Utashi wa Mungu na Upendo wa Mungu - Luisa Piccarreta
43 subscribers
327 photos
64 files
760 links
Fahamu kuhusu kutimia kwa Sala ya Baba Yetu kupitia Maandishi ya Mtumishi wa Mungu Luisa Piccarreta, Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - Kuishi Utashi wa Mungu
Download Telegram
Nakuja kwenu, siyo kama Baba tu, bali nakuja pia kama Mwalimu kati ya wanafunzi Wake ........... Nawaomba mnisikilize kwani nitakuwa nikiwafundisheni mambo ya kushangaza, yaani mafundisho ya Mbingu ambayo yatawaleteeni Nuru ambayo haitaweza kuzimika, na mafundisho hayo yatawaletea Pendo liwakalo na lenye kudumu kwa daima.............. Mafundisho Yangu hayo yatawapatieni nguvu ya kimungu, ujasiri usioshindikana, na utakatifu unaoendelea kuongezeka zaidi na zaidi. Mafundisho hayo yatakuwa yakiiangaza njia ya hatua zenu na kuwaongozeni katika njia iendayo kwenye Makao yenu ya Mbinguni.

Mimi nakuja kwenu kama Mfalme, ili niweze kuishi kati yenu. Siji kwa ajili ya kuwatoza makodi na kutwika mizigo juu yenu. La hasha, hapana kabisa! Ninakuja kwa vile ninataka huo utashi wenu, hayo mahangaiko yenu, hayo madhaifu yenu, na hayo maovu yenu yote. Mamlaka Yangu ni hasa katika neno hili: Ninataka kila jambo linalowaleteeni ninyi uchungu na linalowakosesheni raha, nayataka hayo yote yanifikie kusudi niweze kuficha kila moja lao ndani ya Pendo Langu, na pale niweze kuyachomelea yote na kuyaunguzia mbali. Kwa kuwa Mimi ni Mfalme ambaye ni Mtenda mema, ni Mleta amani, na niliye Mwingi wa fadhili, ninapenda nibadilishane nanyi Utashi Wangu, huku nikichukua huo wa kwenu, ili niwajazeni ninyi kwa Pendo Langu tamu kabisa, niwajazeni kwa utajiri Wangu mwingi, kwa furaha Zangu, na niwajazeni amani Yangu na raha iliyo safi kabisa.

Endapo ninyi mtanipatia utashi wenu wa kibinadamu, basi mambo yote yatatendeka kadiri nilivyosema. Ninyi mtanifurahisha Mimi na ninyi wenyewe mtafurahia pia. Mie sitamani kitu kingine chochote kile, isipokuwa kwamba Utashi Wangu upate kutawala kati yenu. Mbingu na dunia zitakuwa zikitabasamu juu yenu na kuwafurahieni. Mama Yangu wa Mbinguni atapata uhakika wa kuwa Mama na Malkia juu yenu ninyi. Yeye anajua lile jema kubwa ambalo Ufalme wa Utashi Wangu utawaleteeni. Zaidi ya hilo, kwa ajili ya kutuliza matamanio Yangu makubwa na makali, na pia kwa ajili ya kusitisha kilio Changu Mimi, na tena kwa vile anawapendeni ninyi mithili ya watoto wake halisi, sasa hivi Mama Yangu wa Mbinguni, yupo akifanya ziara kuwatembelea watu wa mataifa mbalimbali ili kuwaeleza na kuwaandaa kupokea mamlaka ya Ufalme wa Utashi Wangu. Ndiye yeye Mama aliyekuwa amewaandaa watu kwa ajili Yangu Mimi, hata nikaweza kuteremka toka Mbinguni na kuja duniani. Kwa hiyo hata sasa ninamkabidhi yeye na ninakabidhi kwa Pendo lake la kimama hilo jukumu la kuziandaa roho za watu Wetu ili ziweze kuipokea ile Zawadi kubwa ya namna hiyo.

Kwa hiyo basi, ebu nisikilizeni. Ninawaombeni ninyi Watoto Wangu, myasome kwa umakini kabisa makala haya ninayoyaleta mbele yenu. Mkitekeleza hilo, mtaonja mara hamu ya kuishi katika Utashi Wangu, na Mimi nitakuwa nikisimama kando kabisa yenu wakati huo mtakapokuwa mkisoma, nitakuwa nikigusa akili yenu na moyo wenu ili mweze kuelewa kile mnachosoma na ili papo hapo mweze kutamani hiyo Zawadi ya FIAT Yangu ya kimungu.
Wiito wa Malkia wa Mbingu kwa watoto wake ili waingie katika Ufalme wa Utashi wa Mungu ⬇️⬇️⬇️
(Kutoka Kitabu ‘Bikira Maria Katika Ufalme wa Utashi wa Mungu’)
Binti mpenzi, ninaonja hitaji kali sana lisilozuilika la kushuka toka hapa Mbinguni, ili niweze kuja kukutembelea kama Mama yako.

Endapo utanithibitishia upendo wako wa binti na uaminifu wako kwangu, basi mimi nitakuwa nabaki pamoja nawe daima moyoni mwako ili niwe mwalimu kwako, niwe kwako kielelezo, mfano na Mama kipenzi chako.

Mimi ninakuja kukualika uingie katika ufalme wa Mama yako, yaani katika ufalme wa Utashi wa Mungu, na kwa hiyo ninabisha hodi mlangoni pa moyo wako ili unifungulie.

Je unafahamu? Mimi mwenyewe kwa mikono yangu nakuletea Kitabu hiki kama zawadi. Ninakupatia kwa Moyo wa kimama ili ukisome kwa wakati wako, na ukishasoma, ujifunze namna ya kuishi kimbingu, badala ya kuendelea kuishi kidunia.

Kitabu hiki ni kitu cha dhahabu binti yangu. Kitakuletea bahati yako ya kiroho na hata furaha yako ya hapa duniani.

