BARAKA KATIKA UTASHI WA MUNGU
(Kutoka KITABU CHA MBINGU – Juzuu Na. 14 –T. 6 Julai 1922
na Juzuu Na. 12 – T. 28 Novemba 1920 imerekebishwa)
Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Ninataka nikubariki wewe kwa baraka ile ile aliyotoa Yesu kwa Mama Yake Mtakatifu sana kabla ya yale Mateso Yake.
Kwa maombezi ya Bikira Maria Mtakatifu Mama na Malkia wa Utashi wa Mungu, ninakubariki ili kukugonga mara tatu ule mhuri wa Nafsi Tatu za Mungu, kusudi uweze kuzinduka tena kutoka uozo wako na ukaishi katika Utashi wa Mungu.
Baraka hii katika Jina la Baba, inakuletea na kukutilia mhuri wa Enzi Yake ndani ya Utashi wako.
Na hivyo Baraka hiyo inamrejesha Mungu Baba kama Mtawala Mkuu wa kila kitu.
Baraka hii katika Jina la Yesu Mungu Mwana, ikuletee na kukutia mhuri wa Hekima katika akili yako, na Baraka hii katika Roho Mtakatifu ikuletee na kukutia mhuri wa Pendo lake ndani ya kumbukumbu yako.
Baraka hii irejeshe nguvu za mwili wako na za roho yako; uponywe kutokana na magonjwa yote ya mwilini na ya rohoni; na roho yako itajirishwe na kupambwa kwa mema yote na kwa fadhila zote.
Na kwa lengo la kukuzungushia ulinzi dhidi ya shetani, dhidi ya dunia na dhidi ya mwili, mimi, pamoja na Yesu ninabariki vitu vyote vilivyoumbwa Naye.
Kwa ajili yako naubariki Mwanga, ninaibariki hewa, maji, moto, chakula, na vitu vingine vyote ili vibaki vikiwa vimezamishwa na kugubikwa na baraka hizi zote.
Pamoja na Yesu, ninaubariki huo moyo wako, akili yako, macho, masikio, pua, mdomo, mikono, miguu, mwili wako, viungo vyako, pumzi yako, ujimudu wako na nafsi yako yote.
Ninakubariki ili kukusaidia, ninakubariki ili kukulinda, ili kukusamehe, ili kukuopoa kutoka maovu yote.
Na ninakubariki ili kukufariji na ninakubariki ili kukufanya uwe mtakatifu.
Ninakubariki kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.
Amina.
⬇️⬇️⬇️📚
https://t.me/UTASHIWAMUNGUNAUPENDOWAMUNGU/96
Pro Manuscripto - Kwa matumizi binafsi tu
Email: albert.norbert@hotmail.com
Website: www.divinewilldivinelove.com
TELEGRAM Channel: t.me/utashiwamungunaupendowamungu
RUMBLE Channel: https://rumble.com/c/c-5818809

Telegram
Utashi wa Mungu na Upendo wa Mungu - Luisa Piccarreta
Wiito wa Mfalme Mtukufu Mintarafu Ufalme wa Utashi Wake
Wapenzi Wanangu Wapendwa,
Ninakuja kati yenu nikiwa na Moyo Wangu uliozama kabisa katika miali ya moto wa Pendo. Ninakuja kama Baba kuwa kati yenu ninyi wanangu kwa vile ninawapenda mno. Pendo Langu kwenu ni kubwa hivi kiasi kwamba ninakuja kukaa na kubaki na ninyi ili tuishi pamoja tukiwa na Utashi mmoja pekee. Tuishi tukiwa na Pendo moja pekee...... Katika kuja kwangu kwenu ninawaleteeni pia Mateso na Maumivu Yangu, nawaleteeni Damu Yangu, Kazi Zangu na hata Kifo Changu chenyewe. Ebu nitazameni Mimi. Kila tone la Damu Yangu, kila Teso na Umivu Langu, na kila Hatua Yangu na mambo yote niliyofanya, vyote hivyo hushindana kati yao ili viweze kuwapatieni ninyi Utashi Wangu wa Kimungu. Na hata Kifo Changu hutaka kuhuisha tena ule Uhai wa Utashi Wangu ndani yenu.
