Utashi wa Mungu na Upendo wa Mungu - Luisa Piccarreta
43 subscribers
298 photos
54 files
633 links
Fahamu kuhusu kutimia kwa Sala ya Baba Yetu kupitia Maandishi ya Mtumishi wa Mungu Luisa Piccarreta, Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - Kuishi Utashi wa Mungu
Download Telegram
๐Ÿค๐Ÿค๐Ÿค
Naingia Ndani ya Bahari Kuu ya Utashi Wako
๐Ÿค๐Ÿค๐Ÿค
Ewe Yesu Wangu Mtamu,
mimi ninaingia ndani ya bahari kuu ya Utashi Wako, Ninapigilia utashi wangu ndani ya Utashi Wako na ninakuomba unipe Utashi Wako kama Uhai wangu, kama Uhai wa kila tendo langu, liwe lile la ndani au lile la nje, liwe lile la kiutashi au lile lisilo la kiutashi.
๐Ÿค๐Ÿค๐Ÿค
Ee Bwana,
naomba kwamba kila kitu kiwe ndani ya Utashi Wako wa Kimungu, ili niweze kukulipa kwa pendo, kwa uabudu, na kwa utukufu kana kwamba wanadamu wote wangekulipa hilo deni kwa utimilifu wote.
๐Ÿค๐Ÿค๐Ÿค

(โœ๏ธKitabu cha Mbingu - Juzuu Na. 14 - Mei 27, 1922)
Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua. (Mt 7; 6)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na.20 - Oktoba 2, 1926๐Ÿ–‹๐Ÿ“„๐Ÿ“–๐Ÿ“”

Nilijikuta katika kipindi cha masikitiko na uchungu mno kutokana na kukosekana kwa Yesu Wangu Mtamu. Oh! Kwa jinsi nilivyokuwa nikijisikia vibaya, sikuweza kufanya lolote tena. Hata hivyo, nilipokuwa nimefikia kilele cha mateso, Yeye aliingia pale ndani yangu huku akiwa katika mateso makali kabisa. Ndipo aliniambia:

โ€œBinti Yangu, nipo nikiangalia ni kwa kiasi gani yanipasa kupanua mipaka ya Ufalme wa Utashi Wangu, hata niweze kuukabidhi Ufalme huo kwa wanadamu. Ninafahamu fika kwamba wao hawataweza kutwaa ule upeo usio na ukomo uliopo katika Ufalme wa Utashi Wangu, kwa vile, kwake mwanadamu, haujatolewa bado ule uwezo wa kuuvuka na kuukumbatia Utashi unaouwiana na Ufalme usiokuwa na mipaka. Ni kwa vile, mwanadamu, kwa kuwa kaumbwa, yeye daima huwa ni finyu na mwenye mipaka. Na kwa hoja kwamba ana mipaka kulingana na hali zake za maandalizi na uhiari, Mimi huwa ninampelekea mema zaidi au pungufu, na ninampelekea na kumpatia upana zaidi au pungufu wa mipaka anayotakiwa awe nayo. Ndiyo maana Mimi sasa nipo nachunguza vizazi vijavyo vitakuja kuwa na hali gani ya maandalizi na uhiari, ninachunguza pia vizazi vilivyopo vya sasa kuona hali waliyo nayo sasa hivi, kwani hawa wa sasa budi wawe wanasali, wawe wanasihi, na wawe wanauandaa Ufalme wa ile FIAT Kuu ya Juu kwa ajili ya vizazi vijavyo. Na kulingana na hali ya maandalizi na utayari wa vizazi vijavyo, na kulingana na hamu waliyo nayo vizazi vya sasa, ndivyo na Mimi naendelea kuongeza na kupanua mipaka ya huo Ufalme Wangu. Ni kwa vile vizazi hivi vimeunganika sana kati yao, kiasi kwamba, huwa inatokea jinsi hiyo kila mara, kuwa kizazi kimoja kinasali, kizazi kingine kinaandaa, na kizazi kingine tena kinasihi na kuomboleza na kizazi kingine ndicho kinachoubeba Ufalme.

Ndivyo hivyo hivyo ilitokea katika ule ujio Wangu hapa duniani, nilipofika kushughulikia Ukombozi. Havikuwa ni vizazi vya hivi sasa ambao walikuwa wakisali, waliotweta na waliolia ili kuyapata mema yake - kwani hawa ndio wanaoyafaidi na wanayoyatwaa na kuyabeba - bali walikuwa ni wale waliokuwa wameishi kabla ya ujio Wangu. Na kadiri ya hali ya maandalizi na hiari ya watu wale wa kizazi hiki cha sasa, na kutokana na sala na hali za maandalizi na hiari ya wale wa kizazi kilichopita, ndivyo na Mimi nilivyozidi kupanua mipaka ya yale mema ya Ukombozi. Na kwa kweli, Mimi huwa ninatoa jema fulani pale tu ambapo jema hilo litakuwa na manufaa kwa wanadamu. Lakini, iwapo jema hilo halitaleta manufaa yoyote, kuna haja gani ya kulitoa? Na manufaa hayo huchukuliwa na hao wanadamu iwapo wamekuwa na maandalizi zaidi na uhiari zaidi. Lakini, je, wajua wewe ni lini ninapopanua mipaka yake? Ni pale ninapokueleza na kukuonyesha wewe maarifa fulani mapya yanayohusu huu Ufalme wa Utashi Wangu. Ndiyo maana, kabla sijakueleza na kukuonyesha wewe, huwa kwanza ninatupia jicho Langu kwa watu wote ili kuchunguza kuona hali zao za maandalizi - yaani, kuona kama itakuwa na manufaa kwao, au pengine, itakuwa kwao sawa na kama vile hakikusemwa chochote kabisa. Na wakati ninapokumbuka kuwa Mimi ninanuia kupanua zaidi na zaidi mipaka Yangu kwa ajili ya kuwapatia mema mengi zaidi ya kubeba, kuwapatia furaha zaidi, na kuwapa raha zaidi, na papo hapo ninapogundua kuwa wao hawapo tayari kwa hilo, Mimi huwa naonja kuteseka sana sana, na ndipo huwa ninasubiria sala zako, ninasubiria ziara zako ndani ya Utashi Wangu, nasubiria maumivu yako, ili kusudi niweze kuwaandaa wale wa kizazi cha sasa na wale wa kizazi kilichopita. Na kishapo huwa ninarejea kule kwenye mambo yale ya kushitua ya maelezo Yangu mintarafu Utashi Wangu.
Ndiyo maana huwa ninashikwa na uchungu sana na maumivu pale ninapokuwa sizungumzi nawe. Neno Langu ndiyo zawadi kubwa kupita zote - huwa ni uumbaji mpya. Kutokana na Mimi Mwenyewe kushindwa kulitoa toka ndani Mwangu, kwa vile wanadamu wanakuwa hawapo tayari kulipokea neno hilo, huwa ninaonja ndani Yangu ule uzito wote wa ile zawadi ninayonuia kuitoa, na, kwa kushindwa kuitoa, huwa naendelea kuteseka na ninabaki kunyamaza. Na mateso Yangu huwa yanaongezeka hata zaidi na zaidi pale ninapokuona na wewe unateseka kwa ajili Yangu Mimi. Laiti ungefahamu jinsi ninavyoonja masikitiko yako - na jinsi uchungu wako huo unavyomwagikia ndani ya Moyo Wangu! Utashi Wangu huwa unauingiza uchungu huo hadi kilindini mwa Moyo Wangu. Ni kwa vile Mimi sina tashi mbili, bali ninao utashi mmoja tu. Na kwa vile huo Utashi Wangu ndio unaotawala ndani yako wewe, matokeo yake ni kwamba, huo Utashi Wangu huwa unaleta yale mateso yako hadi kwenye kina cha ndani Mwangu. Kwa hiyo basi, wewe uwe unasali, na hebu ule mruko wako uwe endelevu daima ndani ya ile FIAT Kuu ya Juu, ili pale ukawe unaendelea kusihi kwamba wanadamu wawe wanajiandaa wenyewe, na Mimi niweze kurejea kuja kuzungumzia kwa mara nyingineโ€โ€ฆโ€ฆ
Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba. (Mt 7; 13)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 6 - Juni 23, 1905๐Ÿ–‹๐Ÿ“ƒ๐Ÿ“–๐Ÿ“”