Ndanimo utapata chimbuko la neema yote. Kama wewe u mdhaifu basi utajipatia nguvu; kama u katika majaribu basi utajipatia ushindi; kama umeangukia katika kosa, basi utauona mkono ule wa huruma na wenye uwezo utakaokuinua tena; kama upo katika mateso, utajipatia kitulizo; kama unaona ubaridi basi utapata njia ya uhakika ya kujipasha joto; kama umeshikwa na njaa basi utaonja chakula kitamu kabisa cha Utashi wa Mungu.

Ukiwa na Kitabu hiki basi hutakosa kitu. Hutakuwa tena mpweke, kwani Mama yako atakuwa ni mwenzi mtamu anayetangulizana nawe; na yeye, kwa upendo wake wote wa kimama, atahakikisha anakuletea furaha. Mimi, Mtawala wa Mbinguni, ndiye nitakuwa nashughulikia mahitaji yako yote, ili mradi wewe unakubalia kuishi umeungana na mimi.

Laiti kama ungejua wasiwasi wangu, matarajio yangu, matamanio yangu makali, na hata machozi ninayomwaga kwa ajili ya wana wangu! Laiti ungefahamu jinsi mimi ninavyoungua na tamanio hili, kwamba wewe uweze kusikiliza maelekezo yangu yote ya kutoka Mbinguni, na upate kujifunza namna ya kuishi Utashi wa Mungu!

Katika Kitabu hiki utaona mambo ya kushangaza. Utamkuta Mama anayekupenda kabisa, kiasi kwamba anamtoa hata Mwana wake mpenzi, ambaye katika huyo wewe utaweza kuishi uhai ule ule, ambao Mama huyu mwenyewe aliuishi hapa duniani.

Lo, binti, usiniletee uchungu huu wa kunigomea! Ukubali na kupokea zawadi hii ya Mbinguni ambayo nakuletea. Karibisha ugeni wangu na maelekezo yangu.

Ni vema ujue kwamba mimi nitazunguka dunia yote nikimwendea kila mtu binafsi, katika familia zote, katika jamii za kitawa zote, katika kila taifa, katika makabila yote.

Na kama itawezekana nitazunguka kwa muda wa karne nzima kadhaa, hadi, kama Malkia, nifikie kuwaunda watu wangu, na kama Mama, niwaunde watoto wangu.

Na hao ambao wataufahamu Utashi wa Mungu, ndio watakaofanya Utashi huo wa Mungu utawale popote.

Basi hayo ndiyo maelezo kwako juu ya lengo la Kitabu hiki.

Wale watakaokipokea kwa upendo watakuwa ndio wana wa kwanza wa Ufalme wa FIAT ya Mungu, na mimi nitayaandika majina yao hao katika herufi za dhahabu ndani ya Moyo wangu wa kimama.

Je unaona binti yangu?

Lile lile pendo la Mungu lisilo na mipaka, ambalo katika mpango wa wokovu, liliazimia kunitumia mimi katika kumleta Neno wa Mungu hapa duniani, ndilo sasa linaniita kwa mara nyingine uwanjani, na linanikabidhi jukumu zito, yaani agizo na utume wa kuunda hapa duniani watoto wa Utashi wake wa kimungu.

Kwa hiyo, katika jukumu langu la kimama, ninaanza kutekeleza kazi yangu, na sasa nakuandalia wewe njia ya kuzingatia ili uufikie Ufalme huo wa furaha.
Kwa ajili ya lengo hilo nitakupatia mafunzo ya juu na ya kimbingu, na hatimaye nitakufundisha sala mpya na za aina ya pekee.

Kwa sala hizo utaweza kuhusisha mbingu, jua, viumbe, uhai wangu mimi mwenyewe, na ule uhai wa Mwanangu na matendo yote ya Watakatifu, ili kwa jina lako wewe, wao hao wauombe Ufalme mwabudika wa Utashi wa Mungu.

Sala hizo ndizo zilizo na nguvu ya juu zaidi, kwani zinapatana na utendaji wa kimungu. Kwa nguvu ya sala hizo, Mungu atajiona amevuliwa silaha zake na kushindwa katika mapigano yake dhidi ya kiumbe.

Ukiwa umeimarishwa na msaada huo, wewe utaharakisha ujio wa Ufalme wake wa furaha kuu, na ukiwa pamoja nami, utafanikiwa kuufanya Utashi wa Mungu utekelezwe hapa duniani, kama kule Mbinguni, kulingana na matakwa ya Mwalimu – Mungu.

Haya, jipe nguvu binti yangu. Hebu unifurahishe mimi, na mimi nitakubariki
Wiito Anaotoa Luisa Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu⬇️⬇️⬇️
Mtumishi wa Mungu - Luisa Piccarreta
- Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu

‘Ee Yesu, miguuni pako nakuletea uabudu na utiifu wa familia yote ya wanadamu.

Ninaweka ndani ya Moyo Wako ile kauli ya ‘Nakupenda’ kutoka kwa watu wote. Juu ya Midomo Yako nakupigia busu langu ili kukubandikia mhuri wa busu la watu wa vizazi vyote.

Kwa mikono yangu nakukumbatia ili kukubana kwa kumbatio la mikono ya watu wote, kwa ajili ya kukufikishia utukufu wa matendo yote ya viumbe.’

(Kutoka: KITABU CHA MBINGU, Juzuu Na. 12, Tarehe 22 Mei 1919)
Mtumishi wa Mungu Luisa Piccarreta alizaliwa katika Mji mdogo wa Corato, Mkoa wa Bari, Italia tarehe 23 Aprili 1865.

Alibatizwa katika Kanisa la Parokia yake. Ndipo hapo alipopata na Komunyo ya Kwanza na Sakramenti ya Kipaimara (1874).

Katika umri wa miaka 11 alijiunga na Kikundi cha ‘Mabinti wa Maria’ na baadaye akawa Mtersiari wa Wadominikani.

Alipopata umri wa miaka 16, kwa mapenzi yake Yesu, Luisa Piccarreta alianza kuingia hali ya kuwa ‘mhanga’.