Katika Ubinadamu Wangu, nimeandaa kila kitu kwa ajili yenu. Pia nimewaombeeni na kwa ajili yenu nimezipata tayari zile neema, ile misaada, ile nuru na nguvu za kuwawezesha ninyi kupokea ile Zawadi Kuu kabisa. Kwa upande Wangu Mimi, nimetekeleza tayari kila kitu. Basi sasa ninawangojeeni na ninyi nanyi mtekeleze litakiwalo kwa upande wenu. Ni nani kati yenu, atakayekuwa mtovu wa shukrani, hivi hata anigomee na kunisukumia mbali, na wala asinikaribishe na kuipokea ile Zawadi ninayowaleteeni? Fahamuni kwamba Pendo Langu ni Kuu mno hata nitasahaulia mbali maisha yenu yaliyopita, nitasahau dhambi zenu na maovu yenu yote. Yote hayo nitayazika ndani ya bahari ya Pendo Langu, ili pale nikayachomelee yote na kuyaunguzia mbali. Hatimaye, kwa pamoja tutaanza maisha mapya, yote yakiwa ni maisha ya Utashi Wangu. Ni nani huyo mwenye moyo wa kunigomea na kunifukuzia mbali, hata asiupokee huo ujio Wangu ambao umejaa Pendo la Baba kwa namna hiyo? Lakini, endapo ninyi mtanipokea, Mimi nitabaki nanyi kama Baba kati ya Watoto Wake. Ndipo hakika tutakuwa katika uelewano mkuu kabisa na tutakuwa tunaishi pamoja tukiwa na Utashi mmoja basi.
Oh, ni jinsi gani ninavyolitamani neno hilo! Ni jinsi gani nanavyoomboleza, ni jinsi gani ninavyolia, ni jinsi gani ninavyotetemeka, na kutoa machozi, nikitaka sana Watoto Wangu Wapenzi waje kunizunguka Mimi, na kuishi katika Utashi Wangu Wenyewe. Imekwisha kupita yapata miaka elfu sita. Ni miaka ambapo Ubinadamu Wangu umekuwa unatweta mno, na umekuwa ukimwaga machozi mengi mno ya uchungu, kwa vile ninapenda Watoto Wangu warudi, na kuja kuishi pamoja Nami. Nawataka waje wanizunguke ili niwafanye watakatifu na wenye furaha tena. Ninalia na kulia tena na tena ninapowaita wanirudie Mimi. Ni mtu gani huyo ambaye hataki kuguswa, na kunionea huruma juu ya machozi yangu ninayotoa, na juu ya Pendo Langu ambalo ni kali hivi, hata linafikia kunikaba koo langu la hewa, na hata linanisababishia kikohozi kikali. Pindi nikiwa katika kuhema hivyo, na pindi ninapopata Maumivu makali hayo ya Pendo, najikuta naendelea kurudiarudia kusema: “Watoto Wangu, mko wapi? Ni kwa nini hamtaki kurudi kwa Baba Yenu? Kwa nini mnanitoroka? Kwa nini mnataka kutangatanga katika umasikini, huku mkiwa mmejaa matatizo mengi mno? Mikosi yenu hiyo ni majeraha kwa Moyo Wangu. Mimi nimechoka sana kuwasubiria”. Kwa vile ninyi hamnirudii Mimi, ni Mimi sasa ninakuja kuwatafuteni kwa vile siwezi tena kulihimili hili Pendo linalonimaliza. Na kwa hiyo, napenda kuwaleteeni sasa ile Zawadi Kuu ya Utashi Wangu. Oh, tafadhali sana, nawaombeni na ninawasihi sana. Shitukeni na kuguswa na haya machozi Yangu mengi mno, na mguswe na huku kutweta Kwangu kwa Pendo!”

Nakuja kwenu, siyo kama Baba tu, bali nakuja pia kama Mwalimu kati ya wanafunzi Wake ........... Nawaomba mnisikilize kwani nitakuwa nikiwafundisheni mambo ya kushangaza, yaani mafundisho ya Mbingu ambayo yatawaleteeni Nuru ambayo haitaweza kuzimika, na mafundisho hayo yatawaletea Pendo liwakalo na lenye kudumu kwa daima.............. Mafundisho Yangu hayo yatawapatieni nguvu ya kimungu, ujasiri usioshindikana, na utakatifu unaoendelea kuongezeka zaidi na zaidi. Mafundisho hayo yatakuwa yakiiangaza njia ya hatua zenu na kuwaongozeni katika njia iendayo kwenye Makao yenu ya Mbinguni.
