Utashi wa Mungu na Upendo wa Mungu - Luisa Piccarreta
42 subscribers
311 photos
56 files
688 links
Fahamu kuhusu kutimia kwa Sala ya Baba Yetu kupitia Maandishi ya Mtumishi wa Mungu Luisa Piccarreta, Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - Kuishi Utashi wa Mungu
Download Telegram
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. (Mt 6; 33)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 13 - Oktoba 18, 1921๐Ÿ–‹๐Ÿ“„๐Ÿ“–๐Ÿ“”

Kwa kutwa nzima nilishinda nikiwa na mawazo mbali sana kutokana na mambo niliyokuwa nimeyasikia - mambo ambayo si lazima niyasimulie hapa - na pia nilikuwa nimevurugika kidogo. Licha ya jitihada zangu zote sikufanikiwa kujikomboa kutoka hali hiyo. Kwa hiyo, kwa kutwa nzima sikuwa nimemwona Yesu Wangu Mtamu, Yeye aliye Uhai wa roho Yangu. Zile vurugu zangu zilikuwa ni kama pazia lililosimama kati yangu na Yeye ili kunizuia mimi niweze kuwa ninamwona. Kishapo, katikati ya usiku wa manane, akili yangu iliyokuwa imechoka, ikafikia kutulia. Ndipo Yesu Wangu Mpendevu, kana kwamba ni mtu aliyekuwa akiningoja, alijitokeza, na katika uchungu na masikitiko, aliniambia:

โ€œBinti Yangu, leo, kwa vurugu zako, umekuwa ukizuia Jua la Nafsi Yangu lisichomoze ndani yako. Vurugu huwa ni wingu linalokuja kati Yangu na wewe, linalozuia mionzi toka Kwangu isiweze kushuka na kuingia ndani yako.

Na kama mionzi haiteremki utawezaje wewe kuliona Jua?

Kama ungejua ni nini kulizuia Jua Langu lisichomoze, kama ungejua athari kubwa kwako na kwa dunia nzima, hakika wewe ungekuwa makini kabisa usijiingize katika vurugu.

Kwa kweli, kwa watu waliovurugika, hali yao huwa ni ya usiku.

Na usiku jua huwa halichomozi. Kwa upande mwingine lakini, kwa watu wale wenye amani rohoni, kwao hali huwa daima ni mwanga wa kutwa.

Na Mimi, yaani Jua Langu, katika saa yoyote ile ninapopenda kujichomoza, namkuta mtu huyo yu tayari daima kupokea lile jema la ujio Wangu.

Aidha, hali ya vurugu, siyo kitu kingine, isipokuwa huwa, ni kukosekana kwa hali ya kuachika ndani Yangu.

Na Mimi ninakutaka wewe uwe umeachika kabisa ndani ya mikono Yangu hata usiwe tena na wazo hata moja juu yako wewe mwenyewe. Ni Mimi ndiye nitakayeshughulikia kila kitu. Usiogope.

Yesu Wako hawezi kamwe akakaa bila kukutunza wewe, na bila kukulinda wewe dhidi ya mambo yote.

Wewe ni wa gharama sana Kwangu - nimewekeza mno ndani yako.

Ni Mimi peke Yangu ndiye mwenye haki juu yako. Kwa hiyo basi, kama haki zote ni za Kwangu, hifadhi yote ni ya Kwangu. Kwa hiyo, kaa katika amani na usiogopeโ€.
๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™
Naingia Ndani ya Bahari Kuu ya Utashi Wako
๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™

Ewe Yesu Wangu Mtamu,
mimi ninaingia ndani ya bahari kuu ya Utashi Wako, Ninapigilia utashi wangu ndani ya Utashi Wako na ninakuomba unipe Utashi Wako kama Uhai wangu, kama Uhai wa kila tendo langu, liwe lile la ndani au lile la nje, liwe lile la kiutashi au lile lisilo la kiutashi.

Ee Bwana,
naomba kwamba kila kitu kiwe ndani ya Utashi Wako wa Kimungu, ili niweze kukulipa kwa pendo, kwa uabudu, na kwa utukufu kana kwamba wanadamu wote wangekulipa hilo deni kwa utimilifu wote.

๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™

(Kitabu cha Mbingu - Juzuu Na. 14 - Mei 27, 1922)
Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo (Mk 4, 35)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 20 โ€“ Novemba 3, 1926๐Ÿ–‹๐Ÿ“„๐Ÿ“–๐Ÿ“”

Mimi nikawa ninaendelea kuishi kama mtu aliyejiachia na kujikabidhi kabisa ndani ya Utashi mwambudiwa. Na pindi nikisali, nikawa ninawaza moyoni mwangu: โ€˜Ni jinsi gani ningetamani kuteremka kwenda kule kwenye magereza ya roho za tohorani ili nikawafungulie wote, na, katika mwanga wa Utashi wa Milele, niweze kuwaleta wote kwenye Makao ya Mbinguniโ€™. Katika dakika ile, Yesu Wangu Mtamu, alipoingia ndani mwangu, aliniambia:

โ€œBinti Yangu, kadiri watu waliofariki wanavyozidi kukabidhiwa kwa Utashi Wangu, na kadiri watakavyokuwa wametekeleza matendo mengi zaidi ndani ya Utashi Wangu, ndivyo watakavyokuwa wametengeneza njia nyingi zaidi kwa ajili yao wenyewe, kwa ajili ya kupewa malipo ya roho zao kutokea hapa duniani. Yaani, kwa kadiri watakavyokuwa wametekeleza Utashi Wangu, na kwa hiyo, kwa kadiri watakavyokuwa wamejitengenezea wenyewe zile njia za mawasiliano ya yale mema yaliyopo ndani ya Kanisa na ambayo ni mali Yangu Mimi, hapatakuwa na njia yoyote iliyotengenezwa nao ambayo haitawaletea wengine kitulizo, wengine sala fulani, na kwa wengine punguzo la maumivu.

Hayo malipo yanatembea kupitia njia hizo tukufu za kifalme za Utashi Wangu, ili kumfikishia kila mmoja lile stahili, lile tunda, na ule mtaji ambao kila mmoja wao atakuwa ametengeneza kwa ajili yake mwenyewe ndani ya Utashi Wangu.

Kwa hiyo, bila huo Utashi Wangu, hazipo njia na wala hazipo nyenzo kwa ajili ya kuweza kuyapata malipo. Ingawa kama malipo na kila kitu kingine ambacho Kanisa linatenda, huwa daima yanateremkia tohorani, ni kweli, lakini, huwa yanakwenda kwa wale ambao watakuwa walitengeneza njia kwa ajili yao wenyewe. Kwa wale wengine, ambao hawajatekeleza Utashi Wangu bado, zile njia zimefungwa, au hazipo kabisa.