Ingawa kama kielimu alikuwa ni Darasa la Kwanza tu la Shule ya Msingi, ilipofika tarehe 28 Februari 1899 , kwa kutii agizo la Padre Mwungamishi wake, yeye alianza kuandika Shajara yake ya Kumbukumbu zake za kimistiki (Shajara ambayo Yesu Mwenyewe baadaye aliipa kichwa cha: KITABU CHA MBINGU - LIBRO DI CIELO): Hiki Kitabu hujumuisha Shajara kubwa kubwa 36 ambazo ndanimo husimulia kumbukumbu za siku kwa siku za jinsi Mwalimu wa Mbinguni alivyokuwa akimfunulia ufahamu juu ya Utashi wa Mungu, na namna ya kuuishi ndani ya huo Utashi wa Mungu.

Akiwa daima katika kutii agizo alilopewa, aliandika ‘SAA 24 Za Mateso Ya Bwana Wetu Yesu Kristo’. Na tarehe 6 Mei 1930 aliandika ‘Bikira Maria Katika Ufalme Wa Utashi Wa Mungu”.

Mwaka 1926, akiagizwa na Mwungamishi wake wa pekee, Padre Annibale Maria di Francia, ambaye pia ndiye amekuwa msimamizi na mkaguzi wa maandiko, Luisa aliandika ‘Kumbukumbu za Utoto” (‘Memorie d’ Infanzia’). Ameacha pia idadi kubwa ya barua zake ambazo zinaweza kuwa hazina ya fikara na maoni juu ya mafundisho ya imani juu ya Utashi wa Mungu.

Luisa, ‘Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu’, aliyekuwa amechaguliwa na Mungu kwa ajili ya Utume wa ‘MAPENZI YAKO YATIMIZWE duniani kama Mbinguni’ (“FIAT VOLUNTAS TUA sicut in coelo et in terra), aliaga dunia kwa ajili ya kwenda Mbinguni tarehe 4 Machi 1947.

Yesu alikuwa amemwambia: “Utashi Wangu unayo nguvu ya pekee ya kuzifanya roho ziwe ndogo, naam, kuzifanya ndogo zaidi na zaidi, ili ziweze kuonja hitaji kali kabisa kwa Utashi Wangu kutia uhai ndani yao…… Utashi Wangu wa milele utachukua zama za kale, za leo na zijazo; utazifupisha hadi kuwa nukta tu ambayo itamwagiwa ndani yako...”.

Na Luisa alipofadhaika mbele ya maneno hayo, Yesu alimthibitishia kwa kusema:

“Wewe mwenyewe ilitakiwa uwe umeelewa kwamba ilinipasa kukupatia utume wa pekee wa Utashi Wangu, kutokana na mazungumzo yangu ya daima kwako juu ya Utashi Wangu na pia kutokana na jinsi nilivyokufanya uelewe matokeo Yake ya ajabu…..
Baada ya kukufundisha vema vema, nimekuonyesha utume wako, na pia jinsi ndani yako wewe utatokea mwanzo wa kutimilika kwa neno lile ‘Mapenzi Yako Yatimie’ duniani…..(Fiat Voluntas Tua sicut in coelo….). Wala Usiogope! Utashi Wangu utakuwa ni msaada wako na tegemeo lako
”.

Pro Manuscripto
Prayer Group
‘ Divino Volere e Divino Amore ’
[Divine Will and Divine Love]
EMAIL: albert.norbert@gmail.com
WEBSITE: www.divinewilldivinelove.com
TELEGRAM: t.me/utashiwamungunaupendowamungu
RUMBLE Channel: https://rumble.com/c/c-5818809

Kwa matumizi binafsi tu
“Mimi ndiye Mwalimu Mtukufu,
Mwalimu wa Utashi wa Mungu.
Na watu wale wanaoishi katika Utashi Wangu ndio tabasamu Yangu”

⬇️⬇️⬇️
Yesu Katika Tabasamu Yake
Foto hii ilichukuliwa dakika ile, ambapo Padre alikuwa akiinua Hostia, wakati wa Konsekrasio, katika Misa Takatifu ya kuhitimisha Retriti ya siku tatu juu ya Utashi wa Mungu, katika mji wa Leon, Guanajuato, Mexico, Mei 25, 1998

“Mimi ndiye Mwalimu Mtukufu, Mwalimu wa Utashi wa Mungu. Na watu wale wanaoishi katika Utashi Wangu ndio tabasamu Yangu”

Ukiitazama kwa umakini picha hii, elekeza macho yako kwenye Kifua cha Yesu, hapo penye mwanga mweupe unaoangaza.

Utaweza kugundua umbo la Padre aliyevaa mavazi ya Misa na anaadhimisha Misa Takatifu.

Yupo katika hatua ya kupandisha mikono yake juu akiinua Hostia Takatifu wakati wa Konsekrasio!

Pro Manuscripto
Kwa matumizi binafsi tu

EMAIL: albert.norbert@hotmail.com
WEBSITE: www.divinewilldivinelove.com
TELEGRAM Channel: t.me/utashiwamungunaupendowamungu
RUMBLE Channel: https://rumble.com/c/c-5818809
Luisa Piccarreta - “Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu”

Ziara ya Roho katika Utashi wa Mungu

Adveniat Regnum tuum! Ufalme Wako Ufike!

KWA SALA HII YA MFULULIZO, ROHO ANAJIUNGANISHA NA UTASHI WA MUNGU, KATIKA KAZI ZAKE ZOTE, ILI KUUABUDU, KUUHESHIMU, KUUSHUKURU, NA KUUPENDA, NA MUDA HUO ANAOMBA KUWA UFALME WAKE UFIKE
Na sisi, tukifuata mfano wa Luisa Piccarreta, tunajongea magotini mwa Immakulata, Mama wa Neno, Malkia wa Ufalme wa Utashi wa Mungu. Pale tunamtolea Mama utashi wetu wa kibinadamu, na badala yake tunamwomba tuupate Utashi wa Mungu. Katika unyofu wetu, mithili ya watoto wadogo, tunamwomba atutumbukize katika mabahari ya Utashi wa Mungu ambamo sisi tunatarajia kuambatana na kila moja ya Kazi zake kwa lengo la kuutuliza kwa utovu wa shukrani kutoka upande wa binadamu. Tutautuliza kwa wimbo wetu huu: “Ninakupenda Wewe! Ufalme Wako Ufike hima hapa duniani!”

