Utashi wa Mungu na Upendo wa Mungu - Luisa Piccarreta
42 subscribers
311 photos
56 files
688 links
Fahamu kuhusu kutimia kwa Sala ya Baba Yetu kupitia Maandishi ya Mtumishi wa Mungu Luisa Piccarreta, Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - Kuishi Utashi wa Mungu
Download Telegram
Kwa hiyo, kwa vile wewe ndiye Binti Mdogo wa Utashi Wangu Mkuu wa Juu, basi Mimi ninakushauri kuwa: Tafadhali acha kila kitendo chako kiwe ni mateka ya yale mawimbi ya Utashi Wangu, ili kusudi, wakati hayo mawimbi yatakaporuka na kuifikia miguu ya Kiti Chetu cha utawala kule Mbinguni, Sisi tuweze, zaidi na zaidi, kukuthibitisha wewe kama ndiye Binti Yetu halisi wa Utashi Wetu, na papo hapo, tuweze kukupatia wewe zile hati za neema kwa ajili ya ndugu zako na watoto Wetu”.
Wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia? (Mk 4, 38)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 4 - Januari 6, 1902🖋📃📖📔

Na Yesu akaondoka na kufifia. Lakini, punde tu baadaye akawa amerejea, na, pamoja Naye nikawa ninawaona watu mbalimbali ambao walikuwa wakiogopa sana sana kifo. Ndipo nilipoona hilo nikasema: ‘Ewe Yesu WanguMpendevu, je, itakuwa ni kasoro kwangu mimi, hiyo hali ya kutoogopa kabisa kifo wakati ninashuhudia wengine wakikiogopa sana sana kwa namna hiyo? Mbona mimi, kwa kudhani kwamba kifo kitaniunganisha na Wewe kwa daima, na kwamba kitakomesha kile kifodini kitokanacho na ule utengano mkali kabisa, hilo wazo peke yake la kifo, siyo tu haliniletei hofu yoyote ile, lakini, kwangu mimi linanipatia kitulizo, linaniletea amani, na ninalisherehekea, huku nikiachilia na nikitupilia mbali yale matokeo mengine yote ambayo huwa yanaleta kifo’. Hapo Naye Yesu alijibu akisema:

“Binti, mbona kwa kweli, hiyo hofu kubwa mno ya kufa ni jambo la upuuzi kabisa wakati kila mmoja anayo mastahili Yangu yote, anazo fadhila Zangu zote na zile kazi Zangu zote kama pasipoti kwa ajili ya kuingilia Mbinguni, ikiwa ni baada ya Mimi kuwa nilizitoa kama zawadi kwa wanadamu wote. Na wanaofaidi zaidi zaidi hiyo zawadi ni wale ambao wameongezea chochote kile cha kwao.

Sasa, ukishakuwa na mambo hayo yote, mtu atakuwa na hofu gani tena? Na kwa pasipoti hiyo ya uhakika kabisa, mtu anaweza akaingia kokote anakotaka, na watu wote, wanapoiona hiyo pasipoti, watakuwa wanamheshimu mtu huyo, na watakuwa wanampitisha. Halafu, kwako wewe, suala hilo la kutokuogopa kamwe kifo, linatokana na ukweli kwamba umekuwa ukitenda mambo pamoja Nami, na pia kwa kuwa umekuwa ukionja jinsi gani, ule muungano na Chema Kikuu cha juu, ulivyo ni mtamu na mpendevu. Hata hivyo, ni vema ukajua kwamba, heshima kuu, inayopendeza kupita zote, anayoweza mtu kuitoa Kwangu Mimi, huwa ni kule kutamani kufa kwa ajili ya kujiunganisha na Mimi, na tena, hiyo ndiyo maandalizi yaliyo mazuri na yapendezayo kuliko kila kitu kwa ajili ya mtu kuweza kujisafisha na kujitakasa, na hiyo humwezesha mtu, kupita bila kukatishwa katishwa, moja kwa moja, katika ile njia ya Mbinguni”.

Baada ya kuyasema hayo, Yeye aliondoka na kufifia.
SHEREHE YA KUZALIWA KWA MT. YOHANE MBATIZAJI
⬇️⬇️⬇️
«Mtoto huyu atakuwa wa namna gani?» (Lk 1; 66)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 23 - Desemba 22, 1927🖋📄📖📔

....”Ninapoteua kiumbe fulani kwa ajili ya utume, ambao lazima ulete manufaa kwa familia ya binadamu ya ulimwengu mzima, huwa kwanza kabisa naweka na kuingiza mema yote ndani ya mtu huyo, ambaye lazima ajazwe ndani yake hayo mema yote, katika kiwango cha kufurika kabisa, kwani watu wengine watapasika kuja kuchukua mema hayo, ingawa kama pengine hawatafaulu kuchukua mema yote yaliyopo ndani ya mteule huyo. Hicho ndicho kilichotokea katika Malkia Immakulata, ambaye aliteuliwa kuwa Mama wa Neno wa Milele, na hivyo akawa ni Mama wa watu wote waliokombolewa.

Chochote ambacho walipasika kutenda, na chema chochote walichopasika kukipata, vilikuwa vyote vimefungiliwa na kupigiliwa, kama vile ndani ya tufe la jua, ndani ya Malkia Mtawala wa Mbingu.

