufalme wa FIAT ya Kimungu. Sisi tumemchagua mtu mwingine, ni mtu wa maisha ya ndani, mtu ambaye atazungumza mengi, na atasali kumwomba Mungu alete ule Ufalme unaotarajiwa na kutamaniwa. Matendo ya nje, hata yakiwa ni mema na matakatifu hayataweza kunifurahisha Mimi kama vile yale matendo ya ndani, kwa vile, yale matendo ya nje, kwa kawaida na karibu kila mara, huwa yameingiliwa na kujaa hewa ya utukufu binafsi, heshima za kibinadamu, na tena pengine, huwa yamejaa na lawama fulani. Na moyo ulio duni huwa unaonja sana pale ndani mwake, matokeo ya sifa fulani au ya lawama fulani. Hata baada ya kufanya sadaka fulani, baada ya utashi wa kibinadamu kujitokeza uwanjani, na huo utashi wa kibinadamu, unapoyafunika, kwa hewa yake ya giza giza, yale matendo ya nje ya yule binadamu, ndipo matendo hayo hushindwa kufikia kiwango na ubora ule unaotakiwa. Kumbe lakini, tendo lolote la ndani, huwa halijalaumiwa na yeyote yule, na huwa halijasifiwa na yeyote yule. Na utashi wa kibinadamu huwa haujapata mahali pa kuingilia. Mtu mwenyewe mhusika, kwa kutambua kuwa hajagunduliwa na mtu yeyote yule, hudhania kuwa bado hajatenda jambo lolote kubwa na la pekee. Na kwa hiyo matendo yake huwa yote yamejaa kabisa ile hali na hewa ya Mbinguni. Kwa minajili hiyo, wewe uwe makini sana, na ujitahidi kwamba ule undani wako, uwe daima ukitembea kuuzungukia Utashi Wangu”.

Maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. (Mt 6; 8)
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu na. 19 – Septemba 13, 1926🖋📄📖📔
full text:
⬇️⬇️⬇️
https://telegra.ph/Yesu-kwa-Mtumishi-wa-Mungu-LUISA-PICCARRETA-Binti-Mdogo-wa-Utashi-wa-Mungu---KITABU-cha-MBINGU---JUZUU-na-19--Septemba-13-1926-06-26

Nafsi ya Mungu ipo katika mizani. Zawadi ya FIAT ya Kimungu ndiyo inayoweka kila kitu shirika. Katika kutoa, Hukumu ya Haki, inapenda likute egemeo la matendo ya wanadamu. Baada ya kumaliza ziara yangu katika Utashi Mkuu wa Juu, nikawa ninasali kwa Yesu Mwema.…
"Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni" (Mt 6; 10)
UFALME WAKO UJE
⬇️⬇️⬇️
Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
Mapenzi yako yatimizwe,
hapa duniani kama huko mbinguni.
(Mt 6; -10)
⬇️⬇️⬇️📚
http://divinewilldivinelove.com/Kiswahili-/-Swahili/
Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!
🤍☀️🤍☀️🤍☀️
Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA
⬇️⬇️⬇️
Swahili - Telegram Channel – Utashi wa Mungu na Upendo wa Mungu:
https://t.me/UTASHIWAMUNGUNAUPENDOWAMUNGU
Swahili - Telegram Channel – Saa 24 Za Mateso:
https://t.me/Saa24ZaMateso_Official/5
Swahili - Telegram Channel - Bikira Maria Katika Ufalme wa Utashi wa Mungu
https://t.me/BikiraMaria_Official/6

Ewe Yesu, katika Utashi Wako, mimi ninakupenda kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya watu wote.
☀️💫☀️
Ewe Yesu, katika Utashi Wako, mimi ninakuabudu kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya watu wote.
☀️💫☀️
Ewe Yesu, katika Utashi Wako, mimi ninakushukuru kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya watu wote.
☀️💫☀️
Ewe Yesu, katika Utashi Wako, mimi ninakuheshimu kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya watu wote.
☀️💫☀️
Ewe Yesu, katika Utashi Wako, mimi ninakufariji kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya watu wote.
☀️💫☀️
Ewe Yesu, katika Utashi Wako, mimi ninakulipa fidia, kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya watu wote.
☀️💫☀️
Ewe Yesu, katika Utashi Wako, mimi ninakusifu kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya watu wote.