Sala hii, ya Ziara ya kiroho katika Utashi wa Mungu, inayosaliwa moyoni, kwa mfululizo,
inamletea mwanadamu fursa ya juu kabisa ya kujiyeyushia mwenyewe ndani ya kazi ya Utashi wa Mungu

Ili kurahisisha zoezi la kusali sala hii kwa mfululizo, na ili kuwawezesha watu wa aina zote na wa mazingira tofauti tofauti ya shughuli za kila siku, hata kama zinawashika na kuwahangaisha sana, sala imegawanywa katika sehemu 24 kulingana na saa za siku.

Sala kamili inaitwa Saa za siku katika Utashi wa Mungu. Kila mtu anaweza akazisali sala zote kwa mfululizo, au anaweza akazigawa katika vipindi mbalimbali vya kutwa, au anaweza akasali sala moja tu kwa siku, na kama akitaka kumaliza kusali saa zote kila siku, anaweza akashirikiana na watu wengine katika zoezi hilo moja kwa kugawana saa za sala baina yao.
Y.M.Y (Yesu, Maria, Yosefu)

Mtindo ulio rahisi na wa ufanisi wa kutekeleza Ziara katika Utashi Mtukufu wa Mungu, na ili kuomba kuupata Ufalme wa FIAT ya Kimungu hapa duniani.

Mtu ajiinue mwenyewe na kuelekea mikononi mwa Muumba Wake. Anajitosa mwenyewe ndani ya Kifua cha Kimungu ili ajiunganishe Naye katika matendo yote aliyokuwa ameyatenda katika Uumbaji kwa ajili ya kumpenda yeye. Naam, mtu hatakubali kumwacha Muumba peke yake, anataka kumfuata katika kila kitendo. Kishapo, mtu anarejea kwenye dakika ya asili yake ili akashuhudie mianzo yake. Pale anahudhurisha vitu vyote sawa kama katika dakika ile, pale Mungu alipotekeleza kitendo cha kuumba vitu vyote. Anakuwa kama hifadhi anayepokea kila chema toka kwa Mungu. Anapokea Pendo lote la Kimungu litokalo katika Kifua Chake kwa njia ya FIAT yenye Maweza. Na yeye mtu, kwa Pendo lile lile, anamrudishia Mungu utukufu na uabudu.

Basi baada ya hapo, Mungu anamleta mtu ndani ya Eden ili pale akapokee pumzi ya kwanza ambayo Mungu aliingiza ndani ya Adamu. Ndiyo hiyo pumzi yenye kutengeneza uhai, na ambayo huendelea kutengeneza uhai. Halafu mtu anaanza kwenda kutembelea karne zote akipita kukumbatia binadamu wote na kumjazilisha kila mmoja na mema ya Muumba. Kadhalika anapitia kazi zote za Malkia Mama, anazitwaa na kuzifanya za kwake, na hata hizo anazitoa kwa Mungu Wake kana kwamba zingekuwa ni kazi za kwake mwenyewe.

Kishapo, mtu anaanza kufikiria ile kazi ya Neno kutungwa katika mimba, na matendo yote ambayo Neno ameyatekeleza wakati wa maisha yake. Na kwa kila moja ya matendo hayo, yeye anahusianisha na tendo la kwake la upendo hata lingekuwa ni dogo jinsi gani, anahusianisha na tendo lake la shukrani, na tendo lake la kuomba ujio wa Ufalme Wake. Halafu mtu anaendelea kumfuata Neno hatua kwa hatua hadi kifo chake. Aliendelea kutanguzana naye hadi ndani ya Limbo, anamsubiri pale kaburini ili apate kumwomba, kwa mastahili na nguvu ya Ufufuko Wake, anaomba Ushindi wa Ufalme wa Utashi wa Mungu. Mwishowe mtu anatangulizana na Neno katika tendo lake la Kupaa Mbinguni ili akamwombe alete kwa haraka Ufalme wa FIAT ya Kimungu hapa duniani.

FIAT! FIAT! FIAT!
SAA YA KWANZA

Tuufuate Utashi wa Mungu katika Matendo Yake yote, ili tukeshe pamoja nao na ili tuupate Uhai Wake wa Kimungu ndani yetu. Tuufuate katika tendo la kuumba Mbingu na Jua.

Yesu, Uhai Wangu, pigo la moyo wangu duni, pumzi ya roho yangu ndogo, makao ya akili yangu, udogo wangu wote unazamia ndani Yako, unapotelea ndani Yako. Mimi ni mtoto mchanga ambaye hajaweza kutembea bado. Ninakujongea Wewe, najibana kwenye mkono wako, na pamoja nawe nataka niingie katika Mwanga ule usiokoma wa Utashi Wako wa Kimungu.

Haya basi tazama, Baba wa Mbinguni tayari anatamka ile FIAT ya kwanza, na ndipo anafungulia mwanga mkubwa kabisa ambao unaangaza bila kikomo cha mipaka. Ewe Yesu Wangu, lo, unijalie roho yangu ipate nguvu yote, maweza, utakatifu, na mwanga wa FIAT yako abudiwa, ili mimi nisiweze kusikia kitu kingine tena ndani yangu isipokuwa Uhai wake hiyo FIAT! Nitakapokuwa nimetajirishwa tayari na Uhai wa hiyo FIAT, nitaweza kukumbatia na kubeba kila kitu, nitaweza kujaziliza kwenye kila kitu, na hata nitaweza kuiteka na Yenyewe na kuishusha ifike duniani kusudi irejee kwa shangwe kuja kutawala kati ya wanadamu!

