Global Traders ForeX (GTFX )💵
80 subscribers
130 photos
13 videos
6 files
67 links
Free forex Education,Signals, For All,, Help others and share this groups link
https://t.me/GlobalTradersForeX
ᴼᴾᴱᴺ ᴿᴱᴬᴸ & ᴰᴱᴹᴼ ᵀᴿᴬᴰᴵᴺᴳ ᴬᶜᶜᴼᵁᴺᵀ ᴮᵞ ᵁˢᴵᴺᴳ ᵀᴴᴵˢ ᴸᴵᴺᴷ https://secure.templerfx.com/login/sign_up/205697
Download Telegram
GARTLEY 222 PATTERN

Pattern hii ni miongoni mwa pattern maarufu sana zinazotumika kutambua retracement. Inakuzawadia entry ya mapema wewe kama trader ikiwa na kiasi kidogo kabisa cha risk kwenye uwezekano wa reversal ya trend ya muda mrefu.

Kwa wale ambao wanapenda kutrade muda mfupi, pattern hii inakusaidia vizuri kabisa kutrade level ya juu na level ya chini ndani ya siku husika. Gartley inatusaidia kununua au kuuza kwenye AB=CD pattern ya mwanzo katika uelekeo mpya wa bear au bull, Na hilo ndio ambalo pattern hii itakusaidia kupata entry katika uelekeo (trend) mpya uliotengenezwa. Reversal kubwa zinawezekana zisifuatiwe na pattern hii, lakini unaweza ukapata faida kwa kutumia management skills nzuri ya biashara hii. (kama pattern hii haitakua failure pattern)
GARTLET 222 PATTERN STRUCTURE

Muundo wa pattern hii inakaribiana kufanana na AB=CD pattern, ikiwa na tofauti kubwa moja. Inakua na mguu mmoja wa nyongeza ambao unahitimisha AB=CD, ambapo AB=CD Inaundwa na miguu mitatu, Gartley pattern inaundwa na miguu minne.

Pattern hii ni lazima iwe ina AB=CD pattern ili ikamilishwe kuwa Gartley pattern. Pattern hii inatambulika kutoka inavyoanza kwa kuwekewa herufi X. Baada ya ya mguu X kukamilika. Mwisho wa mguu huu huanza kuunda AB=CD Pattern.

Kama ilivyokuwa kwa AB=CD pattern, Gartley pattern pia inapatikana kwenye timeframe yoyote na katika hali yoyote ya soko. Pttern hii ni retest ya point ya juu au ya chini ya bei na inamzawadia trader entry kwenye uelekeo wa trend husika. Sheria sawa kabisa na ambayo tunaitumia kwenye AB=CD Pattern
VITU GANI HUFANYA PATTERN HII IWE INVALID!?

Kuna mambo matatu ambayo yatafanya pattern hii ionekane invalid;

1. Point D ukamilifu wake hautakiwi kuzidi ponit X

2. Point C haitakiwi kuzidi point A. C inaweza kuwa 100% Fibonacci level, Double top au double bottom ya point X. Japo ikitokea hivo inaweza isiwe na uhakika sana ila inakua valid.


3. Point B haitakiwi kupitiliza point X.
TABIA MUHIMU ZA GARTLEY 222 PATTERN

Pattern hii inaweza kuvunjwa vunjwa katika vipengele vinne ambavyo vina uhusiano na swing ya uelekeo husika. Point X ni point ya juu au ya chini ya swing hii na ndio mwanzo wa muundo wa swing hii. Point X inaweza kupatikana kwenye chati za muda mkubwa kwenye point kuu ya juu au ya chini. Ingawa pia X inaweza kupatika kwenye point ya chini au ya juu ndani ya trend ya chati za muda mkubwa/ Trend kubwa. Kwa lugha nyingine X inaweza kutokea ndani ya swing kubwa bila X kuwa eneo la chini au Juu katika trend kubwa.

Point X huwa hitimisho la bei ambapo technical trader huangalia katika siku. Baada ya Point X kutengenezwa na soko kuanza kutembea kwenye direction moja, mguu XA huanza kutengenezwa. Muda huu inakua ngumu kutambua mwisho wa mguu XA utakapokua.

Kuna tabia fulani ambazo hutoa alama ya uwezekano wa urefu wa mguu XA.

Pindi mguu huu unavyojitengeneza huwa na tabia ya kuvunja support na Resistance zilizopo kwenye data zilizopita kwenye chati. Njia pekee ya kutambua mguu XA umekamilika ni baada ya kukamilika mguu wa pili AB karibu na hitimisho la point A.