Na kama hao watakuja kuokoka, itakuwa tu kwa vile, angalau katika dakika ya kufa ya watu husika, watakuwa wamekiri mamlaka makuu ya juu ya Utashi Wangu, watakuwa wameuabudu, na watakuwa wamejikabidhi wenyewe kwa Utashi Wangu - na tendo lao hilo la mwisho ndilo litakuwa limewaokoa. Vinginevyo wasingeweza kabisa kuokolewa. Kwa yule ambaye amekuwa akitekeleza daima Utashi Wangu, kwake huyo hakuna njia zinazompeleka tohorani - njia zake huyo zinakwenda moja kwa moja Mbinguni. Na kwa yule ambaye ameukiri Utashi Wangu, na hata amejikabidhi kwake, na kama hakujikabidhi katika kila kitu na wala siyo kwa daima, bali kwa sehemu kubwa, huyo atakuwa amejitengenezea njia nyingi sana, na atakuwa anaendelea kupokea maombi kwamba tohorani impeleke Mbinguni mara moja.

Basi, kama vile watu waliopo tohorani, kwa ajili ya kupokea yale malipo walipasika kujitengenezea njia, ndivyo na wale walio bado hai. Kwa ajili ya kuweza kupeleka malipo kwa marehemu tohorani, ni budi watekeleze Utashi Wangu, kwa ajili ya kutengenezea njia mbalimbali ili hayo malipo yaweze kupanda juu mpaka tohorani.

Endapo watatekeleza malipo, lakini wakati huo wakiwa mbali kabisa na Utashi Wangu, kwa vile mawasiliano na Utashi Wangu yatakuwa yamekatika, jambo ambalo ndilo pekee huunganisha na kumfunga kila mtu, hayo malipo yao yatashindwa kuiona njia ya kupandia kwenda juu, yatashindwa kuiona miguu ya kuweza kutembelea, na yatashindwa kupata nguvu ya kuweza kutoa kitulizo.

Yote yatakuwa ni malipo yasiyo na uhai wowote, kwa vile uhai halisi wa Utashi Wangu utakuwa unakosekana, Utashi ambao pekee ndio wenye ile nguvu ya kuweza kutoa uhai kwa yale mema yote. Kwa kadiri mtu anavyoubeba Utashi Wangu zaidi na zaidi, ndivyo kutakuwa na thamani zaidi na zaidi katika sala zake, katika kazi zake, na katika maumivu yake. Kwa njia hiyo, mtu huyo huweza kufikisha kitulizo zaidi kwa wale watu waliobahatika.
Mimi huwa ninapima na kuthaminisha kila jambo analoweza kufanya mtu kulingana na kiasi cha Utashi Wangu anachokibeba. Endapo Utashi Wangu unatenda kazi ndani ya kila moja ya matendo yake, kipimo ninachochukua huwa ni kikubwa kweli kweli. Na tena zaidi zaidi, huwa sikomi kamwe kupima, na huwa ninatia thamani kubwa kabisa ndani ya jambo hilo, kiasi kwamba uzito wake hauwezi ukakadirika. Kinyume chake, endapo mtu hatajali sana juu ya Utashi Wangu, basi kipimo kitakuwa hafifu na thamani itakuwa na bei ndogo tu. Na kama mmoja hajali kabisa kabisa, basi, mtu huyo hata akitenda mambo mengi awezayo, Mimi nitakuwa sina kitu cha kupima na wala sitakuwa na thamani yoyote ya kutoa. Kwa hiyo, kama mambo hayo hayatakuwa na thamani, yatawezaje kuleta kitulizo chochote kwa wale watu ambao, kule tohorani, hawawezi kutambua chochote, na wala hawawezi wakapokea chochote, isipokuwa kile tu kinacholetwa na FIAT Yangu ya Milele?

Lakini, je wewe wajua ni nani huyo awezaye kuleta vitulizo vyote, anayeweza kuleta mwanga unaotakasa, na anayeweza kuleta lile pendo linalobadilisha mambo? Ni yule anayebeba ndani yake uhai wa Utashi Wangu katika kila kitu na ambaye ndani yake Utashi Wangu unaamrisha kwa ushindi mkubwa. Mtu huyo hahitaji hata kuwa na zile njia, kwa vile, kwa kuubeba Utashi Wangu, yeye anayo haki juu ya njia zote. Anaweza akaenda kwenye kila kona, kwa vile ndani yake, anabeba ile njia tukufu ya kifalme ya Utashi Wangu kwa ajili ya kuweza kwenda hata kule ndani ya gereza lenye lindi, ili kuwafikishia marehemu tohorani vile vitulizo vyote na kuwaletea uhuru wao. Zaidi zaidi kwa vile, pale tulipomwumba binadamu, Sisi, tulikuwa tumempatia Utashi Wetu kama urithi wake mahususi kabisa, na Sisi tunatambua kila jambo alilokuwa ametenda ndani ya mipaka ya ule urithi Wetu tuliokuwa tumemzawadia.

Jambo lingine lolote lile halitambuliki Kwetu Sisi - hilo si jambo la Kwetu, na wala hatuwezi tukaruhusu chochote kile kuingia Mbinguni ambacho hakijatendeka na wanadamu au ndani ya Utashi Wetu, au walau, kwa ajili ya kutekeleza Utashi Wetu. Tangu pale Uumbwa ulipotoka kwenye FIAT ya Milele, Utashi Wetu, katika wivu wake, huwa hauruhusu kitendo kiingie katika Makao ya Baba wa Mbinguni, ambacho hakijapitia katika FIAT yake yenyewe.