Kwa hiyo basi, ewe Pendo Langu, uniache niendelee na hija yangu katika Utashi Wako, ili niendelee kufanya ziara ya kufuatilia Matendo Yake yote. Oh! Ni nzuri na inapendeza ilioje kuutafakari Utukufu Mkuu na wa Juu, ambao kwa kutamka FIAT moja tu unaweza mara kulipanua na kulisambaza hili anga samawati likiwa limejaa miliadi ya nyota zinazometameta kwa mwanga wao! Anapotamka FIAT nyingine anaumba jua; anapotamka nyingine tena anaumba upepo, hewa, bahari, na vitu vyote vilivyomo. Na anaviumba na kuvileta vyote hivyo katika mpangilio na uuwiano unaovutia na kuiteka roho ya yule anayetazama.

Ee Yesu Wangu, Chema Changu! Oh, mimi napenda nilitwae na kulifanya la kwangu, hilo Pendo lililobebwa na FIAT yako ya Kimungu wakati ikiumba anga lenye kufurika na nyota. Nataka niweze pia, kwa upande wangu, kupanua na kueneza anga langu la pendo ndani ya FIAT yako yenye Enzi. Kwa njia hiyo, ninapoijaza anga yote kwa pendo langu, nitapenda nitoe sauti yangu kwa kila nyota inayokuwepo ili nayo irudie pamoja na mimi kusema: “Yesu, Mimi ninakupenda!...... Ebu Ufalme Wako ufike hima hapa duniani!..... Utashi Wako wa Kimungu na upewe Utukufu kwa daima!...... Mimi ninauabudu na ninautukuza udumivu wako wa Kimungu na huo Uwepo Wako usiotetereka. Ndivyo hivyo vinavyoleta udumivu wa wanadamu katika mambo mema, na ndivyo pia vinawaandaa vema wanadamu wawe tayari kuupokea Ufalme wa Utashi Wako”.

Ewe Pendo Langu, naendelea na ziara yangu na ndipo ninafika ndani ya jua: Hapo ninakuwazia Wewe ukiwa katika dakika ile ambapo FIAT yako, toka Kifuani mwa Umungu, ilifungulia nje na kutoa mwanga mkubwa kabisa na kutengeneza tufe la jua, yaani ile sayari ambayo ndiyo ingekumbatia na kuibeba dunia pamoja na vitu vyote vinavyokaa ndani yake. Kwa mwanga huo jua lilitoa, kwa kila kimoja ya viumbe, busu lake la mwanga na la pendo. Na kwa njia ya busu lake hilo, kila kitu kiliweza kurembwa, kurutubishwa, kupewa rangi yake, kutajirishwa na kupambika.

Toka ndani ya Umungu Wako, FIAT yako ililifungulia na kulitolea nje hilo jua, yote kwa ajili ya kuonyesha tu Pendo lako kwangu mimi. Kwa minajili hiyo, mimi nataka, ndani yangu, nipate mwanga wake wote, joto lake lote na matokeo yake yote. Hilo ni kwa lengo kwamba, hata mimi niweze kukutolea Wewe, jua langu la kukuza, la kutukuza, na kwa njia yake niweze pia kubariki na kuusifia huo Mwanga wa Milele, kusifia Pendo Lako lisilozimika, Uzuri Wako pekee, Utamu Wako usiokoma na ladha zako zisizohesabika. Ndiyo kweli, Ee Yesu, mimi ninapenda nikukumbatie kwa nguvu ya huohuo mwanga wa jua, napenda nikupe mabusu yangu motomoto pamoja na ujotojoto wake, na kwa sauti yangu napenda kuimbilia huo mwangaza wake wote na pia kuimbilia matokeo yake yote. Nafanya hivyo kusudi nikuombe Ufalme wa FIAT yako kuanzia kule juu kabisa, kwa sayari ya hilo jua hadi kule chini kabisa, ambako mwonzi wake huwa unafikia.
Ewe Pendo Langu, je Wewe huonji jinsi Utashi Wako unavyopenda kuyapasua hayo mapazia ya mwanga ili uweze kuteremka na kuja kutawala kati ya wanadamu? Na mimi, nikiwa juu ya mabawa ya uangazo wa hilo jua, ninakujia ili kukuomba utupelekee haraka huo Ufalme wa FIAT yako. Kutoka pale katikati ya hilo jua, mimi ninakuomba uteremshe mng’ao wake ndani ya moyo wa binadamu ili kuwaangaza kwa Neema Yako, na ili kuwajalia Pendo Lako lenye kuunguza ndani yao chochote kile kilicho kibovu kisichoendana na Utashi Wako. Oh, ni kweli, endapo Mwanga Wako utateremshwa hadi kuwafikia wanadamu, basi uzuri wa Kimungu utawamulika ndani yao, hasira na uchungu vitakoma, na wote watajipatia utamu wako na hivyo uso wa dunia utafanywa kuwa mpya.

Ni kwa jinsi gani ninavyofurahia, Ewe Uhai Wangu, kuweza halafu kukuambia hivi: “Umenipa jua na mimi ninakupa jua! Mimi ninayo sayari chini ya mamlaka yangu, sayari ambayo inakuomba Wewe ulete Ufalme wa FIAT Yako. Je Wewe unataka kuugomea huo mwanga mkubwa ambao unakuomba? .......” . Kwa hiyo basi, Ee Yesu, fanya haraka hima! Hilo jua ndilo mjumbe wako wa Kimungu. Haya basi, Ewe Pendo Langu, fanyiza kwamba mwangaza wake, utakapowagusa tu wanadamu wote, papo hapo uufunue Ufalme wa FIAT Yako, ufunue utakatifu wake, na ufunue lile tamanio la kuwaona wanadamu wakipenya ndani yake FIAT kwa ajili ya kuwafanya wafurahie na wawe watakatifu.