Wakati nikiendelea na ile hali yangu ya siku zote, nikawa ninawaza juu ya jinsi Yesu Kristo alivyokufa, na pia juu ya kwamba Yeye hakuweza kuogopa kifo, kwani, maadam alikuwa ameunganika kabisa na ule Umungu, au tuseme, alikuwa amegeuzwa kuwa katika hali ya Umungu, basi, alikuwa tayari ni salama kabisa sawa na mmoja anayekaa katika jumba lake mwenyewe. Lakini, kwa mtu huyo - lo! Ni tofauti gani kubwa iliyopo. Pindi nikiwazia hayo na ujinga wangu mwingine, Yesu Mhimidiwa alikuja na kuniambia:

โ€œBinti Yangu, yule anayekuwa ameunganika na Ubinadamu Wangu, huyo huwa anajikuta yupo tayari mlangoni pa Umungu Wangu, kwa vile, Ubinadamu Wangu ni kioo cha mtu cha kujitazamia, kwani kutoka hicho kioo Umungu huwa unaweza kuonekana pale ndani ya huyo mtu husika. Na kama mmoja yupo tayari katika picha kioo ya kioo hicho, ni wazi kabisa kwamba nafsi yake yote budi iwe imegeuzwa kuwa ni Pendo. Sasa, Binti Yangu, kwa vile kila kitu kitokacho kwa mwanadamu, hata ule ujimudu mbalimbali wa macho yake, ujimudu wa midomo yake, ujimudu wa mawazo yake, na mengineyo yote - kila kitu budi kiwe ni Pendo, na kiwe kimetekelezwa kwa ajili ya upendo. Na kwa vile nafsi Yangu yote ni upendo mtupu, basi popote pale ninapolikuta pendo, Mimi hapo ninanyonya kila kitu ndani Mwangu, na yule mtu anaingia kukaa kwa utulivu kabisa ndani Yangu Mimi kama vile anavyokaa yeyote yule ndani ya jumba lake mwenyewe.

Basi, sasa mtu, katika saa yake ya kufa, anaweza akawa na hofu gani ya kuja Kwangu Mimi wakati yupo tayari ndani Yangu Mimi?โ€
โฌ‡๏ธโฌ‡๏ธโฌ‡๏ธ
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 9 โ€“ Machi 16, 1910๐Ÿ–‹๐Ÿ“„๐Ÿ“–๐Ÿ“”

Nilipokuwa nikizungumza na Padre Mwungamishi, aliniambia kuwa kuokoka ni suala gumu kwa vile Yesu Kristu Mwenyewe aliwahi kusema hivyo: โ€œMlango ni mwembamba. Ni budi mjitahidi kuuingiaโ€. Halafu, baada ya mimi kupokea Komunyo Takatifu, Yesu aliniambia:

โ€œMasikini Mimi, ni jinsi gani wanavyodhani kwamba Mimi ni bahili. Ebu kamwambie huyo Padre Mwungamishi: wao wananihukumu Mimi kwa kulingana na ubahili wao wenyewe. Hawanihesabu kama ndiye niliye Mkuu, niliye mkubwa mithili ya bahari, niliye bila ukomo, niliye mwenye maweza, niliye bila mipaka katika sifa Zangu zote za ukamilifu, kwamba, ndiye ninayeweza kuyafanya makundi makubwa ya watu yakapita pale penye uwembamba, na wakaweza kupita zaidi kuliko pale penye upana wenyeweโ€.

Na alipokuwa akiyasema hayo, nikawa ninaona kama vile njia nyembamba iliyokuwa ikielekea kwenye mlango mdogo, mwembamba na uliokuwa umejaa kabisa na watu ambao walikuwa wanapigania kati yao nani atangulie zaidi hata akaweze kuingia pale ndani. Yesu akaongeza kusema:

โ€œEwe Binti Yangu, ebu angalia ni kundi kubwa lilioje lile linalojisukuma pale kwenda mbele. Na pale wanashindania kuona nani atakayeweza kuwasili wa kwanza. Katika mashindano huwa kuna kushinda kwingi. Lakini kumbe, kama njia ingekuwa ni pana, pasingekuwa na mtu anayehangaika kuharakisha, kwani, wangejua kwamba kuna nafasi ya kutosha kwa ajili ya kuweza kuendelea kutembea wakati wowote ule wanapotaka. Lakini, pindi wanapopitisha muda wao wakingoja kuanza mwendo wao, kifo chaweza kuwafikia, na wao, wanapojikuta hawatembei katika njia nyembamba, wangeshitukia wanawasili penye lile lango pana la lile geti kuu la motoni mwa milele. Lo, ni faida gani kubwa inayoletwa na huu uwembamba! Jambo hilo huwa linatokea hata hapo kati yenu ninyi wenyewe: Iwapo kunatokea kuwa na sherehe au pakiwa na ibada fulani, na iwapo inafahamika fika kwamba nafasi iliyopo ni ndogo, basi watu wengi sana huwa wanaharakisha kufika, na mwishowe huwa wanahudhuria washiriki wengi sana waliofika kuja kufurahia hiyo sikukuu au ibada. Kumbe lakini, endapo inajulikana kuwa nafasi iliyopo ni kubwa, hakuna mtu anayehangaika kuharakisha na mwishowe huwa ni wahudhuriaji wachache tu wanaofika, kwa vile tu wanajua kwamba kuna nafasi ya kutosha kabisa kwa ajili ya kila mtu. Kila mmoja huwa anakuja kwa raha na kwa wakati wake. Na baadhi huwa wanafika katikati ya sherehe, na wengine wanafika hata mwishoni, na wengine wanapofika, wanakuta sherehe imekwisha kumalizika, na hivyo hawawezi kufaidi chochote. Hilo ndilo ambalo lingetokea iwapo njia ya wokovu ingekuwa ni pana - ni watu wachache tu wangekuwa wanahangaika kuharakisha, na sherehe ile ya Mbinguni ingebaki kuwa ni ya wachache tuโ€™โ€™.
Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. (Mt 7; 14)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU Na. 3 โ€“ July 10, 1900๐Ÿ–‹๐Ÿ“ƒ๐Ÿ“–๐Ÿ“”