Oh! Laiti kama watu wote wangefahamu ni nini maana ya Utashi wa Mungu, na laiti wangefahamu jinsi kazi zote, hata zile tu zinazoonekana kana kwamba ni nzuri wakati kwa kweli, ndani yao, hazina Utashi wa Mungu kabisa, wakati ni kazi zisizo na mwanga wowote, zisizo na thamani yoyote, zisizo na uhai wowote. Na kazi zile zisizo na mwanga, zisizo na thamani, na zisizo na uhai, hizo haziingii kamwe Mbinguni. Oh! Ni jinsi gani watu hao wangekuwa makini katika kutekeleza Utashi Wangu katika kila jambo na kwa daima!โ€.
Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji (Mk 4, 37)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 8 - Machi 15, 1908๐Ÿ–‹๐Ÿ“ƒ๐Ÿ“–๐Ÿ“”

Leo asubuhi, nilikuwa nikionja maumivu makali kupita siku nyingine zote kutokana na kumkosa Yesu aliye ndiye Chema Changu Kikuu mno na cha pekee. Lakini, kwa wakati huo huo, nilikuwa nimetulia na nikiwa ni mwenye raha tu, sikuwa na yale mahangaiko yaliyokuwa yakinifanya niwe ninazungukazunguka Mbinguni na duniani kumtafuta Yeye hadi pale nilipofikia kumkuta, ndipo tu nilikuwa naweza nikasimama na kutulia. Basi nikawa ninajisemea moyoni mwangu: โ€˜Ni mabadiliko makubwa yalioje - mimi mbona ninajionja kufa ganzi mithili ya jiwe kutokana na maumivu yanayosababishwa na kukosekana Kwako. Hata hivyo mimi sitalia machozi. Ninaionja amani ya kina inayonifunika gubigubi. Pumzi kinzani hata moja tu haiingii ndani mwanguโ€™. Katika dakika ile Yesu Mhimidiwa alinijia na kuniambia hivi:

โ€œBinti Yangu, angalia usiwe unapenda kujisumbua wewe mwenyewe. Ni budi ukafahamu kuwa wakati kunapokuwa na dhoruba kali pale baharini, pale panapokuwa na maji ya kina, hapo dhoruba huwa ni ya juujuu tu. Vina mbalimbali vya bahari huwa vinakuwa katika utulivu kamili mno. Pale maji hutulia tuli, na samaki, wanapoihisi dhoruba inakuja, huwa wanakimbilia kwenda kujificha pale ambapo maji ni ya kina zaidi ili pale wakawe salama zaidi. Kwa hiyo, dhoruba yote huwa inakwenda kujipakua yenyewe kule ambako bahari ina maji machache mno, kwa vile, maadam huko kuna maji machache, dhoruba inaweza kuwa na nguvu ya kuitikisa hiyo bahari toka juu mpaka chini kabisa, na huweza hata kuyahamisha maji kutoka mahali pamoja na kuyapeleka kwenye kona mbalimbali nyingine za bahari.

Ndivyo huwa inatokea kwa watu mbalimbali wakati wanapokuwa wamejazwa kitimilifu na Mungu - wanapokuwa wamejazwa pomoni mpaka ukingoni, kiasi cha kuweza kufurikia nje: dhoruba huwa hazina nguvu ya kuwavuruga hata kwa kiwango kidogo kabisa, kwa vile, hakuna nguvu yoyote inayoweza ikamshinda Mungu. Sana sana, watu hao, huweza tu labda wakaionja hiyo dhoruba kwa juujuu sana. Na zaidi, wakati mtu anapoihisi hiyo dhoruba, huwa anaziweka zile fadhila mbalimbali katika mpangilio na taratibu, na yeye mwenyewe anakwenda kujipumzikia pale ndani kwenye vina vya ndani kabisa vya Mungu. Basi, ingawa kama kwa nje huonekana kana kwamba kuna dhoruba, huwa kwa kweli ni uongo kabisa - kwani huwa ni wakati huo ambapo mtu huwa anafurahia amani zaidi, na huwa anapumzika kwa raha na utulivu, pale penye kifua cha Mungu, sawa kabisa kama yule samaki pale ndani ya kifua cha ile bahari.

Mambo huwa ni kinyume kabisa kwa watu wale ambao wapo tupu kabisa bila Mungu ndani yao, au wale ambao wanabeba sehemu ndogo sana ya Mungu: zile dhoruba huwa zinawayumbisha watu hao, popote pale, huko na kule. Na kama watu hao wakiwa na sehemu ndogo tu ya Mungu, wao huwa wanapoteza bure tu hata hicho kidogo walichoambulia. Na wala huwa hapahitajiki dhoruba za nguvu kwa ajili ya kuweza kuwatikisa watu kama hao. Huwa inatosha kaupepo kadogo tu hata kusababisha fadhila mbalimbali zikimbie kuwatoroka watu hao. Aidha, hata yale mambo matakatifu yenyewe, ambayo huwa kwa kawaida ndiyo malisho mazuri na matamu kwa ajili ya wale watu wengine, waliotangulia kutajwa, ambao ndio huwa wanafurahia mpaka kushiba kabisa, kwa hawa wengine, hayo yote hugeuka na kuwa ndiyo dhoruba. Hao huwa wanapigwa na kudondoshwa chini na kila upepo. Hakuna upande hata mmoja ambako kunakuwa na utulivu timilifu, kwa vile, hoja ya akili hudai kwamba, pale ambapo Mungu Mzima hayupo kabisa, urithi wa amani huwa upo mbali kabisa kabisa toka kwa watu kama haoโ€.
โฌ‡๏ธโฌ‡๏ธโฌ‡๏ธ
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 17 โ€“ Februari 15, 1925๐Ÿ–‹๐Ÿ“ƒ๐Ÿ“–๐Ÿ“”


โ€ฆโ€Ah! Wewe huwezi ukaelewa lile linalotokea ndani ya mtu pale anapoupatia Utashi Wangu uhuru kamili wa kutenda mambo ndani yake, na lile linalotokea pale mtu anapotenda mambo ndani ya Utashi Wangu!

Ebu fikiria bahari, wakati mawimbi yake yanavuma kwa nguvu mno na yanaporushwa juu mno, pale ambapo nguvu ya hayo mawimbi yanahamisha siyo yale maji tu, bali yanazirusha hata zile samaki zenyewe - yanazirusha juu, juu mno kiasi kwamba, ndani ya mawimbi yale, mtu anaweza akaona kwamba, kwa kuzolewa na nguvu za dhoruba ile, pia samaki wameweza hamishwa toka kule kilindini mwa bahari, kutoka kule kwenye makao yao ya siku zote, na jinsi sasa samaki hao walivyoweza kurushwa juu kule sawa na mawimbi yenyewe. Mawimbi yameweza kuwaelemea wale samaki, na wao wameshindwa kuzuia nguvu ya mawimbi yale. Lakini kumbe, pasipokuwepo nguvu ya yale mawimbi, samaki huwa hawawezi kutoka nje ya ile bandari ya makao yao. Lo! kama bahari ingekuwa na nguvu isiyo na kikomo, hakika ingeweza kusababisha maji yote yatikiswe na kurushwa toka kule kilindini na kuiacha sakafu yake. Hapo ingetengeneza mawimbi makuu ajabu, na samaki wote wangekuwa wameelemewa mno pale ndani ya mawimbi hayo.