Mimi nakuja kwenu kama Mfalme, ili niweze kuishi kati yenu. Siji kwa ajili ya kuwatoza makodi na kutwika mizigo juu yenu. La hasha, hapana kabisa! Ninakuja kwa vile ninataka huo utashi wenu, hayo mahangaiko yenu, hayo madhaifu yenu, na hayo maovu yenu yote. Mamlaka Yangu ni hasa katika neno hili: Ninataka kila jambo linalowaleteeni ninyi uchungu na linalowakosesheni raha, nayataka hayo yote yanifikie kusudi niweze kuficha kila moja lao ndani ya Pendo Langu, na pale niweze kuyachomelea yote na kuyaunguzia mbali. Kwa kuwa Mimi ni Mfalme ambaye ni Mtenda mema, ni Mleta amani, na niliye Mwingi wa fadhili, ninapenda nibadilishane nanyi Utashi Wangu, huku nikichukua huo wa kwenu, ili niwajazeni ninyi kwa Pendo Langu tamu kabisa, niwajazeni kwa utajiri Wangu mwingi, kwa furaha Zangu, na niwajazeni amani Yangu na raha iliyo safi kabisa.
Endapo ninyi mtanipatia utashi wenu wa kibinadamu, basi mambo yote yatatendeka kadiri nilivyosema. Ninyi mtanifurahisha Mimi na ninyi wenyewe mtafurahia pia. Mie sitamani kitu kingine chochote kile, isipokuwa kwamba Utashi Wangu upate kutawala kati yenu. Mbingu na dunia zitakuwa zikitabasamu juu yenu na kuwafurahieni. Mama Yangu wa Mbinguni atapata uhakika wa kuwa Mama na Malkia juu yenu ninyi. Yeye anajua lile jema kubwa ambalo Ufalme wa Utashi Wangu utawaleteeni. Zaidi ya hilo, kwa ajili ya kutuliza matamanio Yangu makubwa na makali, na pia kwa ajili ya kusitisha kilio Changu Mimi, na tena kwa vile anawapendeni ninyi mithili ya watoto wake halisi, sasa hivi Mama Yangu wa Mbinguni, yupo akifanya ziara kuwatembelea watu wa mataifa mbalimbali ili kuwaeleza na kuwaandaa kupokea mamlaka ya Ufalme wa Utashi Wangu. Ndiye yeye Mama aliyekuwa amewaandaa watu kwa ajili Yangu Mimi, hata nikaweza kuteremka toka Mbinguni na kuja duniani. Kwa hiyo hata sasa ninamkabidhi yeye na ninakabidhi kwa Pendo lake la kimama hilo jukumu la kuziandaa roho za watu Wetu ili ziweze kuipokea ile Zawadi kubwa ya namna hiyo.
Kwa hiyo basi, ebu nisikilizeni. Ninawaombeni ninyi Watoto Wangu, myasome kwa umakini kabisa makala haya ninayoyaleta mbele yenu. Mkitekeleza hilo, mtaonja mara hamu ya kuishi katika Utashi Wangu, na Mimi nitakuwa nikisimama kando kabisa yenu wakati huo mtakapokuwa mkisoma, nitakuwa nikigusa akili yenu na moyo wenu ili mweze kuelewa kile mnachosoma na ili papo hapo mweze kutamani hiyo Zawadi ya FIAT Yangu ya kimungu.

Binti mpenzi, ninaonja hitaji kali sana lisilozuilika la kushuka toka hapa Mbinguni, ili niweze kuja kukutembelea kama Mama yako.
Endapo utanithibitishia upendo wako wa binti na uaminifu wako kwangu, basi mimi nitakuwa nabaki pamoja nawe daima moyoni mwako ili niwe mwalimu kwako, niwe kwako kielelezo, mfano na Mama kipenzi chako.
Mimi ninakuja kukualika uingie katika ufalme wa Mama yako, yaani katika ufalme wa Utashi wa Mungu, na kwa hiyo ninabisha hodi mlangoni pa moyo wako ili unifungulie.
Je unafahamu? Mimi mwenyewe kwa mikono yangu nakuletea Kitabu hiki kama zawadi. Ninakupatia kwa Moyo wa kimama ili ukisome kwa wakati wako, na ukishasoma, ujifunze namna ya kuishi kimbingu, badala ya kuendelea kuishi kidunia.
Kitabu hiki ni kitu cha dhahabu binti yangu. Kitakuletea bahati yako ya kiroho na hata furaha yako ya hapa duniani.