โ€ฆ.Kwa hiyo basi, Yesu Mhimidiwa akaanza kurudia kunielezea ile tofauti iliyopo kati ya kuishi kwa ajili ya Mungu na kuishi ndani ya Mungu. Aliniambia hivi:

โ€œKatika kuishi kwa ajili ya Mungu, mtu anaweza akawa anakabiliwa na vurugu mbalimbali, na machungu mbalimbali, anakabiliwa na utovu wa uthabiti, anaelemewa na mzigo wa matamaa mbalimbali, na anakabiliwa na maelekeo ya kujiingiza katika mambo ya kidunia. Kumbe lakini, kuishi ndani ya Mungu - la hasha, ni jambo tofauti kabisa kabisa, kwa vile, jambo linalokuwa ni muhimu kabisa kwa mtu kuingia na kufanya makao pale ndani ya nafsi nyingine, huwa ni kusalimisha kwa mtu husika yale mambo yote anayoyamiliki - yaani, ni mtu mwenyewe kujivua mambo yake yote, yaani ni kule kuachana kabisa na matamaa yake mwenyewe. Kwa neno moja, ni kuacha mambo yote ili akayaone hayo mambo yote pale ndani ya Mungu.

Sasa basi, kama mtu, siyo tu amejivua kabisa, bali hata amejikondesha na kuwa mwembamba kabisa, ndipo hapo ataweza kupita na kuingia pale penye mlango mwembamba wa Moyo Wangu, na hivyo ataweza kuishi pale ndani Yangu kulingana na mtindo Wangu Mimi, na ataishi kwa nguvu ya Uhai Wangu Mimi Mwenyewe. Na kwa kweli, hata kama Moyo Wangu ni mkubwa na mpana ajabu, mpana jinsi kwamba hakuna ukomo wa mipaka yake, lakini hata hivyo, mlango wa Moyo huo ni mwembamba mno mno. Ndiyo maana, ni yule tu aliyejivua kila kitu ndiye ataweza kupita na kuingia pale.

Na jambo hilo lina sababu yake, kwani, maadam Mimi ni Mtakatifu mno, nisingeweza kamwe kukubali kuingiza chochote kile kije kuishi ndani Mwangu ambacho chenyewe ni kigeni kabisa au ni mbali kabisa na utakatifu Wangu. Kwa hiyo basi, Binti Yangu, wewe jaribu kuishi ndani Mwangu Mimi, na wewe utafikia kuibeba na kuimiliki Paradiso hata kabla ya wakatiโ€.

Sasa hapo, ni nani atakayeweza kuelezea ni kiasi gani nilichokielewa juu ya suala hilo la kuishi ndani ya Mungu? Kumbe halafu, Yeye aliondoka na kufifia, na mimi niliachwa pale nikiendelea kuwa katika ile ile hali yangu.
UFALME WAKO UJE
โฌ‡๏ธโฌ‡๏ธโฌ‡๏ธ
Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
Mapenzi yako yatimizwe,
hapa duniani kama huko mbinguni.
(Mt 6; -10)

โฌ‡๏ธโฌ‡๏ธโฌ‡๏ธ๐Ÿ“š
http://divinewilldivinelove.com/Kiswahili-/-Swahili/

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!

๐Ÿคโ˜€๏ธ๐Ÿคโ˜€๏ธ๐Ÿคโ˜€๏ธ

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

โฌ‡๏ธโฌ‡๏ธโฌ‡๏ธ
Swahili - Telegram Channel โ€“ Utashi wa Mungu na Upendo wa Mungu:
https://t.me/UTASHIWAMUNGUNAUPENDOWAMUNGU

Swahili - Telegram Channel โ€“ Saa 24 Za Mateso:
https://t.me/Saa24ZaMateso_Official/5

Swahili - Telegram Channel - Bikira Maria Katika Ufalme wa Utashi wa Mungu
https://t.me/BikiraMaria_Official/6
Njoo Wewe Mwenyewe, Yesu Wangu, pamoja na Ubinadamu Wako, uyeyushie Moyo Wako ndani ya moyo wangu, ili kusudi mimi niwe ninatumia mapigo ya Moyo Wako wenyewe, niwe ninapumua kwa njia ya pumzi Yako, na niwe ninapenda kwa njia ya Pendo Lako lenyewe....
๐Ÿ”ฅโ˜€๏ธ๐Ÿ”ฅ
Njoo pamoja na Utashi Wako, njoo pamoja na Mama, na pamoja na Moyo wake Immakulata, njoo ndani ya moyo wangu ukawe unagonga humo kwa njia ya Pendo Lako. Na kwa njia hiyo, mimi nitakupatia pendo kwa Pendo, pumzi kwa Pumzi, na moyo kwa Moyo....
๐Ÿ”ฅโ˜€๏ธ๐Ÿ”ฅ
Na kila kitu kitakuwa kinastahilika Kwako, kitakuwa ni cha Kimungu, kitakuwa ni cha kutosha, kwani yote yatakuwa ni katika Utashi Wako na katika Pendo Lako.
๐Ÿ”ฅโ˜€๏ธ๐Ÿ”ฅ
Ndivyo Wewe utaweza kuridhika kwamba ulikuwa umeuumba moyo wangu, na utakuwa umelipwa kwa njia ya Pendo.
๐Ÿ”ฅโ˜€๏ธ๐Ÿ”ฅ
Na katika moyo wangu, mimi nitakuwa nikionja kuwa Moyo Wako unabeba ndanimo moyo wa wanadamu wote. Ndipo sisi sote kwa pamoja tutalipa fidia kwa kila pigo la moyo lililokufuriwa na kwa kila pumzi.
๐Ÿ”ฅโ˜€๏ธ๐Ÿ”ฅ
Kishapo, moyo wangu, ndani ya Moyo Wako na pamoja na Moyo Wako utakuwa ukisema: Enyi roho za watu, Pendo!