☀️💫☀️
Ewe Yesu, katika Utashi Wako, mimi ninakutukuza kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya watu wote. Ninakutukuza kwa utukufu ule ule ambao Wewe unao daima ndani ya Utashi Wako wa Kimungu wa Milele.
☀️💫☀️
Kila hatua, kila pumzi, kila pigo la moyo, kila tendo langu la kujimudu, na lifanyike katika Utashi Wako Mwabudiwa wa Kimungu, ili iwe kana kwamba watu wote wangekusifu, wangekuita, wangekutukuza na wangekushukuru.
☀️💫☀️
Kwa vile Wewe unataka shukrani tu, uabudu na sifa kwa ajili ya kila kitu na kwa niaba ya watu wote.
☀️💫☀️
Asante sana, Ee Yesu, kwa ajili yangu mwenyewe na kwa ajili ya watu wote!!!

"Bali jiwekeeni hazina mbinguni" (Mt 6, 20)
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 7 - Agosti 11, 1906🖋📃📖📔
Nilipojiona kuwa katika ile hali yangu ya siku zote, nikamwona Yesu Wangu Mwabudiwa akiwa na Msalaba mkononi mwake, Msalaba uliokuwa umejaa mapambo ya johari nyeupe. Alipoutoa kwangu huo Msalaba kama zawadi, aliuweka juu ya kifua changu, na wenyewe ukazama ndani ya moyo wangu mithili ya kuingia ndani ya chumba. Halafu aliniambia:
“Binti Yangu, huo Msalaba ni hazina, na mahali pa usalama kabisa unapoweza kuhifadhi hiyo hazina ya gharama ni katika roho yako wewe mwenyewe.
Au tusema, roho yako ni mahali salama kabisa wakati mtu yu tayari kuipokea hazina hiyo katika uvumilivu, katika utulivu na katika fadhila zile nyingine, kwani, zile fadhila ni funguo nyingi kabisa zinazoihifadhi hiyo hazina, ili kwamba isipate kuharibiwa au kuachwa katika hatari ya wevi.
Hata hivyo, endapo hiyo hazina inashindwa kuukuta ule ufunguo wa dhahabu wa uvumilivu, basi, itapambana na wevi wengi sana ambao wataiiba na kuiharibu hiyo hazina”.

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 8 - Februari 7, 1908🖋📃📖📔
Pindi nikiendelea kuwa katika ile hali yangu ya siku zote, nilifikia kuwaza juu ya ule uzito mkubwa mno aliokuwa akiuonja Yesu Mhimidiwa pale alipoubeba Msalaba. Na ndipo nilijisemea moyoni mwangu:
‘Ee Bwana, hata uhai ni uzito pia - lakini ni uzito ulioje, hasa kwa vile Wewe upo mbali mno, Wewe uliye ndiye Chema Changu Kikuu na cha Juu’.
Katika dakika ile Yeye akaja na kuniambia hivi:
“Binti Yangu, ni kweli kabisa kwamba maisha ni uzito mkubwa, lakini pale ambapo uzito huo unabebwa pamoja Nami, na pale ambapo mtu anatambua kwamba mwishoni mwa maisha yake anaweza akautua, ndani Yangu Mimi, huo uzito wake, huyo atakuja kuona kwamba uzito ule umegeuka kuwa ni hazina ambayo ndanimo atavikuta vito mbalimbali, johari, almasi na aina zote za utajiri mbalimbali, kwa jinsi kwamba vitamfanya awe na heri kwa umilele”.

Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako. (Mt 6; 21)
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 17 - Mei 10, 1925 🖋📃📖📔
“Binti Yangu, lile ombwe ni Utashi Wangu Mimi unaowekwa tayari kwa matumizi yako wewe. Utashi huo unakuwa umejazwa na matendo mengi kabisa kulingana na idadi ya matendo yaliyoweza kutendeka na wanadamu kama wangekuwa wametekeleza Utashi Wetu. Hiyo bahari ya ombwe ambalo unaliona, ombwe linalowakilisha Utashi Wetu Sisi, lilikuwa limetokea kwenye Umungu Wetu kwa ajili ya manufaa ya wote waliopo katika Uumbwa, ili kuweza kumfurahisha kila mmoja na kila kitu.