Lakini, kile ambacho bahari haiwezi ikakitenda, kwa vile ina mipaka katika maweza yake, Utashi Wangu unaweza bado kukitenda. Kwa vile, unapotenda mambo pale ndani ya mtu, Utashi Wangu huwa unayageuza matendo ya mtu kuwa ni ya kwake, basi, pale ndani ya mtu, huwa unatengeneza mawimbi yake ya milele. Na ndani ya mawimbi hayo, Utashi Wangu huwa unakielemea kila kitu. Ndani ya mawimbi hayo mtu anaweza akaona kile ambacho Ubinadamu Wangu ulikuwa umekitenda, anaweza akaziona zile kazi za Mama Yangu wa Mbinguni, zile kazi za Watakatifu wote, na ataona kila kitu ambacho Umungu Wenyewe ulikuwa umekitenda. Pale kila kitu huwa kimewekwa katika ujimudu wake.

Utashi Wangu ni zaidi kupita bahari. Zile kazi Zetu na zile kazi za Watakatifu zaweza kufananishwa na wale samaki wanaoishi pale ndani ya bahari. Wakati Utashi Wangu unapotenda mambo yake pale ndani ya mtu, na hata unapotenda nje ya mtu, kila kitu kilichopo pale ndani ya huo Utashi huwa kinajimudu na kinakwea juu. Kazi zote huwa zinajipanga ili ziweze kuanza kurudia kutoa Kwetu utukufu, kurudia kutoa Kwetu Pendo, na kurudia kutoa Kwetu uabudu. Kazi hizo zote hupita mbele Yetu, mithili ya maandamano ya gwaride, zinapita zikisema Kwetu: โ€˜Sisi hapa ni kazi Zenu. Ninyi ni Wakuu na ni wenye maweza, kwa vile mlitufanya tukawa wazuri na wakupendeza mnoโ€™. Utashi Wangu, ndanimo, huwa unabeba kila kitu kilicho kizuri, cha kupendeza na chema. Na unapotenda mambo yake, huwa hauachilii chochote nyuma, ili kusudi, pasiwepo na chochote kilicho ni cha Kwetu, kinachoweza kikakosekana katika hilo tendo husika, jinsi kwamba, utukufu wetu uweze kuwa timilifu. Na kwa hilo, pasiwepo na jambo la kushangaza, kwani, ni suala la utendaji wa milele ambao unaendelea pale ndani ya mtu.

Kwa hiyo, utendaji wa Utashi Wangu waweza ukaitwa ni wimbi la milele, ni wimbi ambalo linaielemea Mbingu na linaielemea dunia kana kwamba ni kona moja pekee, na kishapo hilo wimbi linaenea juu ya mambo yote kama mbebaji wa lile tendo la kimungu.

Lo! ni jinsi gani Mbingu hufurahia inapouona Utashi wa Milele ukitenda kazi pale ndani ya mtu! Kwa kweli, kwa vile kazi Zao zinathibitishwa pale ndani ya Utashi wa Mungu kule Mbinguni, wao wanaziona kazi zao zikitiririka pale ndani ya lile tendo la kimungu, na wanaonja ule utukufu wao, ile raha yao, na zile furaha zao, zikiwa zinarudufiwa.
Kwa hiyo, kwa vile wewe ndiye Binti Mdogo wa Utashi Wangu Mkuu wa Juu, basi Mimi ninakushauri kuwa: Tafadhali acha kila kitendo chako kiwe ni mateka ya yale mawimbi ya Utashi Wangu, ili kusudi, wakati hayo mawimbi yatakaporuka na kuifikia miguu ya Kiti Chetu cha utawala kule Mbinguni, Sisi tuweze, zaidi na zaidi, kukuthibitisha wewe kama ndiye Binti Yetu halisi wa Utashi Wetu, na papo hapo, tuweze kukupatia wewe zile hati za neema kwa ajili ya ndugu zako na watoto Wetuโ€.
Wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia? (Mk 4, 38)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 4 - Januari 6, 1902๐Ÿ–‹๐Ÿ“ƒ๐Ÿ“–๐Ÿ“”

Na Yesu akaondoka na kufifia. Lakini, punde tu baadaye akawa amerejea, na, pamoja Naye nikawa ninawaona watu mbalimbali ambao walikuwa wakiogopa sana sana kifo. Ndipo nilipoona hilo nikasema: โ€˜Ewe Yesu WanguMpendevu, je, itakuwa ni kasoro kwangu mimi, hiyo hali ya kutoogopa kabisa kifo wakati ninashuhudia wengine wakikiogopa sana sana kwa namna hiyo? Mbona mimi, kwa kudhani kwamba kifo kitaniunganisha na Wewe kwa daima, na kwamba kitakomesha kile kifodini kitokanacho na ule utengano mkali kabisa, hilo wazo peke yake la kifo, siyo tu haliniletei hofu yoyote ile, lakini, kwangu mimi linanipatia kitulizo, linaniletea amani, na ninalisherehekea, huku nikiachilia na nikitupilia mbali yale matokeo mengine yote ambayo huwa yanaleta kifoโ€™. Hapo Naye Yesu alijibu akisema:

โ€œBinti, mbona kwa kweli, hiyo hofu kubwa mno ya kufa ni jambo la upuuzi kabisa wakati kila mmoja anayo mastahili Yangu yote, anazo fadhila Zangu zote na zile kazi Zangu zote kama pasipoti kwa ajili ya kuingilia Mbinguni, ikiwa ni baada ya Mimi kuwa nilizitoa kama zawadi kwa wanadamu wote. Na wanaofaidi zaidi zaidi hiyo zawadi ni wale ambao wameongezea chochote kile cha kwao.

Sasa, ukishakuwa na mambo hayo yote, mtu atakuwa na hofu gani tena? Na kwa pasipoti hiyo ya uhakika kabisa, mtu anaweza akaingia kokote anakotaka, na watu wote, wanapoiona hiyo pasipoti, watakuwa wanamheshimu mtu huyo, na watakuwa wanampitisha. Halafu, kwako wewe, suala hilo la kutokuogopa kamwe kifo, linatokana na ukweli kwamba umekuwa ukitenda mambo pamoja Nami, na pia kwa kuwa umekuwa ukionja jinsi gani, ule muungano na Chema Kikuu cha juu, ulivyo ni mtamu na mpendevu. Hata hivyo, ni vema ukajua kwamba, heshima kuu, inayopendeza kupita zote, anayoweza mtu kuitoa Kwangu Mimi, huwa ni kule kutamani kufa kwa ajili ya kujiunganisha na Mimi, na tena, hiyo ndiyo maandalizi yaliyo mazuri na yapendezayo kuliko kila kitu kwa ajili ya mtu kuweza kujisafisha na kujitakasa, na hiyo humwezesha mtu, kupita bila kukatishwa katishwa, moja kwa moja, katika ile njia ya Mbinguniโ€.