(Kitabu cha Sala Mbalimbali - Njoo ewe Utashi wa Mungu, Njoo Ukawe Mapigo ya Moyo Wangu)
"Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya." (Mt 7; 17)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 18 - Januari 28, 1926๐Ÿ–‹๐Ÿ“„๐Ÿ“–๐Ÿ“”

....โ€œBinti Yangu, lengo la kwanza kabisa la Mimi kuja hapa duniani lilikuwa hasa ni hili - kwamba binadamu arudi tena ndani ya tumbo la Utashi Wangu, kwa vile, ndipo mahali alipotokea wakati ule alipoumbwa.

Lakini, ili kulitekeleza hilo, ilibidi Mimi, kwa njia ya Ubinadamu Wangu, nitengeneze ule mzizi, lile shina, yale matawi, yale majani, na yale maua, ambayo kwayo yatatoka yale matunda ya kimbingu ya Utashi Wangu.

Hakuna mtu yeyote atakayeweza kupata tunda bila kuwa na mti. Mti huo ulikuwa umemwagiliwa maji kwa Damu Yangu.

Ulikuwa umelimiliwa na kupaliliwa kwa maumivu Yangu, kwa mitweto Yangu, na kwa machozi Yangu. Jua lililowaka juu ya mti huo lilikuwa ni lile Jua la Utashi Wangu peke yake.

Kwa hiyo, ni uhakika kwamba, yale matunda ya Utashi Wangu, yatapatikana tu. Lakini, ili mtu afikie kuyatamani hayo matunda, ni budi mtu afahamu kwanza jinsi matunda hayo yalivyo ni azizi, budi afahamu manufaa yanayoletwa na matunda hayo, na utajiri ule ambao matunda hayo huzalisha.

Basi, hiyo ndiyo hoja kwa yale maelezo mengi niliyokuwa nimekupatia mintarafu Utashi Wangu. Ni kwa vile, maarifa au ufahamu ndio utakaoleta hamu ya kula huo Utashi Wangu. Na baada ya wanadamu kuonja maana ya kuishi kwa ajili ya kutekeleza Utashi Wangu peke yake, basi, kama siyo watu wote, lakini, baadhi, hakika watarudi kwenye njia ya Utashi Wangu, zile tashi mbili zitabusiana kwa umilele, na wala hapatakuwa tena mvutano na mgongano kati ya utashi wa kibinadamu na Ule Utashi wa Muumba, na ule Ukombozi Wangu, utaongeza kutoa hata lile tunda la Mapenzi Yako Yatimizwe Duniani kama Mbinguni[1].

Basi wewe, na uwe ni wa kwanza kulipokea tunda hilo, na wala usitamani tena chakula kingine, wala uhai mwingine isipokuwa Utashi Wangu peke yakeโ€.

[1] Mapenzi Yako Yatimizwe Duniani kama Mbinguni = Kilatini: Fiat Voluntas Tua sicut in Coelo et in Terra.
๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™

Ewe Yesu Wangu Mtamu,
mimi ninaingia ndani ya bahari kuu ya Utashi Wako, Ninapigilia utashi wangu ndani ya Utashi Wako na ninakuomba unipe Utashi Wako kama Uhai wangu, kama Uhai wa kila tendo langu, liwe lile la ndani au lile la nje, liwe lile la kiutashi au lile lisilo la kiutashi.

Ee Bwana,
naomba kwamba kila kitu kiwe ndani ya Utashi Wako wa Kimungu, ili niweze kukulipa kwa pendo, kwa uabudu, na kwa utukufu kana kwamba wanadamu wote wangekulipa hilo deni kwa utimilifu wote.

๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™

(Kitabu cha Mbingu - Juzuu Na. 14 - Mei 27, 1922)
Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni (Mt 7; 21)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 16 - Mei 13, 1924๐Ÿ–‹๐Ÿ“ƒ๐Ÿ“–๐Ÿ“”

โ€ฆ..โ€œEwe Binti Yangu, je unaona? Kitendo cha kwanza cha Nafsi Tatu za Mungu kimekuwa ni uelewano au upatano kamili wa Utashi Wetu. Utashi Wetu umeunganika mno hivi kwamba Utashi wa Mmoja hauwezi ukatofautiana kutoka Ule Utashi wa Yule Mwingine. Ni ndivyo hivyo kwamba, hata kama Nafsi Zetu ni tofauti - kwa vile tupo Watatu - Utashi Wetu, hata hivyo, ni mmoja tu na huo Utashi mmoja ndio unaozalisha tendo endelevu la uabudu kamili kati ya zile Nafsi Tatu za Mungu - yaani, Mmoja huwa anamwabudu Mwingine. Huo uelewano na mapatano ya Utashi ndio unaozaa usawa katika utakatifu, usawa wa mwanga, usawa wa wema, usawa wa uzuri, wa maweza, wa pendo, na ndio unasimika ndani Yetu Sote ufalme wa kweli, wa utaratibu, na wa amani, na unatupatia Sisi bahari ya furaha mbalimbali na raha mbalimbali, na heri mbalimbali zisizo na mipaka. Kwa hiyo basi, ule uelewano na mapatano ya utashi wa kibinadamu na Utashi wa Mungu, huwa ndicho kiunganisho cha kwanza cha uhusiano kati ya Muumba na mwanadamu. Na kutokana na huo uelewano na mapatano, zile nguvu za kimungu huwa zinateremka kuja ndani ya mwanadamu mithili ya kutiririka ndani ya mfereji, na hivyo kuweza kutengeneza ndanimo ule uabudu wa kweli na pendo kamili kwa ajili ya Muumba Wake. Na kwa kuibuka kutoka ndani ya huo huo mfereji wa uhusiano, mtu huwa anazipokea zile dozi mbalimbali na tofautitofauti za maweza mbalimbali ya kimungu. Na kila mara mtu anapoibuka na kupanda juu ili arukie ndani ya huo Utashi wa Milele, huwa anapambwa na uzuri wa kimungu, na huwa anajipatia, aina nyingi nyingi na mbalimbali za huo uzuri wa kimungu.