Kwa hiyo basi, kama matokeo yake, wanadamu wote wangepasika kulijaza hilo ombwe kwa njia ya malipo ya matendo yao na kwa njia ya kusalimisha zile tashi zao kwa yule Muumba Wao. Kumbe lakini, kwa vile hao wanadamu hawakutenda hivyo, na kwa kosa hilo wakawa wametupatia chukizo kubwa mno kupita yote, Sisi tumekuita wewe na kukupatia utume mahususi na wa pekee kabisa, ili kwa utume huo Sisi tuweze kufidiwa na tuweze kulipwa kwa mambo yale ambayo wale wengine wanatuwia Sisi.
Na hiyo ndiyo hoja kwa nini Sisi, kwanza kabisa, tulikuandaa wewe kwa mlolongo mrefu wa neema mbalimbali, na kishapo, tulikuomba wewe iwapo ungependa kuishi ndani ya Utashi Wetu. Na, kwa bahati, wewe ulikubalia kwa kauli ya ‘ndiyo’, na hivyo ukawa umeufunga utashi wako kwenye miguu ya kiti Chetu cha utawala.
Ukawa umeamua kutokuujua tena utashi wa kibinadamu, kwa vile, utashi huo wa kibinadamu na Utashi wa Kimungu huwa haviendani, na wala huwa haviishi pamoja. Basi, ile ‘ndiyo’ - yaani, utashi wako - unaendelea kuwepo, ukiwa umefungwa kwa nguvu kabisa kwenye kiti Chetu. Na ni kwa hoja hiyo, roho yako wewe, kama kasichana kadogo, huwa inavutwa kufika mbele ya Ukuu Mtukufu wa Juu - kwa vile pale mbele Yetu kuna ule utashi wako ambao unakuvuta wewe kama sumaku.
Na wewe mwenyewe, badala ya kuuangalia ule utashi wako, wewe huwa unashikwa tu na ile shughuli ya kuvileta, pale juu ya goti Letu, vile vitu vyote ulivyoweza kuvitekeleza pale ndani ya Utashi Wetu. Ndipo wewe huwa unauweka ule ule Utashi Wetu, pale ndani ya kifua Chetu, kama ndiyo heshima kuu inayotustahili Sisi, na kama malipo yanayotupendeza Sisi kupita yote mengine. Ile hali yako ya kutojali kabisa ule utashi wako wa kibinadamu, na ukweli kwamba Utashi Wetu ndio pekee unaoishi pale ndani yako, ndiyo mambo ambayo yanatuingiza Sisi katika hewa ya sherehe. Yale matendo yako madogo uliyoyatenda ndani ya Utashi Wetu, ndiyo yanayotuletea Sisi, zile furaha za Uumbwa mzima.
Ndipo hapo, inapoonekana kuwa, kila kitu huwa kinatuchekea na kutabasamu Kwetu Sisi na huwa kinafanya sherehe kwa ajili Yetu Sisi. Na tunapokuona ukiteremka toka pale penye kiti Chetu, bila wewe hata kuelekeza macho yako kule kwenye utashi wako wa kibinadamu, badala yake ukiwa unaubeba kikamilifu Utashi Wetu na kwenda nao, hiyo huwa ni sababu ya furaha kuu kabisa Kwetu Sisi.
Ni kwa sababu hiyo Mimi huwa ninakuambia daima kwamba: ‘Uwe makini ndani ya Utashi Wetu’ - na kwa vile, ndani ya Utashi Wetu kuna mambo mengi sana ya kutenda. Na kadiri unavyoyatenda mengi zaidi, ndivyo utakavyozidi kutuandalia sherehe kubwa zaidi, na Utashi Wetu utaanza kukumwagia mambo katika mikondo ya maporomoko. Utakuwa unakumwagia ndani yako sawa na nje yako”.

…“Binti Yangu, kila kitu nilichokwisha kukueleza mintarafu Utashi Wangu, zimekuwa ni zawadi nilizokupa.
... Utashi Wangu ni vitu vya kimungu, ndiyo maana, maumbile ya kibinadamu huwa yanazawadiwa ufanano na maumbile ya kimungu.