Ndanimo utapata chimbuko la neema yote. Kama wewe u mdhaifu basi utajipatia nguvu; kama u katika majaribu basi utajipatia ushindi; kama umeangukia katika kosa, basi utauona mkono ule wa huruma na wenye uwezo utakaokuinua tena; kama upo katika mateso, utajipatia kitulizo; kama unaona ubaridi basi utapata njia ya uhakika ya kujipasha joto; kama umeshikwa na njaa basi utaonja chakula kitamu kabisa cha Utashi wa Mungu.
Ukiwa na Kitabu hiki basi hutakosa kitu. Hutakuwa tena mpweke, kwani Mama yako atakuwa ni mwenzi mtamu anayetangulizana nawe; na yeye, kwa upendo wake wote wa kimama, atahakikisha anakuletea furaha. Mimi, Mtawala wa Mbinguni, ndiye nitakuwa nashughulikia mahitaji yako yote, ili mradi wewe unakubalia kuishi umeungana na mimi.
Laiti kama ungejua wasiwasi wangu, matarajio yangu, matamanio yangu makali, na hata machozi ninayomwaga kwa ajili ya wana wangu! Laiti ungefahamu jinsi mimi ninavyoungua na tamanio hili, kwamba wewe uweze kusikiliza maelekezo yangu yote ya kutoka Mbinguni, na upate kujifunza namna ya kuishi Utashi wa Mungu!
Katika Kitabu hiki utaona mambo ya kushangaza. Utamkuta Mama anayekupenda kabisa, kiasi kwamba anamtoa hata Mwana wake mpenzi, ambaye katika huyo wewe utaweza kuishi uhai ule ule, ambao Mama huyu mwenyewe aliuishi hapa duniani.
Lo, binti, usiniletee uchungu huu wa kunigomea! Ukubali na kupokea zawadi hii ya Mbinguni ambayo nakuletea. Karibisha ugeni wangu na maelekezo yangu.
Ni vema ujue kwamba mimi nitazunguka dunia yote nikimwendea kila mtu binafsi, katika familia zote, katika jamii za kitawa zote, katika kila taifa, katika makabila yote.
Na kama itawezekana nitazunguka kwa muda wa karne nzima kadhaa, hadi, kama Malkia, nifikie kuwaunda watu wangu, na kama Mama, niwaunde watoto wangu.
Na hao ambao wataufahamu Utashi wa Mungu, ndio watakaofanya Utashi huo wa Mungu utawale popote.
Basi hayo ndiyo maelezo kwako juu ya lengo la Kitabu hiki.
Wale watakaokipokea kwa upendo watakuwa ndio wana wa kwanza wa Ufalme wa FIAT ya Mungu, na mimi nitayaandika majina yao hao katika herufi za dhahabu ndani ya Moyo wangu wa kimama.
Je unaona binti yangu?
Lile lile pendo la Mungu lisilo na mipaka, ambalo katika mpango wa wokovu, liliazimia kunitumia mimi katika kumleta Neno wa Mungu hapa duniani, ndilo sasa linaniita kwa mara nyingine uwanjani, na linanikabidhi jukumu zito, yaani agizo na utume wa kuunda hapa duniani watoto wa Utashi wake wa kimungu.
Kwa hiyo, katika jukumu langu la kimama, ninaanza kutekeleza kazi yangu, na sasa nakuandalia wewe njia ya kuzingatia ili uufikie Ufalme huo wa furaha.

Kwa ajili ya lengo hilo nitakupatia mafunzo ya juu na ya kimbingu, na hatimaye nitakufundisha sala mpya na za aina ya pekee.
Kwa sala hizo utaweza kuhusisha mbingu, jua, viumbe, uhai wangu mimi mwenyewe, na ule uhai wa Mwanangu na matendo yote ya Watakatifu, ili kwa jina lako wewe, wao hao wauombe Ufalme mwabudika wa Utashi wa Mungu.
Sala hizo ndizo zilizo na nguvu ya juu zaidi, kwani zinapatana na utendaji wa kimungu. Kwa nguvu ya sala hizo, Mungu atajiona amevuliwa silaha zake na kushindwa katika mapigano yake dhidi ya kiumbe.
Ukiwa umeimarishwa na msaada huo, wewe utaharakisha ujio wa Ufalme wake wa furaha kuu, na ukiwa pamoja nami, utafanikiwa kuufanya Utashi wa Mungu utekelezwe hapa duniani, kama kule Mbinguni, kulingana na matakwa ya Mwalimu – Mungu.
Haya, jipe nguvu binti yangu. Hebu unifurahishe mimi, na mimi nitakubariki