Baada ya kuyasema hayo, Yeye aliondoka na kufifia.
SHEREHE YA KUZALIWA KWA MT. YOHANE MBATIZAJI
โฌ‡๏ธโฌ‡๏ธโฌ‡๏ธ
ยซMtoto huyu atakuwa wa namna gani?ยป (Lk 1; 66)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 23 - Desemba 22, 1927๐Ÿ–‹๐Ÿ“„๐Ÿ“–๐Ÿ“”

....โ€Ninapoteua kiumbe fulani kwa ajili ya utume, ambao lazima ulete manufaa kwa familia ya binadamu ya ulimwengu mzima, huwa kwanza kabisa naweka na kuingiza mema yote ndani ya mtu huyo, ambaye lazima ajazwe ndani yake hayo mema yote, katika kiwango cha kufurika kabisa, kwani watu wengine watapasika kuja kuchukua mema hayo, ingawa kama pengine hawatafaulu kuchukua mema yote yaliyopo ndani ya mteule huyo. Hicho ndicho kilichotokea katika Malkia Immakulata, ambaye aliteuliwa kuwa Mama wa Neno wa Milele, na hivyo akawa ni Mama wa watu wote waliokombolewa.

Chochote ambacho walipasika kutenda, na chema chochote walichopasika kukipata, vilikuwa vyote vimefungiliwa na kupigiliwa, kama vile ndani ya tufe la jua, ndani ya Malkia Mtawala wa Mbingu.

Kwa jinsi hiyo wakombolewa wote wanatembea kuzunguka jua la Mama wa Mbingu, na kwa hiyo na yeye, zaidi ya kuwa Mama mpendevu kabisa, hatendi kitu kingine isipokuwa kumwaga mionzi yake juu ya wana wake.

Anawamwagia mionzi ili kuwalisha kwa mwanga wake, kuwalisha kwa utakatifu wake na kwa pendo lake la kimama. Lakini ni mionzi mingi mingapi anayoisambaza, ambayo haichukuliwi na wanadamu kwa vile katika ufidhuli wao, hawajitahidi kusogea na kusonga mbele kwenda kumzunguka huyu Mama wa Mbinguni?

Kwa hiyo basi, yule anayekuwa ameteuliwa ni budi ajipatie mambo zaidi kuliko yale wanayotakiwa kupata wengine wote wakiwa wamejumlishwa pamoja.

Kama vile watu wote hujipatia mwanga kutoka kwa jua, lakini hata hivyo ni kwa namna na kiasi kwamba wanadamu hao wote hawachukui na kumaliza mwanga wote wala hawachukui moto wote wa joto la jua, ndivyo ilivyotokea kwa Mama Yangu: Yeye anayo ndani yake mema mengi hivi na ya jinsi mbalimbali hivi kwamba zaidi ya mithili ya jua, anasambaza mema hayo na matokeo ya mionzi yake ya Uhai na inayohuisha. Ndivyo hivyo itakuwa kwa mtu yule atakayeteuliwa kwa ajili ya Ufalme wa Utashi Wangu.

Ebu ona kwa hiyo jinsi utakavyolipwa kwa sadaka yako ya kuandika: Kwanza kabisa, kwa kudumu, unajipatia na kuwekewa ndani yako lile jema la mwonzi wa ule ufahamu.

Kishapo utaona jema hilo, kwa kupitia kwako, likiteremka na kushuka juu ya wanadamu wote na jema hilo likiisha kubadilishiwa ndani ya wanadamu utaona Utukufu, wa jema watakalokuwa wanalitenda, ukipanda juu katika mwanga ule ule. Ni jinsi gani utakavyofurahi na utakavyonishukuru kule Mbinguni kwa sadaka hizo nilizokufanya ukazitekeleza!

Binti Yangu, kama kazi fulani ni kubwa, ni kwa ajili ya ulimwengu, kama inajumlisha ndani yake mema mengi sana wanayoweza kufaidi watu wengi, hapo huhitajika sadaka kubwa zaidi. Na yule aliyeteuliwa wa kwanza hana budi kuwa tayari na hiari kutoa na kujitolea sadaka mara nyingi sana, hata uhai wake, kwa ajili ya yale mema mengi yaliyomo ndani.

Anapotoa mema yale atoe pia hata uhai wake wenyewe kwa ajili ya faida ya ndugu zake wengine. Je Mimi sikutenda hivyo hivyo katika Ukombozi?

Je wewe hutaki kuniiga Mimi?โ€
Akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli. (Lk 1; 80)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 2 โ€“ Mei 23, 1899๐Ÿ–‹๐Ÿ“ƒ๐Ÿ“–๐Ÿ“”

โ€ฆโ€œBinti Yangu, ni kwa hoja hiyo, jambo la kwanza kabisa ninalolipendekeza sana sana kwa wanadamu huwa ni kujitenga na mambo yote na hata kujitenga na nafsi yao wenyewe. Kama mtu amefanikiwa kujitenga kabisa na mambo yote, huyo hatahitaji tena kuchota nguvu zake kwa ajili ya kubakia mbali na mambo hayo yote ya dunia, ambayo, kwa yenyewe, huwa yanamjia toka kila upande. Hata hivyo, mambo hayo, yanapoona kuwa yanazembewa tu, na zaidi zaidi, yanapoona kuwa yanadharauliwa, yenyewe yatasema kwaheri kwa mtu huyo na ndipo yataondoka na kumwacha mtu huyo hata yasiweze kumsumbua zaidiโ€.
โฌ‡๏ธโฌ‡๏ธโฌ‡๏ธ
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 6 - Julai 28, 1904๐Ÿ–‹๐Ÿ“ƒ๐Ÿ“–๐Ÿ“”

โ€ฆ.โ€œBinti Yangu, wakati mtu amejitenga na mambo yote, huyo huwa anamkuta Mungu ndani ya kila kitu. Huwa anamwona Mungu ndani yake yeye mwenyewe, anamwona pale nje yake mwenyewe, na anamwona Mungu ndani ya wanadamu. Kwa hiyo, twaweza kusema kuwa, kwa mtu ambaye amejitenga kitimilifu, mambo yote hugeuka na kuwa Mungu. Na zaidi zaidi, huwa siyo tu anamkuta Mungu, bali huwa anamtafakari, anamwonja, na anamkumbatia. Na kwa vile anamkuta katika kila kitu, ndivyo vitu vyote huwa vinampatia mtu huyo wasaa mzuri wa kumwabudu Mungu, wasaa wa kusali na kumwomba, wa kumshukuru, na wasaa wa kumkaribia Mungu katika upenzi wa ndani zaidi.