... Sheria, maagizo au amri ni kwa ajili ya watumishi, watumwa na waasi: Katika Ufalme wa FIAT Kuu, hapatakuwa watumishi, wala watumwa, wala waasi, kwani Utashi utakuwa ni mmoja tu, yaani ule wa Mungu na ule wa mwanadamu, na kwa hiyo, uhai nao utakuwa ni mmoja.
..Pia ni hoja hiyo kwa nini Mimi nazungumza sana mambo mengi juu ya Utashi Wangu.
..Kwa sababu hiyo, Mimi nisingeweza kutoa neema kubwa zaidi ya hii, katika nyakati hizi za dhoruba za maovu mengi namna hii, na dhoruba ambayo watu wanaikimbilia kama vichaa. Ninayotoa ni neema ya kuwafahamisha kuwa napenda kuwapatia zawadi kuu ya Utawala wa FIAT Kuu.
...Kwa hiyo, uwe makini”.….
(KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 19 - Septemba 9, 1926)

❤️Ewe Malkia wa Utashi wa Mungu, nichukue ukaniweke juu ya magoti yako ya kimama na ukanifundishe namna ya kuishi katika Utashi wa Mungu tu.❤️
Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. (Mt 6; 24)
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 20 - Januari 28, 1927🖋📄📖📔
…”Ni zaidi sana kwa vile, kwa mtu yule anayeubeba Utashi wa Mungu, FIAT huwa inamgawia, kwa ajili ya roho na kwa ajili ya mwili, jicho kali kabisa lipenyezalo, kwa jinsi kwamba, mtu huyo, huwa anapenya ndani ya vitu asilia ambavyo hatimaye, mithili ya pazia, huwa vinaifunika na kuificha ile FIAT. Na kwa kuyapasua hayo mapazia husika, pale ndani ya vitu asilia, huyo Binti atamwona yule malkia adhimu wa Utashi wa Mungu anayetawala na anayeamrisha ndani yake. Kwa hiyo, vitu asilia vinatoweka kutoka kwake Binti, na katika vitu vyote atakuwa akiukuta ule Utashi mwabudiwa aliokuwa nao yeye mwenyewe. Ataubusu, atauabudu, na kila kitu kinageuka kuwa ni Utashi wa Mungu kwa ajili ya mtu huyo. Basi, chochote kile cha asilia kilicho cha ziada, huwa ni tendo moja jipya la Utashi wa Mungu ambao anaubeba. Kwa hiyo, vitu asilia huwa ni nyenzo kwa mmoja aliye ni mtoto wa Utashi Wangu, kwa ajili ya kufahamisha zaidi kile ambacho Utashi Wangu unatenda, kile ambacho unaweza ukatenda, na ambacho unakimiliki, na pia ili kufahamisha ni hadi mahali gani ambapo, hadi kupindukia, Utashi Wangu unavyompenda mwanadamu.
Sasa je wewe ungependa kujua kwa nini wanadamu wanayakosa mahitaji yao ya kawaida, kwa nini, mara nyingi sana, mahitaji hayo huwa wananyang’anywa, na hata wenyewe huwa wanarudia kwenye hali mbaya kabisa ya adha nyingi?.
Kwanza ni kwa vile wao hawana ule ujazo wa FIAT Kuu ya Juu. Pili, ni vile wanavivuruga vitu asilia hata wanaiweka asili kuwa badala ya Mungu. Na wala hawautafuti Utashi Mkuu wa Juu pale ndani ya vitu, ila, katika uchoyo, wanajibandika kwenye vitu hivyo, kwa ajili ya kujitengenezea utukufu bandia, wanatafuta heshima inayowapofusha, na wanatafuta mungu bandia kwa ajili ya mioyo yao. Kutokana na hilo, ni lazima kwamba mahitaji ya lazima yawe yakikosekana kwa ajili ya kuziweka roho zao katika usalama. Lakini kwa yeye aliye ni mwana wa Utashi Wangu, hatari zote hizo zitakuwa hazipo kabisa. Kwa hiyo basi, Mimi ninawataka wajazwe tele tele kwa vitu vyote na wala wasikikose kitu chochote”.

Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. (Mt 6; 33)
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 13 - Oktoba 18, 1921🖋📄📖📔
Kwa kutwa nzima nilishinda nikiwa na mawazo mbali sana kutokana na mambo niliyokuwa nimeyasikia - mambo ambayo si lazima niyasimulie hapa - na pia nilikuwa nimevurugika kidogo. Licha ya jitihada zangu zote sikufanikiwa kujikomboa kutoka hali hiyo. Kwa hiyo, kwa kutwa nzima sikuwa nimemwona Yesu Wangu Mtamu, Yeye aliye Uhai wa roho Yangu. Zile vurugu zangu zilikuwa ni kama pazia lililosimama kati yangu na Yeye ili kunizuia mimi niweze kuwa ninamwona. Kishapo, katikati ya usiku wa manane, akili yangu iliyokuwa imechoka, ikafikia kutulia. Ndipo Yesu Wangu Mpendevu, kana kwamba ni mtu aliyekuwa akiningoja, alijitokeza, na katika uchungu na masikitiko, aliniambia:
“Binti Yangu, leo, kwa vurugu zako, umekuwa ukizuia Jua la Nafsi Yangu lisichomoze ndani yako. Vurugu huwa ni wingu linalokuja kati Yangu na wewe, linalozuia mionzi toka Kwangu isiweze kushuka na kuingia ndani yako.
Na kama mionzi haiteremki utawezaje wewe kuliona Jua?
Kama ungejua ni nini kulizuia Jua Langu lisichomoze, kama ungejua athari kubwa kwako na kwa dunia nzima, hakika wewe ungekuwa makini kabisa usijiingize katika vurugu.
Kwa kweli, kwa watu waliovurugika, hali yao huwa ni ya usiku.
Na usiku jua huwa halichomozi. Kwa upande mwingine lakini, kwa watu wale wenye amani rohoni, kwao hali huwa daima ni mwanga wa kutwa.
Na Mimi, yaani Jua Langu, katika saa yoyote ile ninapopenda kujichomoza, namkuta mtu huyo yu tayari daima kupokea lile jema la ujio Wangu.
Aidha, hali ya vurugu, siyo kitu kingine, isipokuwa huwa, ni kukosekana kwa hali ya kuachika ndani Yangu.
Na Mimi ninakutaka wewe uwe umeachika kabisa ndani ya mikono Yangu hata usiwe tena na wazo hata moja juu yako wewe mwenyewe. Ni Mimi ndiye nitakayeshughulikia kila kitu. Usiogope.
Yesu Wako hawezi kamwe akakaa bila kukutunza wewe, na bila kukulinda wewe dhidi ya mambo yote.
Wewe ni wa gharama sana Kwangu - nimewekeza mno ndani yako.
Ni Mimi peke Yangu ndiye mwenye haki juu yako. Kwa hiyo basi, kama haki zote ni za Kwangu, hifadhi yote ni ya Kwangu. Kwa hiyo, kaa katika amani na usiogope”.

🔥🔥🔥🙏🙏🙏
Naingia Ndani ya Bahari Kuu ya Utashi Wako
🔥🔥🔥🙏🙏🙏
Ewe Yesu Wangu Mtamu,
mimi ninaingia ndani ya bahari kuu ya Utashi Wako, Ninapigilia utashi wangu ndani ya Utashi Wako na ninakuomba unipe Utashi Wako kama Uhai wangu, kama Uhai wa kila tendo langu, liwe lile la ndani au lile la nje, liwe lile la kiutashi au lile lisilo la kiutashi.
Ee Bwana,
naomba kwamba kila kitu kiwe ndani ya Utashi Wako wa Kimungu, ili niweze kukulipa kwa pendo, kwa uabudu, na kwa utukufu kana kwamba wanadamu wote wangekulipa hilo deni kwa utimilifu wote.