Baba yetu...,
Salamu Maria...,
Atukuzwe Baba..
SAA YA PILI

Tuufuate Utashi wa Mungu katika tendo la uumbaji wa bahari na wa upepo

Ewe Yesu, Uhai Wangu, FIAT Yako inanisukuma, na kwa hiyo basi ona, mimi nipo hapa tayari kwa ajili ya kufuatilia lile tendo la kuumba bahari. Lakini ni nini hicho ninachosikia? Ninasikia sauti ya mbubujiko wa maji unaoendelea. Ni ishara ya ujimudu Wako wa tangu milele na usiokoma. Mimi naingia ndani ya huo ujimudu wa Kimungu, ujimudu unaoendelea bila kukoma, ujimudu unaoleta uhai kwa watu wote. Ninaufanya huo uwe ni ujimudu wa kwangu ili hatimaye niweze kuugawa wote kwa watu wote kwa ajili ya kukuomba Wewe Ufalme wa Utashi Wako, kwa niaba ya watu wote.

Ebu ona, Ewe Yesu, nikiwa na FIAT Yako ninateremkia kwenda kilindini mwa bahari na popote ninapopita na kuona mtikisiko au ujimudu, ninapoona uhai fulani, ninapoona mbubujiko wowote wa maji, hapo hapo ninatoa mlio wangu usiokoma nikisema: “Ninakupenda Wewe, ninakuabudu, ninaku-shukuru, ninakutukuza, na ninakushangilia!”. Kwa sauti yangu ninapiga kelele kushinda ule mbubujiko wa maji ya bahari, kupita kelele za maji yanayotikiswa na samaki, kupita kelele zozote za mawimbi madogo na makubwa ya maji, na katika kila nafasi ninapaza sauti kuomba Ufalme wa FIAT Yako! Je, Ee Yesu, Wewe husikii jinsi matone yote ya maji, katika mbubujiko wao, sawa na kelele za sauti nyingi sana, nayo yakisema: “FIAT, FIAT, FIAT!”. Na je husikii jinsi mawimbi ya maji na makelele yao makali yanavyopiga na yanavyojaribu kupasua na kufumua tumbo la bahari, na hivyo kutaka kulazimisha Utashi Wako utoke nje, uwameze ndani yake na ukawatawale wanadamu wote, na ili hatimaye wanadamu hao waweze kuruhusu FIAT ya Kimungu itawale ndani yao wenyewe ?

Ndani ya bahari hii, ninapoona na kusikia mbubujiko wa maji yake, mimi nakuja kusifia na kupenda huo ujimudu Wako usiokoma; katika mawimbi yake yanayopanda juu sana, ninapenda kutafakari juu ya Usafi ule usio na doa lolote; katika ukuu na upana wa bahari, ninatafakari Neema Yako na Ukuu Wako unaopita kila kitu, Ukuu unaoficha kila kitu. Nikiwa na hisia hizo zote, ninakuomba Wewe Ee Yesu, umfanye binadamu awe mtu mwadilifu, awe na nguvu, na awe msafi rohoni. Umjalie aweze kuishi amefichama ndani ya Utashi Wako Mtakatifu, lakini papo hapo akiwa anahusiana nao kikamilifu, ili aweze kutembea daima katika ujimudu uleule wa Kwako ambamo alikuwa ametokea!

Ewe Yesu Uhai Wangu, sasa napenda nitafakari juu ya Upepo na ubaridi wake unaoburudisha, juu ya pepo kali na athari zake za kimbunga, na za kisulisuli, juu ya pepo ambazo huwa zinaathiri, zinabomoa, zinazotulia pengine, halafu zinapanda na kuvuma, zinazoa na kuhamisha vitu. Hapo ninawaza juu ya kupenda, juu ya kusifu, juu ya kutukuza, na juu ya kushangilia himaya na mamlaka ambayo Utashi Wako unayo juu ya Upepo. Kuna wakati upepo unalia kimya kimya na kuna wakati upepo unapiga makelele kwa nguvu. Ni Pendo la Utashi Wako wa Kimungu kwa Yule anayelia katika upepo akiwa anatamani ajulikane. Na pale anapoona kuwa hasikilizwi na mtu, huyo anapiga makelele, anazungumza kwa sauti za ajabu ajabu. Ni kwa vile Yeye anataka atawale na kwa vile anadai kuwa na himaya yake mwenyewe kati ya wanadamu. Kwa kutumia mamlaka ya Utashi Wako Mkuu wa Juu, fanyiza kwamba Ufalme Wake FIAT Yako ufike kati ya wanadamu, na ukatawale juu yao wanadamu, kwa namna kwamba pasitokee kamwe mwanadamu anayeweza kuthubutu kuipinga hiyo FIAT. Kwa nguvu ya ubaridi wake mwanana, uwavute na kushawishi hao wanadamu. Tumia nguvu ya mabavu yake na ya mhemuko wake ili kuubomoa utashi wa kibinadamu ndani yao ili kusudi uweze kuwainua na kuwateka waingie katika Utashi Wako. Uwawezeshe hao wanadamu kusikia vilio vyako vyote vinavyoendelea, uwawezeshe pia kuelewa kuwa Wewe unataka kutawala kati yao. Kama utaona kuwa husikilizwi nao, basi piga kelele, zungumza kwa sauti kali ukitumia sauti zako zile za ajabu na za mafumbo, hata masikio yao yapate uziwi kutokana na kelele hizo. Hatimaye fanyiza kwamba kila mtu afikie kutambua na kukiri kwamba huo Utashi Wako Mtakatifu ndio Bwana Mkuu wake.
Kwa hiyo basi, Ewe Pendo Langu, hata mimi sasa napenda kukimbia juu ya mabawa ya huu upepo kusudi, kwa kupitia upepo huo, niweze kukuomba ujio wa Ufalme wa FIAT Yako. Katika kila wimbi la upepo huo napenda nipeleke, busu la FIAT hiyo, kwa kila mwanadamu. Niwapelekee mapapaso yake, na pia makumbatio yake matamu.

Baba yetu...,
Salamu Maria...,
Atukuzwe Baba..
SAA YA TATU

Pindi tunapofuata Utashi wa Mungu , tunaruka juu ya dunia nzima tukipita kugonga mhuri wa kauli yetu ya ‘Nakupenda’ juu ya kila kitu kilichoumbwa
.