Kwa jinsi hiyo wakombolewa wote wanatembea kuzunguka jua la Mama wa Mbingu, na kwa hiyo na yeye, zaidi ya kuwa Mama mpendevu kabisa, hatendi kitu kingine isipokuwa kumwaga mionzi yake juu ya wana wake.

Anawamwagia mionzi ili kuwalisha kwa mwanga wake, kuwalisha kwa utakatifu wake na kwa pendo lake la kimama. Lakini ni mionzi mingi mingapi anayoisambaza, ambayo haichukuliwi na wanadamu kwa vile katika ufidhuli wao, hawajitahidi kusogea na kusonga mbele kwenda kumzunguka huyu Mama wa Mbinguni?

Kwa hiyo basi, yule anayekuwa ameteuliwa ni budi ajipatie mambo zaidi kuliko yale wanayotakiwa kupata wengine wote wakiwa wamejumlishwa pamoja.

Kama vile watu wote hujipatia mwanga kutoka kwa jua, lakini hata hivyo ni kwa namna na kiasi kwamba wanadamu hao wote hawachukui na kumaliza mwanga wote wala hawachukui moto wote wa joto la jua, ndivyo ilivyotokea kwa Mama Yangu: Yeye anayo ndani yake mema mengi hivi na ya jinsi mbalimbali hivi kwamba zaidi ya mithili ya jua, anasambaza mema hayo na matokeo ya mionzi yake ya Uhai na inayohuisha. Ndivyo hivyo itakuwa kwa mtu yule atakayeteuliwa kwa ajili ya Ufalme wa Utashi Wangu.

Ebu ona kwa hiyo jinsi utakavyolipwa kwa sadaka yako ya kuandika: Kwanza kabisa, kwa kudumu, unajipatia na kuwekewa ndani yako lile jema la mwonzi wa ule ufahamu.

Kishapo utaona jema hilo, kwa kupitia kwako, likiteremka na kushuka juu ya wanadamu wote na jema hilo likiisha kubadilishiwa ndani ya wanadamu utaona Utukufu, wa jema watakalokuwa wanalitenda, ukipanda juu katika mwanga ule ule. Ni jinsi gani utakavyofurahi na utakavyonishukuru kule Mbinguni kwa sadaka hizo nilizokufanya ukazitekeleza!

Binti Yangu, kama kazi fulani ni kubwa, ni kwa ajili ya ulimwengu, kama inajumlisha ndani yake mema mengi sana wanayoweza kufaidi watu wengi, hapo huhitajika sadaka kubwa zaidi. Na yule aliyeteuliwa wa kwanza hana budi kuwa tayari na hiari kutoa na kujitolea sadaka mara nyingi sana, hata uhai wake, kwa ajili ya yale mema mengi yaliyomo ndani.

Anapotoa mema yale atoe pia hata uhai wake wenyewe kwa ajili ya faida ya ndugu zake wengine. Je Mimi sikutenda hivyo hivyo katika Ukombozi?

Je wewe hutaki kuniiga Mimi?”
Akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli. (Lk 1; 80)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 2 – Mei 23, 1899🖋📃📖📔

…“Binti Yangu, ni kwa hoja hiyo, jambo la kwanza kabisa ninalolipendekeza sana sana kwa wanadamu huwa ni kujitenga na mambo yote na hata kujitenga na nafsi yao wenyewe. Kama mtu amefanikiwa kujitenga kabisa na mambo yote, huyo hatahitaji tena kuchota nguvu zake kwa ajili ya kubakia mbali na mambo hayo yote ya dunia, ambayo, kwa yenyewe, huwa yanamjia toka kila upande. Hata hivyo, mambo hayo, yanapoona kuwa yanazembewa tu, na zaidi zaidi, yanapoona kuwa yanadharauliwa, yenyewe yatasema kwaheri kwa mtu huyo na ndipo yataondoka na kumwacha mtu huyo hata yasiweze kumsumbua zaidi”.
⬇️⬇️⬇️
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 6 - Julai 28, 1904🖋📃📖📔

….“Binti Yangu, wakati mtu amejitenga na mambo yote, huyo huwa anamkuta Mungu ndani ya kila kitu. Huwa anamwona Mungu ndani yake yeye mwenyewe, anamwona pale nje yake mwenyewe, na anamwona Mungu ndani ya wanadamu. Kwa hiyo, twaweza kusema kuwa, kwa mtu ambaye amejitenga kitimilifu, mambo yote hugeuka na kuwa Mungu. Na zaidi zaidi, huwa siyo tu anamkuta Mungu, bali huwa anamtafakari, anamwonja, na anamkumbatia. Na kwa vile anamkuta katika kila kitu, ndivyo vitu vyote huwa vinampatia mtu huyo wasaa mzuri wa kumwabudu Mungu, wasaa wa kusali na kumwomba, wa kumshukuru, na wasaa wa kumkaribia Mungu katika upenzi wa ndani zaidi.