🔥🔥🔥🙏🙏🙏
(Kitabu cha Mbingu - Juzuu Na. 14 - Mei 27, 1922)

Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo (Mk 4, 35)
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 20 – Novemba 3, 1926🖋📄📖📔
Mimi nikawa ninaendelea kuishi kama mtu aliyejiachia na kujikabidhi kabisa ndani ya Utashi mwambudiwa. Na pindi nikisali, nikawa ninawaza moyoni mwangu: ‘Ni jinsi gani ningetamani kuteremka kwenda kule kwenye magereza ya roho za tohorani ili nikawafungulie wote, na, katika mwanga wa Utashi wa Milele, niweze kuwaleta wote kwenye Makao ya Mbinguni’. Katika dakika ile, Yesu Wangu Mtamu, alipoingia ndani mwangu, aliniambia:
“Binti Yangu, kadiri watu waliofariki wanavyozidi kukabidhiwa kwa Utashi Wangu, na kadiri watakavyokuwa wametekeleza matendo mengi zaidi ndani ya Utashi Wangu, ndivyo watakavyokuwa wametengeneza njia nyingi zaidi kwa ajili yao wenyewe, kwa ajili ya kupewa malipo ya roho zao kutokea hapa duniani. Yaani, kwa kadiri watakavyokuwa wametekeleza Utashi Wangu, na kwa hiyo, kwa kadiri watakavyokuwa wamejitengenezea wenyewe zile njia za mawasiliano ya yale mema yaliyopo ndani ya Kanisa na ambayo ni mali Yangu Mimi, hapatakuwa na njia yoyote iliyotengenezwa nao ambayo haitawaletea wengine kitulizo, wengine sala fulani, na kwa wengine punguzo la maumivu.
Hayo malipo yanatembea kupitia njia hizo tukufu za kifalme za Utashi Wangu, ili kumfikishia kila mmoja lile stahili, lile tunda, na ule mtaji ambao kila mmoja wao atakuwa ametengeneza kwa ajili yake mwenyewe ndani ya Utashi Wangu.
Kwa hiyo, bila huo Utashi Wangu, hazipo njia na wala hazipo nyenzo kwa ajili ya kuweza kuyapata malipo. Ingawa kama malipo na kila kitu kingine ambacho Kanisa linatenda, huwa daima yanateremkia tohorani, ni kweli, lakini, huwa yanakwenda kwa wale ambao watakuwa walitengeneza njia kwa ajili yao wenyewe. Kwa wale wengine, ambao hawajatekeleza Utashi Wangu bado, zile njia zimefungwa, au hazipo kabisa.
Na kama hao watakuja kuokoka, itakuwa tu kwa vile, angalau katika dakika ya kufa ya watu husika, watakuwa wamekiri mamlaka makuu ya juu ya Utashi Wangu, watakuwa wameuabudu, na watakuwa wamejikabidhi wenyewe kwa Utashi Wangu - na tendo lao hilo la mwisho ndilo litakuwa limewaokoa. Vinginevyo wasingeweza kabisa kuokolewa. Kwa yule ambaye amekuwa akitekeleza daima Utashi Wangu, kwake huyo hakuna njia zinazompeleka tohorani - njia zake huyo zinakwenda moja kwa moja Mbinguni. Na kwa yule ambaye ameukiri Utashi Wangu, na hata amejikabidhi kwake, na kama hakujikabidhi katika kila kitu na wala siyo kwa daima, bali kwa sehemu kubwa, huyo atakuwa amejitengenezea njia nyingi sana, na atakuwa anaendelea kupokea maombi kwamba tohorani impeleke Mbinguni mara moja.
Basi, kama vile watu waliopo tohorani, kwa ajili ya kupokea yale malipo walipasika kujitengenezea njia, ndivyo na wale walio bado hai. Kwa ajili ya kuweza kupeleka malipo kwa marehemu tohorani, ni budi watekeleze Utashi Wangu, kwa ajili ya kutengenezea njia mbalimbali ili hayo malipo yaweze kupanda juu mpaka tohorani.
Endapo watatekeleza malipo, lakini wakati huo wakiwa mbali kabisa na Utashi Wangu, kwa vile mawasiliano na Utashi Wangu yatakuwa yamekatika, jambo ambalo ndilo pekee huunganisha na kumfunga kila mtu, hayo malipo yao yatashindwa kuiona njia ya kupandia kwenda juu, yatashindwa kuiona miguu ya kuweza kutembelea, na yatashindwa kupata nguvu ya kuweza kutoa kitulizo.
Yote yatakuwa ni malipo yasiyo na uhai wowote, kwa vile uhai halisi wa Utashi Wangu utakuwa unakosekana, Utashi ambao pekee ndio wenye ile nguvu ya kuweza kutoa uhai kwa yale mema yote. Kwa kadiri mtu anavyoubeba Utashi Wangu zaidi na zaidi, ndivyo kutakuwa na thamani zaidi na zaidi katika sala zake, katika kazi zake, na katika maumivu yake. Kwa njia hiyo, mtu huyo huweza kufikisha kitulizo zaidi kwa wale watu waliobahatika.