Aidha, yale manungโ€™uniko yako juu ya kukosekana Kwangu hayana sababu za kutosha. Kama wewe unanionja Mimi hapo ndani mwako, basi ni alama tosha kwamba, Mimi, siyo tu nipo nje ya wewe, bali nipo hata hapo ndani, na nipo hapo kama kwenye makao Yanguโ€.....
โฌ‡๏ธโฌ‡๏ธโฌ‡๏ธ
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 14 - Juni 26, 1922๐Ÿ–‹๐Ÿ“ƒ๐Ÿ“–๐Ÿ“”

Nilikuwa nikiendelea na ile hali yangu ya siku zote. Ndipo Yesu Wangu Mpendevu wa daima alikuja. Na kwa vile kwa siku kadhaa nilikuwa nimeterereka kabisa kiafya, kiasi kwamba nikawa nimejikunyata na nisiweze kujimudu kwa lolote, Yesu alitwaa mikono yangu na kuishika ndani ya mikono Yake, huku akiniambia: โ€œBinti Yangu, ebu niache nikunyoshe Mimiโ€. Halafu, alinisogelea na akachukua mikono yangu na kuiweka juu ya mabega Yake akiniambia:

โ€œSasa umenyoka. Ebu nikumbatie na kunibania kwako kwani nimekuja ili nikeshe pamoja nawe na wewe unilipe kwa kukesha pamoja Nami. Ebu ona, Mimi ni Mungu niliyetengwa na wanadamu, Mimi ninaishi kati yao, Mimi ni uhai wa kila tendo lao, na Mimi ninajifanya kana kwamba sipo kabisa pamoja nao. Oh, ni jinsi gani ninavyorudia kulia mintarafu upweke Wangu! Kwangu kunatokea kitu kile kile kinachotokea kwa jua. Yaani, wakati hilo jua, pamoja na mwanga wake na joto lake, linaishi kati ya watu wote, na wakati hakuna nguvu ya rutuba yoyote ambayo haitoki kwake, na wakati, kwa joto lake, linaisafisha ardhi isipate mipasuko mingi, na wakati linayashusha kwa ukarimu kabisa, juu ya watu wote, manufaa yake yasiyohesabika, hata hivyo, lenyewe bado linaishi daima, kule juu likiwa peke yake kabisa. Na binadamu aliye mtovu wa shukrani hajawahi kusema kwake neno la asante kama uthibitisho wa kunitambua na kunikiri. Ndivyo nilivyo Mimi: Mpweke, daima peke Yangu! Wakati ninapokuwa kati yao Mimi ni mwanga wa kila wazo, Mimi ni sauti ya kila neno, Mimi ni ujimudu wa kila kazi, Mimi ni hatua ya kila mguu, Mimi ni pigo la kila moyo! Na huyu binadamu, mtovu wa shukrani, ananiacha peke Yangu kabisa, haniambii asante yoyote ile, wala hanitamkii kauli ya Ninakupenda.

Huwa ninabaki nimetengwa katika akili, kwa vile ule mwanga ninaoutoa kwa akili yao wanautumia kwa mambo yao na pengine kwa ajili ya kuniudhi Mimi. Nimetengwa katika maneno, kwa vile, mara nyingi, sauti wanayotoa, hutumika kwa ajili ya kunikufuru Mimi. Ninabaki nimetengwa katika kazi mbalimbali kwa vile wanazitumia kwa ajili ya kuniua Mimi. Ninatengwa katika hatua za miguu, na katika moyo kwa vile huwa wananuia kunikaidi tu Mimi na wananuia kupendelea kile ambacho hakinihusu Mimi. Oh, ni jinsi gani upweke huo unavyonitesa Mimi! Hata hivyo, Pendo Langu, Wema na Ukarimu Wangu ni mkubwa hivi, kiasi kwamba, zaidi kupita hata jua, Mimi ninaendelea na njia Yangu ya maamuzi, na katika njia hiyo, ninaendelea kuchunguza iwapo kuna mtu fulani ambaye angependa kuja kukesha Nami katika upweke Wangu huo mkubwa. Ninapomkuta, basi najenga uhusiano wa kukesha naye kwa daima na ninammwagia mtu huyo neema Zangu zote.

Ndiyo maana Mimi nimekujia wewe - nilikuwa nimechoka na hali hiyo ya upweke. Tafadhali, Binti Yangu, usiniache peke Yanguโ€.
๐Ÿ’ฆโ˜€๏ธโ˜€๏ธโ˜€๏ธ๐Ÿ’ฆ
Ewe Uhai wangu na Ewe uliye Chote Changu, unijalie hatua zako ziongoze hatua zangu na kila nikanyagapo ardhi, mawazo yangu yawe mbinguni.
๐Ÿ’ฆโ˜€๏ธโ˜€๏ธโ˜€๏ธ๐Ÿ’ฆ
๐Ÿค๐Ÿค๐Ÿค
Naingia Ndani ya Bahari Kuu ya Utashi Wako
๐Ÿค๐Ÿค๐Ÿค
Ewe Yesu Wangu Mtamu,
mimi ninaingia ndani ya bahari kuu ya Utashi Wako, Ninapigilia utashi wangu ndani ya Utashi Wako na ninakuomba unipe Utashi Wako kama Uhai wangu, kama Uhai wa kila tendo langu, liwe lile la ndani au lile la nje, liwe lile la kiutashi au lile lisilo la kiutashi.
๐Ÿค๐Ÿค๐Ÿค
Ee Bwana,
naomba kwamba kila kitu kiwe ndani ya Utashi Wako wa Kimungu, ili niweze kukulipa kwa pendo, kwa uabudu, na kwa utukufu kana kwamba wanadamu wote wangekulipa hilo deni kwa utimilifu wote.
๐Ÿค๐Ÿค๐Ÿค