Aidha, yale manung’uniko yako juu ya kukosekana Kwangu hayana sababu za kutosha. Kama wewe unanionja Mimi hapo ndani mwako, basi ni alama tosha kwamba, Mimi, siyo tu nipo nje ya wewe, bali nipo hata hapo ndani, na nipo hapo kama kwenye makao Yangu”.....
⬇️⬇️⬇️
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 14 - Juni 26, 1922🖋📃📖📔

Nilikuwa nikiendelea na ile hali yangu ya siku zote. Ndipo Yesu Wangu Mpendevu wa daima alikuja. Na kwa vile kwa siku kadhaa nilikuwa nimeterereka kabisa kiafya, kiasi kwamba nikawa nimejikunyata na nisiweze kujimudu kwa lolote, Yesu alitwaa mikono yangu na kuishika ndani ya mikono Yake, huku akiniambia: “Binti Yangu, ebu niache nikunyoshe Mimi”. Halafu, alinisogelea na akachukua mikono yangu na kuiweka juu ya mabega Yake akiniambia:

“Sasa umenyoka. Ebu nikumbatie na kunibania kwako kwani nimekuja ili nikeshe pamoja nawe na wewe unilipe kwa kukesha pamoja Nami. Ebu ona, Mimi ni Mungu niliyetengwa na wanadamu, Mimi ninaishi kati yao, Mimi ni uhai wa kila tendo lao, na Mimi ninajifanya kana kwamba sipo kabisa pamoja nao. Oh, ni jinsi gani ninavyorudia kulia mintarafu upweke Wangu! Kwangu kunatokea kitu kile kile kinachotokea kwa jua. Yaani, wakati hilo jua, pamoja na mwanga wake na joto lake, linaishi kati ya watu wote, na wakati hakuna nguvu ya rutuba yoyote ambayo haitoki kwake, na wakati, kwa joto lake, linaisafisha ardhi isipate mipasuko mingi, na wakati linayashusha kwa ukarimu kabisa, juu ya watu wote, manufaa yake yasiyohesabika, hata hivyo, lenyewe bado linaishi daima, kule juu likiwa peke yake kabisa. Na binadamu aliye mtovu wa shukrani hajawahi kusema kwake neno la asante kama uthibitisho wa kunitambua na kunikiri. Ndivyo nilivyo Mimi: Mpweke, daima peke Yangu! Wakati ninapokuwa kati yao Mimi ni mwanga wa kila wazo, Mimi ni sauti ya kila neno, Mimi ni ujimudu wa kila kazi, Mimi ni hatua ya kila mguu, Mimi ni pigo la kila moyo! Na huyu binadamu, mtovu wa shukrani, ananiacha peke Yangu kabisa, haniambii asante yoyote ile, wala hanitamkii kauli ya Ninakupenda.

Huwa ninabaki nimetengwa katika akili, kwa vile ule mwanga ninaoutoa kwa akili yao wanautumia kwa mambo yao na pengine kwa ajili ya kuniudhi Mimi. Nimetengwa katika maneno, kwa vile, mara nyingi, sauti wanayotoa, hutumika kwa ajili ya kunikufuru Mimi. Ninabaki nimetengwa katika kazi mbalimbali kwa vile wanazitumia kwa ajili ya kuniua Mimi. Ninatengwa katika hatua za miguu, na katika moyo kwa vile huwa wananuia kunikaidi tu Mimi na wananuia kupendelea kile ambacho hakinihusu Mimi. Oh, ni jinsi gani upweke huo unavyonitesa Mimi! Hata hivyo, Pendo Langu, Wema na Ukarimu Wangu ni mkubwa hivi, kiasi kwamba, zaidi kupita hata jua, Mimi ninaendelea na njia Yangu ya maamuzi, na katika njia hiyo, ninaendelea kuchunguza iwapo kuna mtu fulani ambaye angependa kuja kukesha Nami katika upweke Wangu huo mkubwa. Ninapomkuta, basi najenga uhusiano wa kukesha naye kwa daima na ninammwagia mtu huyo neema Zangu zote.

Ndiyo maana Mimi nimekujia wewe - nilikuwa nimechoka na hali hiyo ya upweke. Tafadhali, Binti Yangu, usiniache peke Yangu”.
💦☀️☀️☀️💦
Ewe Uhai wangu na Ewe uliye Chote Changu, unijalie hatua zako ziongoze hatua zangu na kila nikanyagapo ardhi, mawazo yangu yawe mbinguni.
💦☀️☀️☀️💦
🤍🤍🤍
Naingia Ndani ya Bahari Kuu ya Utashi Wako
🤍🤍🤍
Ewe Yesu Wangu Mtamu,
mimi ninaingia ndani ya bahari kuu ya Utashi Wako, Ninapigilia utashi wangu ndani ya Utashi Wako na ninakuomba unipe Utashi Wako kama Uhai wangu, kama Uhai wa kila tendo langu, liwe lile la ndani au lile la nje, liwe lile la kiutashi au lile lisilo la kiutashi.
🤍🤍🤍
Ee Bwana,
naomba kwamba kila kitu kiwe ndani ya Utashi Wako wa Kimungu, ili niweze kukulipa kwa pendo, kwa uabudu, na kwa utukufu kana kwamba wanadamu wote wangekulipa hilo deni kwa utimilifu wote.
🤍🤍🤍

(✍️Kitabu cha Mbingu - Juzuu Na. 14 - Mei 27, 1922)
Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua. (Mt 7; 6)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na.20 - Oktoba 2, 1926🖋📄📖📔

Nilijikuta katika kipindi cha masikitiko na uchungu mno kutokana na kukosekana kwa Yesu Wangu Mtamu. Oh! Kwa jinsi nilivyokuwa nikijisikia vibaya, sikuweza kufanya lolote tena. Hata hivyo, nilipokuwa nimefikia kilele cha mateso, Yeye aliingia pale ndani yangu huku akiwa katika mateso makali kabisa. Ndipo aliniambia:

“Binti Yangu, nipo nikiangalia ni kwa kiasi gani yanipasa kupanua mipaka ya Ufalme wa Utashi Wangu, hata niweze kuukabidhi Ufalme huo kwa wanadamu. Ninafahamu fika kwamba wao hawataweza kutwaa ule upeo usio na ukomo uliopo katika Ufalme wa Utashi Wangu, kwa vile, kwake mwanadamu, haujatolewa bado ule uwezo wa kuuvuka na kuukumbatia Utashi unaouwiana na Ufalme usiokuwa na mipaka. Ni kwa vile, mwanadamu, kwa kuwa kaumbwa, yeye daima huwa ni finyu na mwenye mipaka. Na kwa hoja kwamba ana mipaka kulingana na hali zake za maandalizi na uhiari, Mimi huwa ninampelekea mema zaidi au pungufu, na ninampelekea na kumpatia upana zaidi au pungufu wa mipaka anayotakiwa awe nayo. Ndiyo maana Mimi sasa nipo nachunguza vizazi vijavyo vitakuja kuwa na hali gani ya maandalizi na uhiari, ninachunguza pia vizazi vilivyopo vya sasa kuona hali waliyo nayo sasa hivi, kwani hawa wa sasa budi wawe wanasali, wawe wanasihi, na wawe wanauandaa Ufalme wa ile FIAT Kuu ya Juu kwa ajili ya vizazi vijavyo. Na kulingana na hali ya maandalizi na utayari wa vizazi vijavyo, na kulingana na hamu waliyo nayo vizazi vya sasa, ndivyo na Mimi naendelea kuongeza na kupanua mipaka ya huo Ufalme Wangu. Ni kwa vile vizazi hivi vimeunganika sana kati yao, kiasi kwamba, huwa inatokea jinsi hiyo kila mara, kuwa kizazi kimoja kinasali, kizazi kingine kinaandaa, na kizazi kingine tena kinasihi na kuomboleza na kizazi kingine ndicho kinachoubeba Ufalme.

Ndivyo hivyo hivyo ilitokea katika ule ujio Wangu hapa duniani, nilipofika kushughulikia Ukombozi. Havikuwa ni vizazi vya hivi sasa ambao walikuwa wakisali, waliotweta na waliolia ili kuyapata mema yake - kwani hawa ndio wanaoyafaidi na wanayoyatwaa na kuyabeba - bali walikuwa ni wale waliokuwa wameishi kabla ya ujio Wangu. Na kadiri ya hali ya maandalizi na hiari ya watu wale wa kizazi hiki cha sasa, na kutokana na sala na hali za maandalizi na hiari ya wale wa kizazi kilichopita, ndivyo na Mimi nilivyozidi kupanua mipaka ya yale mema ya Ukombozi. Na kwa kweli, Mimi huwa ninatoa jema fulani pale tu ambapo jema hilo litakuwa na manufaa kwa wanadamu. Lakini, iwapo jema hilo halitaleta manufaa yoyote, kuna haja gani ya kulitoa? Na manufaa hayo huchukuliwa na hao wanadamu iwapo wamekuwa na maandalizi zaidi na uhiari zaidi. Lakini, je, wajua wewe ni lini ninapopanua mipaka yake? Ni pale ninapokueleza na kukuonyesha wewe maarifa fulani mapya yanayohusu huu Ufalme wa Utashi Wangu. Ndiyo maana, kabla sijakueleza na kukuonyesha wewe, huwa kwanza ninatupia jicho Langu kwa watu wote ili kuchunguza kuona hali zao za maandalizi - yaani, kuona kama itakuwa na manufaa kwao, au pengine, itakuwa kwao sawa na kama vile hakikusemwa chochote kabisa. Na wakati ninapokumbuka kuwa Mimi ninanuia kupanua zaidi na zaidi mipaka Yangu kwa ajili ya kuwapatia mema mengi zaidi ya kubeba, kuwapatia furaha zaidi, na kuwapa raha zaidi, na papo hapo ninapogundua kuwa wao hawapo tayari kwa hilo, Mimi huwa naonja kuteseka sana sana, na ndipo huwa ninasubiria sala zako, ninasubiria ziara zako ndani ya Utashi Wangu, nasubiria maumivu yako, ili kusudi niweze kuwaandaa wale wa kizazi cha sasa na wale wa kizazi kilichopita. Na kishapo huwa ninarejea kule kwenye mambo yale ya kushitua ya maelezo Yangu mintarafu Utashi Wangu.
Ndiyo maana huwa ninashikwa na uchungu sana na maumivu pale ninapokuwa sizungumzi nawe. Neno Langu ndiyo zawadi kubwa kupita zote - huwa ni uumbaji mpya. Kutokana na Mimi Mwenyewe kushindwa kulitoa toka ndani Mwangu, kwa vile wanadamu wanakuwa hawapo tayari kulipokea neno hilo, huwa ninaonja ndani Yangu ule uzito wote wa ile zawadi ninayonuia kuitoa, na, kwa kushindwa kuitoa, huwa naendelea kuteseka na ninabaki kunyamaza. Na mateso Yangu huwa yanaongezeka hata zaidi na zaidi pale ninapokuona na wewe unateseka kwa ajili Yangu Mimi. Laiti ungefahamu jinsi ninavyoonja masikitiko yako - na jinsi uchungu wako huo unavyomwagikia ndani ya Moyo Wangu! Utashi Wangu huwa unauingiza uchungu huo hadi kilindini mwa Moyo Wangu. Ni kwa vile Mimi sina tashi mbili, bali ninao utashi mmoja tu. Na kwa vile huo Utashi Wangu ndio unaotawala ndani yako wewe, matokeo yake ni kwamba, huo Utashi Wangu huwa unaleta yale mateso yako hadi kwenye kina cha ndani Mwangu. Kwa hiyo basi, wewe uwe unasali, na hebu ule mruko wako uwe endelevu daima ndani ya ile FIAT Kuu ya Juu, ili pale ukawe unaendelea kusihi kwamba wanadamu wawe wanajiandaa wenyewe, na Mimi niweze kurejea kuja kuzungumzia kwa mara nyingine”……
Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba. (Mt 7; 13)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 6 - Juni 23, 1905🖋📃📖📔