Mimi huwa ninapima na kuthaminisha kila jambo analoweza kufanya mtu kulingana na kiasi cha Utashi Wangu anachokibeba. Endapo Utashi Wangu unatenda kazi ndani ya kila moja ya matendo yake, kipimo ninachochukua huwa ni kikubwa kweli kweli. Na tena zaidi zaidi, huwa sikomi kamwe kupima, na huwa ninatia thamani kubwa kabisa ndani ya jambo hilo, kiasi kwamba uzito wake hauwezi ukakadirika. Kinyume chake, endapo mtu hatajali sana juu ya Utashi Wangu, basi kipimo kitakuwa hafifu na thamani itakuwa na bei ndogo tu. Na kama mmoja hajali kabisa kabisa, basi, mtu huyo hata akitenda mambo mengi awezayo, Mimi nitakuwa sina kitu cha kupima na wala sitakuwa na thamani yoyote ya kutoa. Kwa hiyo, kama mambo hayo hayatakuwa na thamani, yatawezaje kuleta kitulizo chochote kwa wale watu ambao, kule tohorani, hawawezi kutambua chochote, na wala hawawezi wakapokea chochote, isipokuwa kile tu kinacholetwa na FIAT Yangu ya Milele?
Lakini, je wewe wajua ni nani huyo awezaye kuleta vitulizo vyote, anayeweza kuleta mwanga unaotakasa, na anayeweza kuleta lile pendo linalobadilisha mambo? Ni yule anayebeba ndani yake uhai wa Utashi Wangu katika kila kitu na ambaye ndani yake Utashi Wangu unaamrisha kwa ushindi mkubwa. Mtu huyo hahitaji hata kuwa na zile njia, kwa vile, kwa kuubeba Utashi Wangu, yeye anayo haki juu ya njia zote. Anaweza akaenda kwenye kila kona, kwa vile ndani yake, anabeba ile njia tukufu ya kifalme ya Utashi Wangu kwa ajili ya kuweza kwenda hata kule ndani ya gereza lenye lindi, ili kuwafikishia marehemu tohorani vile vitulizo vyote na kuwaletea uhuru wao. Zaidi zaidi kwa vile, pale tulipomwumba binadamu, Sisi, tulikuwa tumempatia Utashi Wetu kama urithi wake mahususi kabisa, na Sisi tunatambua kila jambo alilokuwa ametenda ndani ya mipaka ya ule urithi Wetu tuliokuwa tumemzawadia.
Jambo lingine lolote lile halitambuliki Kwetu Sisi - hilo si jambo la Kwetu, na wala hatuwezi tukaruhusu chochote kile kuingia Mbinguni ambacho hakijatendeka na wanadamu au ndani ya Utashi Wetu, au walau, kwa ajili ya kutekeleza Utashi Wetu. Tangu pale Uumbwa ulipotoka kwenye FIAT ya Milele, Utashi Wetu, katika wivu wake, huwa hauruhusu kitendo kiingie katika Makao ya Baba wa Mbinguni, ambacho hakijapitia katika FIAT yake yenyewe.
Oh! Laiti kama watu wote wangefahamu ni nini maana ya Utashi wa Mungu, na laiti wangefahamu jinsi kazi zote, hata zile tu zinazoonekana kana kwamba ni nzuri wakati kwa kweli, ndani yao, hazina Utashi wa Mungu kabisa, wakati ni kazi zisizo na mwanga wowote, zisizo na thamani yoyote, zisizo na uhai wowote. Na kazi zile zisizo na mwanga, zisizo na thamani, na zisizo na uhai, hizo haziingii kamwe Mbinguni. Oh! Ni jinsi gani watu hao wangekuwa makini katika kutekeleza Utashi Wangu katika kila jambo na kwa daima!”.

Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji (Mk 4, 37)
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 8 - Machi 15, 1908🖋📃📖📔
Leo asubuhi, nilikuwa nikionja maumivu makali kupita siku nyingine zote kutokana na kumkosa Yesu aliye ndiye Chema Changu Kikuu mno na cha pekee. Lakini, kwa wakati huo huo, nilikuwa nimetulia na nikiwa ni mwenye raha tu, sikuwa na yale mahangaiko yaliyokuwa yakinifanya niwe ninazungukazunguka Mbinguni na duniani kumtafuta Yeye hadi pale nilipofikia kumkuta, ndipo tu nilikuwa naweza nikasimama na kutulia. Basi nikawa ninajisemea moyoni mwangu: ‘Ni mabadiliko makubwa yalioje - mimi mbona ninajionja kufa ganzi mithili ya jiwe kutokana na maumivu yanayosababishwa na kukosekana Kwako. Hata hivyo mimi sitalia machozi. Ninaionja amani ya kina inayonifunika gubigubi. Pumzi kinzani hata moja tu haiingii ndani mwangu’. Katika dakika ile Yesu Mhimidiwa alinijia na kuniambia hivi:
“Binti Yangu, angalia usiwe unapenda kujisumbua wewe mwenyewe. Ni budi ukafahamu kuwa wakati kunapokuwa na dhoruba kali pale baharini, pale panapokuwa na maji ya kina, hapo dhoruba huwa ni ya juujuu tu. Vina mbalimbali vya bahari huwa vinakuwa katika utulivu kamili mno. Pale maji hutulia tuli, na samaki, wanapoihisi dhoruba inakuja, huwa wanakimbilia kwenda kujificha pale ambapo maji ni ya kina zaidi ili pale wakawe salama zaidi. Kwa hiyo, dhoruba yote huwa inakwenda kujipakua yenyewe kule ambako bahari ina maji machache mno, kwa vile, maadam huko kuna maji machache, dhoruba inaweza kuwa na nguvu ya kuitikisa hiyo bahari toka juu mpaka chini kabisa, na huweza hata kuyahamisha maji kutoka mahali pamoja na kuyapeleka kwenye kona mbalimbali nyingine za bahari.
Ndivyo huwa inatokea kwa watu mbalimbali wakati wanapokuwa wamejazwa kitimilifu na Mungu - wanapokuwa wamejazwa pomoni mpaka ukingoni, kiasi cha kuweza kufurikia nje: dhoruba huwa hazina nguvu ya kuwavuruga hata kwa kiwango kidogo kabisa, kwa vile, hakuna nguvu yoyote inayoweza ikamshinda Mungu. Sana sana, watu hao, huweza tu labda wakaionja hiyo dhoruba kwa juujuu sana. Na zaidi, wakati mtu anapoihisi hiyo dhoruba, huwa anaziweka zile fadhila mbalimbali katika mpangilio na taratibu, na yeye mwenyewe anakwenda kujipumzikia pale ndani kwenye vina vya ndani kabisa vya Mungu. Basi, ingawa kama kwa nje huonekana kana kwamba kuna dhoruba, huwa kwa kweli ni uongo kabisa - kwani huwa ni wakati huo ambapo mtu huwa anafurahia amani zaidi, na huwa anapumzika kwa raha na utulivu, pale penye kifua cha Mungu, sawa kabisa kama yule samaki pale ndani ya kifua cha ile bahari.
Mambo huwa ni kinyume kabisa kwa watu wale ambao wapo tupu kabisa bila Mungu ndani yao, au wale ambao wanabeba sehemu ndogo sana ya Mungu: zile dhoruba huwa zinawayumbisha watu hao, popote pale, huko na kule. Na kama watu hao wakiwa na sehemu ndogo tu ya Mungu, wao huwa wanapoteza bure tu hata hicho kidogo walichoambulia. Na wala huwa hapahitajiki dhoruba za nguvu kwa ajili ya kuweza kuwatikisa watu kama hao. Huwa inatosha kaupepo kadogo tu hata kusababisha fadhila mbalimbali zikimbie kuwatoroka watu hao. Aidha, hata yale mambo matakatifu yenyewe, ambayo huwa kwa kawaida ndiyo malisho mazuri na matamu kwa ajili ya wale watu wengine, waliotangulia kutajwa, ambao ndio huwa wanafurahia mpaka kushiba kabisa, kwa hawa wengine, hayo yote hugeuka na kuwa ndiyo dhoruba. Hao huwa wanapigwa na kudondoshwa chini na kila upepo. Hakuna upande hata mmoja ambako kunakuwa na utulivu timilifu, kwa vile, hoja ya akili hudai kwamba, pale ambapo Mungu Mzima hayupo kabisa, urithi wa amani huwa upo mbali kabisa kabisa toka kwa watu kama hao”.