Jinsi Ya Kupika
953 subscribers
50 photos
3 links
Tunatoa Huduma Ya Catering | Wapishi | Cake | Mapambo | Photography | Mziki | Mc Na Huduma Zingine Zote Za Chakula.

Admin Account @TanzaniaCatering

Official Group @MapishiGroup
Download Telegram
Channel created
JINSI YA KUPIKA BISKUTI ZA JAM - JAM BISCUIT.

VIPIMO


Unga 2 Β½ gilasi

Sukari ΒΎ gilasi

Samli 1 gilasi

Mayai 2

Baking powder 2 kijiko vya chai

Vanilla 1 Β½ kijiko cha chai

Maganda ya chungwa 1


NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Tia kwenye machine ya kusagia (blender) mayai, sukari, vanilla, samli na maganda ya chungwa, saga vizuri.

2. Tia unga kwenye bakuli pamoja na baking powder, mimina vitu ulivyosaga kwenye bakuli, changanya.

3. Punguza unga uliochanganya kidogo weka pembeni.

4. Unga uliobakia tia kwenya tray ya kuchomeya, utandaze vizuri, tia jam juu yake.

5. Chukua la kukwaruzia carrot (grater) ukwaruze unga uliuopunguza juu ya jam.

6. Choma kwa muda dakika 20 moto wa 180 C.

7. Acha ipowe kidogo, zikate vipande vya mraba (square) Tayari kwa kula.

@JinsiYaKupika
JINSI YA KUPIKA CAKE YA MAZIWA - MILK CAKE .

Vipimo

πŸ‘‰ Siagi Kikombe 1

πŸ‘‰ Sukari Kikombe 1

πŸ‘‰ Unga Vikombe 2

πŸ‘‰ Maziwa 1/2 (nusu) Kikombe

πŸ‘‰ Mayai 4

πŸ‘‰ Baking Powder 1 Kijiko cha supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Washa oveni 350 - 400 Deg C liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki.

2. Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.

3. Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.

4. Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja.

5. Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)

6. Chukua trey ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Treya isiwe nzito sana au nyepesi sana bali iwe wastani.