Wakati nikiendelea na ile hali yangu ya siku zote, nikawa ninawaza juu ya jinsi Yesu Kristo alivyokufa, na pia juu ya kwamba Yeye hakuweza kuogopa kifo, kwani, maadam alikuwa ameunganika kabisa na ule Umungu, au tuseme, alikuwa amegeuzwa kuwa katika hali ya Umungu, basi, alikuwa tayari ni salama kabisa sawa na mmoja anayekaa katika jumba lake mwenyewe. Lakini, kwa mtu huyo - lo! Ni tofauti gani kubwa iliyopo. Pindi nikiwazia hayo na ujinga wangu mwingine, Yesu Mhimidiwa alikuja na kuniambia:

“Binti Yangu, yule anayekuwa ameunganika na Ubinadamu Wangu, huyo huwa anajikuta yupo tayari mlangoni pa Umungu Wangu, kwa vile, Ubinadamu Wangu ni kioo cha mtu cha kujitazamia, kwani kutoka hicho kioo Umungu huwa unaweza kuonekana pale ndani ya huyo mtu husika. Na kama mmoja yupo tayari katika picha kioo ya kioo hicho, ni wazi kabisa kwamba nafsi yake yote budi iwe imegeuzwa kuwa ni Pendo. Sasa, Binti Yangu, kwa vile kila kitu kitokacho kwa mwanadamu, hata ule ujimudu mbalimbali wa macho yake, ujimudu wa midomo yake, ujimudu wa mawazo yake, na mengineyo yote - kila kitu budi kiwe ni Pendo, na kiwe kimetekelezwa kwa ajili ya upendo. Na kwa vile nafsi Yangu yote ni upendo mtupu, basi popote pale ninapolikuta pendo, Mimi hapo ninanyonya kila kitu ndani Mwangu, na yule mtu anaingia kukaa kwa utulivu kabisa ndani Yangu Mimi kama vile anavyokaa yeyote yule ndani ya jumba lake mwenyewe.

Basi, sasa mtu, katika saa yake ya kufa, anaweza akawa na hofu gani ya kuja Kwangu Mimi wakati yupo tayari ndani Yangu Mimi?”
⬇️⬇️⬇️
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 9 – Machi 16, 1910🖋📄📖📔

Nilipokuwa nikizungumza na Padre Mwungamishi, aliniambia kuwa kuokoka ni suala gumu kwa vile Yesu Kristu Mwenyewe aliwahi kusema hivyo: “Mlango ni mwembamba. Ni budi mjitahidi kuuingia”. Halafu, baada ya mimi kupokea Komunyo Takatifu, Yesu aliniambia:

“Masikini Mimi, ni jinsi gani wanavyodhani kwamba Mimi ni bahili. Ebu kamwambie huyo Padre Mwungamishi: wao wananihukumu Mimi kwa kulingana na ubahili wao wenyewe. Hawanihesabu kama ndiye niliye Mkuu, niliye mkubwa mithili ya bahari, niliye bila ukomo, niliye mwenye maweza, niliye bila mipaka katika sifa Zangu zote za ukamilifu, kwamba, ndiye ninayeweza kuyafanya makundi makubwa ya watu yakapita pale penye uwembamba, na wakaweza kupita zaidi kuliko pale penye upana wenyewe”.

Na alipokuwa akiyasema hayo, nikawa ninaona kama vile njia nyembamba iliyokuwa ikielekea kwenye mlango mdogo, mwembamba na uliokuwa umejaa kabisa na watu ambao walikuwa wanapigania kati yao nani atangulie zaidi hata akaweze kuingia pale ndani. Yesu akaongeza kusema:

“Ewe Binti Yangu, ebu angalia ni kundi kubwa lilioje lile linalojisukuma pale kwenda mbele. Na pale wanashindania kuona nani atakayeweza kuwasili wa kwanza. Katika mashindano huwa kuna kushinda kwingi. Lakini kumbe, kama njia ingekuwa ni pana, pasingekuwa na mtu anayehangaika kuharakisha, kwani, wangejua kwamba kuna nafasi ya kutosha kwa ajili ya kuweza kuendelea kutembea wakati wowote ule wanapotaka. Lakini, pindi wanapopitisha muda wao wakingoja kuanza mwendo wao, kifo chaweza kuwafikia, na wao, wanapojikuta hawatembei katika njia nyembamba, wangeshitukia wanawasili penye lile lango pana la lile geti kuu la motoni mwa milele. Lo, ni faida gani kubwa inayoletwa na huu uwembamba! Jambo hilo huwa linatokea hata hapo kati yenu ninyi wenyewe: Iwapo kunatokea kuwa na sherehe au pakiwa na ibada fulani, na iwapo inafahamika fika kwamba nafasi iliyopo ni ndogo, basi watu wengi sana huwa wanaharakisha kufika, na mwishowe huwa wanahudhuria washiriki wengi sana waliofika kuja kufurahia hiyo sikukuu au ibada. Kumbe lakini, endapo inajulikana kuwa nafasi iliyopo ni kubwa, hakuna mtu anayehangaika kuharakisha na mwishowe huwa ni wahudhuriaji wachache tu wanaofika, kwa vile tu wanajua kwamba kuna nafasi ya kutosha kabisa kwa ajili ya kila mtu. Kila mmoja huwa anakuja kwa raha na kwa wakati wake. Na baadhi huwa wanafika katikati ya sherehe, na wengine wanafika hata mwishoni, na wengine wanapofika, wanakuta sherehe imekwisha kumalizika, na hivyo hawawezi kufaidi chochote. Hilo ndilo ambalo lingetokea iwapo njia ya wokovu ingekuwa ni pana - ni watu wachache tu wangekuwa wanahangaika kuharakisha, na sherehe ile ya Mbinguni ingebaki kuwa ni ya wachache tu’’.
Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. (Mt 7; 14)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU Na. 3 – July 10, 1900🖋📃📖📔

….Kwa hiyo basi, Yesu Mhimidiwa akaanza kurudia kunielezea ile tofauti iliyopo kati ya kuishi kwa ajili ya Mungu na kuishi ndani ya Mungu. Aliniambia hivi:

“Katika kuishi kwa ajili ya Mungu, mtu anaweza akawa anakabiliwa na vurugu mbalimbali, na machungu mbalimbali, anakabiliwa na utovu wa uthabiti, anaelemewa na mzigo wa matamaa mbalimbali, na anakabiliwa na maelekeo ya kujiingiza katika mambo ya kidunia. Kumbe lakini, kuishi ndani ya Mungu - la hasha, ni jambo tofauti kabisa kabisa, kwa vile, jambo linalokuwa ni muhimu kabisa kwa mtu kuingia na kufanya makao pale ndani ya nafsi nyingine, huwa ni kusalimisha kwa mtu husika yale mambo yote anayoyamiliki - yaani, ni mtu mwenyewe kujivua mambo yake yote, yaani ni kule kuachana kabisa na matamaa yake mwenyewe. Kwa neno moja, ni kuacha mambo yote ili akayaone hayo mambo yote pale ndani ya Mungu.

Sasa basi, kama mtu, siyo tu amejivua kabisa, bali hata amejikondesha na kuwa mwembamba kabisa, ndipo hapo ataweza kupita na kuingia pale penye mlango mwembamba wa Moyo Wangu, na hivyo ataweza kuishi pale ndani Yangu kulingana na mtindo Wangu Mimi, na ataishi kwa nguvu ya Uhai Wangu Mimi Mwenyewe. Na kwa kweli, hata kama Moyo Wangu ni mkubwa na mpana ajabu, mpana jinsi kwamba hakuna ukomo wa mipaka yake, lakini hata hivyo, mlango wa Moyo huo ni mwembamba mno mno. Ndiyo maana, ni yule tu aliyejivua kila kitu ndiye ataweza kupita na kuingia pale.

Na jambo hilo lina sababu yake, kwani, maadam Mimi ni Mtakatifu mno, nisingeweza kamwe kukubali kuingiza chochote kile kije kuishi ndani Mwangu ambacho chenyewe ni kigeni kabisa au ni mbali kabisa na utakatifu Wangu. Kwa hiyo basi, Binti Yangu, wewe jaribu kuishi ndani Mwangu Mimi, na wewe utafikia kuibeba na kuimiliki Paradiso hata kabla ya wakati”.

Sasa hapo, ni nani atakayeweza kuelezea ni kiasi gani nilichokielewa juu ya suala hilo la kuishi ndani ya Mungu? Kumbe halafu, Yeye aliondoka na kufifia, na mimi niliachwa pale nikiendelea kuwa katika ile ile hali yangu.
UFALME WAKO UJE
⬇️⬇️⬇️
Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
Mapenzi yako yatimizwe,
hapa duniani kama huko mbinguni.
(Mt 6; -10)

⬇️⬇️⬇️📚
http://divinewilldivinelove.com/Kiswahili-/-Swahili/

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!