(โœ๏ธKitabu cha Mbingu - Juzuu Na. 14 - Mei 27, 1922)
Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua. (Mt 7; 6)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na.20 - Oktoba 2, 1926๐Ÿ–‹๐Ÿ“„๐Ÿ“–๐Ÿ“”

Nilijikuta katika kipindi cha masikitiko na uchungu mno kutokana na kukosekana kwa Yesu Wangu Mtamu. Oh! Kwa jinsi nilivyokuwa nikijisikia vibaya, sikuweza kufanya lolote tena. Hata hivyo, nilipokuwa nimefikia kilele cha mateso, Yeye aliingia pale ndani yangu huku akiwa katika mateso makali kabisa. Ndipo aliniambia:

โ€œBinti Yangu, nipo nikiangalia ni kwa kiasi gani yanipasa kupanua mipaka ya Ufalme wa Utashi Wangu, hata niweze kuukabidhi Ufalme huo kwa wanadamu. Ninafahamu fika kwamba wao hawataweza kutwaa ule upeo usio na ukomo uliopo katika Ufalme wa Utashi Wangu, kwa vile, kwake mwanadamu, haujatolewa bado ule uwezo wa kuuvuka na kuukumbatia Utashi unaouwiana na Ufalme usiokuwa na mipaka. Ni kwa vile, mwanadamu, kwa kuwa kaumbwa, yeye daima huwa ni finyu na mwenye mipaka. Na kwa hoja kwamba ana mipaka kulingana na hali zake za maandalizi na uhiari, Mimi huwa ninampelekea mema zaidi au pungufu, na ninampelekea na kumpatia upana zaidi au pungufu wa mipaka anayotakiwa awe nayo. Ndiyo maana Mimi sasa nipo nachunguza vizazi vijavyo vitakuja kuwa na hali gani ya maandalizi na uhiari, ninachunguza pia vizazi vilivyopo vya sasa kuona hali waliyo nayo sasa hivi, kwani hawa wa sasa budi wawe wanasali, wawe wanasihi, na wawe wanauandaa Ufalme wa ile FIAT Kuu ya Juu kwa ajili ya vizazi vijavyo. Na kulingana na hali ya maandalizi na utayari wa vizazi vijavyo, na kulingana na hamu waliyo nayo vizazi vya sasa, ndivyo na Mimi naendelea kuongeza na kupanua mipaka ya huo Ufalme Wangu. Ni kwa vile vizazi hivi vimeunganika sana kati yao, kiasi kwamba, huwa inatokea jinsi hiyo kila mara, kuwa kizazi kimoja kinasali, kizazi kingine kinaandaa, na kizazi kingine tena kinasihi na kuomboleza na kizazi kingine ndicho kinachoubeba Ufalme.

Ndivyo hivyo hivyo ilitokea katika ule ujio Wangu hapa duniani, nilipofika kushughulikia Ukombozi. Havikuwa ni vizazi vya hivi sasa ambao walikuwa wakisali, waliotweta na waliolia ili kuyapata mema yake - kwani hawa ndio wanaoyafaidi na wanayoyatwaa na kuyabeba - bali walikuwa ni wale waliokuwa wameishi kabla ya ujio Wangu. Na kadiri ya hali ya maandalizi na hiari ya watu wale wa kizazi hiki cha sasa, na kutokana na sala na hali za maandalizi na hiari ya wale wa kizazi kilichopita, ndivyo na Mimi nilivyozidi kupanua mipaka ya yale mema ya Ukombozi. Na kwa kweli, Mimi huwa ninatoa jema fulani pale tu ambapo jema hilo litakuwa na manufaa kwa wanadamu. Lakini, iwapo jema hilo halitaleta manufaa yoyote, kuna haja gani ya kulitoa? Na manufaa hayo huchukuliwa na hao wanadamu iwapo wamekuwa na maandalizi zaidi na uhiari zaidi. Lakini, je, wajua wewe ni lini ninapopanua mipaka yake? Ni pale ninapokueleza na kukuonyesha wewe maarifa fulani mapya yanayohusu huu Ufalme wa Utashi Wangu. Ndiyo maana, kabla sijakueleza na kukuonyesha wewe, huwa kwanza ninatupia jicho Langu kwa watu wote ili kuchunguza kuona hali zao za maandalizi - yaani, kuona kama itakuwa na manufaa kwao, au pengine, itakuwa kwao sawa na kama vile hakikusemwa chochote kabisa. Na wakati ninapokumbuka kuwa Mimi ninanuia kupanua zaidi na zaidi mipaka Yangu kwa ajili ya kuwapatia mema mengi zaidi ya kubeba, kuwapatia furaha zaidi, na kuwapa raha zaidi, na papo hapo ninapogundua kuwa wao hawapo tayari kwa hilo, Mimi huwa naonja kuteseka sana sana, na ndipo huwa ninasubiria sala zako, ninasubiria ziara zako ndani ya Utashi Wangu, nasubiria maumivu yako, ili kusudi niweze kuwaandaa wale wa kizazi cha sasa na wale wa kizazi kilichopita. Na kishapo huwa ninarejea kule kwenye mambo yale ya kushitua ya maelezo Yangu mintarafu Utashi Wangu.
Ndiyo maana huwa ninashikwa na uchungu sana na maumivu pale ninapokuwa sizungumzi nawe. Neno Langu ndiyo zawadi kubwa kupita zote - huwa ni uumbaji mpya. Kutokana na Mimi Mwenyewe kushindwa kulitoa toka ndani Mwangu, kwa vile wanadamu wanakuwa hawapo tayari kulipokea neno hilo, huwa ninaonja ndani Yangu ule uzito wote wa ile zawadi ninayonuia kuitoa, na, kwa kushindwa kuitoa, huwa naendelea kuteseka na ninabaki kunyamaza. Na mateso Yangu huwa yanaongezeka hata zaidi na zaidi pale ninapokuona na wewe unateseka kwa ajili Yangu Mimi. Laiti ungefahamu jinsi ninavyoonja masikitiko yako - na jinsi uchungu wako huo unavyomwagikia ndani ya Moyo Wangu! Utashi Wangu huwa unauingiza uchungu huo hadi kilindini mwa Moyo Wangu. Ni kwa vile Mimi sina tashi mbili, bali ninao utashi mmoja tu. Na kwa vile huo Utashi Wangu ndio unaotawala ndani yako wewe, matokeo yake ni kwamba, huo Utashi Wangu huwa unaleta yale mateso yako hadi kwenye kina cha ndani Mwangu. Kwa hiyo basi, wewe uwe unasali, na hebu ule mruko wako uwe endelevu daima ndani ya ile FIAT Kuu ya Juu, ili pale ukawe unaendelea kusihi kwamba wanadamu wawe wanajiandaa wenyewe, na Mimi niweze kurejea kuja kuzungumzia kwa mara nyingineโ€โ€ฆโ€ฆ
Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba. (Mt 7; 13)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 6 - Juni 23, 1905๐Ÿ–‹๐Ÿ“ƒ๐Ÿ“–๐Ÿ“”