Baada ya kutambua kuwa mguu XA umekamilika, hatua inayofuata ni kutazama kuundwa kwa mguu AB. Mguu huu ni muitikio wa kwanza wa juu au chini kutoka kwenye impulsive wave ya kwanza kutoka point X. Vitu ya muhimu kuviangalia katika uundaji huu ni;

1. Uwiano wa Fibonacci retracement ambapo soko limefanya correction.

2. Idadi ya candlestick ambazo zimetengeneza mguu huu.

3. Ulinganishwaji wa muinuko na mteremko.
SAIKOLOJIA YA GARTLEY 222 PATTERN

Inatengeneza kwenye level za tamaa na hofu ya washiriki wa soko. Pindi pattern hii ikitengenezwa kwenye point kuu ya juu ya bei. Move ya kwanza kutoka juu hutafuta support katika point A.

Tutumie Bearish Pattern kwa Mfano;

Soko linaweza likapanda au kushuka bila correction yoyote. Point hii katika pattern hutengenezwa pindi washiriki wa kutosha katika soko wanapolitambua eneo hilo kama eneo sahihi la kubuy na bei inatengeneza rally kutoka hapo.

Hii pia inatokea kwenye point C ya hii pattern. Kutokana na kuwa na wanunuaji na wauzaji sokoni pindi soko linavyotengeneza pindi B na D, Sellers wanaangalia eneo hilo kama wanatoka au kuanza kuweka oda za kuuza.

Point D kwenye pattern hii ni eneo la kutambua ukweli kama buyers au sellers watashinda. Bei kushindwa kutawanufaisha sellers, Bei ikienda juu ya X kutaleta kushindwa kwa pattern hii.

Kama pattern hii ikifanikiwa. Bei inaweza kwenda mpaka kwenye point A. Na hiki kinavyotokea support nyingi zinavunjwa na wale watu ambao walinunua juu ya point wanaanza kukutana na loss katika trade zao.

Ni ukweli wa uhalisia wa binadamu, wachache wataamua kufunga trade zao haraka baada ya loss ndogo na wakati kundi kubwa wakisubiri bei ije tena kwenye eneo waliloingilia jambo ambalo linaweza likatokea au lisitokee.

Kadri bei inavyozidi kuwakataa, traders wengi ambao wapo kwenye loss kubwa hujokuta wanalazimika kuongeza order nyingine katiak maeneo ambayo sio sahihi, Ambapo inakua inaanza kutoa viasharia vya kuisha kwa safari ya kuuza inayoonesha ukomo na support inapatikana baada ya oda mpya za kubuy zinapowekwa.

NAMNA YA KUTRADE PATTERN HII.

Pattern hii inadadavua uhitaji wa kutrade Kwenye Point za chini na juu pindi inavyoretest kwenye point za juu au chini kwa muda husika. Kama ambavyo tunatambua Tunanunua kwenye higher low na kuuza kwenye lower high, ambao ni msingi wa kutrade kulingana na trend husika. Trend inatambulika kwa higher low na higher high kwenye uptrend na Lower low na lower high kwenye downtrend.

Oda aina ya Limit juu kidogo mwa 0.786 inaweza kutumika katika aina hii ya trade na stop loss ya kwanza ikiwa chini kidogo ya 1.00 (X) level, Ingawa hii muda mwingine inawezekana ikawa kubwa sana kulingana na lotsize unayotumia na idadi ya pips ambayo upo tayari kuziweka katika riski (Stop loss)

Daima kumbuka kuangalia kiasi cha riski na eneo gani ambalo utaweza stop loss katika trade yoyote. Kama hautapata stoploss level ambayo inazidi management plan yako, Trade hio inapaswa kuachwa na kutafuta trade nyingine ambayo itakubaliana na management plan yako ya riski. Tunaweza kurudia kuingia kwenye trade ambayo tumetolewa kwa stop loss kama bado pattern ipo valid na stoploss level inakubaliana na management plan yetu.

A limit order juu kidogo ya 0.786, Stop loss chini kidogo ya 1.00 (X) level, malengo ya faida ya kwanza yanapaswa kuwa na kiasi cha risk katika trade ambapo baada ya kufikia lengo hilo unahamisha stop loss kuja kwenye breakeven huku malengo yakiwa kutoka kwenye 0.618 .
Follows us Instagram, Tumewashaa Motoo 🔥🔥🔥💥😂😂
🔥🔥🔥❤️❤️❤️❤️❤️
You can email templer through

support@templerfx.com


TELL THEM👇🏼👇🏼

Hello, make me under the agent with Account 205697 my account is...... Put you're ACCOUNT NUMBER

Thanks for cooperation👏

After let me know you will be added VIP SIGNAL GROUP 99% PROFIT
The account of the user that owns this channel has been inactive for the last 5 months. If it remains inactive in the next 20 days, that account will self-destruct and this channel will no longer have an owner.
The account of the user that owns this channel has been inactive for the last 5 months. If it remains inactive in the next 7 days, that account will self-destruct and this channel will no longer have an owner.