🤍☀️🤍☀️🤍☀️

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

⬇️⬇️⬇️
Swahili - Telegram Channel – Utashi wa Mungu na Upendo wa Mungu:
https://t.me/UTASHIWAMUNGUNAUPENDOWAMUNGU

Swahili - Telegram Channel – Saa 24 Za Mateso:
https://t.me/Saa24ZaMateso_Official/5

Swahili - Telegram Channel - Bikira Maria Katika Ufalme wa Utashi wa Mungu
https://t.me/BikiraMaria_Official/6
Njoo Wewe Mwenyewe, Yesu Wangu, pamoja na Ubinadamu Wako, uyeyushie Moyo Wako ndani ya moyo wangu, ili kusudi mimi niwe ninatumia mapigo ya Moyo Wako wenyewe, niwe ninapumua kwa njia ya pumzi Yako, na niwe ninapenda kwa njia ya Pendo Lako lenyewe....
🔥☀️🔥
Njoo pamoja na Utashi Wako, njoo pamoja na Mama, na pamoja na Moyo wake Immakulata, njoo ndani ya moyo wangu ukawe unagonga humo kwa njia ya Pendo Lako. Na kwa njia hiyo, mimi nitakupatia pendo kwa Pendo, pumzi kwa Pumzi, na moyo kwa Moyo....
🔥☀️🔥
Na kila kitu kitakuwa kinastahilika Kwako, kitakuwa ni cha Kimungu, kitakuwa ni cha kutosha, kwani yote yatakuwa ni katika Utashi Wako na katika Pendo Lako.
🔥☀️🔥
Ndivyo Wewe utaweza kuridhika kwamba ulikuwa umeuumba moyo wangu, na utakuwa umelipwa kwa njia ya Pendo.
🔥☀️🔥
Na katika moyo wangu, mimi nitakuwa nikionja kuwa Moyo Wako unabeba ndanimo moyo wa wanadamu wote. Ndipo sisi sote kwa pamoja tutalipa fidia kwa kila pigo la moyo lililokufuriwa na kwa kila pumzi.
🔥☀️🔥
Kishapo, moyo wangu, ndani ya Moyo Wako na pamoja na Moyo Wako utakuwa ukisema: Enyi roho za watu, Pendo!

(Kitabu cha Sala Mbalimbali - Njoo ewe Utashi wa Mungu, Njoo Ukawe Mapigo ya Moyo Wangu)
"Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya." (Mt 7; 17)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 18 - Januari 28, 1926🖋📄📖📔

....“Binti Yangu, lengo la kwanza kabisa la Mimi kuja hapa duniani lilikuwa hasa ni hili - kwamba binadamu arudi tena ndani ya tumbo la Utashi Wangu, kwa vile, ndipo mahali alipotokea wakati ule alipoumbwa.

Lakini, ili kulitekeleza hilo, ilibidi Mimi, kwa njia ya Ubinadamu Wangu, nitengeneze ule mzizi, lile shina, yale matawi, yale majani, na yale maua, ambayo kwayo yatatoka yale matunda ya kimbingu ya Utashi Wangu.

Hakuna mtu yeyote atakayeweza kupata tunda bila kuwa na mti. Mti huo ulikuwa umemwagiliwa maji kwa Damu Yangu.

Ulikuwa umelimiliwa na kupaliliwa kwa maumivu Yangu, kwa mitweto Yangu, na kwa machozi Yangu. Jua lililowaka juu ya mti huo lilikuwa ni lile Jua la Utashi Wangu peke yake.

Kwa hiyo, ni uhakika kwamba, yale matunda ya Utashi Wangu, yatapatikana tu. Lakini, ili mtu afikie kuyatamani hayo matunda, ni budi mtu afahamu kwanza jinsi matunda hayo yalivyo ni azizi, budi afahamu manufaa yanayoletwa na matunda hayo, na utajiri ule ambao matunda hayo huzalisha.

Basi, hiyo ndiyo hoja kwa yale maelezo mengi niliyokuwa nimekupatia mintarafu Utashi Wangu. Ni kwa vile, maarifa au ufahamu ndio utakaoleta hamu ya kula huo Utashi Wangu. Na baada ya wanadamu kuonja maana ya kuishi kwa ajili ya kutekeleza Utashi Wangu peke yake, basi, kama siyo watu wote, lakini, baadhi, hakika watarudi kwenye njia ya Utashi Wangu, zile tashi mbili zitabusiana kwa umilele, na wala hapatakuwa tena mvutano na mgongano kati ya utashi wa kibinadamu na Ule Utashi wa Muumba, na ule Ukombozi Wangu, utaongeza kutoa hata lile tunda la Mapenzi Yako Yatimizwe Duniani kama Mbinguni[1].

Basi wewe, na uwe ni wa kwanza kulipokea tunda hilo, na wala usitamani tena chakula kingine, wala uhai mwingine isipokuwa Utashi Wangu peke yake”.

[1] Mapenzi Yako Yatimizwe Duniani kama Mbinguni = Kilatini: Fiat Voluntas Tua sicut in Coelo et in Terra.
🔥🔥🔥🙏🙏🙏

Ewe Yesu Wangu Mtamu,
mimi ninaingia ndani ya bahari kuu ya Utashi Wako, Ninapigilia utashi wangu ndani ya Utashi Wako na ninakuomba unipe Utashi Wako kama Uhai wangu, kama Uhai wa kila tendo langu, liwe lile la ndani au lile la nje, liwe lile la kiutashi au lile lisilo la kiutashi.

Ee Bwana,
naomba kwamba kila kitu kiwe ndani ya Utashi Wako wa Kimungu, ili niweze kukulipa kwa pendo, kwa uabudu, na kwa utukufu kana kwamba wanadamu wote wangekulipa hilo deni kwa utimilifu wote.