Ndiyo maana Mimi ninasema kwamba mtu anayetekeleza Utashi Wangu huwa ni burudani Yangu, na ni raha Yangu. Na kwa ajili ya kujiburudisha Mimi Mwenyewe, Mimi huwa ninashika daima brashi ya Utashi Wangu mikononi Mwangu, na mara tu anaporukia na kuingia ndani ya Utashi Wangu, Mimi ninamgusa mara, na, kwa kutumia ile brashi Yangu ya kupakia rangi, ninaanza kujiburudisha Mimi Mwenyewe kwa kumbandika kivuli cha ziada cha uzuri Wangu, cha Pendo Langu, cha utakatifu Wangu, na cha maweza Yangu yote. Basi, Kwangu Mimi, kuwepo Kwangu ndani yake huyu na kuwepo Kwangu kule Mbinguni ni kitu kile kile kabisa - pale ninauona uabudu ule ule wa zile Nafsi Tatu za Mungu, ninaukuta pale Utashi Wangu na ninalikuta na Pendo Langu. Na kwa vile kipo pale daima kitu kinachoweza kikatolewa kwa mwanadamu, Mimi hapo huwa ninatenda kama fundi stadi anayepaka rangi kwa kubandika sura Yangu ndani ya mtu huyu. Halafu ninatenda kama mwalimu kwa kumfundisha zile doktrina za juu kabisa na tukufu kabisa. Halafu ninatenda kama mtu wa mapenzi na upenzi mkali kwa kumpatia penzi Langu na kwa kulitaka penzi lake. Kwa kijumla, hapo huwa ninatumia na kutekeleza ustadi Wangu wote katika mbinu za kuburudishana na mtu huyo. Na Pendo Langu, baada ya kuchukizwa na wanadamu, linapokuwa limekosa hata kupata mahali pa kukimbilia, yaani pa kutorokea kutokana na wale wanaonikimbiza Mimi ili kunisababishia kifo au wale wanaotaka niruke kwenda juu kwenye anga la Mbingu - Mimi huwa ninapata kimbilio Langu ndani ya mtu yule anayekuwa na Utashi Wangu pale ndani yake mwenyewe, na pale huwa nayakuta maweza Yangu yanayonitetea, nalikuta Pendo Langu linalonipenda Mimi, naikuta amani Yangu inayonipatia pumziko. Yaani, ninakuta pale mambo yote ninayoyataka. Kwa hiyo basi, Utashi Wangu ndio unaounganisha kila kitu pamoja - unaunganisha Mbingu na dunia, na unaunganisha mema yote - na hatimaye unayafanya yawe ni kitu kimoja. Na kutokana na kitu hicho kimoja peke yake, ndiyo huibuka yale mema yote yanayowezekana na yanayofikirika. Kwa hiyo, naweza nikasema kwamba, mtu yule anayetekeleza Utashi Wangu, ndiye aliye ni chote na chochote Kwangu Mimi, na Mimi Mwenyewe, kwa mtu huyo, ninakuwa ndiye chote na chochoteโ€โ€ฆ..
Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya (Mt 7: 24)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 13 - Novemba 19, 1921๐Ÿ–‹๐Ÿ“ƒ๐Ÿ“–๐Ÿ“”

โ€ฆ.. Halafu niliendelea kuwaza moyoni peke yangu juu ya hayo maneno aliyokuwa akiyasema Yesu, nikawa najisemea peke yangu: โ€˜Je hayo yote yanaweza kutekelezwa namna gani?โ€™. Hapo Yesu alirudia na kuongeza kusema:

โ€œBinti Yangu, ili kuweza kuzijua Kweli mbalimbali ni budi pawepo na utashi, yaani pawepo na tamaa ya kutaka kuzijua. Ebu fikiria chumba fulani ambacho madirisha na milango yake yote vimefungwa kabisa na kuzibwa: Mamoja jua likiwaka namna gani huko nje, chumba hicho kitabaki kuwa katika giza totoro. Hapo, kitendo cha kufungua milango na madirisha kina maana ya kuupenda na kuutaka mwanga, lakini hata tendo hilo halitoshi endapo yule anayefungua milango na madirisha hatataka kutumia fursa ile ya mwanga katika kusafisha chumba, kuweka taratibu pale ndani, na kuanza mara kazi fulani aliyopanga. Mtu huyo asipopenda kufanya hayo anakuwa kama vile anauulia mbali ule mwanga ulioletwa kwake bila gharama yoyote; tabia hiyo inakuwa ni utovu wa shukrani kabisa. Ndiyo maana, haitoshi kuwa na utashi wa kujua Kweli mbalimbali, kama wakati mtu anapoingia katika mwanga wa Ukweli unaomwangaza, mtu huyo hataki kuanza kujisafisha, na kuvua madhaifu yake, na kujipanga vema kadiri ya mwanga wa Ukweli anaopata kuujua.

Na akiisha kuupata mwanga huo wa Ukweli, akaanze kufanya kazi yake, akafanye uwe ni tabia yake mwenyewe. Pia aanze kuwaangazia na watu wengine kwa njia ya neno la mdomoni mwake, kutokana na vitendo vya mikono yake, kutokana na mwenendo wake, yote hayo yakiwa ni kutokana na tendo la kuwaletea mwanga wa ukweli, alioupata yeye na akauingiza ndani mwake. Mtu asiyefanya hayo, ni sawa na yule anayeulia mbali Ukweli, na kwa kutoutekeleza Ukweli huo kwa matendo, huyo mtu mwenyewe atakuwa anaishi katika vurugu, fujo na bila taratibu mbele ya mwanga alioletewa. Masikini chumba hicho ambacho kimejaa mwanga, lakini kimebaki katika vurugu ovyo, na vitu vimepinduka juu na chini na katika uchafu tu.

Na ebu fikiria kumwona mtu ndani ya chumba hicho ambaye hajali kabisa kusafisha na kuweka taratibu katika chumba hicho. Masikini mtu huyo angetuletea uchungu na huruma ya jinsi gani? Ndivyo anavyokuwa mtu yule anayezijua Kweli mbalimbali na asitake kuzitekeleza kwa matendo.