Ewe Yesu Wangu, Moyo Wangu, Uhai Wangu. Uumbwa wote umekunywa na kunyonya hadi ukajaa Utashi Wako mwabudiwa. Matendo ya Utashi Wako ni mengi wala hayahesabiki katika vitu vyote vilivyoumbwa. Kwa sababu hiyo mimi, ili niweze kuyafuatilia matendo hayo, naamua kuanza kufanya hija kuzunguka ulimwengu mzima. Nafanya ziara kuzunguka kwenye hewa na pale ndani yake ninagonga mhuri wangu wa ‘Ninakupenda’, ili kukuomba kuwa, wanadamu hawa, wakati wanapopumua, wawe wanavuta hewa ya huo Uhai unaotawala ndani ya Utashi Wako.

Kwa kauli yangu ya ‘Ninakupenda’, ninapenda nibariki, nitukuze, na nipige muhuri juu ya utaratibu na harmonia iliyopo katika Uumbwa wote, ili niwafikishie wanadamu wote ule mpangilio na harmonia ya Ufalme wa Utashi wa Mungu. Nataka niruke juu ya dunia yote na kupita kugonga muhuri wangu wa kauli ya ‘Ninakupenda’, iwe juu ya unyasi mdogo kabisa, juu ya vimimea vyovyote vidogodogo, juu ya maua yote, juu ya miti yote iliyo mirefu kabisa, juu ya vilele vya milima, na hivyo hivyo hadi kule kwenye vilindi vyeusi totoro. Nitapita naruka na kubariki vyote hivyo ili kusudi nikuombe ueneze popote Ufalme wa FIAT Yako. Nitaviimbilia vitu vyote na nitatoa sauti yangu kwa vyote, ili kusudi vitu vyote vifikie kusema hivi: “Utashi Wako ufike kutawala hapa duniani”.

Ebu sikiliza Ee Yesu, mimi nagonga mhuri wa ‘Ninakupenda’ yangu hata ndani ya huyo ndege mdogo anayeimbilia, anayetetemesha, na hata anayekoromesha sauti yake. Pamoja na huyo ndege bado ninakuomba utuletee Ufalme wa FIAT Yako. Naendelea kugonga mhuri wa Ninakupenda yangu hata ndani ya huyo kondoo mdogo anayelia akiita, ndani ya huyo njiwa anayelia kama anasikitika. Hata kwa milio ya hao mimi ninakuomba Wewe utuletee Ufalme wa FIAT Yako. Hamna kitu kingine chochote ambacho hakina hamu ya kuchangia katika kurudia kiitikio hiki: ‘FIAT, FIAT’. Ewe Yesu Wangu, ninataka nipenye hadi ndani na katikati ya dunia, ili nikaweke huu moyo wangu pale ndani. Pigo la moyo wangu, wakati litakapokuwa linagonga, liwe linakupenda kwa niaba ya watu wote, liwe linawapenda watu wote, liwe linawakumbatia wote, na kutoka pale katikati ya dunia, moyo wangu uwe unapiga kelele nakulia: Ufike Ufalme Wako na Utashi Wako utawale!

Baba yetu...,
Salamu Maria...,
Atukuzwe Baba..
SAA YA NNE

Pindi tunapokusanyika sote katika Bustani ya Eden, hapo tunajiunga katika sherehe ya Mungu ya kumwumba Mwanadamu.

Ewe Yesu, Uhai Wangu, ninaonja kuwa Pendo Lako linanisukuma likinilazimisha niendelee kuzunguka, na Utashi Wako unaniita ukinitaka niwe pamoja na matendo Yake yote. Inaelekea kuwa Wewe huridhiki iwapo Binti Yako Mdogo hatakuwa pamoja na matendo ya Utashi Wako. Hata kama hajui bado kitu chochote, hata hivyo kwako Wewe ni raha, ili mradi awepo kama mtazamaji na awe hapo kwa ajili ya kurudia kiitikio cha “Ninakupenda, Ninakuabudu, Ninakuheshimu, Ninakushukuru”.

Ndipo mimi naendeleo na mzunguko wangu hadi ninafikia pale ndani ya Bustani ya Edem. Hapo ninakuona ukiwa katika tendo lile ambapo, Wewe Pendo Langu, pamoja na Utatu Mtakatifu, ulipokuwa ukitengeneza pambo lako penzi, yaani ile sanamu nzuri kabisa ya binadamu. Ni kwa pendo kubwa jinsi gani unavyomtengeneza! Ni uzuri mwingi kiasi gani hujamjazia bado! Ni marembo ya rangi ngapi na mitindo mitindo ya kimungu mingapi ambayo hujamwagia juu yake mpaka kufurika! Na wakati huo unapoendelea kumtengeneza, nakuona ukirudia kumtazama tazama, na unasema: “Ah, ni nzuri ilioje hii sanamu yangu!”. Halafu Pendo Lenu linafurika na kufurika kwa nguvu. Na kwa kukosa kujizuia, Ninyi mnaikumbatia hiyo sanamu nzuri na ya kupendeza, ingawa kama haijapewa roho bado, mnaikumbatia na kuibana kwa nguvu, na kwa nguvu zaidi kifuani penu. Halafu mnailisha kwa kuipatia uhai, na mnaipatia na ufanano wa Kwenu. Kishapo Nyinyi Wenyewe mnaingia ndani yake na kuijaza kabisa, kiasi kwamba hii sanamu, iliyo ni johari lenu, inashindwa kuwabeba ndani yake. Kwa hiyo, na yenyewe inajaa na kufurikia nje yake yenyewe, na inajikuta ikitengeneza bahari zake kwa ajili ya kumpenda Muumba wake. Hilo pendo lililotengenezwa, nalo linavimba sana na kutengeneza mawimbi makubwa makubwa yanayoruka na kuja kujipiga juu ya Pendo umbaji. Yanazuka mashindano ya upendo, ya uabudu, na ya utukufu baina ya Muumba na mwanadamu.