Wakati nikiendelea na ile hali yangu ya siku zote, nikawa ninawaza juu ya jinsi Yesu Kristo alivyokufa, na pia juu ya kwamba Yeye hakuweza kuogopa kifo, kwani, maadam alikuwa ameunganika kabisa na ule Umungu, au tuseme, alikuwa amegeuzwa kuwa katika hali ya Umungu, basi, alikuwa tayari ni salama kabisa sawa na mmoja anayekaa katika jumba lake mwenyewe. Lakini, kwa mtu huyo - lo! Ni tofauti gani kubwa iliyopo. Pindi nikiwazia hayo na ujinga wangu mwingine, Yesu Mhimidiwa alikuja na kuniambia:

โ€œBinti Yangu, yule anayekuwa ameunganika na Ubinadamu Wangu, huyo huwa anajikuta yupo tayari mlangoni pa Umungu Wangu, kwa vile, Ubinadamu Wangu ni kioo cha mtu cha kujitazamia, kwani kutoka hicho kioo Umungu huwa unaweza kuonekana pale ndani ya huyo mtu husika. Na kama mmoja yupo tayari katika picha kioo ya kioo hicho, ni wazi kabisa kwamba nafsi yake yote budi iwe imegeuzwa kuwa ni Pendo. Sasa, Binti Yangu, kwa vile kila kitu kitokacho kwa mwanadamu, hata ule ujimudu mbalimbali wa macho yake, ujimudu wa midomo yake, ujimudu wa mawazo yake, na mengineyo yote - kila kitu budi kiwe ni Pendo, na kiwe kimetekelezwa kwa ajili ya upendo. Na kwa vile nafsi Yangu yote ni upendo mtupu, basi popote pale ninapolikuta pendo, Mimi hapo ninanyonya kila kitu ndani Mwangu, na yule mtu anaingia kukaa kwa utulivu kabisa ndani Yangu Mimi kama vile anavyokaa yeyote yule ndani ya jumba lake mwenyewe.

Basi, sasa mtu, katika saa yake ya kufa, anaweza akawa na hofu gani ya kuja Kwangu Mimi wakati yupo tayari ndani Yangu Mimi?โ€
โฌ‡๏ธโฌ‡๏ธโฌ‡๏ธ
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 9 โ€“ Machi 16, 1910๐Ÿ–‹๐Ÿ“„๐Ÿ“–๐Ÿ“”

Nilipokuwa nikizungumza na Padre Mwungamishi, aliniambia kuwa kuokoka ni suala gumu kwa vile Yesu Kristu Mwenyewe aliwahi kusema hivyo: โ€œMlango ni mwembamba. Ni budi mjitahidi kuuingiaโ€. Halafu, baada ya mimi kupokea Komunyo Takatifu, Yesu aliniambia:

โ€œMasikini Mimi, ni jinsi gani wanavyodhani kwamba Mimi ni bahili. Ebu kamwambie huyo Padre Mwungamishi: wao wananihukumu Mimi kwa kulingana na ubahili wao wenyewe. Hawanihesabu kama ndiye niliye Mkuu, niliye mkubwa mithili ya bahari, niliye bila ukomo, niliye mwenye maweza, niliye bila mipaka katika sifa Zangu zote za ukamilifu, kwamba, ndiye ninayeweza kuyafanya makundi makubwa ya watu yakapita pale penye uwembamba, na wakaweza kupita zaidi kuliko pale penye upana wenyeweโ€.

Na alipokuwa akiyasema hayo, nikawa ninaona kama vile njia nyembamba iliyokuwa ikielekea kwenye mlango mdogo, mwembamba na uliokuwa umejaa kabisa na watu ambao walikuwa wanapigania kati yao nani atangulie zaidi hata akaweze kuingia pale ndani. Yesu akaongeza kusema:

โ€œEwe Binti Yangu, ebu angalia ni kundi kubwa lilioje lile linalojisukuma pale kwenda mbele. Na pale wanashindania kuona nani atakayeweza kuwasili wa kwanza. Katika mashindano huwa kuna kushinda kwingi. Lakini kumbe, kama njia ingekuwa ni pana, pasingekuwa na mtu anayehangaika kuharakisha, kwani, wangejua kwamba kuna nafasi ya kutosha kwa ajili ya kuweza kuendelea kutembea wakati wowote ule wanapotaka. Lakini, pindi wanapopitisha muda wao wakingoja kuanza mwendo wao, kifo chaweza kuwafikia, na wao, wanapojikuta hawatembei katika njia nyembamba, wangeshitukia wanawasili penye lile lango pana la lile geti kuu la motoni mwa milele. Lo, ni faida gani kubwa inayoletwa na huu uwembamba! Jambo hilo huwa linatokea hata hapo kati yenu ninyi wenyewe: Iwapo kunatokea kuwa na sherehe au pakiwa na ibada fulani, na iwapo inafahamika fika kwamba nafasi iliyopo ni ndogo, basi watu wengi sana huwa wanaharakisha kufika, na mwishowe huwa wanahudhuria washiriki wengi sana waliofika kuja kufurahia hiyo sikukuu au ibada. Kumbe lakini, endapo inajulikana kuwa nafasi iliyopo ni kubwa, hakuna mtu anayehangaika kuharakisha na mwishowe huwa ni wahudhuriaji wachache tu wanaofika, kwa vile tu wanajua kwamba kuna nafasi ya kutosha kabisa kwa ajili ya kila mtu. Kila mmoja huwa anakuja kwa raha na kwa wakati wake. Na baadhi huwa wanafika katikati ya sherehe, na wengine wanafika hata mwishoni, na wengine wanapofika, wanakuta sherehe imekwisha kumalizika, na hivyo hawawezi kufaidi chochote. Hilo ndilo ambalo lingetokea iwapo njia ya wokovu ingekuwa ni pana - ni watu wachache tu wangekuwa wanahangaika kuharakisha, na sherehe ile ya Mbinguni ingebaki kuwa ni ya wachache tuโ€™โ€™.