Inafaa ufahamu pia kuwa katika suala nzima la Kweli zote, kitu kinachoingia kama lishe ya awali kabisa huwa ni unyenyekevu na unyofu. Kama Kweli zisingekuwa ni wazi na safi bila kuchanganyika na chochote, kweli hizo zisingeweza kuwa ni mwanga na wala zisingeweza kupenya katika akili za kibinadamu ili kuziangaza. Na pale ambapo hapana mwanga, hapo mahali vitu mbali mbali havionekani na havitofautishiki. Usafi, unyofu na unyenyekevu siyo tu ni nuru, bali ni pia hewa na mazingira anayopumua mtu. Na ingawa kama watu hawaoni, lakini vinaleta hewa nzuri na pumzi kwa watu wote na kwa kila kitu. Na kama ilivyo kwa ardhi, kama pasingekuwepo na hewa, ardhi yenyewe na kila kitu vingebaki katika hali ya kuwa na utovu wa nguvu ya kujimudu. Kwa hiyo kwa kweli, endapo fadhila mbalimbali, na Kweli mbalimbali hazitaleta na kuacha mhuri wa usafi, unyenyekevu, unyofu na uwazi, basi fadhila hizo na kweli hizo zitakuwa zinakosa kuwa na mwanga na zitakosa kuwa na hewaโ€.
๐Ÿ™๐Ÿ‘‘๐Ÿ™
Ewe Utatu Mtakatifu, katika Maweza yako yote, katika Hekima na Wema Wako, harikisha ujio wa Ufalme wa Utashi Wako wa Kimungu, na wa Ufalme wa Pendo Lako hapa duniani.
๐Ÿ™๐Ÿ‘‘๐Ÿ™
Njoo ewe Utashi Mkuu, njoo uitawale dunia! Njoo uwafunike vizazi vyote vya wanadamu! Njoo uwashinde na kuwateka wote!
๐Ÿ™๐Ÿ‘‘๐Ÿ™
Ewe Mungu Mwenyezi, uliyemwumba mwanadamu ili awe anatekeleza ule Utashi, ambao yeye, kwa kukosa kuwa na shukrani, aliuvuruga wakati alipokugomea Wewe, ufanye haraka kuja kurekebisha tena kile kifungo cha utashi huu wa binadamu, ili Mbingu na dunia zibaki zimefungamana na kuungana ndani Yako.
๐Ÿ™๐Ÿ‘‘๐Ÿ™
Ee Maria Mtakatifu sana, Mama na Malkia wa Utashi wa Mungu, fungilia Utashi wa Mungu ndani ya roho yetu.
๐Ÿ™๐Ÿ‘‘๐Ÿ™
Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa (Mt 8; 2)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 21 โ€“ Mei 26, 1927๐Ÿ–‹๐Ÿ“ƒ๐Ÿ“–๐Ÿ“”

โ€ฆ..Kishapo mimi nikawa ninawaza moyoni mwangu: โ€œYesu anaupenda sana Utashi Wake, na yaelekea kwamba Yeye anatamani sana sana huo Utashi Wake ujulikane ili hatimaye utawale na utamalaki. Lakini, kwangu mimi, yaonekana kama vile ni vigumu kwa Utashi wa Mungu kufahamika, kwa vile, mpaka sasa hivi, hakuna mtu anayelishughulikia jukumu hilo, na wala hakuna mtu mwenye mwelekeo kwa suala hilo wala anayelipenda. Hamu kwa suala hilo naiona kwa Yesu tu, lakini katika wanadamu hakuna hamu yoyote ile. Sasa, endapo hawa wanadamu wanashindwa kutoa ule utukufu mkuu kwa Mungu, na kama pia wanashindwa kutoa ule ujazo wa mema yote na kuufikisha kwa wanadamu, itakuja kuwezekaneje Ufalme wa FIAT ya Milele ujulikane kwa watu?โ€ . Basi, pindi nikiwaza hivyo, Yesu Wangu Mtamu aliingia pale ndani mwangu na akaniambia hivi:

โ€œBinti Yangu, jambo ambalo kwako wewe laonekana kuwa ni gumu, hilo siyo gumu kabisa kwa Mungu. Kama vile katika kazi ya Ukombozi hapakuwepo na ugumu wowote ule, na wala ule ufidhuli wote wa kibinadamu haukuweza kuuzuia ule mkondo wa Pendo Letu, na kabisa kabisa, huo ufidhuli na njama za kibinadamu hazitaweza kamwe kuzuia uhitimisho wa Utashi Wetu, yaani, uhitimisho wa uamuzi Wetu wa kuja duniani kukikomboa hiki kizazi cha binadamu. Pale Umungu unapoamua kutekeleza tendo fulani, unapotaka kuhitimisha kazi fulani, mamoja kuwe kuna hoja gani, mamoja kuwe na mazingira gani, na hata pawepo vipingamizi gani, Umungu huwa unapita na kusherehekea yote kwani huwa unashinda kila kitu, na unatekeleza jambo lile ulioliazimia. Kwa jinsi hiyo basi, dakika ya kilele na muhimu kabisa kwa Mungu huwa ni katika tendo la kuazimia jambo analotaka kulitenda. Akiisha azimia, basi jambo limekwisha kutendeka.

Kwa hiyo basi, kama ndani Mwetu imekwisha kuazimiwa kwamba Utashi Wetu budi ujulikane, na kwamba Ufalme Wake utafika duniani, basi, hilo ni kama limekwisha kutendeka tayari. Kama vile Ukombozi ulivyokuja kutekelezwa, kwa vile ulikwisha kuazimiwa na Sisi, ndivyo itakavyokuja kutekelezwa kuhusu Utashi Wetu. Na zaidi zaidi ni kwamba, katika zoezi la Uumbaji, kutoka pale ndani mwa Umungu, uliletwa nje huo Ufalme Wake, ukiwa wote katika taratibu zake, kwa vile ulikuwa ukitawala na kutamalaki. Na katika ule mwanguko wa binadamu, huo Ufalme haukubomolewa, bali ulibaki ukiwa mzima na bado upo hata sasa hivi, isipokuwa tu Ufalme huo ulikuwa umesimamishwa kwa ajili ya binadamu. Katika kazi ya Ukombozi Mimi nilisawazisha kila kitu, na kama vile nilivyofanya kila kitu ili binadamu aweze kukombolewa, ndivyo nilifanya yote ili kuhakikisha kuwa ile adhabu ya kusimamishwa inaondolewa, ili mwanadamu aweze kuingia katika Ufalme wa FIAT ya Kimungu. Nilitoa kwanza nafasi kwa kazi ya Ukombozi, na kadiri muda ulivyozidi kupita, nilitoa pia nafasi kwa Utashi Wangu. Kwa jinsi hiyo, kwa ufalme wowote ule, kwa kazi yoyote ile, tatizo huwa ni kule kulitekeleza. Lakini jambo likiisha kutendeka, suala la kulitambua na kulifahamu au kulijua huwa ni rahisi kabisa. Zaidi zaidi ni kwamba Yesu Wako, huwa hapungukiwi maweza. Juu ya kutaka kutenda au kutotenda kazi fulani yoyote ile, Mimi naweza nikakosekana, lakini kuhusu maweza yenyewe, siwezi nikayakosa kamwe. Mimi huwa ninayaandaa mambo, ninayaandaa mazingira, huwa nawaandaa na wanadamu, na hata nayaandaa matukio, kwa jinsi hii kwamba nitaweza kurahisisha kule kufahamika na kujulikana kwa Utashi Wanguโ€.
akisema Nataka; takasika. (Mt 8; 3)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 12 - Machi 6, 1919๐Ÿ–‹๐Ÿ“ƒ๐Ÿ“–๐Ÿ“”

Nilikuwa ninasumbuliwa sana na mawazo juu ya kile ambacho Yesu Wangu Mtamu alikuwa akinielezea juu ya Utashi wa Mungu. Ndipo nikawa ninasema moyoni mwangu: โ€˜Inawezekanaje kwamba mtu anaweza kufikia mapaka huko hata akawa anaishi zaidi kule Mbinguni kuliko hapa duniani?โ€™. Na Yesu alipokuja kwangu akawa ameniambia:

โ€œBinti Yangu, kile kisichowezekana kwa mwanadamu, chote kinawezekana kwa Mimi.