Pendo la kwangu linatetemeka mbele ya hilo tendo la ibada namna ile la kumwumbwa kwa binadamu. Ninasikia sauti yako ya uumbaji isiyokoma kurudia rudia ikisema: “Ni nzuri ilioje hii sanamu iliyotengenezwa na Sisi! Mwangwi wa pendo lake, ni jinsi gani unavyotuvuta na kutushawishi, na kutujeruhi! Ni jinsi gani sauti yake ilivyo tamu, na jinsi gani inavyosikika vizuri! Na ukumbatio wake anaotupatia, ni jinsi gani ulivyo ni laini na papo hapo ni wa nguvu! Ni jinsi gani tupatavyo raha kutambua kwamba tulimpatia uhai! Hii sanamu itaendelea kuwa ni raha yetu, furaha yetu, na itaendelea kuwa ni mchezo wetu wa kutufurahisha.
Yesu Wangu, katika kutetemeka kwangu kutokana na Pendo, ndivyo ninavyoingia kwa kweli ndani ya tendo lile ambamo Utukufu wako Mkuu mno, ukiwa unafurika Pendo, ulianza kuvuta pumzi kwa nguvu, pumzi iliyomvutia binadamu ndani Yenu ili kumjazia pumzi ya uhai. Pamoja na uhai, unampatia ufanano Nanyi, na kama urithi wake, mnampatia FIAT Yako ya Kimungu. Hata mimi napenda nipokee hiyo pumzi Yenu inayohuisha. Ninataka niwapende, na niwaabudu katika ukamilifu na utakatifu ule ule aliotumia yule Baba wa kwanza Adamu. Ninataka nipate yale mabahari Yenu ya Pendo na ya Mwanga. Na ingawa kama mimi ni mdogo bado, hata mimi nataka nitengeneze mawimbi yangu makubwa kabisa ya pendo. Hayo mawimbi yatavimba na kupanda hadi kufikia kifuani penu, yatapiga na kugonga kwenye mawimbi ya Kwenu yasiyokoma wala kukatika. Ndipo nami nitaanza kushindana na Muumba Wangu. Nitakuwa nampa Pendo langu ili niweze kuyapata mabahari mengine zaidi ya upendo. Katika mawimbi hayo, nitakuwa nikikuomba Wewe kwamba Ufalme Wako Ufike na FIAT Yako ijulikane. Ninaingia ndani ya ule umoja wa Utashi Wako, ukiwa ni umoja ule ule uliokuwa ndani ya lile johari lako penzi, naingia hapo ili utashi wangu mimi na Utashi Wako Wewe viwe ni Utashi mmoja, na pendo liwe ni moja. Katika huo umoja unaobeba mambo yote, napenda sauti yangu isikike hadi Mbinguni, na ikawafikie wanadamu wote, ikapenye hadi kwenye giza totoro ya vilindini, na ikapige kelele kwa nguvu ikisema: “Ufike Ufalme wa Utashi wa Mungu! FIAT, FIAT VOLUNTAS TUA, hapa duniani kama kule Mbinguni!”. Na katika umoja huo wa Utashi wa Mungu, nitakuwa ninautwaa utakatifu na kuufanya uwe wa kwangu, na ndivyo nitatwaa na utukufu, uabudu, shukrani za mawazo, za mitazamo, za maneno, za matendo, na za hatua mbalimbali za yule Adamu aliyekuwa bila waa lolote. Kwa namna hiyo nitakuwa nakurudishia Wewe, kwa kurudia rudia, yale matendo yake, ili utakapokuwa unaona ndani yangu huo Utashi Wako wa Kimungu unavyotenda kazi, Wewe utaridhia kuwa Ufalme Wako uweze kufika.

Katika Bustani hii ya Edeni, kulikuwepo daima na sherehe baina ya mwanadamu na Muumba. Binadamu alikuwa ndiye doli la Kimungu, alikuwa furaha Yao, alikuwa ndiye raha iliyomfurahisha zaidi Baba wa Mbinguni. Katika huo umoja wa muungano wa Utashi wa Mungu aliokuwa nao, binadamu alifaidi kuchukua nafasi ya kwanza kati ya Uumbwa wote. Kwa hiyo, mambo yote yalikuwa katika harmonia, na katika mpangilio. Anga, nyota, Jua, na bahari, vyote vilionja kuwa vimepata heshima ya pekee kuweza kumtumikia na kumtii Adamu kila alipokuwa anawaashiria kufanya lolote. Alikuwa yeye ndiyo tabasamu ya vitu vyote, alikuwa ni furaha yao, na mtamaniwa wa kila kitu. Na yeye Adamu alikuwa akipeleka kila kitu kwa Muumba Wake, na Mungu alikuwa akielekeza daima macho Yake juu ya Adamu, ili kuhakikisha kuwa pasikosekane kitu chochote kwa ajili ya kumletea raha zake kikamilifu.

Mungu, akimwangalia na kumwona kuwa yu katika upweke, akapenda kuongeza raha yake Adamu iwe maradufu. Alimtia usingizi wa namna ya ekstasi nzito kabisa, na akamfanya alale mikononi Mwake. Ndipo akamtoa ubavu wake mmoja ambao kwayo alimtengeneza mwanamke aliyekabidhiwa kwake awe mwenzi wa kufanana naye. Kwa tendo hilo alimjalia ujazo wa uwingi wa furaha. Na, lo, huyu Eva, akiwa ndiye mama wa kwanza kabisa, alipoingia na yeye katika muungano wa umoja wa Utashi wa Mungu, naye alijiunga kufanya mashindano na Adamu.

Walikuwa wakishindana kati yao, kuona ni nani kati yao, wakiwa ndani ya mabahari yao ya pendo, angeweza kutengeneza mawimbi mengine makuu zaidi ya pendo, ambayo yangeruka juu zaidi na kwenda kugongana na yale mabahari ya Kimungu katika ukuu wao usio na ukomo. Kwa njia hiyo Adamu na Eva wangefikia kujipatia mabahari mengine ya pendo, na kujipatia neema nyingine za Kimungu. Na mawimbi ya pendo lao yalizidi kupanda na kushuka hata kufanya mabahari yao yazidi kuongezeka, kupanuka na kuenea.