🔥🔥🔥🙏🙏🙏

(Kitabu cha Mbingu - Juzuu Na. 14 - Mei 27, 1922)
Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni (Mt 7; 21)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 16 - Mei 13, 1924🖋📃📖📔

…..“Ewe Binti Yangu, je unaona? Kitendo cha kwanza cha Nafsi Tatu za Mungu kimekuwa ni uelewano au upatano kamili wa Utashi Wetu. Utashi Wetu umeunganika mno hivi kwamba Utashi wa Mmoja hauwezi ukatofautiana kutoka Ule Utashi wa Yule Mwingine. Ni ndivyo hivyo kwamba, hata kama Nafsi Zetu ni tofauti - kwa vile tupo Watatu - Utashi Wetu, hata hivyo, ni mmoja tu na huo Utashi mmoja ndio unaozalisha tendo endelevu la uabudu kamili kati ya zile Nafsi Tatu za Mungu - yaani, Mmoja huwa anamwabudu Mwingine. Huo uelewano na mapatano ya Utashi ndio unaozaa usawa katika utakatifu, usawa wa mwanga, usawa wa wema, usawa wa uzuri, wa maweza, wa pendo, na ndio unasimika ndani Yetu Sote ufalme wa kweli, wa utaratibu, na wa amani, na unatupatia Sisi bahari ya furaha mbalimbali na raha mbalimbali, na heri mbalimbali zisizo na mipaka. Kwa hiyo basi, ule uelewano na mapatano ya utashi wa kibinadamu na Utashi wa Mungu, huwa ndicho kiunganisho cha kwanza cha uhusiano kati ya Muumba na mwanadamu. Na kutokana na huo uelewano na mapatano, zile nguvu za kimungu huwa zinateremka kuja ndani ya mwanadamu mithili ya kutiririka ndani ya mfereji, na hivyo kuweza kutengeneza ndanimo ule uabudu wa kweli na pendo kamili kwa ajili ya Muumba Wake. Na kwa kuibuka kutoka ndani ya huo huo mfereji wa uhusiano, mtu huwa anazipokea zile dozi mbalimbali na tofautitofauti za maweza mbalimbali ya kimungu. Na kila mara mtu anapoibuka na kupanda juu ili arukie ndani ya huo Utashi wa Milele, huwa anapambwa na uzuri wa kimungu, na huwa anajipatia, aina nyingi nyingi na mbalimbali za huo uzuri wa kimungu.

Ndiyo maana Mimi ninasema kwamba mtu anayetekeleza Utashi Wangu huwa ni burudani Yangu, na ni raha Yangu. Na kwa ajili ya kujiburudisha Mimi Mwenyewe, Mimi huwa ninashika daima brashi ya Utashi Wangu mikononi Mwangu, na mara tu anaporukia na kuingia ndani ya Utashi Wangu, Mimi ninamgusa mara, na, kwa kutumia ile brashi Yangu ya kupakia rangi, ninaanza kujiburudisha Mimi Mwenyewe kwa kumbandika kivuli cha ziada cha uzuri Wangu, cha Pendo Langu, cha utakatifu Wangu, na cha maweza Yangu yote. Basi, Kwangu Mimi, kuwepo Kwangu ndani yake huyu na kuwepo Kwangu kule Mbinguni ni kitu kile kile kabisa - pale ninauona uabudu ule ule wa zile Nafsi Tatu za Mungu, ninaukuta pale Utashi Wangu na ninalikuta na Pendo Langu. Na kwa vile kipo pale daima kitu kinachoweza kikatolewa kwa mwanadamu, Mimi hapo huwa ninatenda kama fundi stadi anayepaka rangi kwa kubandika sura Yangu ndani ya mtu huyu. Halafu ninatenda kama mwalimu kwa kumfundisha zile doktrina za juu kabisa na tukufu kabisa. Halafu ninatenda kama mtu wa mapenzi na upenzi mkali kwa kumpatia penzi Langu na kwa kulitaka penzi lake. Kwa kijumla, hapo huwa ninatumia na kutekeleza ustadi Wangu wote katika mbinu za kuburudishana na mtu huyo. Na Pendo Langu, baada ya kuchukizwa na wanadamu, linapokuwa limekosa hata kupata mahali pa kukimbilia, yaani pa kutorokea kutokana na wale wanaonikimbiza Mimi ili kunisababishia kifo au wale wanaotaka niruke kwenda juu kwenye anga la Mbingu - Mimi huwa ninapata kimbilio Langu ndani ya mtu yule anayekuwa na Utashi Wangu pale ndani yake mwenyewe, na pale huwa nayakuta maweza Yangu yanayonitetea, nalikuta Pendo Langu linalonipenda Mimi, naikuta amani Yangu inayonipatia pumziko. Yaani, ninakuta pale mambo yote ninayoyataka. Kwa hiyo basi, Utashi Wangu ndio unaounganisha kila kitu pamoja - unaunganisha Mbingu na dunia, na unaunganisha mema yote - na hatimaye unayafanya yawe ni kitu kimoja. Na kutokana na kitu hicho kimoja peke yake, ndiyo huibuka yale mema yote yanayowezekana na yanayofikirika. Kwa hiyo, naweza nikasema kwamba, mtu yule anayetekeleza Utashi Wangu, ndiye aliye ni chote na chochote Kwangu Mimi, na Mimi Mwenyewe, kwa mtu huyo, ninakuwa ndiye chote na chochote”…..