Ni kweli kabisa kwamba huo ndio muujiza ulio mkuu kabisa wa maweza Yangu yote na wa Pendo Langu. Lakini, Mimi ninapotaka, huwa ninaweza yote. Na kile kinachoonekana kuwa ni jambo gumu, Kwangu Mimi huwa ni rahisi mno.

Hata hivyo, Mimi ninapenda nipate โ€˜ndiyoโ€™ ya mwanadamu na ninapenda ajitoe, na aonyeshe hiari yake, kama nta laini, kutekeleza chochote kile ninachotaka kutoka kwake.

Tena, zaidi ya hilo, lazima ufahamu kwamba, kabla ya kuhitimisha kwake wito wa kuishi ndani ya Utashi Wangu, huwa kwanza ninamwita mara kwa mara sana, halafu huwa ninamnyangโ€™anya na kumvua kila kitu, huwa ninamfanya apitie kwa lazima katika aina fulani ya hukumu, kwani ndani ya Utashi Wangu hamna hukumu zozote - mambo yote huwa yanabaki yamethibitishwa na Mimi.

Jambo lolote la hukumu huwa ni nje ya Utashi Wangu.

Kwani lakini, nani huyo ambaye atadiriki kulitia hukumuni jambo lolote lile linaloingia ndani ya Utashi Wangu? Na kamwe Mimi Mwenyewe huwa sihukumu.

Wala siyo hilo tu, bali mara nyingi sana huwa ninamfanya mtu huyo afe pia kimwili, na halafu huwa ninamrudishia uhai tena. Na yule mtu huwa anaendelea kuishi kana kwamba hakuwahi kuishi kabla. Moyo wake unakuwa upo Mbinguni, na kuendelea kuishi huwa ndiyo kifo dini chake kikubwa kabisa.

Je ni mara nyingi ngapi sikukutendea wewe hivyo? Hayo yote ni maandalizi mbalimbali kwa ajili ya kumwandaa mtu aweze kuishi ndani ya Utashi Wangu.

Kishapo, ile minyororo ya neema Zangu, minyororo ya ziara Zangu za mara kwa mara - je ni mingapi sijawahi kukuletea? Yote hayo yalikuwa ni kwa ajili ya kukuandaa wewe kwa ajili ya kile kilele cha kuishi ndani ya bahari kuu ya Utashi Wangu. Kwa minajili hiyo, usiwe unapenda kuulizia ulizia au kupeleleza, ila tu uendelee na safari yako ya kurukaโ€.
โฌ‡๏ธโฌ‡๏ธโฌ‡๏ธ
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 24 - Juni 12, 1928๐Ÿ–‹๐Ÿ“ƒ๐Ÿ“–๐Ÿ“”

โ€ฆ..โ€œBinti Yangu, maweza hayakosekani ndani Yangu na hata Utashi haukosekani. Kwa hiyo basi, inabidi Mimi nimwamshe na kumwinua binadamu aliyekuwa ameanguka, ili nimtengeneze upya, kwa vile utashi wa kibinadamu uliibomoa kazi ya Mikono Yetu ya uumbaji.

Kwa hoja hiyo, akiwa anasikitika na kuteseka sana kwa ajili ya masikini binadamu, alikaa kimya kwa muda na baadaye mimi nikawa nawaza moyoni mwangu: 'Itawezekanaje kurudi nyuma kwenye hali ile ya awali ya Uumbwa wakati utashi wa binadamu umekwisha kumwangusha binadamu katika kilindi cha matatizo na hata umemchafua kabisa kutoka hali yake aliyokuwa ameumbwa nayo?โ€™.

Hapo Yesu Wangu Mtamu amejibu kwa kuongeza kusema:

โ€œBinti Yangu, Utashi Wangu unaweza kila kitu; na kama vile ulivyomfanya mtu kutoka si kitu, ndivyo utaweza kumtoa binadamu mpya kutoka kwenye matatizo yake bila kubadili mtindo tuliotumia pale mwanzoni tulipomuumba.

Tutamwachia uhuru wake wa kuchagua na tutatumia sasa jeuri nyingine ya kimapenzi, yaani: mwanga wa Utashi Wetu utatikisatikisa kwa nguvu zaidi mionzi yake mikali kabisa. Mwanga huo utasogea karibu hadi kutazama na kumulika uso kwa uso ndani ya utashi wa binadamu.

Nao utashi huu wa binadamu utakapopokea uzuri na mvuto wa mwanga mkali na wenye nguvu ya kupenya namna ile, mwanga unaopofusha na papo hapo unavutia kuelekea kwake, nao utavutwa na huo mwanga unaoangaza na wenye uzuri wa aina yake na utapenda sana kuona na kujua kuna nini cha pekee katika uzuri ule wa huo mwanga mkali.

Utashi wa binadamu, kadiri unavyozidi kuutazama mwanga huo, utaingiwa na mshangao mkubwa, na bila kujitambua utaanza kufurahia na kupendelea kuishi ndani ya Utashi Wetu, siyo kwa kulazimishwa, bali kwa hiari yake wenyewe.

Je, mwanga wa jua hauna nao nguvu kama hiyo? Mbona kama mtu anapenda kukaza macho auangalie, mboni ya jicho la binadamu huwa inachomwa na kupofushwa na mwanga huo.

Unapojaribu wewe kuendelea kutazama, hutaona kitu chochote isipokuwa mwanga tu na nguvu ya mwanga inaizuia mboni isivitazame vitu vile vinavyoizunguka.

Kama binadamu hulazimika kuteremsha macho yake ili kuepuka mwanga mkali wa jua, ni kwa vile mwanga huo mkali kupita kiasi huwa unamtesa na kwa hiyo unamkosesha raha.

Kama angekuwa anapata raha, asingekuwa anatorosha haraka haraka mboni yake kutoka kwenye mwanga wa jua. Kinyume chake lakini, mwanga wa Utashi Wangu hautesi mboni ya mtu. Kwa kweli ni mtu mwenyewe ndiye atapata faida ya kuona matendo yake mwenyewe yakiwa yamebadilika kuwa mwanga na hatimaye atapenda mwanga huo utikise kwa nguvu zaidi mionzi yake hata aweze kuyaona matendo yake katika mvuto, mngโ€™ao na katika uzuri wa mwanga huo wa kimungu.