7. Ipike (Bake ) mpaka iwive.

8. Epua iache ipoe ndio ukate kate vipande.

@JinsiYaKupika
JINSI YA KUPIKA VANILLA CUPCAKES

VIPIMO

πŸ‘‰ Siagi ΒΎ kikombe

πŸ‘‰ Sukari kikombe 1Β½

πŸ‘‰ Mayai 2 

πŸ‘‰ Vanilla viJiko 2 chai

πŸ‘‰ Baking powder viJiko 2Β½ chai

πŸ‘‰ Chumvi ΒΌ KiJiko chai

πŸ‘‰ Unga wa ngano vikombe 2Β½ 

πŸ‘‰ Maziwa ya maji kikombe 1ΒΌ

JINSI YA KUOKA

1. Washa oven joto 175Β°c. Tia paper liners katika muffin tins au paka mafuta kila tundu la muffin tray.

2. Katika bakuli chekecha unga, chumvi pamoja na baking powder, koroga kuchanganya vizuri kisha weka pembeni.

3. Katika bakuli piga siagi hadi iwe laini,tia vanilla na sukari kisha piga tena hadi mchanganyiko uwe mweupe.

4. Tia yai moja baada ya jingine ukipiga vizuri kila unapotia.

5. Kwa kutumia mwiko au spatula tia unga taratibu pamoja na maziwa,ukianza na kumaliza na unga.

6. Mimina katika muffin tins kisha oka hadi zipate kuwa rangi ya brown.

7. Acha zipoe kabisa katika wire rack, Kisha Unaweza KuPambia kwa icing uipendayo.

NB ; UKILA NA JUICE UNAWEZA UKAMALIZA VYOTE PEKE YAKO BAADAE UKAANZA KUTAMANI TENA πŸ˜‚

@jinsiyakupika
JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA VIAZI

MAHITAJI

♦DONGE

πŸ‘‰ Unga wa ngano vikombe 4

πŸ‘‰ Mafuta viJiko 2 chakula

πŸ‘‰ Maji kiasi

πŸ‘‰ Siagi Β½ kikombe

♦UPANDE WA VIAZI

πŸ‘‰ Viazi vilivyochemshwa na kupondwa 4

πŸ‘‰ Chumvi kiasi

πŸ‘‰ Binzari ya unga Β½ kiJiko chai

πŸ‘‰ Pilipili ya unga Β½ kiJiko chai/ukipenda

πŸ‘‰ Kitunguu kilichokatwa katwa 1

MATAYARISHO NA JINSI YA KUPIKA.

1. Changanya mahitaji yote ya unga kisha kanda kufanya unga mlaini.

2. Funika acha ukae Β½ saa, fanya madonge size upendayo.

3. Changanya mahitaji yote ya viazi weka pembeni.

4. Chukua donge moja sukuma kufanya chapati ndogo, chota mchanganyiko wa viazi kisha funika vizur na zungusha kufanya donge tena. Rudia kwa madonge yote.

5. Sukuma chapati zako na choma kama kawaida katika moto wa kiasi hadi zipate rang nzuri.

6. Chapati za viazi tayari kwa kula na curry yoyote.

NB ; UKIWA UNASHUSHIA NA FANTA PEMBENI LAZIMA USAHAU SHIDA ZA DUNIA πŸ˜‚

@JinsiYaKupika
JINSI YA KUPIKA CAKE ZA NAZI

♦VIPIMO

πŸ‘‰ Unga Β½

πŸ‘‰ Β½ kikombesukari

πŸ‘‰ ΒΌ kikombe mayai

πŸ‘‰ baking powder Β½ kijiko cha chai

πŸ‘‰ maziwa kiasi tuu / Tui LA Nazi

πŸ‘‰ vanilla Β½ kijiko

♦NAMNA YA KUTAYARISHA

1.Tia siagi sukari na baking powder piga kutumia mashine(mchapo)mpaka iwe laini

2.Tia mayai na uendelee kupiga

3.Tia unga polepole huku ukiendelea kuupiga ongeza na tui la nazi (coconut milk)

4.Tia maziwa na vanilla piga kidogo tumia treya ya vishimo(muffin tray) weka karatasi zake kisha mwaga ule mchanganyiko katika vishimo kiasi kiasi chunga usivijaze sana

5.choma(bake) katika moto wa 325Β°c kwa dakika 10-15mpaka iwe rangi ya uthurungi(brown)

6.Epua Hapo itakuwa Tayari kuliwa

NB ; KAMA HAUJAZOEA KULAMBA LAMBA LIPS BORA USIPIKE πŸ˜‚

@JinsiYaKupika
JINSI YA KUTENGENEZA PEANUT BUTTER - SIAGI YA KARANGA

♦MAHITAJI

πŸ‘‰ Karanga vikombe 2

πŸ‘‰ Asali au sukari kijiko 1 na nusu cha chakula

πŸ‘‰ Mafuta ya kupikia kijiko 1 na nusu cha chakula

πŸ‘‰ Chumvi Β½ kijiko cha chai

♦NAMNA YA KUTAYARISHA

1.Kaanga karanga bila mafuta mpaka zikaangike vizuri yani maganda yaanze kutoka yenyewe

2.Ziache zipoe kisha toa maganda

3.Mimina karanga,chumvi na mafuta katika blender ama food processor...saga hadi iwe laini

4.Ongeza asali,chumvi ,sukari au asali na mafuta saga hadi iwe laini...

5.Hifadhi katika chupa yako kisha weka kwenye FriJi

NB ; UKILA NA MKATE USISHANGAE KUSIKIA KITU KINAKUAMBIA UKANUNUE MKATE MWINGINE MZIMA πŸ˜‹

@JinsiYaKupika