Swahili News
3.77K subscribers
109K photos
59K videos
28 files
267K links
🐾
Download Telegram
https://millardayo.com/mfanyabiashara-maarufu-wa-madini-arusha-saitoti-afiwa-na-baba-yake/

Mfanyabiashara Maarufu Mkoa wa Arusha na Manyara na mmiliki wa kampuni za uchimbaji wa madini ya Tanzanite Azo Africa Limited na Germ and Rock Ventures,Joel Saitoti amefiwa na baba yake Mzazi Emmanuel Laidoson Mollel ambaye alikuwa ni Mkulima na Mfugaji katika Kijiji cha Nduruma marurani Wilayani Arumeru,Mkoani Arusha

Taarifa iliyotolewa na familia imesema kwamba baba yao aliugua kwa muda mrefu kwa kipindi cha miaka mitano na kufariki dunia February 2,2023 hivyo Mazishi yatafanyika January 7,2023 kijiji cha Marurani kata ya Nduruma Wilayani Arumeru.

NYUMBA, MALI ZATEKETEA MOTO, LAWAMA KWA ZIMAMOTO, WATUMIA NDOO KUZIMA, “SIMU INAITA WIMBO WA TAIFA”.
https://millardayo.com/makalla-awapeleka-machinga-rwanda/

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla na Benki ya NMB leo February 03,2023 wamekabidhi ticket za ndege kwa Viongozi 12 kwenda Nchini Rwanda ziara ya mafunzo, makabidhino ya tiketi hizo yamefanyika katika Ukumbi wa DMDP Ilala Jijini Dar es Salaam.

RC Makalla ameishukuru Benki ya NMB kwa kuwezesha tiketi za ndege 12 kwa Viongozi watano wa Machinga, watano wa Bodaboda na Wataalamu wawili kwenda na kurudi ziara ya mafunzo Nchini Rwanda.

RC Makalla amesema Viongozi hao wanatarajia kusafiri February 6,2023 na kurejea Dar es Salaam February 10, 2023 “Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo maalum ya kulea makundi ya Machinga na Bodaboda ambapo ninachokifanya ni kutekeleza maono ya Mhe Rais”

Makalla amewataka Wamachinga na Bodaboda kutumia ziara hiyo kujifunza na kutangaza biashara kwa kuwa Rwanda hutumia Soko la Karikaoo kununua bidhaa mbalimbali ambazo wanakwenda kuziuza kwao.
https://millardayo.com/wafungwa-wote-wanakula-ugali-maharage-wenye-ukimwi-wanadhoofika/

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI leo imewasilisha taarifa Bungeni Dodoma na kueleza kuwa Wafungwa na Mahabusu Tanzania wanapewa chakula cha aina moja tu ambacho ni ugali na maharagwe kila siku hali inayofanya wale walioathirika na virusi vya UKIMWI wanapokuwa wanatumia dawa za kufubaza virusi (ARVs) wazidi kudhoofika kiafya kwani dawa wanazotumia ni kali na zina nguvu sana.

Kamati hiyo imeishauri Serikali kuhakikisha lishe bora inatolewa kwa WAVIU waliopo magerezani ambapo takwimu zilizotolewa na Kamati hiyo zinaonesha kuwa magereza yote nchini yana jumla ya Wafungwa na Mahabusu 888 waliogundulika kuwa na VVU na wanatumia dawa.
https://millardayo.com/sbl-yatenga-milioni-36-kwa-ajili-ya-kapu-la-wana/

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya PILSNER imetenga Tsh. milioni 36 kwa ajili ya kuwazawadia Watanzania 12 wataoshinda katika kampeni yake ya “Kapu la Wana” ambayo ina zawadi mbalimbali kama gari, bodaboda, TV na simu za mkononi ambapo Meneja wa Bia hiyo Wankyo Marando amesema siku zote bia hiyo ipo kwa ajili ya kusherehekea mafanikio ya walaji na kuwatunza kwa umaridadi wao kwenye kutimiza ndoto na kuchapa kazi.

“Kampeni hii itadumu kwa miezi 8, Pilsner Lager ni bia ya Vijana ambao hawakati tamaa na wenye kiu ya kutimiza mafanikio makubwa, tunawawezesha Vijana kwa kuwapatia vitendea kazi ili wasonge mbele hivyo tunawahamasisha walaji wote wa PILSNER LAGER kuitumia kampeni hii ili kusogeza juhudi zao mbele” Wankyo Marando.

“Ukinunua bia ya Pilsner Lager utapata kadi ya kukwangua ili kujipata zawadi kila unun...

View original post
https://millardayo.com/katibu-wa-ccm-anena-haya-kuhusu-malezi-ya-watoto-wa-kike-wilayani-morogoro/

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Daniel Chongolo amesema tabia ya wazazi na walezi Wilayani Morogoro kuwatumia watoto wa kike katika shughuli za kimila ikiwemo kucheza ngoma na kuwaozesha wakiwa bado na umri kinda kuwakosesha haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Katibu Mkuu Daniel Chongolo amesema hayo baada ya kuwasili Wilayani Morogoro kutokea Wilayani Ulanga katika muendelezo wa ziara yake ya siku tisa ya kuimarisha chama Mkoani Morogoro.

Morogoro Wilaya yenye mila na desturi kama ilivyo maeneo mengine nchini lakini mila za wenyeji wa kabila la Waluguru zinadaiwa kuwa kikwazo kikubwa kwa mtoto wa kike kufikia malengo kielimu.

.
.
.
.
.
.
.
Azam TV

#NBCPL Shughuli imekwisha bila goli……

FT: TZ Prisons 0-0 Mtibwa Sugar

Inafuata mechi kubwa……. Si ushajua ni ipi? Bado tuko LIVE #AzamSports1HD

#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPLUpdates #NBCPL #SisiNiSoka #SokaLetuBambam #TanzaniaPrisons #MtibwaSugar #PrisonsMtibwa
Azam TV

SIMBA vs SINGIDA: Kazadi, Baleke, Wawa na Inonga ni miongoni mwa vichwa 22 vinavyoanza leo huku Kibu na Ndemla wakianzia mkekani.

Tukutane saa 1:00 usiku

#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPLUpdates #NBCPL #SisiNiSoka #SokaLetuBambam #SimbaSC #SingidaBigStars