Utashi Wangu unashika uwezo wa kutatua shida ya binadamu, lakini ni budi utumie tendo la kiwango cha juu zaidi kuliko kile cha kawaida cha ukarimu mkubwa zaidi wa FIAT Yetu Kuu. Basi wewe usali na uomboleze kwa ajili ya masikini wanadamuโ€.....

Click on the link below to read the full passage. Fiat!
TAYARI KUSOMWA
โฌ‡๏ธโฌ‡๏ธโฌ‡๏ธ
https://telegra.ph/Yesu-kwa-Mtumishi-wa-Mungu-LUISA-PICCARRETA-Binti-Mdogo-wa-Utashi-wa-Mungu---KITABU-cha-MBINGU---JUZUU-na-24---Juni-12-1928-10-18
๐Ÿ’žโญ๏ธ๐Ÿ’ž
Utukufu Mkuu wa Juu, mimi ninakushukuru sana, ninakusifu, ninakutukuza na ninakuheshimu kwa shukrani zilezile, kwa sifa ile ile, kwa utukufu ule ule na kwa baraka ya Ubinadamu Mtukufu wa Yesu; na sifa ile ile, pamoja na Utukufu ule ule, mimi naviweka juu ya midomo ya ndugu wote waliopo na juu ya midomo ya kila mtu, ili kusudi, kutoka kila mdomo wa mwanadamu, Wewe upate utukufu na Baraka ya kimungu.
๐Ÿ’žโญ๏ธ๐Ÿ’ž
UTUKUFU WA WATAKATIFU PETRO NA PAULO - MITUME
โฌ‡๏ธโฌ‡๏ธโฌ‡๏ธ
Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? (Mt 16; 15)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU Na. 2 - Juni 2, 1899๐Ÿ–‹๐Ÿ“„๐Ÿ“–๐Ÿ“”

Leo asubuhi Yesu Wangu Mtamu kabisa alipenda kunifanya mimi, kwa mikono yangu mwenyewe, niuguse u-sikitu wangu. Katika lile tendo Lake la kujionyesha kwangu, maneno ya kwanza kabisa aliyoyaelekeza kwangu mimi yalikuwa ni haya:

โ€œJe Mimi ni nani, na wewe u nani?โ€

Katika maneno hayo mawili nikawa ninaiona mianga mikuu miwili: Katika mwanga mmoja niliweza kumwelewa Mungu, na katika ule mwanga mwingine niliuona u-sikitu wangu na makuruhu yangu. Nilijiona kuwa si kitu chochote isipokuwa ni kivuli tu, kama kile kivuli ambacho jua hukitoa wakati linapoiangaza ardhi: kivuli hicho huwa kinalitegemea jua. Kadiri jua linavyohama kutoka ardhi husika kwenda mahali pengine tofauti tofauti, hicho kivuli huwa kinakoma kuwepo nje ya ule uangazo wake. Kitu hichohicho hutokea kwa kivuli changu - yaani, hii nafsi yangu: nafsi yangu inalitegemea lile Jua la fumbo, yaani Mungu, ambaye, katika sekundi moja tu, anaweza akakiondoa au kukibadili hicho kivuli. Sasa niseme nini kuhusu namna nilivyokiharibu hiki kivuli ambacho Bwana alikuwa amenipatia, kivuli ambacho wala siyo cha kwangu mwenyewe? Wazo lenyewe peke yake tayari linanitisha na kuniletea kihoro: mimi ninayenuka, niliyeoza, niliyejaa usubi. Hata hivyo, nikiwa katika hali hiyo ya kutisha nikawa nimelazimishwa kusimama mbele ya Mungu aliye Mtakatifu namna ile! Lo! ni jinsi gani ningefurahia kama ningebahatika kujificha mimi mwenyewe katika malindi yenye giza totoro! Baada hapo Yesu aliniambia:

โ€œMapendeleo makubwa kupita yote ninayoweza kumtendea mtu ni kule kumfanya ajijue yeye mwenyewe. Kujijua nafsi na kumjua Mungu ni mambo yanayokwenda pamoja, yaani, kadiri unavyozidi kujijua wewe mwenyewe, ndivyo utakavyozidi kumjua Mungu. Mtu yule ambaye amekwisha kujijua yeye mwenyewe, kwa kutambua kuwa hawezi akatenda jema lolote lile kwa maweza yake mwenyewe, anakibadili hicho kivuli cha nafsi yake ili kiwe ni Mungu, na hapo huwa inatokea kwamba anaanza kutekeleza vitendo vyake vyote ndani ya Mungu. Hutokea kwamba mtu huyo anakuwa ndani ya Mungu, na anakuwa akitembea kando ya Mungu, bila kuangalia, na bila kuuliziaulizia kitu, na hata bila kuzungumzazungumza - kwa neno moja, anatembea kama vile angekuwa amekufa. Na kwa kweli, kwa kukijua fika kina cha u-sikitu wake, anafikia kutodiriki kutenda lolote lile kwa maweza yake, ila tu yeye, kama kipofu, anafuata mwelekeo wa vitendo mbalimbali vya Nenoโ€.

Kwangu mimi, inaonekana kwamba, kwa mtu anayejijua mwenyewe, huwa inatokea sawa kama inavyotokea kwa wale watu wanaosafiri katika mashua: wanaposafiri kutoka mahali pamoja kwenda mahali pengine, wao wenyewe, bila kuchukua hatua yoyote ile, wanafanya safari kadhaa ndefu, lakini mambo yote huenda kwa nguvu ya ile mashua yao inayowasafirisha. Hali kadhalika, mtu, kwa kujiweka mwenyewe ndani ya Mungu, sawa na wale watu wanaokuwa ndani ya mashua, anafikia kutekekeleza miruko mizuri mikubwa kabisa katika safari yake ya ukamilifu, huku akitambua, lakini, kwamba, siyo kwa nguvu zake, ila kwa nguvu ya yule Mungu Mhimidiwa ambaye huwa anambeba ndani Mwake. Lo! ni jinsi gani Bwana anavyompendelea, anavyomtajirisha, na anavyomgawia zile neema kuu kabisa, Bwana anafanya vile kanawa sababu anafahamu kwamba mtu huyo, kwa yote yanayotokea, yeye huwa anaelekeza sifa na utukufu, siyo kwake mwenyewe, bali kwa Mungu. Lo! ewe mtu unayejijua mwenyewe, ni jinsi gani ulivyobahatika!โ€™โ€™